JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, July 31, 2018

Injili Ya Maji Na Roho [SEHEMU YA PILI]

 Sadick Kilasi     July 31, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Habari rafiki?  Natumai unaendelea vizuri kabisa. Karibu katika sehemu ya pili ya injili ya maji na Roho ambapo najaribu kukuonyesha kwa undani kabisa kuhusu ubatizo wa Yesu aliobatizwa na Yohana Mbatizaji.

Natumai kwa sasa umeanza kuelewa kuhusu ubatizo, karibu tena ili tuendelee kuuchimbua kwa undani ubatizo huu na kufahamu siri kubwa ambayo ipo ndani yake, karibu sana.
                                                         Jipatie kitabu hiki.

Yohana alimbatiza Yesu ili kumtwisha dhambi za ulimwengu na hii ndio sababu ambayo ilimfanya Yohana awe anabatiza. Sababu kubwa ya Yohana kubatiza watu katika mto Yordani ilikuwa ni kumtambua Yesu ni yupi baada ya kumbatiza, ikisha kkupitia ubatizo huo amtwishe dhambi Yesu. Yeye aliyemtuma Yohana alimwambia kwamba utakaye mbatiza na Roho akimshukia basi huyo ndiye mwanakondoo ambaye atachukua dhambi ya ulimwengu.
Yohana 1:29-34, Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya Ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua;  lakini kusudi adhihrishwe kwa Israeli ndiyomaana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Tena Yohana alishuhudia akisema, nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.

Ilikuwa ni muhimu kwa Yesu kubatizwa na Yohana maana Yohana alikuwa kuhani wa mwisho wa wanadamu na Yesu kwa sababu alifanyika mwana kondoo ambaye ataichukua dhambi ya ulimwengu basi Yohana kama kuhani wa uzao wa Haruni na ni kuhani mkuu wa wanadamu alimtwisha dhambi Yesu kwa kumwekea mikono juu yake, dhambi zote Yesu alizibeba. Mfumo huu ndio ambao hata makuhani wa zamani waliutumia kuondoa dhambi za wana wa Israeli lakini kwa sababu zile zilikuwa dhabihu ubatizo haukukamilika na ndiomaana iliwalazimu kila baada ya mwaka mara moja walifanya tendo la kuondoa dhambi. Lakini Yesu alifanya mara hii moja na kwa wakati wote dhambi zote ziliondolewa kwa sasa hatuna dhambi kabisa. Utajiuliza mbona mimi nina dhambi wakati namwamini Yesu? Ndio, pasipo kuitambua vema injili hii ya maji na Roho huwezi kuokolewa hata kama unamwamini Yesu. Sio kumwamini Yesu pekee ndio kutakupa haki ya wewe kutokuwa na dhambi bali ni kuiamini injili yake ambayo yeye mwenyewe alisema, Yohana 3:5, Yesu akajibu, Amini, amini, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Wapaswa kumwamini Ysu na kuamini maneno yake ni muhimu muhimu zaidi kuitambua injili ya maji na Roho vizuri

Jambo la ubatizo wa Yesu lilitabiliwa na manabii na kupitia ubatizo wake hivi leo sisi sote tumepokea neema ambayo inatufanya kutokuwa na dhambi na kushiriki utukufu wa Mungu kwa kufanyika familia moja na Yesu. Mambo haya yote hufanyika kwa imani, tukiisha kuamini ndipo Yesu yeye anatubatiza kwa Roho Mtakatifu, wewe unapaswa kuamini tu, kwamba mimi sina dhambi, dhambi zangu zote zilitwishwa kwa Yesu miaka 2000 iliyopita na Yohana ambaye ndiye aliyemtwisha dhambi Yesu. Ubatizo huu ndio unatupa haki ya kusafishwa dhamiri zetu mioyo yetu haihukumiwi tena maana tumeiamini injili ya maji na Roho na Yesu ametubatiza Roho wake.

1Petro 3:21, Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi siku hizi; [siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu,] kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Ni katika imani si katika matendo, jibu la dhamiri safi mbele za Mungu, tunashiriki utukufu huu kwa imani si kwa matendo yetu hapana lazima utambue hili vema, ubatizo huu ndio unatufnya hatuna dhambi, tunashiriki mambo yote aliyoyafanya Yesu kwa imani na ndiomaana lazima uamini maji, damu na Roho, haya yote Yesu aliyapitia lakini mwanzo wake ulikuwa ni ubatizo ambao wengi kwa sasa wanaupuuzia, wengine hubatizwa baharini lakini nataka nikuambie hivi rafiki, tunashiriki kwa imani. Ikiwa utashiriki ubatizo wake kwa matendo basi wapaswa pia kuteswa msalabani maana huwezi kushiriki nusu na inapaswa ufufuliwe baada ya kufa kwa sababu mateso ya msalabani. Lazima utambue kitu kimoja, mpango wa Mungu ni nini? Mpango wa Mungu ni kumwamini mwanaye Yesu na yale aliyoyafanya basi si matendo yetu, si kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Lazima utambue kitu kimoja mwanadamu atatenda dhambi mpaka kufa na Mungu amesema ondoeni matendo yenu mbele zangu. Haleluya!

Unapaswa kuliamini neno la Mungu na kulitii, wengine nikiwahubiria injili hii husema, imani bila matendo imekufa, na mimi nakubari, lakini wapaswa kutambua hayo matendo unayaelekezea wapi, kama kweli unamwamini Mungu na unataka kufanya jambo la shukrani kwa matendo basi wasaidie wanae maana sisi sote ni wana wa Mungu, Yesu aliwafundisha hivi mafalisayo, Mathayo 23:23, Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na binzari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani adili, na rehema na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Anaposema, adili na rehema anamaanisha haki na huruma yaani upendo. Mambo ya kufanya kwa haki na huruma tunapaswa kuwatendea watu vema, kama unampenda Mungu basi watendee watu mema na imani yako ipeleke kwa Mungu. Haleluya!

Kwa leo naommba tuishie hapa, wakati unaokuja tutaendelea kuuchimbua kwa undani ubatizo wa Yesu. Kwa hapa tulipofikia ikiwa utaiamini injili hii basi utaokolewa. Warumi 10:10, Kwa maana kwa moyo wa mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Basi, wewe unapaswa kuamini tu na kukiri kwa maombi  na maombi unayokiri yanapaswa kuwa kama mtu ambaye hajaokolewa Warumi 10:3, Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuthibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa hiyo ni muhimu katika kulielewa hili nalo litakujenga, unapaswa kutambua kila hatua na kutambua nafasi yako.

                                         OMBI:
Omba hvi; Mimi ni mwenye dhambi na kwaajili ya dhambi zangu napaswa kwenda motoni lakini sasa namwamini Yesu ya kwamba amechukua dhambi zangu zote alipobatizwa na Yohana katika mto Yordani na mimi sina dhambi tena, namtwisha Yesu dhambi kwa kumwani ubatizo wake, kupitia Yohana kama kuhani wangu alimtwisha dhambi Yesu, akateswa msalabani kwa sababu ya dhambi zangu na kufufuliwa kutoka kwa wafu kwa uweza wa Roho Mtakatifu na sasa yu hai Yesu Kristo. Nakuomba Yesu unibatize kwa Roho Mtakatifu. AMINA.

Pia unaweza kumwomba Mungu akupe ishara baada ya kumpokea Roho Mtakatifu. Fanya maombi kila siku, maombi yako sasa yawe ya shukrani na siyo yaulalamishi na jikite sana katika kusoma neno la Mungu wakati wote.

Ukimpokea tafadhari naomba ushuhuda wako, ili unitie moyo na tuendelee kwa pamoja kuihubiri injili hii njema. Asante sana

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ▼  July (12)
      • Injili Ya Maji Na Roho [SEHEMU YA PILI]
      • Maneno Matatu Ambayo Yanapaswa Kudumu Katika Maish...
      • Neno La Pekee Ambalo Hunijaza Furaha Wakati Wote
      • Injili Ya Maji Na Roho.
      • Kumpa Nafasi Mungu Atawale Kila Eneo La Maisha Yako.
      • Mungu Anakuona Kila Kitu Unachofanya.
      • Mambo Mawili Yanayolenga Ibada Ya Kweli.
      • Injili Ya Maji Na Damu Ambayo Ni Kweli Yenyewe
      • Mambo Mawili Ya Kuzingatia Wakati Wa Kufanya Chaguo.
      • Sababu Moja Kwanini Unapaswa Kusoma Neno La Mungu...
      • Tafuta Mtu Huyu Popote Alipo.
      • Mimea Midogo Chini Ya Kivuli Cha Mti Mkubwa.
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates