Adui mkubwa wa maisha ya mtu ni woga. Na woga husababishwa na hofu, ambayo hofu ni kiashilia cha kukutaka uwe umakini.
Hofu inapatikana kwenye kitengo cha usawa (kiasi). Mtu anapokuwa mtumwa wa hofu anaitwa mwoga.
Moja ya maadui wakubwa wa mtu ni woga. Ukiachilia mbali adui mwingine ambaye huwa anasumbua watu, adui ubinafsi, woga ni mbaya sana.
Mara nyingi kitu ambacho unakiogopa huwa hakina ukweli ndani yake, yaani si sawa na vile ambavyo unaogopa. Kumbuka hofu huja ili kukupa tahathari tu.
Chochote ambacho unakiogopa ukikumbana nacho huwezi kukiogopa tena. Haijarishi ni hatari kiasi gani? Kikisha kukumba huwezi kuogopa tena.
Kwa hiyo kitu cha kuogopa katika maisha ni hofu yenyewe. Ogopa hofu isije ikakupeleka kwenye woga, lakini usiogope hofu kwani si kitu ambacho ni kweli.
Angalia ni maeneo gani ambayo yanasumbua na kukutia hofu wakati wote, harafu jiulize je! Ni kweli napaswa kuogopa? Kama ni kifo utakishinda kifo kwa kufa. Kama ndo unamwamini Kristo, ndo kabisa, umeushinda ulimwengu, maana wewe huwezi kufa tens. Kwa hiyo angalia ni kitu gani kinakufanya uwe mtumwa wa hicho.
Umeushinda ulimwengu. Wewe ni mkuu kuliko chochote kilichopo ulimwenguni.
Tawala kila kitu, tambua eneo lako.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment