JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, October 9, 2018

Ujumbe Uliobeba Ndani Yako.

 Sadick Kilasi     October 09, 2018     KUFURAHIA MAISHA, NJOZI     No comments   

Ukweli ni huu, ni kwamba, kila mtu amebeba ujumbe ndani yake. Kama tumezaliwa tukiwa tupo tofauti basi ni wazi kwamba kila mtu amebeba ujumbe wa siri ndani yake ili kuiletea dunia. Kuna watu ambao tayari wameujua ujumbe ambao wanapaswa kuipa dunia lakini kuna watu ambao bado hawajajua ni ujumbe gani ambao wanapaswa kuipatia dunia.

Hakuna mtu ambaye alizaliwa hivi hivi, kila mtu anasehemu yake ambayo anaoongoza na anapaswa kuleta ujumbe wa upekee ambao Mungu amemtuma alete duniani. Kila mtu ni barua, haijarishi unapaswa kuwafikia watu wangapi? Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anapaswa kuleta ujumbe kwa watu fulani. Haijarishi ni watu wachache kiasi gani ama ni wengi kiasi gani lakini kuna ujumbe ambao Mungu ametaka kila mtu auwasilishe duniani.

Ikiwa kama Ibrahimu  na mkewe sara walikosa matumaini hapo mwanzo, walikuwa hawana mtoto, lakini Mungu akawajalia mtoto uzeeni naye ni mmoja tu, ambaye ni Isaka. Huo ndio ujumbe ambao Mungu alimpatia Ibrahimu aulete duniani. Kwa macho ya wanadamu ni ujumbe mdogo lakini Mungu aligeuza kuwa ujumbe mkubwa sana. Mungu alifanya kizazi kikubwa sana kupitia mtu mmoja tu na leo hii maelfu ya watu humtukuza Mungu kwa sababu ya ujumbe ambao Ibrahimu aliuleta kupitia kwa mwanae Isaka. Vizazi elfu na elfu ambavyo unavisoma kwenye Biblia, kutoka Agano la Kale mpaka Agano jipya na mpaka mataifa ni kwaajili ya mtu mmoja tu ambaye ni Ibrahimu, ambaye alipata mtoto katika uzee, lakini leo kuna mamilioni ya watu ni watoto wa Ibrahimu kwa sababu ya mtu mmoja tu.

Mpendwa msomaji, upekee ambao Mungu kaweka ndani yako ni dhamani ya kipekee. Hakuna mtu ambaye anaweza kufananishwa na wewe kutokana na upekee ulionao. Haijarishi unaweza kuwafikia watu wangapi kwa ujumbe ulioubeba, Mungu ndiye anayejua siri hizi, usihesabu kwa macho ya ubinadamu ila cha msingi ni kuelewa kwamba una ujumbe ambao unapaswa kuipatia dunia. Kama kwa macho ya wanadamu Mungu alifanya mtu mmoja kwa Ibrahimu basi ndivyo hivyo hivyo hata kwako. Mungu ndiye tumaini lenye nguvu, usinung'unike mtumainie yeye tu.

Wapowatu ambao walionekana kana kwamba wao ni maskini wa kutupwa lakini leo hii wameibadilisha dunia kabisa, leo hii watu wanafurahia maisha kwa sababu yao. Walionekana hawafai kwa macho ya wanadamu lakni mbele za Mungu walikuwa ni jiwe ambalo lilikuwa linabubujisha maji tena jangwani. Kitu kimoja ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba jambo ambalo mwanadamu hudhamini mbele za Mungu huwa ni upuuzi tu.

Yakobo ambaye baadae aliitwa Israeli, kwa macho ya Isaka alionekana kana kwamba hafai kitu ukilinganisha na Esau, lakini Mungu alimwona kwa macho ya kuwa ndiye mwanzo wa uzao wa Israeli, atakaye zaa makabila kumi na mbili, na Mungu alitimiza ahadi yake.

Yusufu ambaye alikataliwa na ndugu zake, baada ya kuwambia juu ya ndoto yake, walimwuza kama mtumwa akapitia maisha magumu na mwisho akawaokoa ndugu zake kwa njaa kali bila wao wenyewe kutegemea.

Kwa macho ya wanadamu Daudi alionekana kana kwamba hafai kuwa Mfalme wa Yuda, lakini Mungu alimwona kwa jicho la tofauti kabisa.
1Samweli 16:6-7, walipofika na Samweli alimwona Eliabu, alijisemea moyoni mwake, hakika, mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu ndiye huyu aliye mbele ya Mwenyezi Mungu! Lakini Mwenyezi Mungu alimwambia, usiangalie sura yake na urefu wa kimo chache. Mimi nimemkataa kwani siangalii mambo kama wanavyoangalia binadamu wenye kufa.Binadamu huangalia uzuri wa nje, lakini mimi naangalia moyoni.
Kwa macho ya Samweli Eliabu alionekana kana kwamba anafaa mbele za Mwenyezi Mungu lakini haikuwa hivo mbele za Mungu.

Je! unamkumbuka Mordekai?  Hamani alimwambia awe anamsujudia yeye, maana Mordekai alikuwa akikaa nje ya geti na kumwangalia binti yake Esta, Hamani alikuwa akimtisha kila siku lakini Mungu aligeuza kuwa furaha baadae kwa kumwondolea mbali adui yake Hamani na kwa imani Mordekai alikataa kusujudia Hamani.

Ayubu naye, alichukuliwa  mali zake na baadae alichkuliwa mwili wake, mwili ukabaki madonda matupu lakini Mungu alikuja kugeuza hadidhi hiyo.

Haijarishi upo katika hali gani? Lakini, kama unamtumainia mwenyezi Mungu, bado kuna barua ambayo umeleta duniani. Yohana mbatizaji, alionekana hafai kitu mbele za wanadamu kwa mavazi yake ambayo alikuwa amevaa lakini Yesu alisema hakuna mtu mkubwa ambaye amezaliwa na mwanadamu kama Yohana Mbatizaji.

Yesu mwenyewe ambaye alikuwa anajilalia milimani lakini hivi leo mamilioni ya watu wamekuwa wafuasi wake.
Wapo watu wengi ambao tunaweza kujifunza kutoka kwao, ambao walionekana kana kwamba hawafai mbele ya jamii lakini tumepokea ujumbe waliouleta duniani na sisi tunafurahia maisha kwaajili yao. Lazaro ambaye alikuwa maskini wa kutupwa, mwili wake ulikuwa umejaa vidonda mtupu, akiwa anatamania kula makombo ya tajiri lakini na yeye pia mbwa walikuwa wanalamba vidonda vyake. Hii inaonyesha kwamba, usijikinai, wapo wanaokutegemea chini yako, endelea mbele.

Bartimayo kipofu, alikuwa mtu ambaye anaonekana ombaomba tu lakini ndani yake alikuwa na matumaini alipomwona Yesu alichukua hatua na kulifufua tumaini lake, akapaza sauti. Mwana wa Daudi, unirehemu, akapona. Si kwamba alikuwa ombaomba peke yake, lakini yeye alikuwa anasubiria tumaini wakati wote litimie.

Ikiwa utamtumainia Mungu aliye hai, yeye atakuonyesha ujumbe ambao umeubeba ndani yako. Usijikinai, yeye aliyekuumba anakutambua vizuri tu, anakupenda na wewe unapaswa kupokea upendo wake. Zaburi 27:14, Mtegemee Mwenyezi Mungu! Uwe na moyo, usikate tamaa! Naam, mtegemee Mwenyezi Mungu!

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ▼  October (29)
      • Maisha Yenye Maana.
      • Wapi Ulipo?
      • Sala Ya Kuomba Amani.
      • Sicho Hicho Ndugu Yangu Unachohitaji.
      • Mwili Wako Ni Zawadi Kwa Wengine.
      • Utabiri Unaonesha Kwamba Wewe Utafurahia Maisha Ka...
      • Unachohitaji Katika Maisha Yako.
      • Kutambua Dalili Za Kujiliwa Kwa Jambo Jipya.
      • Ishi Kwa Kudhamiria Jambo Jema.
      • Ubatizo Ni Nini?
      • Upekee Unagharama Yake Ya Kulipa.
      • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache,...
      • Uogope Woga unaokufanya Uwe Mwoga.
      • Jifunze Kwa Bidii Ili Uwe Huru.
      • Wakati Jama Wakati.
      • Madamu Unayo Leo Unaweza.
      • Viungo Vya Mwili Hufanya Kazi Kwa Ushilikiano.
      • Dunia Mama Haimtupi Mwenye Mwili.
      • Mwalimu Nyerere Zawadi Ya Afrika Na Dunia Kwa Ujumla.
      • Mambo Ya Kujua Na Kuepuka Ili Kudumisha Furaha Kat...
      • Unabadilisha Nguo Kila Siku, Kwanini Usibadilishe ...
      • Angalia Mbegu Unazokazana Kupanda.
      • Usikazane Kutafuta Raha Katika Maisha Bali Kazana ...
      • Ujumbe Uliobeba Ndani Yako.
      • Kila Mtu Yupo Bize Na Lugha Yake.
      • Mambo Ya Kuyatambua Katika Maisha Lakini Kuzingati...
      • Mwenyezi Mungu Ni Nani?
      • Hata Kama Umezaliwa Kwa Injili Ya Maji Na Roho Una...
      • Tujifunze Kutoka Kwa Panya Na Kuishi Maisha Yenye...
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates