JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Wednesday, October 31, 2018

Maisha Yenye Maana.

 Sadick Kilasi     October 31, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Huwezi kuzungumzia maisha, bila maeneo haya matatu kuhusika; Imani, Utayari na Matumaini.

Huwezi kuzungumzia kuishi bila ya kuwa na utayari wa kuishi matumaini kwa imani.

Maisha yetu hubebwa na leo, leo ndio siku ya kipekee ambayo ndiyo zawadi yako. Huu ndio utayari, utayari wa kufanya maamuzi sasa.

Katika maisha shida ni kuishi utayari chanya. Utayari ambao umebebwa matarajio madogo ambayo yatakupeleka katika tumaini kuu.

Kuwa na nidhamu na matarajio yako ndio jambo la muhimu sana katika maisha. Kama wewe mwenyewe huwezi kupangilia matarajio yako basi hisia zako zitapangilia matarajio yako.

Maisha yenye maana ni yale maisha yenye kupangilia kwa imani matarajio yako.

Kuna matarajio ya aina mbili; Matarajio binafsi, na matarajio juu ya wengine. Na uzuri ni kwamba ukiweza kujitarajia vizuri wewe mwenyewe pia unaweza kutarajia wengine kwa mazuri. Ndio maana kuna amri kuu mbili, Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa imani yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Mpende jilani yako, kama unavojipenda mwenyewe.

Rekebisha mtazamo wako, juu yako wewe mwenyewe. Ishi matarajio chanya, ukiwa huna fedha tegemea kupata fedha kwa sababu palipo tupu hujazwa. Kama huna furaha tarajia kupata furaha, kama wewe ni maskini tarajia kupata utajiri. Tarajia mambo mazuri yatokee juu yako. Jenga mtazamo chanya juu ya wewe kwenye kila kitu.


 Tunaishi katika mwili, mwili ambao unatufanya tuhusiane na wengine, ambao kwa hao tumepewa mwili ili tuache alama kwao watusome kwa matendo yetu.

Unatarajia nini juu ya wengine. Usipotarajia kitu kutoka kwa watu tarajia maumivu kutoka kwao.

Weka mpango juu ya wengine. Ukiweza kujihimili wewe mwenyewe binafsi basi, pia unaweza kuwahimili wengine.

Tarajia kutoa badala ya kupokea. Tarajia kuwatia faraja wengine badala ya kujionea huruma. Tumainia katika Nuru ili tumaini lako kuu litie nanga katika Kiti cha Enzi huko mbinguni kwa Mungu, Mfalme wa utukufu wote.

Maisha yenye maana ni kufurahia maisha. Maisha yenye maana ni kuwafanya waliokosa matumaini wahisi kwamba kuna matumaini mapya kupitia wewe. Maisha yenye maana ni kuacha funzo kwa wengine wajifunze kutoka kwako kwa mapito yako.

Kuwa kiwanda cha uzarishaji wa matumaini yenye nguvu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, October 29, 2018

Wapi Ulipo?

 Sadick Kilasi     October 29, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, USWAZI TRICK     No comments   


Kuna aina mbili za hema ambazo watu hujiingiza;
1. Hema ya ushindi na
2. Hema ya kushindwa.

Kuna aina mbili za kambi ambazo huwazunguka watu;

1. Kambi ya furaha na
2. Kambi ya maumivu.

Kuna aina mbili za njia ambazo huwaongoza watu;

1. Njia ya hekima na
2.Njia ya upumbavu.

Kuna aina mbili za dhamira ambazo mtu anaweza kudhamiria;

1.Dhamira yenye mwelekeo chanya na
2. Dhamira yenye mwelekeo hasi.



Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, October 28, 2018

Sala Ya Kuomba Amani.

 Sadick Kilasi     October 28, 2018     TAFAKARI NENO YA SIKU     No comments   


Ee Mungu, Mfalme wa kila kitu, uketiye katika kiti cha enzi, wewe ndiye Mfalme wa utukufu wote.

Utuoshe wana wako, kwa Yesu Kristo aliyechukua dhambi ya Ulimwengu. Yeye aliwaosha wanafunzi miguu yao ili waendelee kukua na kushiriki utukufu wako. Yeye huyu aliye kuhani wetu mkuu wa patakatifu pa mbinguni kwa mfano wa ukuhani wa Melkisedeki. Huu ni ukuhani wa haki na Amani, basi, uimimine amani yako katika mioyo yetu.

Roho wako abubujishe amani hii ndani ya mioyo yetu. Mioyoni mwetu uijaze haki yako na hekima yako. Midomo yetu, ibubujishe hekima yako iliyo katika mioyo yetu.

Lifanye tumaini letu kuu litie nanga katika patakatifu pako pa huko mbinguni. Utukufu wa huko mbinguni, umeeshe utukufu hapa duniani.

Utufundishe neno lako na kusikia sauti yako. Zitakase dhamiri zetu ili matendo yetu yajae haki yako. Lifanye neno lako takatifu kuwa matamshi yetu. Kwa kweli, mwili wetu na ububujike utukufu wako ulioko ndani yetu.

Utufanye tuwe Nuru ya ulimwengu kwa utukufu wako. Tuwalete watu kwako kwa uweza wako. Tufurahi sisi sote kwa pamoja kwa amani iliyo ndani mwetu na katikati yetu.

Zifanye shughuli zetu, zitiishwe kwa nguvu zako na uweza wako. Bariki kazi zetu. Sisi sote na mali zetu, tusimike na kutusimika kwako kwa uweza Na nguvu zako ili tusitoke katika nguvu na uwepo wako. Sisi ni wadhaifu peke yetu hatuwezi.

Wewe ni Mungu wetu nasi ni watoto wako, kwa pamoja amani tele. AMINA.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, October 27, 2018

Sicho Hicho Ndugu Yangu Unachohitaji.

 Sadick Kilasi     October 27, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   



Ukichukua andazi na kumpa mwingine yale mafutafuta na harufu nzuri ndicho kitu ambacho unahitaji. Huu ni ukweli na ndio uhalisi wenyewe.

Ukijenga nyumba kubwa, siyo nyumba hiyo ndiyo ulikuwa unahitaji. Ni sehemu ndogo tu, ambayo unaweka kitanda na si sehemu yote ya kitanda utalalia bali sehemu. Huu ndio ukweli na ndio uhalisi wenyewe.

Si chakula chote ambacho unakula ndicho unahitaji, bali ni sehemu ndogo sana ambayo hufyozwa kama mafuta ya maandazi ambayo hubaki mkononi, ambacho baadae kufanya, damu. Huu ndio ukweli halisi ambao hauwezi kupingwa.

Si kila kitu ambacho unasima ni kinakufaa, bali ni sehemu ndogo sana ambayo katika kitabu utaikumbuka. Huu ndio ukweli halisi na hauwezi kupingika.

Siyo maneno ninayoandika ndiyo unahitaji, bali ukielewa hutahitaji tena maneno yangu. Huu ndio ukweli halisi na hauwezi kupingika.

Je! Ni kitu gani ambacho unahitaji? Ni kitu gani kilicho chako?

Ni kile ambacho huna ndicho chako. Kile ambacho hujashika ndicho chako.

Chochote ambacho unacho siyo chako. Chochote ambacho umeshika na kumiliki si chako.

Aliyenacho huwa anagawa na asiye nacho huwa anapokea.

Usifikiri kijinga, kuwa kile ambacho huna ndicho huna. Lakini pia usifikiri kijinga kwamba kile ambacho unacho ndicho chako.

Tunachohitaji sisi ni uhai. Vyote vinavyopita katika mikono yetu vinatuachia alama. Mapito ya maisha yetu yametuachia alama. Alama ndio zawadi yetu.

Tunaishi sasa kwa utambuzi kwa  utambuzi, utambuzi unaotokana na makovu ya hapo nyuma. Haijarishi tulipitia katika mabaya ama mazuri, yote yaliacha kovu, kama mafuta na harufu ya andazi inayobaki katika mikono yako.

Mpendwa msomaji, kama bado mpaka leo huishi maisha ya furaha na umebahatika kusoma makala hii fupi, basi, leo hii nenda nyumbani, kajifungie mlango, peke yako, kafanye sala ya shukrani, kamshukuru Mungu kwa mapito uliyopitia na yakakuachia kovu la kumbukumbu. Mchukuru Mungu kwa kila kitu, haijarishi mapito yako yalikuwaje, mabaya ama mazuri. Lakini kwa sababu leo unatambua tifauti, hiyo ndiyo zawadi yako.

Ona wema kwenye kila jambo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Mwili Wako Ni Zawadi Kwa Wengine.

 Sadick Kilasi     October 27, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Mwili Wako Ni Zawadi Ya Wengine.

Tunaishi katika dunia ya wenye mwili, tumetoka katika hali ya kutokuwa na mwili yaani katika Ulimwengu wa Roho. Tulikuwepo kabla ya kuwepo, tumepewa mwili ili kuonekana kwa wengine kama zawadi yao.

Waebrania 10:5-7, Kwahiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo ulisema, tazama, nimekuja, [katika gombo la chuo nimeandikiwa] niyafanye mapenzi yako.

Kristo Yesu alikuja kama zawadi ya ulimwengu, alikuja kama mwanadamu wa kawaida ili kwa yeye dhambi ya ulimwengu ichukuliwe katika mwili wake. Lakini pia Yesu aliacha ukumbusho wa nano lake. Leo hii ulimwengu unasafishwa na kufanywa upya kupitia yeye. Yesu alikuja kwa ajli ya ulimwengu, na kama Yesu alikuja kwaajili ya ulimwengu basi ni wazi kwamba aliacha mfano ambao kila mwenye mwili anapaswa kuufuata.

Kama umekuwa unajihesabia haki kupitia mwili wako ni wazi kwamba unajikosea wewe mwenyewe. Wewe ni zawadi kwa wengine, wewe ni kwaajili wengine. Kazana kutoa thamani kwa wengine ili kutimiza lengo ambalo Mungu alitaka utimize.

Haijarishi upo katika hali gani? Bali kuna upekee ambao Mungu alitaka uwasilishe katika ulimwengu. Usiangalie ni kitu gani huna, bali angalia ni kitu gani unacho na ukifanye kikue. Usiangalie watu wanafanya nini bali angalia namna ambavyo unaweza kuupa ulimwengu kile ulichhonacho. Ikiwa kama utaangalia  kile ambacho huna huwezi kujikubali, ikiwa itaiga vile ambavyo wengine wanavyo, basi, mwili wako hauna maana kuwepo duniani.

1Wakorintho 14:7,  Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni vilimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na utofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

Angalia ni namna gani na sehemu gani ambayo ulimwengu unapaswa kulishwa na wewe. Ikiwa unafanya vitu ambavyo wanafanya wengine, itakuwa ni makelele sasa. Hata kama wengine hufanya jambo zuri kiasi gani? Lazima utambue kwamba hata wewe unauzuri wa kipekee. Simaanishi labda usifanye kizuri cha mwingine, hapana, bali tambua chako cha kipekee kiwe shina lako. Hata mti huwa unashina ambalo hubeba matawi makubwa na madogo.

Tumezaliwa tofauti, tuna sura tofauti, tuna sauti tofauti, na hii ndio zawadi kubwa ya ulimwengu, huo upekee wako. Ikiwa unakitu kizuri ndani yako si chako, hicho ni kwaaajili ya wengine.

Waebrania 13:10, Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.

Je mtu anaweza kujidaia kipawa chake yeye mwenyewe bila kudhihirisha kipawa hicho kwa wengine? Lazima kuwepo na wengine wanaopenda kipawa chako. Kila unachofunua nje ya ulimwengu hicho si chako.

Kazana utoe thamani kwa wengine uwape watu zawadi hiyo. Kilicho chako ni kile ambacho huna.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, October 26, 2018

Utabiri Unaonesha Kwamba Wewe Utafurahia Maisha Kama Ukinena Hivi.

 Sadick Kilasi     October 26, 2018     No comments   



Katika maisha kuna nyanja tatu, imani, maneno na matendo. Imani na Mungu, maneno kukiri kwa kinywa imani iliyonayo na matendo ni kutimiza imani yako kwa matendo.

Imani hufufua matumaini, maneno huburudisha na kutia Amani kwenye moyo wa mtu na matendo huacha alama kwa mhusika juu ya imani yake.

Utabiri unaonyesha kwamba utaishi maisha ya furaha endapo ukijitabiria maneno ya ushindi.  Wote wanao mtumainia Mungu hupokea haki ya Mungu kwa imani. Ikiwa utamwamini Mungu na kukiri kwa kutabiri kwa imani tumaini lako utapokea haki ya Mungu.

Mungu ndiye Mfalme wa vyote, Mungu huweza kibadilisha chochote kile ambacho anataka kubadilisha. Alimwambia Ezekiel atabiri kwenye bonde la mifupa.

Mifupa ilianza kujikusanya pole pole, baadae nyama na mwisho Mungu alimwambia Ezekiel kwamba natia Roho yangu kwa watu hawa ambao matumaini yao yamekufa.

Mungu tayari ametia Roho wake kwa wote wanaomwamini Yesu Kristo.  Kupitia kwa Yesu Kristo tayari Roho wa Mungu anaishi ndani mwetu.

Kinywa chako tangu sasa kinatabiri nini? Tabiri sasa. Kiri kwa kinywa chako. Tabiri jibu la matarajio yako. Burudisha moyo wako kwa kutabiri utabiri wenye mwelekeo chanya kwa kumwamini Mungu kwa imani kupitia kwa Kristo Yesu, Bwana na mokozi wetu. Tabiri hivi sasa. Ama unataka kubaki katika hema ya maumivu ya watu wasio na matumaini?

Unayo leo ndugu yangu, jitabirie maneno ya ushindi hivi sasa, mtabirie mwingine maneno ya ushindi hivi sasa, tabiri matarajio yako madogo madogo kwa kunenea mtazamo chanya, watabirie marafiki matazanio chanya kwa kile unachofanya.

Ama wewe ni mmoja wa watu ambao huwatia hofu watu? Tabiri sasa, nitabirie hata mimi. Kinywa chako ni zawadi ya mwili wako na watu wengine. Tumia kipawa cha kinywa chako kuwa ushindi katika mazingira yanayozunguka. Maneno yana nguvu, maneno hufanya uumbaji, maneno huzaa matendo, maneno huujanga moyo.

Usinene maneno ya hovyo Ndugu Yangu, haijarishi unamwbia nani, maneno hutoka na kurudi masikioni mwako na kuujenga moyo ama kuubomoa. Tabiri hivi sasa taraji lako. Nena sasa taraji lako.

Umeubwa kwa uwezo wa Mungu, umeumbwa kwa mfano wa Mungu, na pia kama unamwamini Yesu Kristo una Roho wa Mungu ndani yako.

 Tabiri hivi sasa, utabiri wako ndio maisha yako. Ukitabiri hivi sasa, matumaini yatajivuta na utaishi sasa. Kuishi maisha ya furaha ama la vinategemea utabiri wako.

Uandae moyo wako kwa kutabiri kwa kinywa chako maneno ya ushindi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Unachohitaji Katika Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     October 26, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Habari Ndugu Yangu?

Tumaini lenye mwelekeo chanya ndicho kitu ambacho kila mmoja mwenye mwili anahitaji kuwa nacho. Kila kiumbe hufikiri kuendelea mbele na kuiandaa baadae kwa imani.

Kwa wenye imani na Mungu hutumaini kupokea haki ya Mungu huku tumaini lao la
 mwisho ni kuingia katika paradiso. Imani ni kuvuta tumaini la baadae na kuishi sasa.

Watu wengi hawana furaha katika maisha yao kwa sababu meli yao haina sehemu ya kutia nanga. Meli yao yaani maisha yao hubaki kuzurura huku na huko huku wakiwa hawana tumaini lolote.  Imani ni kuwa na hakikika na mambo yatarajiwayo yasiyoonekana kwa macho. Uhakika wa mambo ya baadae ndio hufanya kila kiumbe kile chakula, kukua na mengineyo.

Kama mtu amekosa tumaini na imani, basi, amekosa maana ya maisha na hana maisha, amekufa kwa lugha nyingine. Kwa sababu kifo huwatawala watu walio hai na sio waliokufa.

Tunachohitaji sasa ni tumaini lenye mwelekeo chanya, na tuishi sasa kwa imani. Kilicho muhimu sasa imani ya kuishi matumaini. Hakuna kitu chenye thamani kubwa kama sasa, maamuzi ambayo utachukua sasa ndiyo yatafanya ulifikile lile tumaini lako kuu. Haijarishi ni tajiri ama maskini ni lazima kuwa na matumaini. Wote wenye mwili wanaishi matumaini kwa imani. Matarajio madogo madogo ambayo huyafikilia na kufanya haya ndiyo hutupeleka Mwenye tumaini kuu mwisho.

Usiishi kama mfungwa wa mtazamo hasi, bali ishi kama mfungwa wa matumaini. Usijihesabie haki mwenyewe bali jiweke chini ya uwepo wa Mungu ambaye kwa yeye utapokea haki ya imani na kukufanya uendelee kusonga mbele. Mungu alimeambia Abraham, mimi ni Ngao yako na tuzo lako. Ikiwa Mungu yeye aliyeumba mbingu na nchi amekupa leo ahadi hii ni wazi kwamba utakuwa na furaha ya kutosha na utaishi kwa imani. Na ndivyo ilivyo hata sasa, sisi tunaishi kwa imani, imani ambayo Kristo Yesu ameanzisha.  Wakati huo Abramu alikuwa ni mzee lakini bado aliamini kwamba Mungu atatimiza ahadi yake. Mungu alimwambua toka nje angalia juu, nitakujalia watoto kama nyota juu angani.

Mungu yule yule ambaye alimwahidi Abramu ndiye hata sasa, sisi tunayemtumainia kwa imani kwa njia ya Kristo Yesu, anatuambia tumutumainie yeye. Katika Zaburi ya ishirini na saba, anatuambia kwamba tutumainie kwake. Lakini katika kutoka anatuambia kwamba tusimame imara naye atatupigania. Je! Wewe umewekeza wapi tumaini lako? Meli yako imetia wapi nanga?

Kitu pekee ambacho unapaswa kuwa nacho ni kumtumainia Mwenyezi Mungu na kuishi kanuni za Mungu kwa imani. Zipokee ahadi zake kwa imani. Timiza mapenzi yake kwa imani.

Haijarishi wewe unaona kana kwamba bado, ama imani yako ndogo, hapana, kwa kadili ambavyo unawekeza imani yako kwa Mungu, ndivyo unazidi kupokea haki yake. Kwa kadili ambavyo unavaa utayari wa kusoma neno la Mungu ndivyo imani yako inakua.

Ni bora kumtumainia Mwenyezi Mungu, na kuishi maisha ya furaha kuliko kukosa tumaini na kuishi maisha ya hovyo ya kuandamwa na kifo hapa hapa  duniani.

Mtumainie Mwenyezi Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa, naam, mtumainie Mwenyezi Mungu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, October 24, 2018

Kutambua Dalili Za Kujiliwa Kwa Jambo Jipya.

 Sadick Kilasi     October 24, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Habari Ndugu yangu?

Dunia inaendeshwa kwa kanuni na mfumo maalumu unaoeleweka. Kila kitu kimepangwa katika sehemu yake. Ndio maana ukiitazama jana utaona ipo sawa tu na leo, lakini ili ufikie leo kulikuwepo na dalili za kuifikia leo. Kila kitu kipo katika mfumo wake unaoeleweka.

Asili huwa inabadilika, na kwa sababu huwa inabadilika basi niwazi kwamba kuna dalili ambazo zinaweza kukutamburisha kujiliwa kwa jambo jipya. Maisha yetu hayabaki katika hali moja bali huwa na mabadiliko, na mabadiliko ambayo huwa yanatokea huwa ndiyo yanafanya maisha yetu yawe hai ama la. Lakini japokuwa mabadiliko haya yanapotokea huupa kuhesabiwa uhai mwili.

Mabadiliko ndiyo yanatufanya tusonge mbele, licha ya kwamba yanatuweka katika hatari ya maisha yetu. Yapo mabadiliko ya aina mbalimbali katika kila eneo la kitu chochote ambacho ni hai kilichopo ndani ya dunia.

Zipo dalili za mabadiliko kwa mtu yeyote katika maisha yake. Dalili hizi huambatana na viashilia fulani. Ikiwa mtu anaamani, upo wakati ambao hufanya mtu akose amani. Zipo dalili ambazo huashilia muunganiko uliopo kati ya tukio la mwanzo na linalofuata. Hii tunaita JOINT ya maisha yako.
Luka 19:41-44, Alipokalibia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia akasema: Laiti ungelijua leo hii mambo yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako. Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukuzonga pande zote. Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako; hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa.

Kuna wakati ambao huwa ni wakati wako. Unaweza kujikuta unafanya jambo fulani bila wewe mwenyewe kujijua lakini hizi zote ni dalili. Dalili ya mchana ni asubuhi, dalili ya usiku ni jioni, dalili ya mavuno ni kukomaa kwa mazao. Kila kitu kina majira yake na kila kitu kina wakati wake. Mungu alifanya hivi kwa kila kitu.

Kama weweni muombaji wa maombi, ushawahi kujiuliza kwanini kuna wakati maombi yako yananza kwa kulalamika, ama kunung'unika, ama kwa shukrani ama kwa kuomba kitu fulani? Kila kitu kinamaana katika maisha, kila dalili inamaanisha kitu. Unapoaza kuomba kwa staili fulani inamanisha hali iliyopo ndani unaiwasilisha kwa nje. Ni vema kulitambua hili mapema li kulipa umuhimu wake na kuomba maombi yanayofanana na wakati husika.

Kumbuka, kila kitu ambacho hufanya mabadiliko inamaanisha kwamba kitu hicho kwa ndani kimebadilika na dalili za mabadiliko ya ndani huanza kuonekana nje wakati mabadiliko hajatimia.

Angalia maisha yako kwa umakini, ikisha unganika na wakati maalumu. Wakati mwingine unaweza kujiona kana kwamba wewe ni mwanafunzi wakati wewe mwenyewe husomi, hizi ni dalili ambazo zinaashili jambo fulani. Ndoto unazoota nazo huashilia mabadiliko.

Kama unavoona dunia inafanya mabadiliko ya hali ya hewa na ndivyo kila kiumbe hupitia hali hiyo. Mti hufanya mambadiliko wakati wake kwa kupukutisha majani na dalili hii huonesha jambo linalofuata kwenye mti huo. Ni muhimu sana kusoma nyakati na dalili za wakati fulani. Mabadiliko ndio uhai wa kiumbe hai lakini pia ikiwa kuna mabadiliko madogomadogo basi ni wazi kuwa lazima kuna mabadiliko ya mwisho ambayo ni makubwa zaidi ambayo haya hutegemea mabadiliko madogo madodo yaliyo ndani yake.

Naandika kitabu cha DUNIA MAMA, HAIMTUPI MWANAYE,  kwenye kitabu hichi nimefafanua kwa undani zaidi juu ya somo hili la dalili na mabadiliko. Pia nimetumia mazingira ya asili tunayoishi ili kujifunza na kuelewa kuishi maana ya maisha. Tunayo zawadi ya mazingira ya vitu, wanyama, wadudu, mimea, watu, historia za matukio, tukiunganisha hivi vyote maisha yetu hayatakosa uelewa pale tu, tutakapokuwa tayari kujifunza.

Yapo mengi katika kitabu hichi ya kujifunza na utajifunza kanuni za asili kabisa za kuishi maisha yenye maana. Wakati Yesu alipouwa anawafundisha watu alitumia mifano ya vitu vya kawaida kabisa ili kuwaelewesha.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 ama sadikila65@gmail.com.





Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, October 23, 2018

Ishi Kwa Kudhamiria Jambo Jema.

 Sadick Kilasi     October 23, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Kosa kubwa ambalo watu wengi tumekuwa tunafanya ni kuishi bila kudhamiria. Watu wengi tumekuwa tunaishi maisha yale ya amka twende. Mtu mmoja alishawahi kusema,  watu wengi wanaamka kimwili na sio kiakili.

Hili ndilo kosa kubwa wengi tumekuwa tukifanya. Wengi wetu tumekuwa tukiamka na kukurupuka tu bila kujali nini kinaendelea katika maisha yetu. Maisha haya mara nyingi yamekuwa yakikosa ubora kwa sababu ni rahisi kwa mtu kuharibiwa siku na mwingine kwa sababu hakuna kitu mtu amedhamiria kuindesha siku yake.

Mtu mmoja alisema, usipo simama na chochote, utadondoka na chochote.
Dhamiria kufanya jambo linalofaa kabla ya kufanya, dhamiria kusamehe kabla ya kukosewa, dhamiria wema kwenye kila jambo.

Yesu alisema, ikiwa mtu ametokwa na pepo, harafu, pepo ikaenda jangwani kutangatanga na sehemu za maji, hujisemea, nitarudi nyumbani kwangu, akisha kurudi na kuona nyumba imefagiliwa vizuri, huenda kuwaita pepo wengine saba walio wabaya zaidi, na mtu atakuwa na hali mbaya zaidi ya mwanzo.

Rafiki, ubongo wako isiwe sehemu ya pepo wachafu kuishi. Dhamiria kufanya mazuri, dhamiria kifanya makubwa. Njia rahisi ya kuishi maisha yenye maana ni kudhamiria.

Dhamiria kumsaidia mwingine, dhamiria kufanya kitu kikubwa. Katika kitabu cha Zaburi, neno linasema, wokovu wake u karibu na wamchao, utukufu ukae katika nchi yetu. Maisha so bahati, maisha ni ukweli.

Utapata haki endapo upi jilani na haki, chakula kitaingia mdomoni endapo umefungua mdomo. Utasamehe endapo ulidhamiria kusamehe.

Usitegemee bahati katika kuishi, bali dhamiria kila kitu. Joyce Meyer anasema, tarajia mambo mazuri yatokee. Ishi kwa kudhamiria kuishi ili usiendeshwe na kuishi.

Ishi kwa kudhamiria kwenye kila kitu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, October 22, 2018

Ubatizo Ni Nini?

 Sadick Kilasi     October 22, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

1.Ubatizo ni nini?
2.Asili yake ni nini?
3.Kwanini tubatizwe?
4.Hutusaidia nini?
5.Je! Ni ubatizo upi unaofaa?
6.Maji Na Roho vinahusianaje katika ubatizo?
Amani.

Habari za wakati huu Ndugu yangu? Natumai unaendelea vizuri kabisa. Hayo hapo juu ni maswali ambayo yameulizwa na Ndugu yetu Amani, kwahiyo nikwenda kuyajibu kwa kadili Mungu atakavyo nijalia.

Kwanza kabisa nakushukuru Amani kwa kuuliza maswali haya maana kwa kuuliza kwako wengi wanapata kuelewa. Na ni jambo zuri kwa mtu kuuliza jambo ambalo anaona hailewi nini maana ya kile ambacho kinaelezwa kila wakati. Ni maswali mzuri sana na ni ya muhimu kujua.

1.Ubatizo ni nini?
Ubatizo maana yake, kuzamisha. Kidini ni tendo la kumtia mtu maji baada ya kumwamini Yesu Kristo. Lakini maana halisi na ya kawaida ni kuzama katika jambo fulani. Unapokuwa umejivisha kwenye jambo fulani, hapo tunasema umebatizwa au umejibatiza. Unaweza kusama, kwa sasa mimi sitaitwa Sadick bali nitaitwa Antoni, hapo unakuwa umejibatiza jina jipya. Umeacha jina la kwanza na kuzamia jina la pili. Sasa kupatiza, hakupo katika jina pekee yaweza ikawa matendo fulani, yaani unaacha matendo fulani na kuingia matendo mengine. Kama umechukua hatua mwenyewe, tutasema umejibatiza na kama ni mtu kakushawishi, tunasema umebatizwa. Hii ndio maana ya ubatizo, kwa ujumla ni kutoka sehemu fulani na kuingia sehemu ngingine na kuzama kabisa. Tutazidi kuelewa kwa kadili ambavyo ninajibu maswali huko mbele.
Mathayo 3:11, Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwaajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

2. Asili yake ni nini?
Dunia imekuwa inabadilika tangu kuumbwa.  Na mabadiliko ambayo yanatokea ni kutokana na mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu kufanya mambo kinyume na Mungu. Mungu alianza kuiumba nchi kutoka katika maji, lakini dunia haikuwa sawa, ilikuwa utupu na ukiwa. Mungu akaifanya dunia kuwa sawa. Akamweka mwanadamu aitawale nchi na vyote vilivyomo ndani yake. Lakini badae Mungu baadae Mungu alimwona mwanadamu amepotoka akaangamiza dunia kwa maji hayo hayo ambayo ni mwanzo wa dunia kuummbwa, wakati wa Nuhu. Alipokuwa anaingamiza dunia hakuwa na lengo la kuifuta kabisa dunia bali lengo ni kufuta kizazi kiovu na kuingiza kizazi kipya ambacho si kiovu. Habari hizi ni kutoka kitabu cha Mwanzo 6 na kuendelea.

Lakini ile asili ya uovu bado ilikuwemo ndani ya mwanadamu, licha ya kizazi kimpya. Mungu hakuazimia kuharibu dunia kwa maji tena. Mpango mpya wa Mungu ni kuiharibu dunia kwa moto na mfano wake tayari umeshakuwepo ni Sodoma na Gomora. Lakini lazima uelewe kwamba, kila kitu ambacho kinatokea Mungu tayari alisha maliza kazi yake siku ya sita, kila kitu kipo tayari. Katika Agano la Kale watu waliishi wakiwa bado wana dhambi licha ya kwamba Mungu alifanya kizazi kipya cha Nuhu. Mungu akaazimia kwamba, kwa sababu hii, itaiharibu dunia kwa moto na mfano wake tayari umeonekana wa Sodoma na Gomora. Sisi wenyewe tunatazamia uharibifu utakao kuja kwa moto. Lakini pia Mungu ametumia maji kujenga dunia lakini pia ametumia moto huo huo kujenga dunia. Wale wote ambao wametazamia kufanya mambo mazuri wakiwa chini ya ubatizo wa maji, licha ya kwamba si wakamirifu lakini wanatazamia kufanya mambo mema, Mungu amefanya agano lililo bora zaidi ambalo ni ubatizo wa moto. Hii ndio Asili ya ubatizo.
1Petro 3:21, Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi, [siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu], kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

3. Kwanini tubatizwe?
Mwanadamu alizaliwa katika uzao wa kizazi cha dhambi baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, sasa ile asili bado inatembea nasi. Hakuna ambaye anaweza kukataa kwamba hana dhambi, asili ya ndani. Mungu alimruhu shetani amgonge kisigino mzawa wa Hawa na yeyote mwenye mwili amezaliwa katika uzao wa hawa. Ni mtu mmoja pekee ambaye hakuzaliwa na mwanadamu, Adamu, lakini pia Hawa alitoka katika mifupa ya Adamu. Kwa sababu kila mwenye mwili amezaliwa na Hawa ni lazima awe na asili ya Hawa. Hawa alipotii maneno ya shetani ilibidi awe chini ya utawala wa shetani. Lakini Mungu aliandaa mpango wa kumkomboa mwanadamu, akamwambia shetani, uzao wa mwanamke huyu atakuponda kichwa, na Huyu ndiye Yesu Kristo. Sasa ubatizo ambao  tunabatizwa ni ubatizo ambao unatutoa kutoka utawala mwingine kwenda utawala mwingine. Kama hujabatizwa inamaana utabaki katika utawala ule ule wa mwanzo. Hata kama hutendi dhambi, bado unaasili ile ya dhambi ambayo ipo ndani yako. Moyo wa mtu umejaa uovu, hakuna hata mmoja ambaye hajatenda dhambi. Ndani ya moyo hutoka, wivu, kiburi, kuabudu sanamu, uaji, kuzini, hakuna mtu ambaye hajatenda dhambi. Kuna aina kumi na mbili ambazo zipo ndani ya moyo wa mtu na ndio maana waweza kujikuta unafanya jambo ambalo hata wewe mwenyewe hukutazamia kufanya, hiyo ni asili, hutakuwa na uwezo wa kujimiriki mwenyewe, asili ndiyo itakayo kumiriki, Paulo alilalamika kwamba lile ninalo azimia ndani yangu kulifanya silifanyi, nafanya lile nisilo lipenda. Na ndiomaana unaweza kujikuta una hasira na jambo fulani harafu baadae unakuja kujutia. Kikubwa ambacho shetani anataka kutoka kwako ni wewe ukose furaha.
Mwanzo 3:15, nami naweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino.

Unapobatizwa inaondolewa ile asili ya kwanza na kuwekwa asili mpya.

4.Husaidia nini?
Kwanza kabisa lazima utambue kila mmoja anamatumaini. Licha ya matumaini madogo madogo ambayo unatarajia kufanya lipo tumaini la mwisho kabisa ambalo hili unalitumania maada ya kifo chako. Tumaini kuu. Sasa ikiwa huna matarajio yoyote inamaana upo chini ya uzao wa nyoka yaani utawala wa shetani. Na tumaini hili ambalo lipo chini ya shetani ni kuchomwa moto. Ubatizo unakuondoa katika hali hiyo, la kutoka katika tumaini la kuelekea kifo na kuelekea uhai. Ubatizo unaondoa dhambi ndani yako, kama nilivosema hapo juu, unapobatizwa unaondolewa kutoka asili ya kwanza na kuingia asili mpya. Asili mpya ni pale unapotumainia kuvishwa mwili mpya baada ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ambao ndio kwa moto.

Unapokuwa duniani ni lazima uishi ufalme wa mbinguni hapa dunia, kwa sababu ufalme wa Mungu upo ndani yako na kwa sababu unatumaini la kuingia katika ufalme wa mbinguni ni lazima ukae katika njia inayoelekea katika ufalme huu. Mbinguni kuna fuaraha na haki basi kwa sababu wewe tumaini lako ni huko ni lazima ufurahie maisha hapa duniani. Lakini pia kwa wale ambao wapo chini ya utawala wa ibilisi, watakosa furaha, furaha yao ni burudani, kutegemea vitu ili kupata furaha, bila kitu fulani hawezi kuwa na furaha, tuaimaini lao ni kilio kwa sababu analia kwanza hapa hapa duniani. Ikiwa mtu unataka kupokea jambo fulani ni lazima ukae katika mkao wa jambo hilo, ni ngumu kuingiza chakula mdomoni wakati umefunga mdomo.
1Timotheo 8:5, Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu ni tumaini la wokovu.

5.Je! ni ubatizo upi unaofaa?
Ubatizo unaofaa na usiofaa kwa kweli ubatizo ni mmoja tu, wa kumwamini Yesu. Hakuna ubatizo wa aina mbili. Kama nilivosema hapo mwanzo ubatizo ni kujizamisha katika jambo fulani. Sasa injli ya maji na Roho ndiyo ubatizo wenyewe yaani ni kama mlango wa kujizamisha kwenye tumaini jipya. Mara nyingi watu tumekuwa tunatazama kwa matendo ya nje lakini hivyo, unaweza kwenda kubatizwa kwenye maji mengi lakini ukaendelea kufanya mambo yasiyo faa, lakini pia unaweza kwenda kubatizwa katika maji machache harafu ukaendelea kufanya mambo yasiyofaa. Unapokuwa unaamini injli ya kweli hilo ndilo jambo linalofaa. Unapaswa kuamini na kutenda kile kinachofaa kutendwa.

Hakuna ubatizo wa aina mbili ni aina moja tu, ni kuamini ubatizo ambao Yesu alibatizwa. Unapoamini ndipo aunapokea haki. Hii haitegemei wewe kubatizwa, inategemea imani yako, pale ambapo unaamini unashiriki kile ambacho Yesu alifanya. Kwa imani, na ili kuonyesha kwamba kweli umeamini basi yakupasa ufanye mapenzi ya Mungu. Lakini si kumwamini Yesu peke yake, hapana bali lazima utambue na umani namna Yesu alivokuja. Kwa hiyo hakuna namna ni kuamini injili ya kweli iliyo moja tu na kupokea haki ya Mungu.Sijasema kubatizwa bali kuamini.
1Yohana 5:9, Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, ipokuwa ni yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Munu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa mana wapo watatu washuhudiao [mbinguni,, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wapo watatu washuhudiano duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukipokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zadi; kwa maana ushuda wa Mungu ndio huu amemshuhudia Mwanaye.

6.Maji na Roho vinahusianaje katika ubatizo?
Ni swali zuri sana Ndugu hili, tena sana. injili ya maji na Roho ni injili ambayo Yesu mwenyewe aliihubiri. Alimwambia Nikodema kwamba, mtu hawezi kuzaliwa upya pasipo injili yamaji na Roho. Tunaweza kusema Yesu mwenyewe aliipa jina injili hii.

Uhusiono kati ya ubatizo na injili ya maji na Roho ni ubatizo wake Yesu aliobatizwa. Inamaana hakuna ubatizo pasipo injili ya maji na Roho, na neno ubatizo linasimama kwenye eneo la ubatizo ambao Yesu alibatizwa na ubatizo ambao Yesu anawabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.

Mwanzo wa injili ni Yohana Mbatizaji, Yohana  alitokea jangwani akihubiri ili watu watubu. Yohana alikuwa anawandaa watu kukaa katika njia ya ubatizo ambao Yesu baadae alikungekuja kuwabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Unaweza kujiuliza kwanini Yohana alikuwa anawabatiza pale Yordani watu? Lengo kubwa ni kumjua Yesu, ili apate kumtwisha dhambi. Yohana alikuja kama kuhani wa wanadamu na Yesu alikuwa ni mwana-kondoo wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuwa hamjui Yesu ni nani ilibidi aanze kuwabatiza watu, na yeye aliyemtuma Yohana alimwambia yeye utakayemwona Roho anamshukia kama hua ndiye. Yohana ametokea katika uzao wa makuhani, uzao wa Haruni, kwahiyo tendo ambalo alikuwa analifanya ni tendo la kikuhani. Katika Agano la Kale ili dhambi za watu zipate kuondole ilikuwa ni lazima pawepo fahali ama kondoo wa ondoleo la dhambi lakini pia palikuwa na fahali ama mbuzi, ama mwana kondoo kwaajili ya upatanisho, hyu alikuwa anachinjwa na damu yake inakwenda kupatanishwa madhabahuni.

Tendo ambalo alikuwa analifanya Yohana alikuwa nafanya tendo la kikuhani, kama Babu zao walivyokuwa wanafanya. Sasa kwa hali hiyo ni kwamba, Yesu alikuja kama mwanakondoo ama mbuzi ambaye angechukua dhambi ya ulimwengu, Yohana mwenyewe alichuhudia kwamba , huyu ndiye mwana kondoo achukuaye dhambi ya ulimwengu. Tendo ambalo alifanya Yohana lilikuwa ni kumtwisha dhambi Yesu, sisi kubaki hatuna dhambi, kwa imani. Kama ilivyokuwa katika agano la kale, kuhani alisimama malangoni, na kuweka mikono yake juu ya fahali na kukiri dhambi, kwa imani dhambi za watu wote zilisafishwa. Watu wakuwa wabamwangalia kuhani wao alichokuwa anfanya. Hii ndio sababu ya Yesu kubatizwa katika mto Yordani lakini. Roho inamanishwa  kupokea Roho mtakatifu na kupatanishwa na Mungu. Tunapatanishwa na damu ya Yesu na kufanya agano takatifu.

Ili mtu azaliwe upya lazima aamini katika maji, ambayo ni ubatizo wa Yesu, damu, mateso yake msalabani ambayo yalitupatanisha na yeye kuwa kitu kimoja na Roho, ambao ni ufufuko wake Yesu baada ya kuteswa msalabani na sasa yupo hai anawabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.

Ndugu, nimejibu kiufupi sana, jambo la muhimu ni hili, pata kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, ili kujua zaidi na pia endeleo kusoma neno la Mungu baada ya kuamini. Tia juhudi katika kusoma. Yapo mengi ambayo atakuonyesha kipekee.

Ikiwa mtu anaaminiinjili hii atapokea haki ya Mungu, jambo la muhimu ni hili, kwenye kukiri, lazima utambue kwamba ulikuwa katika hatua fulani na unahitaji kwenda hatua nyingine. ASANTE.
Uliza lolote, upo huru.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, October 21, 2018

Upekee Unagharama Yake Ya Kulipa.

 Sadick Kilasi     October 21, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Ndiyo, lazima ulipe gharama.

Asili ni kitu ambacho hukuzwa. Na yule ambaye ameikuza asili, siku zote naye anakazana kuliinda na kuikuza. Sasa pale ambapo iinatokea mtu anakwenda tofauti na asili yake na hapo ndipo upinzani hutokea. Hapa ndipo panahitaji kulipa gharama.

Upekee ukikuzwa, ndiyo asili yenyewe. Upekee huu ndio unafanya maendeleo yawepo. Sasa inapotokea kwamba mtu anaanzisha kitu cha kipekee katika maisha lazima wapinzani wajitokeze. Watu tumekuwa tukiishi kwa mazoea sana sana. Hata yule ambaye amekuuza upekee mara nyingi kama mtu ambaye hatofautishi mambo anaweza kujikuta anadumaa kwa sababu ya kung'ang'ania eneo moja. Kumbuka, asili huwa inabadilika, asili inahitaji mabadiliko.

Lazima uwe tayari kulinda upekee wako lakini pia lazima uwe tayari kwenda na mabadiliko. Watu watakupinga, watu watakuona wewe ni hamnazo lakini hakikisha unalinda na kukua katika upekee wako.

Upekee ndio unaleta maendeleo, upekee ndio wewe mwenyewe, upekee ndio unaleta ubora. Kuwa tayari,hakikisha unasimamia ukweli, hakikisha unabadilika. Mabadiliko ni muhimu katika asili, ikiwa hakuna mabadiliko chanya basi kuna kunadondoka, mabadiliko hasi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, October 20, 2018

Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?

 Sadick Kilasi     October 20, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache.

Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule ubatizo wa maji machache. Walio katika ubatizo wa maji mengi hujiona wao wapo sahihi na walio katika ubatizo wa maji machache, hujiona na wapo sahihi. Sasa kwa hili, husababisha mgongano wa kimathehebu.

Ikiwa unanuia kuutafuta ukweli unaweza kujikuta upo katika wakati mgumu sana. Maana siku zote pakiwa na mabishano kati ya sehemu mbili ni wazi kwamba lazima kuna sehemu moja haipo sahihi, ama pande zote mbili hazijatambuana, zaweza kuwa zote zipo sahihi. Wapo watu ambao hawapendi kudanganywa, haijarishi ni mzazi anasema, lakini wao ni lazima wautafute ukweli. Watu hawa huwa wanajikuta katika wakati mgumu sana kabla hawajapata ukweli kwa sababu hawana sehemu ya kuweka mguu wao.

Najua wapo watu ambao mpaka sasa, wapo katika hali hiyo kuhusu ubatizo, hawa ndio watu ambao hawapendi kupelekwa hovyo hovyo. Ni ubatizo wa maji mengi ama ni ubatizo wa maji machache?

Warumi 3:21-31, Lakini haki ya Mungu inadhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katiika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotanguliwa kufanywa, apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kuhesabu haki yeye amwaminiye Yesu. Kuwa wapi basi kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La!Bali kwa sheria ya imani. Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, ni Mungu wa mataifa pia; kama kweli Mungu ni mmoja, atakayehesabia haki wale waliotahahiriwa katika imani, nao waliotahiriwa watahesabiwa haki kwa njia ya imani iyo hiyo.Basi, je!Twathibitisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twathibitisha sheria.

Paulo amezungumzia jinsi ya kupokea haki ya Mungu kwa imani. Yesu alifanyika haki ya Mungu, hapana mtu anayeweza kusema mimi nimebatizwa kwa maji mengi ama mimi kwa maji machache. Mungu atawahesabia haki wale waliotahiriwa  katika imani na wale wasiotahiriwa kwa njia ya imani.

Ikiwa unajihesabia haki kwa matendo yako basi niwazi kwamba bado upo katika Agano la Kale. Inashangaza kuona bado watu wanaendelea kuishi kwa mfumo wa zamani kushikilia matendo badala ya imani yao.

Abramu alihesabiwa haki kabla ya kutahiliwa kwake na ubatizo ambao tunauzungumzia hapa ni kama tohara kwa kufuata watu wa kale. Watu wengi tunafeli hapo, hebu fikiria, ikiwa wewe umemwamini Yesu mahala fulani baada ya kuhubiriwa, harafu ni mahala ambapo papo mbali na tendo la kufanyia ubatizo, kama utajihesabia haki kwa njia ya matendo yako, ikatokea unaenda kubatizwa harafu ukapata ajali kabla ya kufika eneo la kubatizia, Je! inamaana Mungu hatakuhesabia haki? Mungu atakuhesabia haki. Yule mtu ambaye aliteswa pamoja na Yesu akamkiri pale msalabani, je! kuna kuhani ama mtumishi aliyembatiza kwa maji mengi ama machache?

Hakuna mtu ambaye anaweza kupata haki kwa njia ya matendo yake. Kama watu wa zamani ili kuonyesha kwamba wao ni watu wa Mungu walitolewa govi yaani tohara inamaana kwa sasa alama ya kuzaliwa upya ni kupokea Roho Mtakatifu.Na hii ni siri kwa kila mmoja. Hakuna hata mmoja ambaye anaweza kumlingia mwingine.

Ikiwa utaenda kubatizwa kwa maji mengi ama machache, hiyo ni ishara kwa watu wanaokuzunguka lakini si mbele za Mungu maana Mungu humwangalia mtu ndani ya moyo wake.

Warumi 2:29,  bali yeye ni myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa mwanadamu bali kwa Mungu.

Lakini mtu aliyezaliwa kwa injili ya maji na Roho anajitambua, na siku zote atakusudia kutenda yaliyo haki na si kuishia kubisha tu Kutimiza mapenzi ya Mungu ndilo kusudi la mtu aliyezaliwa mara ya pili, kuhubiri injili ndilo kusudi la mtu aliyezaliwa mara ya pili.

Hakikisha unapata kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, bure kabisa ambacho ndiyo injili ya kuzaliwa upya.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, October 19, 2018

Uogope Woga unaokufanya Uwe Mwoga.

 Sadick Kilasi     October 19, 2018     No comments   


Adui mkubwa wa maisha ya mtu ni woga. Na woga husababishwa na hofu, ambayo hofu ni kiashilia cha kukutaka uwe umakini.

Hofu inapatikana kwenye kitengo cha usawa (kiasi). Mtu anapokuwa mtumwa wa hofu anaitwa mwoga.

Moja ya maadui wakubwa wa mtu ni woga.  Ukiachilia mbali adui mwingine ambaye huwa anasumbua watu, adui ubinafsi, woga ni mbaya sana.

Mara nyingi kitu ambacho unakiogopa huwa hakina ukweli ndani yake, yaani si sawa na vile ambavyo unaogopa. Kumbuka hofu huja ili kukupa tahathari tu.

Chochote ambacho unakiogopa ukikumbana nacho huwezi kukiogopa tena. Haijarishi ni hatari kiasi gani? Kikisha kukumba huwezi kuogopa tena.

Kwa hiyo kitu cha kuogopa katika maisha ni hofu yenyewe. Ogopa hofu isije ikakupeleka kwenye woga, lakini usiogope hofu kwani si kitu ambacho ni kweli.

Angalia ni maeneo gani ambayo yanasumbua na kukutia hofu wakati wote, harafu jiulize je! Ni kweli napaswa kuogopa? Kama ni kifo utakishinda kifo kwa kufa. Kama ndo unamwamini Kristo, ndo kabisa, umeushinda ulimwengu, maana wewe huwezi kufa tens. Kwa hiyo angalia ni kitu gani kinakufanya uwe mtumwa wa hicho.

Umeushinda ulimwengu. Wewe ni mkuu kuliko chochote kilichopo ulimwenguni.

Tawala kila kitu, tambua eneo lako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, October 18, 2018

Jifunze Kwa Bidii Ili Uwe Huru.

 Sadick Kilasi     October 18, 2018     No comments   



Ukiona unagombana na mtu ujue bado hujaanza kuishi uhalisia wa maisha ila upo tu katika kuishi. Kama bado unashangazwa na matukio jua bado una safari ndefu sana ya kufikia uhuru wa maisha.

Katika maisha yapo mambo mengi ambayo hutukia na ili kuyashinda ni muhimu zaidi kujifunza kwa kila tukio ambalo unapitia. Kama kwa sasa wewe ni kijana mtu mzima wa miaka ishirini na kuendelea ni wazi kwamba yapo mengi ambayo yametukia huko nyuma na inaweza ikawa zawadi yako kubwa sana ya kuishi maisha yenye maana kama utajifunza kwa yele ambayo umepitia.

Tuna mambo mengi sana ya kujifunza katika maisha, mahusiano, shughuli zetu, na mambo mengine ambayo tunapaswa kufahamu. Ili ufikie angalau kiwango cha kuweza kutatua matatizo kiurahisi, basi, utambuzi wa kutofautisha lazima uwe nao na lazima uwe na utambuzi wa kuielewa lugha.

Wengi huwa tunapuuzia katika swala la kujinza lakini swala la kujifunza ni sehenu muhimu sana kuliko jambo jingine.
Methali 4:7, Bora hekima, basi jipatie hekima; naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.

Dunia sio sehemu ambayo inauhalisia wa mambo, wakati wote kila jambo tunalolifanya ni lazima liende na mapungufu, ikiwa huna ufahamu hutaelewa hili. Ni muhimu zaidi kujifunza ni muhimu sana.

Kama wewe ni mmoja wa watu wazima sasa, unatambua kabisa, wakati mwingine unaweza ukawa unataka kuwasilisha jambo lakini watu wakawa wamelichukulia tofauti kabisa na namna ambavyo wewe ulikuwa unamaanisha. Unajikuta umeingia kwenye migogoro ambayo hukutarajia, lakini chanzo kikuu ni ukosefu wa ufahamu. Ufahamu unakupa utambuzi, utambuzi wa kutambua mazingira na lugha.

Mapito yako ni moja ya zawadi ambayo inaweza kukufanya kwa sasa ukafanya vizuri, na Mungu hutufanya tupitie katika wakati fulani na hawezi kuacha tuondoke hapo bila kuhakikisha tumeacha kovu ambalo ni ukumbusho kwetu. Wakati wana wa Israeli walipokuwa wanavuka katika joint ya mto Yordani, Mungu aliwataka wachukue mawe ya ukumbusho ili wawasimulie wanaye jambo lililo tukia hapo. Hii ndio zawadi ya mapito, mapito yanakufunza lakini usipofunzwa na mapito yako basi ni wazi mapito yako yatakuwa mapigo kwako.

Huwa ninakumbuka sana mapito ya nyuma, kwa kweli hapa ndipo ambapo siwezi kuacha kutafakari kwenye kila kitu. Nilisha wahi kuwakosea watu wengi sana kwa namna moja ama nyingine lakini leo mapito yangu ni zawadi kwangu. Naweza kufanya maamuzi sahihi kutokana na mapito yangu na makosa niliyofanya huko nyuma.

Ushawahi kujiuliza kwanini Mungu katumia gharama kubwa sana katika kutimiza neno la Mungu? Inawezekana hujawahi, lakini rafiki yangu, Mungu ametupa zawadi kubwa na yakipekee, wapo watu ambao walikufa kwenye biblia ili wewe ujifunze na uishi maisha ya maana, wapo watu ambao walipitia maisha magumu kwenye biblia ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watu walifanya mambo mabaya kwenye biblia mambo yamerekodiwa ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watu wamepigania kitabu kitakatifu ili wewe uishi maisha ya maana, wapo watawale ambao walikuwa na hekima ili wewe uishi maisha ya maana. Isitoshe, bado umepewa zawadi ya mapito yako. Roho Mtakatifu hukufundisha kila siku, mazingira ya asili ambayo unaishi nayo ni kwaajili yako, watu wanaokuzunguka waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa yote kwa sababu yako. Mungu amekupa kila kitu na mwisho bado anakwambia yeye ndio ngao yako na tuzo lako.

Ndugu yangu, tujifunze, tuvae utayari wa kujifunza kutoka kwake, haijarishi wewe ni mtu wa namna gani? Hata kama umeishia darasa la saba, wewe unafikiri watu wa zamani walikuwa wasomi? Akina Paulo watu ambao walikuwa na hekima ya kutosha na akina Sulemani, mtu mwenye hekima zaidi. Inawezekana ukanambia kwamba wao walitumiwa na Mungu, lakini kumbuka kwamba, Mungu alimaliza kazi yake siku ya saba na lazima utambue maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, ukiuandaa moyo kwa kusudi la kupokea haki ya Mungu utapokea haki yake.

Leo hii changamoto nyingi hasa za migogoro ni kwa sababu ya kutokujifunza. Utambuzi na ufahamu ni kwaajili ya kushi maisha yenye maana. Tusitembee kama vipofu, tutajikuta tunafanya mambo yasiyofaa kwa sababu hatuna utayari wa kujifunza.

Mathayo 11:25-30,Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Namshukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Asema, nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Njoni kwangu, nyinyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu mkajifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Ikiwa Yesu anamshukuru Mungu kwa sababu yeye amekabidhiwa kila kitu, basi nasi pia tunamshukuru Mungu kwani nasi ni ndugu wa Yesu kwa imani na pia amesema tujifunze kwake, tuvae nira yake tuwe kama yeye, ndipo tutapumzishwa. Na kuvaa nira yake inakupasa kujifunza, unajifunza kupitia neno lake  na kila kitu. Lakini yeye anasema yeye ni mpole na mnyenyekevu, kwa hiyo tunapaswa kuwa wanyenyekevu na wapole wakati tunajifunza.

Je! unataka kuishi maisha ya kustuka kila siku, mtu aliye  kama kipofu? Maana jibu la wakati ujao limefichwa ndani ya wakati. Lazima utambue kwamba Mungu anakupenda, kaa chini tafakari fikiri, acha kulaumu kila jambo. Ili watu wa dunia hii tufikie uhuru ni pale kila mmoja wetu atafikia kiwango cha kujitambua kipekee na ndipo hata kuwepo mtu wa kumlaumu mwingine. Watoto wanao zaliwa ni rahisi kuwasamehe kwa sababu hawatambui kitu lakini kwa mtu mzima akikuuzi ni lazima mgongano uwepo kwa sababu tunatambua kwa watu wazima wanajitambua. Lakini kwa sababu hata watu wazima hawana utayari wa kujinza changamoto inabaki pale pale. Lakini kama umejifunza ni rahisi kusamehe wengine.

Je! unatumia muda gani kujiadhibu wewe kama wewe kwa kutowafanyia wengine jambo la kufaa? Je! unatumia muda gani kusoma vitabu vitakatifu? Biblia ni kitabu ambacho kipo katika lugha ya kiswahili na kwa sasa mambo ni rahisi zaidi maana mpaka kwenye simu zipo Biblia. Je! unatumia muda gani kusoma vitabu vya kawaida. Paulo alikuwa ni msomaji wa vitabu, alikuwa anamwagiza Timotheo, wakati anakuja amletee koti lake bamoja vitabu vyake hasa vile vya ngozi. Je! unatumia muda gani kujisoma kwa mapito yako? Neno la Mungu linavutabu vya historia ndani yake. Je! unatumia muda gani kutafakari? Roho Mtakatifu humfundisha mtu anayetafakari. Je! unatumia muda gani kujinenea maneno ya kutaka kujifunza na kuomba Mungu akufundishe hekima yake? Vitabu vya unabii ni kwaajili ya kujinenea mambo hayo. Je! unatumia muda gani kutafakari mazingira yanayokuzunguka? Vitabu vya hekima vinafunza juu ya mambo haya, jifunze mpaka kwa sisimizi.

Mwisho wa yote Mungu ndiye Mfalme wa kila kitu, pale ambapo sisi hatuwezi basi yeye hutuvusha. Walipofika Yordani Mungu aligandisha maji, walikuwa hawezi kuvuka lakini Mungu akahusika kuwavusha. Mtumainie Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa. ASANTE.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, October 16, 2018

Wakati Jama Wakati.

 Sadick Kilasi     October 16, 2018     NJOZI     No comments   



1.Muda jamani wakati,
Na tulinde wakati,
Nafasi nayo wakati,
Tusipoteze wakati,
Hali nayo ni wakati,
Na tufanye kwa wakati,
Wakati jama wakati,
Hakuna tena wakati.

2.Na tufanye kwa wakati,
Sababu tuna wakati,
Na utafika wakati,
Kukosa tena wakati,
Tusipo linda wakati,
Wa kifanya kwa wakati,
Wakati jama wakati,
Hakuna tena wakati.

3.Sekunde nayo wakati,
Inakwenda kwa wakati,
Dakika nayo wakati,
Inagonga kwa wakati,
Lisaa nalo wakati,
Linaisha kwa wakati,
Wakati jama wakati,
Hakuna tena wakati.

4.Saba nne kwa wakati,
Si kwenda nao wakati,
Na ukafika wakati,
Nikaukosa wakati,
Wa kufanya kwa wakati,
Nikafeli kwa wakati,
Wakati jama wakati,
Hakuna tena wakati.

5.Me naenda na wakati,
Sina tena na wakati,
Nimeishiwa wakati,
Na siandiki wakati,
Kwa heri tena wakati,
Nimekwenda kwa wakati,
Wakati jama wakati,
Hakuna tena wakati.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Madamu Unayo Leo Unaweza.

 Sadick Kilasi     October 16, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Habari Ndugu yangu?

Hongera kwa siku hii ya leo, siku ambayo ni ya kipekee katika maisha yako. Hongera sana Ndugu yangu kwa kuingia katika siku hii ya leo.

Maadamu unayo leo unawezakugeuza historia yako katika maisha kwa kufanya maamuzi tofauti kabisa namna ambavyo umezoea kufanya. Madamu unayo leo unalotumaini la kuishi maisha ya furaha.

Inawezekana umezoea kulaumu watu na kuwatwisha mizigo watu lakini maadamu unayo leo, acha kuwalaumu wengine katika maisha yako na jipe wakati wa kufikiri namna gani unaweza kujijenga na kuwa msaada kwa jamii.

Inawezekana hujawahi kufikilia kuwa unaweza kuwa msaada kwa mtu mwingine, kwa sababu ya umaskini ulionao unafikiri kwamba huwezi kuwa msaada kwa wengine lakini maadamu unayo leo nenda katmie kipawa chako cha mdomo ama chochote kile ulichonacho kumfanya mwingine ambaye ni maskini zaidi yako ajihisi kwamba bado anamatumaini.

Inawezekana kwamba unafikiri wewe ni mtu ambaye jamii inakuchukulia kama ni mtu mlevi, ni mtu ambaye huwezi kuwa msaada kwenye jamii lakini maadamu unayo leo tubu kwa kuacha huo uraibu wa hicho unachokifanya kila siku, tabiri kwa kinywa chako kwa utaishi maisha ya ushindi na huta kuwa mzigo kwa jamii bali utakuwa msaada kwa jamii, Yesu yupo kwaajili yako.

Maadamu unayo leo hata kama jana ilikuwa siyo siku yako ya furaha, leo, ndiyo siku ambayo unaweza kuishi kwa furaha pale tu unatakapo amua kuishi hivo.

Inawezekana kuna changamoto ambayo inaendelea katika maisha yako, madeni na kila aina ya usumbufu na unafikiri kabisa kwamba huna nafasi ya kuondoa hiyo mizigo lakini maadamu unayo leo bado unamatumaini. Leo hii inaweza kubadilisha historia ya kesho tarajia kitu kizuri kikutokee.

Unayo leo, Mungu uponaye leo, leo ndiyo ya kwako, ishi maisha ya ushindi kwa kuikubali leo. Hakuna kinachokuzuia ktokufurahia maisha yako leo, usisumbuke kwa ajili ya kesho, ipe thamani leo, lipa gharama inayopaswa kulipwa leo ili kesho uende hatua inayofuata.

Ipe dhamani siku ya leo maana kila kitu kimefichwa ndani ya wakati. Ulipo upo, tunza sana pale ulipo, thamani ya wewe ni pale ulipo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, October 15, 2018

Viungo Vya Mwili Hufanya Kazi Kwa Ushilikiano.

 Sadick Kilasi     October 15, 2018     KUFURAHIA MAISHA, NJOZI     No comments   

Udhaifu Ndiyo Nguvu Yako.

Vipi kama mwili wote ungekuwa umejaa mfupa mmoja? Je! mwili ungekuwa unaushirikiano? Mwili umejitenga kwa mfumo wa viungo, lakini na maisha nayo yamejitenga kwa mfumo wa viungo. Kubali ukatae, maisha lazima yawe na kiungo na kama hayana kiungo basi hayana ubora ndani yake.

Viungo vya mwili, sehemu ambazo huonyesha kana kwamba ndizo sehemu dhaifu yaani sehemu za jointi, hizo ndizo sehemu ambazo huleta nguvu katika mwili. Na vivyo hivyo katika maisha, sehemu ya changamoto ambayo unaona ni sehemu kana kwamba ni sehemu ya mateso, hiyo ndiyo jointi ambayo inaunganisha  maisha yako kukupeleka katika mafanikio makubwa zaidi.

Ndugu yangu, nyosha mkono wako, harafu jaribu kuukunjakunja, harafu nyosha tena, kaza mkono, kunja ngumi, fanya hivi wakati unasoma hapa. Ndugu yangu, kwa mafano huu mdogo, unaona namna gani ambavyo sehemu dhaifu za jointi zinavofanya mwili uwe na ushirikiano na kuzaa nguvu ya ajabu.

Mapito yako mabaya ndiyo sehemu ya ushindi wako,  mapito  ambayo unahisi yalikuumiza na yanakuumiza kwa sasa, ndiyo sehemu pekee ambayo inakupeleka katika ushindi. Usipopitia ugumu wa maisha utasimlia nini? utajifunza nini juu ya utofauti? Jointi ambayo inakuunganisha wewe na mafanikio ni sehemu zile ambazo unahisi ndiyo sehemu za maumivu.

Usibaki hapo ulipo, ulizaliwa usogee, kama unakua, basi, kua katika kila eneo la maisha yako.

Angalia vidole vyako namna vinavyofanya ushilikiano, angalia miguu yako inavotembea sehemu za jointi ambazo ni sehemu zinazounganisha viungo na viungo, ni sehemu ambazo hazina mfupa lakini ndizo sehemu ambazo zinaunganisha na kusapoti nguvu kati ya kiungo na kiungo. Nakuambia kitu ambacho mwenyewe unacho na ndiomaana nilikwambia dunia haimtupi mwenye mwili, huyo ni mtoto wake. Jifunze kutokana na mwili wako, jiangalie namna mwili ulivotengenezwa.

Fikiria namna gani ambavyo Mungu kakufanya. Husianisha akili yako na matendo yako, chukua hatua. Fikiri namna gani ulivyo jiniasi. Ukitaka kujua wewe ni kiasi gani ni mwenye nguvu na mwenye kasi katika matendo, fikiria unapoungua namna gani akili yako inaweza kujiunganisha na matendo yako. Hivi vyote vinawezekana katika maisha. Mungu aliyefanya mbingu na nchi, wakati wote anasema ombeni nanyi mtapewa.

Ndugu yangu, Paulo anasema usilegee, kaza viuongo vyako, na mimi nasema silegei, nitakaza viungo vyangu, nitahubiri injili, silegei. Wewe ndugu yangu unasemaje?

Angalia namna ambavyo muwa huwa mtamu, lakini kuna kiungo ambacho ni kidogo ambacho hutofautisha utamu na utamu, na hivyo ndivyo maisha yalivyo. Ukiwa upepitia magumu sana utashinda sana. Ukienda safari ya mbali, utarudi kutoka safari ya mbali, ukienda safari ya karibu, utarudi kutoka safari ya karibu. Yesu alisema, mwenye kingi huongezewa.

Haijarishi upo chini kiasi gani? Haijarishi nipo chini kiasi gani? Nikiwa chini sana nahitaji kupanda sana. Mapito yako magumu ndiyo nguvu yako, endapo tu, utajifunza kuona wema kwenye kila jambo, utaishi kwa shukrani kwenye kila eneo la maisha yako. Na hapo ndipo unapotakiwa kujifunza.

Jifunze kutoka kwenye neno la Mungu, ndipo utaelewa mazingira ya maisha unayoishi. Mtegemee Mwenyezi Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa, naam, mtegemee Mwenyezi Mungu. Zaburi 27:14.

Maisha ni zawadi ya pekee, tupo duniani tunapita, tunaangalia tumaini letu kuu, la mwisho kabisa ni kuingia Ufalme wa Mungu. Wana wa Israeli walikuwa wanalalamika wakaishia kugongwa na nyoka. Hatulegei, maana tunazidi kuimarika siku baada ya siku, siku baada ya siku. Mungu ndiye ngao yetu na tuzo letu. Tumia uzaifu wako, kukupeleka katika ushindi. ASANTE Mungu awe nawe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, October 14, 2018

Dunia Mama Haimtupi Mwenye Mwili.

 Sadick Kilasi     October 14, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Dunia Mama Haimtupi Mwenye Mwili.

Tupo duniani na dunia ndiyo Mama yetu ambaye anatutunza. Mungu aliifanya dunia ili itutunze na kamwe dunia haiwezi kumtupa mwenye mwili. Ardhi ya dunia hii na vitu vya asili yake, siku zote za maisha havibadiliki hata binadamu ajaribu kubadilika vipi, mambo yapo vile vile. Dunia Mama haimtupi mwenye mwili, ndio unaweza kusema kwani, jinsi Mungu alivyoiumba dunia ilikuwa ni kwaajili ya kumsaidia mwanadamu.

Mazingira ya dunia yatabaki vile vile hata kama ukiyasaliti bado, asili ile itabaki vile vile na inakusubiri wewe ufikiri kwa njia ya shukrani ili upate yaliyo mema ya dunia. Miti, mito, wanyama, wadudu na kila aina ya viumbe hai na visivyo hai ni zawadi kwa yeyote mwenye mwili hapa duniani.

Unaweza kuichukia dunia, unaweza kuanza kutangatanga kama Kaini lakini bado utakuwa ndani ya dunia na dunia inakusubiri utubu tu wewe mwenyewe kwa kukubali kwamba upo duniani na zipo kanuni za dunia ambazo unapaswa kufuaata. Unaweza usikubali mazingira unayoishi kwa kutazama mbele tu, usiweze kutazama chini ya miguu yako ulipokanyaga ili kuona vizuli ni kitu gani kilichokuzunguka, uone namna mama dunia anavokujali na kukupenda.

Mama yetu dunia yupo vilevile, lakini mwanadamu hurusha macho mbali sana na asikubali pale alipokanyaga kwamba panamlinda na pana fursa za kufanya kila kitu ambacho anataka kufanya. Ukitazama mbali unaweza kuona kule mbali ni bora kuliko ulipo lakini ukweli ni kwamba dunia ni ileile tu, ukikufikia unaotazama unaweza usikubali pia.

 Dunia haimtupi mwenye mwili, mazingira ambayo yalikuwa yameandaliwa yalikuwa ni kwa sababu ya mwenye mwili. Kila maeneo yana asili kutokana na mwenye mwili wa eneo hilo, ukienda jagwani, utakuta michanga mitupu basi, wanaoishi huko ni watu wa asili ya huko na wenye kumdu asili ya huko. Ukienda majini, utakuta samaki na wadudu wa majini, basi, nao huishi kutokana na asili ya majini. Mbugani ni kwaajili ya wanyama wa mbugani, nyumbani ni kwaajili ya wanyama wa nyumbani. Hivi ndivyo tunavyoishi dunia mama yetu wenye mwili anatulea namna hiyo. Hakuna mwenye mwili anayetupwa, hakuna mwenye mwili anayekataliwa, wenye mwili wote huishi kufuatana na asili yake.

Mwanadamu mwenye mwili amepewa anazawadi zaidi ya wenye mwili wengine na zawadi yenyewe ni kufikiri zaidi ya wenye mwili wengine. Sio kwamba wenye mwili wengine hawafikiri, wanafikiri sana na ndiomaana wanaweza kuhendo mazingira wanayoishi, lakini mwanadamu amepewa ufikiri zaidi ya wengine yaani amezidishiwa ubunifu. Hii ni zawadi kubwa sana kwa mwanadamu kati ya wenye mwili, anaweza kuhendo mazingira yeyote yale anayoishi kwa sababu ya utambuzi wa kufikiri.

Hii ni zawadi kwa mwanadamu kwani anaweza kuelewa mazingira anayoishi, Paulo alisema, mimi nafurahia kila mazingira ninayopitia kwa naelewa kila jambo, liwe gumu ama la. Natambua kupitia magumu na wakati mzuri. Hivi ndivyo maisha yanakuwa yenye maana kwa kila mwanadamu. Unapokuwa unatafakari mazingira uliyopo na kuyaelewa inakuwa ni rahisi kuishi kwa utambuzi wa kueleweka.

Kwa Mwanadamu kila kitu ni zawadi yake, anaweza kuangalia kitu chochote kile na kutengeneza chochote anachotaka. Usishangazwe kuona kwamba, taa iliigwa mfano wa mwezi, gari iliigwa mfano wa ng'ombe na mengine mengi sana. Hivi ndivyo tunasema, dunia haimtupi mwenye mwili.

Unaweza ukafikiri huna pa kuanzia lakini ukikubali mazingira yanayokuzunguka ni wazi kwamba utaona kila jambo ambalo linakuzunguka ni la kwako wewe, yaani hiyo ni zawadi yako. Watu mimea, ardhi, wadudu, ndege  na kila aina ya kinachokuzunguka. Tulipewa amri ya kwenda kutawala viru vyote vya dunia na si kumiliki. Kwa sababu hiyo, kama kila kitu tunaweza kukitambua basi, ni wazi kwamba tunaweza kufanya jambo lingine linalofanana na lile jambo bila kuadhiliwa na lile jambo uliloliiga. Ukimiriki kitu unajipunguzia vya kutawala na ukimiriki kitu unakuwa chini ya hicho kitu lakini ukitawala vitu vyote vinakuwa chini yako.

Popote pale ulipo, umezungukwa na mazingira, unaweza ukafanya jambo lolote ambalo litakupatia faida na kuendelea kufurahia mazingira uliyopo na kuwa mmoja wa mtumiaji mzuri wa mazingira. Tazama mazingira uliyopo harafu fikiria kishukrani, ona namna ambavyo umepewa na Mungu kila kitu ambacho kitakufanya uendelee mbele.

Dunia Mama haimtupi mwenye mwili, usiikatae dunia, dunia haiwezi kukusikia kwa sababu unaenda nje ya asili yake na siku ukifa kwa sababu hutakkuwa na uwezo wa kuikataa itakupokea kama mtoto wake na kukuhifadhi chini ya ardhi. Anza kukubari mazingira unayoishi, anza kuona wema kwenye kila jambo katika mazingira unayoishi, usikubali kuwa mkimbizi kama Kaini mwenye tamaa, kubali kila jambo na mrudishie shukrani Mwenyezi Mungu maana yeye ndiye Muumba wa kila kitu.

Ukawe na siku bora ukimrudishia shukrani Mungu kwenye kila jambo, jifunze kwenye kila jambo harafu uone namna siku ya leo itakavyokuwa siku bora kuwahi kutokea, wewe shukuru kweny kila jambo, chochote ambacho utakishika rudisha shukrani kwa Mungu haijarishi ni kitu gani na ni kidogo kiasi gani. Utaona mabadiliko ndani yako, utaona ufikiri wa tofauti. Harafu siri nyingine ya kumwomba Mungu jambo unalolitaka ni kukubali kwanza vitu ambavyo tayari amekwisha kupatia.
ASANTE.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Mwalimu Nyerere Zawadi Ya Afrika Na Dunia Kwa Ujumla.

 Sadick Kilasi     October 14, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   

Tafakari, Nyerere Day.

Mimi ni kijana wa miaka 25 tu, sina ufahamu wa siasa wala sijamfahamu Nyerere kwa undani zaidi. Sijabahatika kusoma vitabu vya Mwalimu Nyerere kwa sababu vitabu vyake vingi vimeandikwa kwa lugha ya kingereza. Ila nimebahatika kuangalia hotuba zake mtandaoni na kusikiliza redioni, Mwalimu alikuwa ni mtu wa kipee sana.

Mwalimu alikuwa mwanasiasa lakini mtu yeyote yule ambaye atasikiliza maneno yake atajifunza kitu kikubwa sana na kuishi maisha ya maana sana. Mwalimu alitumia kipawa chake vizuri kuhakikisha analijenga Taifa na Afrika kwa ujumla. Napenda kuingia mtandaoni na kuangalia hotuba zake mara kwa mara na nimekuwa namwelewa kuwa Mwalimu alikuwa na Elimu ya upendo yenye ujazo.

Mwalimu ni zawadi kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa sio mtu wa kujali makundi ya watu bali yeye alijali utu kwa ujumla. Ukisikiliza hotuba zake, alianza kwa kuunganisha makabila ya Tanganyika, Tanganyika na Zanziber na mpango wake endelevu ulikuwa ni kuunganisha Uganda, Kenya na Tanzania kuwa nchi moja. Sasa kwa mfumo huu unaweza kuelewa kwamba angelikuwa bado anaishi angefanya Afrika kuwa nchi moja na asingeishia hapo, angefanya hata dunia kwa ujumla kuwa nchi moja. Mwalimu alikuwa ni mtu wa utu,Mwalimu hakujali makundi japo alitambua uwepo wa makundi.

Unaweza kujifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa Mwalimu, hata kama wewe sio mwanasiasa kwani Elimu yake ilikuwa katika mfumo wa upendo. Mwalimu alipinga sana mambo ya udini, ukabila, rushwa, pesa halamu na mengine mengi maovu. Sasa haya yote ni maadui ya upendo, kwani huwa yanasababisha mtengano wa watu.

Mwalimu pia alikuwa mhamasishaji mzuri sana. Moja kati ya hotuba ambazo huwa napenda kusikiliza ni ya watu kugeuka kuwa mawe. [SIKILIZA HOTUBA YAKE HAPA]. Hii ni moja ya hotuba ambazo zinatia hamasa sana katika kuyafikia matumaini ambayo umejiwekea.

Ni ukweli usiopingika, Watanzania tulipata zawadi ambayo ni Mwalimu. Kwa lugha ya kiswahili alitufanya tuishi kwa pamoja kwa undugu, na ndiomaana amani Tanzania ipo kwa sababu watu wote tumeungana kwa lugha moja ambayo ni kiswahili. Watanzania huishi kama ndugu, na hata kama kuna mambo ya chini kwa chini lakini kwa ujumla sisi tunajihesabia kama ni ndugu wa umoja.

Wale wote ambao wapo tayari kujifunza kutoka kwa Mwalimu Nyerere , basi, Mwalimu ni zawadi yao kwani elimu yake ilikuwa haina mipaka, mtu yeyote anaweza kujifunza kitu na kuishi maisha ya maana. Hata kama unaishi nchi gani unaweza kujifunza elimu ya Mwalimu na kufaidi kitu kutoka kwake.Watanzania, kuna sababu ya kumenzi Mwalimu, tujifunze kitu kutoka kwake na tufikiri kama yeye.

Umoja, amani, kuondoa umaskini ni mambo ambayo alikuwa anayapigania sana Mwalimu, basi na tuvae utayari wake kwa kuenzi kazi zake.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, October 12, 2018

Mambo Ya Kujua Na Kuepuka Ili Kudumisha Furaha Katika Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     October 12, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Habari Ndugu yangu?

Kuwa na furaha katika maisha ni kitu kingine na kudumisha furaha uliyonayo ni kitu kingine kabisa. Furaha ambayo naiongelea hapa sio furaha ambayo watu wengi huitafsiri kama furaha, naizungumzia furaha ya kudumu, ambayo mwanzo wake ni amani ya moyo.

Furaha hii ambayo ni ya kweli na halisi huwa inategemea utambuzi na haitegemei kufurahishwa. Kwa mtu mwenye furaha ya kweli sio jambo gumu kwake kutabasamu akiwa peke yake. Mtu huyu huwa hategemei kile ambacho kinaingia kwake bali anategemea kile ambacho anakitoa ndani yake.

Ikiwa huna furaha ya kweli bado hujachelewa, kama upo hai bado una fursa ya kufurahia maisha. Kama bado hujaanza kufurahia maisha jambo la kwanza kulielewa ni hili, Mungu ndiye mwanzo wa mambo yote na unapaswa kupokea kile kitu ambacho anakupatia. Itambue injili ya maji na Roho na hiyo ndiyo funguo ya furaha katika maisha.

SOMA:INJILI YA MAJI NAROHO.

Sasa furaha na amani ndiyo humfanya mtu awe na amani na afanye shughuri zake kwa usahihi bila bughudhi yoyote. Furaha ndiyo nguvu ya kuendelea kufanya lile ambalo unalifanya. Sasa baada ya kupata funguo ya furaha, kuna haja ya sisi kuendelea kuilinda furaha tulionayo. Dunia ambayo tunaishi si makao yetu bali tunapita kwa muda tu kwahiyo unachokipata unapaswa kukilinda kwani hatujaufikia ukamirifu bado kwa hapa tunaishi matumaini yaani furaha ya mbinguni tunaiishi hapa duniani.

Zipo tabia ambazo mhusika ambaye anataka kuwa na furaha ya kudumu anapaswa kuwa nazo. Tabia hizi unapaswa kuishi, furaha itakuja yenyewe bila kusababishwa na kitu chochote kwani Mungu ndiye atakujaza furaha hii.

Kwanza kitu cha kwanza unapwa kuondoa kuabudu miungu mingine. Na kuabudu miungu mingine simaanishi kwamba utaenda kuipigia magoti ama kusujudu, hapana, namaanisha kibanzi ambacho kipo ndani yako. Je! ushawahi kujikuta kana kwamba kwenye dhamiri yako kama kumewekwa kitu ama kunasishwa kitu namna hii, harafu kichwa huwa kinakuwa kizito sana. Kwa hiyo unapaswa kuondoa hicho kitu ambacho kipo ndani yako, wewe ni hekalu takatifu la Mungu.

Kitu hiki husababisha uchungu sana kwa mtu, kuhukumu wengine huleta jambo hili, tamaa ya jambo fulani huleta jambo hili, hofu kubwa huleta jambo hili, kung"ong'a mtu kwa siri huleta jambo hili, na tabia nyingine ambazo hazizingatii kiasi na Elimu ya kiungu.

Hakikisha dhamiri yako inakuwa tupu kabisa, hata kama ulikuwa unafanya jambo zuri sana, kwa mfano; kama ulikuwa unasoma kitu hakikisha unaelewa tu na neno hilo lijazwe ndani mwako siyo kukairiri. Ubongo wako unapaswa kuwa tupu, achilia kila jambo linalokuja. Wewe ni hehalu la Mungu kwa hiyo unaposhikilia kitu fulani unaondoa uwepo wa Mungu ndani yako.

Hii ni amri kuu katika neno la Mungu, Kumbukumbu La Torati, 6:5, Nawe mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Hii ni amri kuu katika amri zote, lakini Mungu anakwambia kwamba ondoa kila kitu ndani yako. Kumbukumbu La Torati 7:25-26, Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni chukizo kwa Bwana, Mungu wako; na chukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kirichoharimishwa.

Jambo la muhimu kufahamu katika hili ni kwamba, usiingize vitu vya mwilini na kuviweka ndani ya dhamiri yako. Hakikisha ndani ya dhamiri yako mnakuwa tupu, usihifadhi tumaini lako ambalo ni kubwa kwa kujiuliza itakuwajekuwaje? Jambo la muhimu kwako ni kutambua na kuanza kufanyia kazi yako, tekeleza sasa kwa mwili baada ya dhamiri yako kufika kiroho.

Uwepo. Hii ni changamoto kwa watu wengi kutnza uwepo, yaani mtu kimwili anakuwepo lakini kifikra anatoka na kwenda mbali sana. Usikubali kuingiliwa na jambo lolote katika shughuri zako.
Kumbukumbu La Torati, 12:27, nawe zisogeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya Bwana, Mungu wako; na damu ya dhabahu zako uimwage juu juu ya madhabahuya Bwana, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake.
Kwa hiyo unapofanya shughuri zako hakikisha unatunza uwepo wako, yaani unajitoa mzimamzima kwa kila kitu. Hii itatunza umilele wako na utajiona mkamirifu yaani hakuna kipande cha wewe ambacho kitakuwa kimetoka kwako ni kama vile kufanya tahajudi. Wanao fanya tahajudi hulifahamu hili.

Luka 11:34, Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote nao unakuwa mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao unakuwa giza.

Sasa ukiona kuna kitu ambacho kimenasa ndani yako, yaani kwenye dhamiri yako, hapa ndipo ambapo unamhitaji Kristo, asafishe dhamiri yako. Wakati wana wa Israeli walipokuwa wananung'unika jangwani Mungu aliachilia nyoka wenye sumu kali wakawauma na kuwauwa lakini maadae walipoona wanakufa wakamwambia Musa, tumetenda dhambi, Musa akamwomba Mungu, Mungu akamwambia Musa atengeneze sanamu ya nyoka ambaye kila mtu atakayetazama atapona. Hivi sasa ameinuliwa Yesu katika msalaba. Nilizungumzia hili kwa undani katika makala hii;

SOMA: HATA KAMA UMEZALIWA UPYA.

Lakini pia usiendekeze tabia ya kuwategemea watu, kwa sababu ukiwategemea watu lazima utaumizwa nao ni hilo ni jambo amekataa kabisa. Maana kuna watu wengi saizi hujisemea wenyewe kwamba bila mtumishi fulani mimi haiwezekani, mpendwa, wewe ni wewe na yeye ni yeye, jifunze tu kwa watu ila tambua hata watu wanakitu cha kujifunza kutoka kwako.

Makala hizi kwa watu ambao wapo makini ni makala za uponyaji kabisa. Amri zozote ambazo Mungu alitoa ni kwaajili yako, inakuhitaji utafakari kwa umakini na kuhakikisha unaelewa uhalisi wake ni nini, ni kitu gani ambacho Mungu alikuwa anakilenga kitu gani. Hata kama jambo unalifahamu jitaidi sana lile neno lisipite kwako bali liwe ndani mwako, kwenye moyo wako. Watu wengi huwa hatufahamu hili kwamba, ukitaja jina Sadick, ndani yake kabeba mambo mengi ambayo unapaswa kuyajua. Mungu amesema, mpende jilani yako kama unavojipenda mwenyewe. Kwa kawaida amri hii inaweza ikawa kama rahisi kuelewa lakini inahitaji utafakari wa ndani zaidi.

Ombo langu Ngudu yangu, makala hizi hakikisha unawasambazia watu wengi zaidi. Ni makala za uponyaji kuanzia kiroho mpaka kimwili. Hata wewe mwenyewe kwenye milango ambayo nimetaja ya Biblia hakikisha unajipa muda kusoma zaidi, mlango mzima kwenye mstari ambao nimetaja. Nakusihi Ndugu yangu, itafakari milango hiyo. Asante.

Sadick Kilasi wa jiolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Unabadilisha Nguo Kila Siku, Kwanini Usibadilishe Ufikiri Wako.

 Sadick Kilasi     October 12, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, NJOZI, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Unabadilisha Nguo Kila Siku, Kwanini Usibadili Na Ufikiri Wako?

Maisha yana kanuni zake, tukiwa hapa duniani tunaendeshwa na kanuni za miili. Tunaishi ulimwengu wa miili, kwa hiyo ni lazima tufuate kanuni za miili.

Kila siku huwa tunabadilisha nguo, hivi, rafiki yangu ushawahi kujiuliza kwanini tunabadilisha nguo? Tendo la kawaida kama unaishi kwa mazoea lakini kama unaishi maisha yenye maana utajiuliza kwanini nabadilisha nguo? Hivi ndivyo maisha jinsi yalivyo, ikiwa utakuwa tayari kuelewa katika kila jambo unalofanya utaelewa kwanini unafanya. Inawezekana ukasema mimi hubadilisha nguo kwa sababu zimechafupa, lakini je! ni kweli? Maana kila mtu anakiwango chake cha kuchafuka kwa nguo na ikifika wakati huo anabadili nguo.

Tunapaswa kujiuliza ni nani ambaye alianzisha mfumo wa kubadili nguo? Unavua hii, unavaa hii. Ni kitu gani kipo nyuma ya hilo unalolifanya la kubadili nguo?

Ukweli ni kwamba, tunabadili nguo kwa kuzingatia kanuni ya NJE, NDANI. Hapa ndipo unaondoa mazoea ya kufanya kitu fulani kwa wakati wote. Kanuni hii inataka ubadilike, kanuni hii inataka uishi kwa kiasi, kanuni hii inakutaka ujijali wewe mwenyewe. Lakini kubadili kwetu nguo, tunataka tusitoe harufu, na katika maeneo mengine ya maisha ni hivo hivo, usipobadili utaoza.

Wakati Yesu alipokuwa akifundisha makundi ya watu, alikuwa anapata muda wa kukaa peke yake lakini pia hakuka pekee yake wakati wote bali wakati mwingine alijihusisha na watu. Hivi ndivyo jinsi maisha yanaendeshwa kwa kanuni, na ukifeli kufuata kanuni za kuishi, utafeli kuishi maisha yenye maana.

Tunabadili nguo kila siku lakini tunaweza kujifunza jambo la maana kabisa ambalo litajenga mahusiano yetu vizuri, bila kujali wewe ni mtu wa namna gani? au unaishi kwa namna gani? Ni lazima utambue kwamba utawahitaji wngine katika maisha yako lakini pia unaupekee wako.

Ikiwa unaishi kwa kuiheshimu kanuni hii, utaishi maisha yenye maana. Kila kitu huwa kinadalili yake, ukiona dalili fulani kwenye jambo fulani basi, utajitoa katika wakati huo. Mfano; Unajua wanadamu tunaishi kwa utani lakini unapozama sana kwenye utani unaleta magomvi, kitu ambacho mwanzo wake haukuwa ni ugomvi lakini kwa sababu hamjazingatia usawa na kiasi inapelekea huo ugomvi. Hakuna mtu ambaye hawezi kuishi kwa utani maana utani huleta ladha katika maisha.

Kuna wakati mwingine usitende haki sana, ukazidi, lazima utambue kwamba wewe ni binadamu. Kwa hili watu wengi wanaweza kunielewa vibaya lakini ndio ukweli wenyewe, hata neno la Mungu limethibitisha hilo. Sulemani amethibitisha hilo katika kitabu cha mhubiri. Lkaini rafiki kwenye hili uwe makini, tambua eneo lako ni lipi na ufanye kwa usahihi, hakuna wakati ambao sio sahihi wa kufanya jambo sahihi.

SOMA:INJILI YA MAJI NA ROHO.[ SEHEMU YA PILI].

 Kwa hiyo matukio ambayo tunayafanya kila siku yanaweza, kama kubadilisha nguo kila siku, tunaweza tukajifunza kitu na kuishi maisha yenye maana. Chagua kujifunza, chagua kufikiri, chagua utofauti, angalia kila kitu na ujiulize kwanini. Anayeishi kwa kanuni ya nje, ndani hawezi kuwa mtu wa itikadi bali atajifunza kila tukio linalotukia. Yesu alikuwa anatolea mifano kwenye nneno lake na mifano yake ilikuwa ni katika mazingira haya tunayoishi.


Usiishi kwa itikadi rafiki yangu, jiulize kwanini? ilikuwa inamaanisha nini?, kwanini nipo hapa? Biblia inatufunza tuvae siraha za kiroho, na siraha za kiroho ndio hizi, kuishi kwa utambuzi katika mazingira unayoishi.

Moja ya fundisho ambalo lipo kwenye Biblia, ambalo Yesu alitolea kuhusu mtu ambeye alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, lakini kabla hajafika, katikati, alikutana na wanyang'anyi, wakavua nguo, wakampiga wakamwacha karibia kufa. Mtu wa kanisani, kuhani akamfikia, akapita pembeni na mlawi naye ni mtu wa hekaluni akampita lakini Msamaria akafikia akamsaidia.

Watu hawa wote walikuwa wanakwenda katika shughuli flani, lakini, wale watu wa Mungu, hawakufanya chochote, lakini mpitaji ambaye ni Msamaria akamsaidia japo naye alikuwa anakwenda kushughurika. Kwa sababu ya itkadi watu wa Mungu hawakufanya lolote, kwa sababu ya kuelekea labda hekaluni lakini kila siku wanajifunza jambo hilo hilo la kuwasaidia watu.

Jifunze kanuni hii na kuitendea kazi. Haijarishi lile ambalo limekuwa linafanywa kwa muda mrefu kiasi gani? Na linaonekana ni sahihi kabisa machoni pa watu, unapaswa kulielewa.Usiishi kwa mazoea,usiishi kwa udini, na usiishi kwa itikadi. Tafuta ukweli nao utakuweka huru, kwani sio kila jambo huwa linakuwa kweli wakati wote. Chunguza, tumia asili kujifunza mambo licha ya kusoma vitabu, unaweza ukachukua hata mbegu ya mmea, ukajiuliza mbona huu mmea upo mmoja tu harafu mbegu yake haipo hivo, mbegu yake inaonekana inakiini ndani, utapata majibu.

Mungu anakupenda, Mungu hataki uishi kwa bahati mbaya anataka uishi maisha. Asante.

Sadick kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, October 11, 2018

Angalia Mbegu Unazokazana Kupanda.

 Sadick Kilasi     October 11, 2018     NJOZI     No comments   

Angalia Mbegu Unazokazana Kupanda.

Maisha ni safari ambayo inahitaji utulivu mkubwa sana. Kila siku tunaingiza kwenye ghala ya ubongo mambo mbalimbali. Kila neno ambalo utalisema, kila neno ambalo utalisikia na kila neno ambalo utaliona ipo siku utalipia gharama. Haijarishi wewe ni nani, upo wapi, unafanya nini, lakini ipo siku utalipa gharama kwa hilo ambalo umelisema, umeona na umesikia.

 Kama kwa sasa unakazana kupanda mbegu mbovu ni wazi kwamba kuna wakati ambao itakubidi ulipie gharama ya mbegu unazopanda. Kama ukienda safari ndefu sana tegemea kabisa kwamba, wakati wa kurudi kwako utarudi kwa ile ile safari ambao umeiendea. Inawezekana kwa sasa huna mpango wa kutubu yale ambayo unayafanya lakini ninakwambia ukweli yaleyale ambayo unayapanda ipo siku yatakushitaki siku ambayo umeamua kutubu. Siku ambayo umeamua kufanya mabadiliko hayo mambo ndiyo yatakayo kuwa chanzo cha hofu yako. Watu wengi huwa hatulitambui hili, kwamba tunajengeka kutokana na ujazo mdogomdogo ambao tunaujaza sisi wenyewe.

Zaburi 120:5-7, Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Meshaki;Na kufanya maskani yangu katika hema za Kedari. Nafsi yangu imekaa siku nyingi, pamoja naye aichukiaye amani. Mimi ni wa amani; bali ninenapo, wao huelekea vita.

 Kwa hiyo, ni bora tulinde mapema hatua za maisha yetu. Daudi analalamika kuhusu maisha yake ya nyuma, yanamshitaki wakati anapomwita Mungu.

 Picha za hofu zitakusumbua sana wakati ambao unataka kufanya jambo lako la kukupeleka katika tumaini lako. Kujenga lugha mpya ya hekima itakuwa ngumu kwako kwa sababu umezoea lugha za uovu. Kila ambacho umekipanda ndani yako hakiwezi kutoka mpaka siku utakayokishi hicho kitu kwa wema. Kila utakapo shinda hili litaingia hili ambalo utahitaji kulishinda.

 Mtumainie Mungu wakati wa ujana wako, usisubiri uzeeke. Wakati ndio huu, panda mbegu njema mapema ili uvune mema mapema. Ukiishi kwa kukazana upanda mbegu za magugu kwa muda mrefu, tambua kwamba ipo siku utalipa gharama.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, October 10, 2018

Usikazane Kutafuta Raha Katika Maisha Bali Kazana Kutafuta Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     October 10, 2018     KUFURAHIA MAISHA, NJOZI     No comments   

Watu wengi maisha kwao yamekuwa kama mtego. Tunaishi kwenye dunia yenye miili lakini mara nyi kila jambo limefishwa uhali. Kila kitu kilichopo duniani kimefichwa uhali wake na kinachoonekana ni upekee wake na asili ya kitu hicho. Ukiuangalia mti ni tofauti kabisa jinsi zilivyo mbegu zake. Huu ndio ukweli wenyewe katika kila jambo.

Kutokana na mazingira ambayo tunaishi, tumekuwa tunaishi kwenye vivuli vya ukweli na ndio maana inakuhitaji utambue asili ya kila jambo na mwisho uufikie uhalisi wa jambo hilo. Ninapozungumzia asili namaanisha hivi; kwa mfano mimi Sadick, asili yangu ni ukoo wa akina Kilasi. Lakini hiyo ni asili tu ya mwili, lakini katika uhalisia nipo tofauti kabisa na mwili wangu na siwezi kuonekana kwa macho. Lakini ikiwa naiishi hapa duniani ni lazima niunganike kiroho, nafsi na mwili na huo ndio uhalisia wangu. Nje ya hapo mara nyingi inakuwa sio mimi bali ni eneo dogo tu la mimi na ndiomaana kiasili naweza kubadilika umbo lakini katika uhali huwezi kubadilika.

Nimejaribu kuzungumzia asili na uhalisi ili nikufanye uone utofauti na uanze kufikiri tofauti na jinsi ambavyo umekuwa unafikiri na kujichukulia.

Tunaishi kwenye dunia ya miili yaani katika asili lakini maisha yetu yana mengi kwa sababu duniani tunapita tu, tupo katika mwendo. Yapo mengi tunayopitia duniani lakini na ni mengi pia ambayo tunatamania kupata, na hapa ndipo tunahitaji kuisoma asili vizuri ili tutambue kwamba tutaanzia wapi katika hicho tunachokitafuta na tutaishia wapi. Ikiwa tunaishi kwenye dunia ya miili basi kuna mipaka ambayo ipo na inapaswa kufwatwa.

Katika maisha inayotafutwa kwa kiasi kikubwa na kwa gharama kubwa ni furaha lakini wengi tumejikuta tunajiingiza kutafuta raha ama burudani kwa sababu hatujatambua ni kipi chanzo cha furaha.

Sisi ni miili ambayo tumepewa tusafilie kwa muda lakini matumaini yetu si katika miili bali katika vitu ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho. Ikiwa tunamtumainia Mungu asiye onekana basi katika uhali wetu nasi hatuonekani kwa macho na huo ndio ukweli wenyewe. Kutafuta furaha kunattegemea sisi hatua zetu tunazopiga ndizo zitatupeleka katika furaha. Ikiwa unatafuta pesa tu bila kutambua kwamba asili yako wewe si kutegemea pesa basi ni wazi lazima ufanye la kwanza na la pili bila kukosea.

 Tunahitaji kutambua kwamba tunapaswa kuanzia wapi na kuishia wapi, kwani raha ambayo hutafutwa kwa njia ya kutegemea mazingira ya nje haidumu na wala haiwezi kutupa furaha kamili.
2Wakorintho 4:18, Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyooneka ni vya muda tu; lakini vile visivyo onekana ni nya milele.
Ikiwa tunaasili ya kutoonekana basi niwazi kwamba tunapaswa kutambua ya kwamba tunahitaji kujijenga katika huko kutoonekana na kujijenga pia katika kuonekana kwani pia bado tuna mwili.

Leo nitakupa njia moja ya kujenga furaha yako ya kudumu ambayo biblia imekazia kwa umakini zaidi na hichi nndicho kiini cha furaka katika maisha yako.
Mithali 4:23, Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemichemi za uzima.

 Hapa ndipo unahitaji kujifunza kwa umakini kabisa  amri za Mungu zinasemaje, lakini moyo wako unapaswa kuulinda kama nini. Ikiwa utapangilia kuishi maisha ya upendo basi ni wazi kwamba tayari umeenza kuishi maisha ya maana na ukidumu katika kujifunza neno la Mungu , utaupata ukweli nao ukweli utakuweka huru.

Kaa na pangilia maisha yako, tafuta ukweli kama unavyotafuta pesa na ndipo ukweli utakuweka huru katika maisha yako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

 Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ▼  October (29)
      • Maisha Yenye Maana.
      • Wapi Ulipo?
      • Sala Ya Kuomba Amani.
      • Sicho Hicho Ndugu Yangu Unachohitaji.
      • Mwili Wako Ni Zawadi Kwa Wengine.
      • Utabiri Unaonesha Kwamba Wewe Utafurahia Maisha Ka...
      • Unachohitaji Katika Maisha Yako.
      • Kutambua Dalili Za Kujiliwa Kwa Jambo Jipya.
      • Ishi Kwa Kudhamiria Jambo Jema.
      • Ubatizo Ni Nini?
      • Upekee Unagharama Yake Ya Kulipa.
      • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache,...
      • Uogope Woga unaokufanya Uwe Mwoga.
      • Jifunze Kwa Bidii Ili Uwe Huru.
      • Wakati Jama Wakati.
      • Madamu Unayo Leo Unaweza.
      • Viungo Vya Mwili Hufanya Kazi Kwa Ushilikiano.
      • Dunia Mama Haimtupi Mwenye Mwili.
      • Mwalimu Nyerere Zawadi Ya Afrika Na Dunia Kwa Ujumla.
      • Mambo Ya Kujua Na Kuepuka Ili Kudumisha Furaha Kat...
      • Unabadilisha Nguo Kila Siku, Kwanini Usibadilishe ...
      • Angalia Mbegu Unazokazana Kupanda.
      • Usikazane Kutafuta Raha Katika Maisha Bali Kazana ...
      • Ujumbe Uliobeba Ndani Yako.
      • Kila Mtu Yupo Bize Na Lugha Yake.
      • Mambo Ya Kuyatambua Katika Maisha Lakini Kuzingati...
      • Mwenyezi Mungu Ni Nani?
      • Hata Kama Umezaliwa Kwa Injili Ya Maji Na Roho Una...
      • Tujifunze Kutoka Kwa Panya Na Kuishi Maisha Yenye...
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates