Ukiona unagombana na mtu ujue bado hujaanza kuishi uhalisia wa maisha ila upo tu katika kuishi. Kama bado unashangazwa na matukio jua bado una safari ndefu sana ya kufikia uhuru wa maisha.
Katika maisha yapo mambo mengi ambayo hutukia na ili kuyashinda ni muhimu zaidi kujifunza kwa kila tukio ambalo unapitia. Kama kwa sasa wewe ni kijana mtu mzima wa miaka ishirini na kuendelea ni wazi kwamba yapo mengi ambayo yametukia huko nyuma na inaweza ikawa zawadi yako kubwa sana ya kuishi maisha yenye maana kama utajifunza kwa yele ambayo umepitia.
Tuna mambo mengi sana ya kujifunza katika maisha, mahusiano, shughuli zetu, na mambo mengine ambayo tunapaswa kufahamu. Ili ufikie angalau kiwango cha kuweza kutatua matatizo kiurahisi, basi, utambuzi wa kutofautisha lazima uwe nao na lazima uwe na utambuzi wa kuielewa lugha.
Wengi huwa tunapuuzia katika swala la kujinza lakini swala la kujifunza ni sehenu muhimu sana kuliko jambo jingine.
Methali 4:7, Bora hekima, basi jipatie hekima; naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Dunia sio sehemu ambayo inauhalisia wa mambo, wakati wote kila jambo tunalolifanya ni lazima liende na mapungufu, ikiwa huna ufahamu hutaelewa hili. Ni muhimu zaidi kujifunza ni muhimu sana.
Kama wewe ni mmoja wa watu wazima sasa, unatambua kabisa, wakati mwingine unaweza ukawa unataka kuwasilisha jambo lakini watu wakawa wamelichukulia tofauti kabisa na namna ambavyo wewe ulikuwa unamaanisha. Unajikuta umeingia kwenye migogoro ambayo hukutarajia, lakini chanzo kikuu ni ukosefu wa ufahamu. Ufahamu unakupa utambuzi, utambuzi wa kutambua mazingira na lugha.
Mapito yako ni moja ya zawadi ambayo inaweza kukufanya kwa sasa ukafanya vizuri, na Mungu hutufanya tupitie katika wakati fulani na hawezi kuacha tuondoke hapo bila kuhakikisha tumeacha kovu ambalo ni ukumbusho kwetu. Wakati wana wa Israeli walipokuwa wanavuka katika joint ya mto Yordani, Mungu aliwataka wachukue mawe ya ukumbusho ili wawasimulie wanaye jambo lililo tukia hapo. Hii ndio zawadi ya mapito, mapito yanakufunza lakini usipofunzwa na mapito yako basi ni wazi mapito yako yatakuwa mapigo kwako.
Huwa ninakumbuka sana mapito ya nyuma, kwa kweli hapa ndipo ambapo siwezi kuacha kutafakari kwenye kila kitu. Nilisha wahi kuwakosea watu wengi sana kwa namna moja ama nyingine lakini leo mapito yangu ni zawadi kwangu. Naweza kufanya maamuzi sahihi kutokana na mapito yangu na makosa niliyofanya huko nyuma.
Ushawahi kujiuliza kwanini Mungu katumia gharama kubwa sana katika kutimiza neno la Mungu? Inawezekana hujawahi, lakini rafiki yangu, Mungu ametupa zawadi kubwa na yakipekee, wapo watu ambao walikufa kwenye biblia ili wewe ujifunze na uishi maisha ya maana, wapo watu ambao walipitia maisha magumu kwenye biblia ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watu walifanya mambo mabaya kwenye biblia mambo yamerekodiwa ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watu wamepigania kitabu kitakatifu ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watawale ambao walikuwa na hekima ili wewe uishi maisha ya maana. Isitoshe, bado umepewa zawadi ya mapito yako. Roho Mtakatifu hukufundisha kila siku, mazingira ya asili ambayo unaishi nayo ni kwaajili yako, watu wanaokuzunguka waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa yote kwa sababu yako. Mungu amekupa kila kitu na mwisho bado anakwambia yeye ndio ngao yako na tuzo lako.
Ndugu yangu, tujifunze, tuvae utayari wa kujifunza kutoka kwake, haijarishi wewe ni mtu wa namna gani? Hata kama umeishia darasa la saba, wewe unafikiri watu wa zamani walikuwa wasomi? Akina Paulo watu ambao walikuwa na hekima ya kutosha na akina Sulemani, mtu mwenye hekima zaidi. Inawezekana ukanambia kwamba wao walitumiwa na Mungu, lakini kumbuka kwamba, Mungu alimaliza kazi yake siku ya saba na lazima utambue maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, ukiuandaa moyo kwa kusudi la kupokea haki ya Mungu utapokea haki yake.
Leo hii changamoto nyingi hasa za migogoro ni kwa sababu ya kutokujifunza. Utambuzi na ufahamu ni kwaajili ya kushi maisha yenye maana. Tusitembee kama vipofu, tutajikuta tunafanya mambo yasiyofaa kwa sababu hatuna utayari wa kujifunza.
Mathayo 11:25-30,Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Namshukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Asema, nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Njoni kwangu, nyinyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu mkajifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Ikiwa Yesu anamshukuru Mungu kwa sababu yeye amekabidhiwa kila kitu, basi nasi pia tunamshukuru Mungu kwani nasi ni ndugu wa Yesu kwa imani na pia amesema tujifunze kwake, tuvae nira yake tuwe kama yeye, ndipo tutapumzishwa. Na kuvaa nira yake inakupasa kujifunza, unajifunza kupitia neno lake na kila kitu. Lakini yeye anasema yeye ni mpole na mnyenyekevu, kwa hiyo tunapaswa kuwa wanyenyekevu na wapole wakati tunajifunza.
Je! unataka kuishi maisha ya kustuka kila siku, mtu aliye kama kipofu? Maana jibu la wakati ujao limefichwa ndani ya wakati. Lazima utambue kwamba Mungu anakupenda, kaa chini tafakari fikiri, acha kulaumu kila jambo. Ili watu wa dunia hii tufikie uhuru ni pale kila mmoja wetu atafikia kiwango cha kujitambua kipekee na ndipo hata kuwepo mtu wa kumlaumu mwingine. Watoto wanao zaliwa ni rahisi kuwasamehe kwa sababu hawatambui kitu lakini kwa mtu mzima akikuuzi ni lazima mgongano uwepo kwa sababu tunatambua kwa watu wazima wanajitambua. Lakini kwa sababu hata watu wazima hawana utayari wa kujinza changamoto inabaki pale pale. Lakini kama umejifunza ni rahisi kusamehe wengine.
Je! unatumia muda gani kujiadhibu wewe kama wewe kwa kutowafanyia wengine jambo la kufaa? Je! unatumia muda gani kusoma vitabu vitakatifu? Biblia ni kitabu ambacho kipo katika lugha ya kiswahili na kwa sasa mambo ni rahisi zaidi maana mpaka kwenye simu zipo Biblia. Je! unatumia muda gani kusoma vitabu vya kawaida. Paulo alikuwa ni msomaji wa vitabu, alikuwa anamwagiza Timotheo, wakati anakuja amletee koti lake bamoja vitabu vyake hasa vile vya ngozi. Je! unatumia muda gani kujisoma kwa mapito yako? Neno la Mungu linavutabu vya historia ndani yake. Je! unatumia muda gani kutafakari? Roho Mtakatifu humfundisha mtu anayetafakari. Je! unatumia muda gani kujinenea maneno ya kutaka kujifunza na kuomba Mungu akufundishe hekima yake? Vitabu vya unabii ni kwaajili ya kujinenea mambo hayo. Je! unatumia muda gani kutafakari mazingira yanayokuzunguka? Vitabu vya hekima vinafunza juu ya mambo haya, jifunze mpaka kwa sisimizi.
Mwisho wa yote Mungu ndiye Mfalme wa kila kitu, pale ambapo sisi hatuwezi basi yeye hutuvusha. Walipofika Yordani Mungu aligandisha maji, walikuwa hawezi kuvuka lakini Mungu akahusika kuwavusha. Mtumainie Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa. ASANTE.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment