JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Monday, April 30, 2018

Mtu Anaweza Kukumbuka Kwa Hiki. $#Tafakari Hekima Za Wazee$#

 Sadick Kilasi     April 30, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Nimejifunza kuwa mtu anaweza asikumbuke ulichokisema wala ulichikifanya lakini katu hawezi kusahau namna ulivyomfanya ajisikie kutokana ulivyofanya.    Maya Angelou. 

Japokuwa unapomfanyia mtu jambo fulani mara nyingi watu wanapokea wanavyojisikia wao wajisikie vizuri au vibaya japo wewe labda ulikuwa unataka ajisikie tofauti na alivyo jisikia.

Ukweli ni kwamba mtu atakukumbuka namna ulivofanya ajisikie yeye haijairishi unamaana hiyo au la, lakini vile alivyojisikia ndivyo atakavyokumbuka.

Swali la kujiuliza ni kwamba, wewe unakazana watu wajisikiaje? Wewe ni unakazana watu wajisijikie vibaya au unakazana watu wajisikie vizuri? Kwa sababu kwa kadili unavyofanya watu watakuelewa baadae kwa unawajenga au unawabomoa.

SOMA:Ni Rahisi Kuona Kitu Hiki Kwa Watu Wengine.

Kama unakazana kubomoa watu basi hivyo ndivyo watu watakavyo kukumbuka.

Kama unakazana kujenga watu basi hivyo ndivyo utakavyo kumbukwa.

Yanini ubomoe watu? Jenga watu ili ujiwekee msingi mzuri katika maisha yako.

Ukawe na siku bora na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, April 29, 2018

Usitawanye Watu Kusanya Watu, Fanya Kitu Hiki Kukusanya Watu.

 Sadick Kilasi     April 29, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ili kuushinda ubinafsi na tabia za umimi basi huna budi kuchagua watu ambao unajua kabisa kwamba mimi hawa siwapendi ikisha nenda kawambie nakupenda.

Ni jambo gumu najua lakini hii itakusaidia wewe mwenyewe. Ni kitu kigumu kama utaanza kujilinganisha nao kwa kweli kitakuwa kitu kigumu kwa hapo utazidi kujionyesha mwenyewe ya kwamba unakibuli na mbinafsi.

SOMA:Kama Hujawahi Kuona Kichogo Chako Ya Nini Yote Hayo?

Rafiki, kila mtu ni zawadi yako wewe huna haja ya kujilinganisha na mtu. Wewe sio mwili huo rafiki yangu, mwili wako ni zawadi ya wanaokuona na wao ni zawadi yao.

Hakuna lisilowezekana kwenye upendo, upendo hauhesabu muda wala mabaya. Watazame watu kwa mazuri yao na si kwa mabaya. Mpendwa rafiki, si lazima awe amekutendea mazuri ya kupewa kitu hapana fikiri zaidi ya hapo. Kumwona tu mtu mshukuru Mungu kwamba umeniweka kwenye hii dunia nzuri ambayo unakutana na watu ambao nawambia ninachojisikia. Vipi ungekuwa huko msituni na huoni watu wa kuwambia kitu, upo peke yako.

Wachague unawajua kabisa kwamba hawa nawachukia nenda kawambie nakupenda na kama ukishindwa kuwambia nakupenda wasifie kwa jambo lolote lile ambalo ni zuri wanalofanya, rudia tena kusifia na iwe tabia yako.

Ajishushaye hukwezwa, imeandikwa kwenye BĂ­blia. Usitawanye watu, kusanya watu kwa upendo.

Ukawe na siku bora rafiki yangu na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, April 28, 2018

Nyoosha Mikono Juu Iambie Jamii Nimeshindwa.

 Sadick Kilasi     April 28, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Wakati mambo yanapokuwa magumu watu huwa hatutaki kabisa kukubali kwamba mambo ni magumu.

Sisemi kwamba tuwe tunakubali mambo yanapokuwa magumu hapana lazima ukubali kwamba mimi siwezi ili ujifunze kutokea hapo.


Watu hatutaki kabisa kukubali kwamba sisi tunamapungufu ubinafsi unatesa sana. Mpendwa msomaji, kubali sasa mwambie Mungu mimi siwezi sasa kuwapenda watu na nataka kupenda watu, siwezi kuwa shujaa nataka kuwa shujaa, siwezi kujitegemea mwenyewe nataka kukutegemea wewe kumbuka Yesu alisema msipo rudi na kuwa watoto hamwezi kuuona Ufalme wa Mbinguni.

Ukikubali kwamba huwezi huo ndio utakuwa mwanzo wako wa kuweza huwezi kukiri kwamba naweza pasipo kukiri kwamba siwezi.

SOMA:Binadamu Ameumbwa Akiwa Na Tabia Hizi.


Penye utupu panajazwa ili pawe tele. Mwisho upo kwa sababu ya mwanzo. Inyoshee jamii mikono ila usiwambie watu nimenyoosha mikono yangu nashindwa kuwapenda. Utakapo nyoosha mikono utajiona wewe ni nani na utakapo jiona wewe ni nani hutapotea unapokwenda. Mungu anapatikana kwa watu wake.

Ukawe na siku bora kabisa na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, April 27, 2018

Kama Wewe Hujawahi Kuona Hata Kisogo Chako Ya Nini Yote Hayo?

 Sadick Kilasi     April 27, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Kati ya kitu ambacho binadamu wanathamini hasa kwa kizazi hilo basi ni miili yao. Miili yao inawapa kiburi cha kujiona wao ndio wao.

Wanaligia uzuri wa miili yao, wanalingia tamaa ya miili yao, wanalingia kiburi cha miili yao lakini wanasahau kitu kimoja tu.

Kitu ambacho wanasahau wao ni kwamba wao sio wanaojiona vizuri, kama hujawahi kuona hata kisogo chako kwanini malingo yote hayo, kama huwezi hata kujiangalia mwenyewe yanini chote kiburi hicho.

Mpendwa wangu, rafiki yangu, anayaweza kukuangalia vizuri na kwa usahihi ni mwenzako wewe hata hujijui vizuri na ndiomana hata ukijiangalia kwenye kioo huwezi kujimaliza, mwisho utajisahau mwenyewe.

SOMA:Maajabu Niliyokutana Nayo Nilipojiangalia Kwenye Kioo.

Mpendwa msomaji, wewe si wako wewe ni wa mwenzako, wewe huna unachomiliki juu yako, wewe ni zawadi kwa wengine na mwingine vinyo hivyo ni zawadi kwa mwingine.

Tupendane, tupendane, tupendane na hivyo ndivyo inavyotakiwa, Mungu katuumba kwa njia ya ajabu anataka tupendane.

Hebu waangalie watu wote wanao kuzunguka, kwa kweli wote hao ni zawadi yako kwa sababu unawakati wa kuwapenda ambao ni sasa. Na unawaangalia vizuri wote. Wapende kwa wakati, kwa sababu unawakati, utafika wakati utashindwa kuwapenda kwa wakati kwa sababu hutakuwa na wakati wa kuwapenda kwa wakati.

Ukawe na siku bora rafiki yangu, ukienenda kwa upendo. Endelelea kutembelea blogu hii kwa kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, April 26, 2018

Hasira Ni Kama Maji Yanayochemka. Je Mwisho Wake Huwaje?

 Sadick Kilasi     April 26, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Hata ukichemsha maji kwa moto mkali kiasi gani joto la moto likipungua na maji yanaanza kupungua kasi ya kuchemka. Moto ukizima kabisa maji nayo hupoa kabisa na kurudi kama zamani na yatabaki maji kama maji na hayabadilika.

Tukichemshwa tunachemka lakini hasira ikipoa unakuwa vile vile na hubadiliki kitu chochote.

Wakati unapokuwa na hasira kumbuka ya ya kwamba wewe ni wewe tu kwa hiyo usijaribu kufanya maamuzi ambayo ni ya kuwaumiza wengine usije ukajuta ukipoa.

SOMA:Usiwanyanyapae Watu Kwa Sababu Wanayofanya Ni Maovu.

Katika wakati ambao shetani humtumia vizuri mtu ni wakati ambao mtu katawaliwa na hasira. Shetani hukaa pembeni ili aitumie vizuri fursa hiyo kwa kuwaumiza wengine. Siku zote shetani anataka wewe ukose furaha baada ya hali hiyo.

Hata kama ukiwa na hasira kiasi gani wewe ni yule yule tunaye kutambua, kuwa mvumilivu mambo yote yatakwenda vizuri.

Ukweli ni kwamba hasira sio dhambi lakini hatua utakazo chukua ndo zinaweza kukupa ushujaa au la. Hakuna mtu ambaye hana hasira lakini tunatofautiana jinsi tunavyoyachukulia mambo. Kuna wengine wana hasira za karibu na wengine kinyume na hivyo.

Siku zote nimekuwa nakupa namna ya kupambana na hasira. Kanuni yenyewe ni pambana na hali na usipambane na mtu. Tengeneza mtazamo ya kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuchukia peke yake kwa hiyo na wewe ni chanzo cha ugomvi. Ubaya wako upo ndani yako umeamshwa tu, wewe ndo kila kitu.

Hasira ni kama maji yanayochemka kwa muda lakini uhalisia wake haupotei. Kuwa mvumilivu unapokuwa kwenye hali ya hasira usije ukapoteza utu wako.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii, ukawe na siku bora rafiki.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Hivi Ndivyo Vikwazo Katika Kuupata Ukweli Halisi.

 Sadick Kilasi     April 26, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   

Ili kuupata ukweli ambao umekuwa ukiutafuta kila siku kuna vikwazo ambayo vinaweza kukuzuia usiupate ukweli halisi.

Ukweli ni wa muhimu katika maisha kwa sababu kweli inakuweka huru na ukiwa huru unakuwa na furaha.

Vikwazo katika kuupata ukweli:

1.Tamaa yako. Tampa yako itakuzuia kuupata ukweli kwa sababu utatumia mbinu zaidi badala ya kanuni zaidi.

2.Ushabiki unaweza kukuzuia kupata ukweli. Ukiwa shabiki utashindwa kubainisha mambo kutokana na mapenzi ambayo umeweka kwenye kitu au jambo hilo.

3.Vya ziada. Watu wanao tia chumvi ukweli wanapotosha ukweli hata kama wanasema kweli. Kwa hiyo kuwa makini na mtu wa namna hiyo anaweza kusababisha kushindwa kukamirisha lengo kwa sababu ameashilia tofauti na uhalisi wake. Watu kama hawa hufanya kazi kuwavutia wengine.

SOMA:Tunatakiwa Kuwa Kama Chumvi Si Kama Sukari.

Kuamini unacho amini. Wapo watu ambao wanaamini wanavyo amini. Watu hawa hawapo tayari kubadilika kabisa hata kama ukweli upo wazi.

4.Kulidhika na ulicho nacho. Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Katika jamii zetu ndivyo tunavyo ishi, watu hawajishugulishi na chochote japokuwa wanatambua kabisa tulipo sipo. Kwa kweli hili nalo ni 🔥 changamoto katika kuupata ukweli halisi.

Hivyo ni vikwazo katika kuupata ukweli halisi. Na ili kupata ukweli basi epuka kufanya kama hayo. Tafuta kweli nayo kweli itakuweka huru.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, April 25, 2018

Wengi Tunafanya Nusu Nusu Hatufanyi Kweli Kweli.

 Sadick Kilasi     April 25, 2018     NJOZI     No comments   

Moja kati ya sifa kubwa ya Ulimwengu huu ni kwamba chochote kile ukikifanya kwa kujitoa na kuwa king'ang'anizi lazima utalipwa sawa sawa na kazi yako.

Uwe unafanya ujinga au la, dunia hawezi kuacha kukupa matokeo unayota. Kikubwa tu  kuwa king'ang'anizi utapa unachotaka.

Kuwa shujaa kwenye hii dunia ni kulipa gharama, ikisha unapokea unachotaka.

SOMA:Kipi Kinakusukuma Kukua?

Angalia mashujaa wa dunia hii kwa kweli wapo tofauti tofauti, tabia mbalimbali. Kuwa king'ang'anizi utapa unachotaka.

Endelea kutembelea blogu hii kijifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, April 24, 2018

Ni Rahisi Sana Kuona Kitu Hiki Kwa Watu Wengine.

 Sadick Kilasi     April 24, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni rahisi sana kuona makosa ya wengine na mapungufu yao. Ni jambo rahisi kabisa kumwona mtu mwingine anatabia fulani ambayo ni mbaya, mimi huyo simpendi na mambo mengine kama hayo.

Ukweli ni kwamba ni ngumu kupokea ujumbe kama huo kutoka kwa mwingine, ni ngumu sana kijinyoshea kidole mwenyewe, huwezi kumkuta mtu analalamika kwamba mimi ninatabia hii mbaya, napenda kuongea sana na siwapi nafasi wengine, kwa kweli hiyo ni ngumu kumkuta mtu kama huyo na kama wapo ni wachache sana.

SOMA:Binadamu Ameumbwa Akiwa Na Tabia Hizi.

Ukweli ni kwamba, asili imekuwa ikitutesa sana, asili imekuwa ni mwiba kwa wengine. Kiasili kila binadamu ni mbinafsi, hii inapelekea kuona wengine hawafai na sisi ndo tunafaaa zaidi.


Tabia kama hii sio nzuri kwa sababu inaleta mugawanyiko na kutawanyika kwa watu. Kuna kila sababu ya kujitambua wewe mwenyewe kwanza, kila binadamu anampungufu yake, usiangalie zaidi mapungufu ya wengine, wakati mwingine jiangalie wewe kwanza, je unatabia njema ambayo unaweza kumshawishi? Ukiona huna, kwanini unalaumu? 

Kama upepitia hali kama yake na umebadilika kwa kweli usingekuwa na sababu ya kumchukia zaidi ya kumwonea huruma. Tunachukiana bure tu, tunatawanyana bure tu, leo hii hata dini hamna utulivu kwa sababu ya kukosoana, kila mtu anavutia kwake, ubinafsi umekuwa mwingi sana, kumbuka wote tupo katika dunia ya upotevu, tupendane, tuvumiliane na tuwe na umoja.

Mpendwa msomaji, ukianza kumfuatilia mtu utaona vitu vya ajabu ambavyo hukutarajia kabisa kuona. Angalia mapungufu yako kwanza ikisha boresha harafu tengeneza urafiki na huyo ambaye unamnyoshea kidole. 

Ukawe na siku bora na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

(SEHEMU YA NNE) Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu (II).

 Sadick Kilasi     April 24, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Nina furaha kweli kweli ninapokushirikisha mambo mazuri ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu hiki. Mafunzo haya yatakuwa msaada kwako ikiwa utakuwa tayari kuelewa na kutimia veja. Kwa kweli ninaamini ya kwamba upo salama kabisa Mungu kakujalia kusoma makala haya. Hongera sana rafiki yangu kwa kukutana tena kwenye makala  ya leo.  Leo naenda kukushirikisha sehemu ya nne ya mambo ninayokushikisha niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu II kilichoandikwa na Paulo C.  Jong.

Tuliangalia namna gani ukiwa umepokea Haki ya Mungu, Roho Mtakatifu ndiye atakaye kuongoza katika maisha yako. Tunapewa na kuongozwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu.

Jamani nani asiyependa kuongozwa na Mungu? Kwa kweli hapana mtu, kila mmoja anapenda kuongozwa na Mungu. Ukweli ni kwamba tukiwa tunaishi kwa kutegemea haki yetu wenyewe tunaishi kwa kugugumia na kunung'unika, maisha yanakuwa magumu sana. Haijarishi uwe na mali au la, kwa kweli hatuwezi kuishi kwa kutegemea haki yetu sisi wenyewe.

Ukifikia maisha ya utauwa,  ukweli Mungu anapenda sana kila mmoja wetu kufikia katika kiwango hicho. Miili yetu haiwezi kuacha kutendenda dhambi, lazima tuamini katika injili ya maji na Roho ili tuweze kupokea zawadi nzuri ambayo Mungu anatupatia ambayo ni kutuongoza kupitia Roho Mtakatifu.

Nisikuchoshe msomaji wangu karibu katika ya leo lakini kama hukusoma makala yaliyopita hakikisha unasoma ili kuelewa vema. Soma kwenye kiungo hapo chini.

SOMA:Soma Sehemu Ya Tatu Ya Mambo Niliyo Jifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu.

Karibu sana,

1. Mungu anawapenda waamini waliozaliwa tena upya. Wakati mwingine Mungu anaweza kuwaachilia hata adui zako kwa ajili ya kukujenga zaidi lakini mwisho anawaadhibu adui hao. Je wewe unatia shaka wakati wa kuachiliwa adui? Kwa kweli hutakiwi kuwa na shaka kabisa, amini katika haki ya Mungu.

2.Mungu anatupenda sana, alipanda mti wa mema na mabaya katika bustani ya Edeni, na kisha akawaamulu Adamu na Hawa kutokula matunda ya mti huo. Huo ulikuwa ni mpango wa Mungu, ili wanae wapate kumrudia yeye. Alitambua ya kwamba mwananadamu hawezi kumtumikia Mungu bila sababu lazima ataasi. Waweza  kushangazwa na hili lakini huo ndo ukweli wenyewe. Sawa sawa na mtu ambaye anachukua kitu ambacho hukifahamu akaweka juu ya meza na kusema, humu kwenye boksi kuna kitu kitamu sana, lakini ole ufunue box uangalie. Hapo ushawishi unakuwa mkubwa zaidi kuliko angeficha na kutokwambia.

3.Wale ambao wanakiri ya kwamba wao ndio wenye dhambi, basi hao ndio Mungu amewaita, wale ambao ni wadhaifu, Mungu ndio anawaita waende akawafanye wawe huru. Kwa kweli Mungu anawapenda wadhaifu wale ambao wamekosa haki. Lakini kama wewe una haki yako Mungu hakuhitaji.

4.Wakati mwingine hujisikia kama tumedhalilishwa kana kwamba tunataka kujificha pale tunapojifahamu kwa jinsi tulivyo. Lakini Mungu anauwezo wa kugeuza mzaituni mwitu na kuwa mzaituni halisi. Kwa asili sisi ni mzaituni mwitu lakini tuligeuzwa kuwa mzaituni halisi kwa injili ya Yesu ambayo ametupatia. Kwa hiyo tunapojitambua ya kuwa sisi tu wenye dhambi lazima tutambue ya kwamba Mungu anatuita na tutegemee katika haki yake, haki ya Mungu.

5.Kuna wakati tunafikiri kwamba, wakati bado sijalisikia Neno la Mungu nilikuwa sijazitambua dhambi zangu lakini sasa nazitambua dhambi zangu na naona siwezi kumtumikia Mungu kikamilifu. Lakini hiyo si sahihi. Badala yake tunapaswa kufikiri, nilikuwa sifahamu dhambi zangu hata pale nilipokuwa nazitenda. Neno la Mungu lote ni sahihi lazima niamini katika Neno lake. Siwezi kuishi kwa kufuata Neno hilo kikamirifu. Kwa kweli mimi ni mwenye dhambi ambaye nimepangiwa kwenda kuzimu na hii ndo sababu Kristo Yesu alikuja.

6.Tunahesabiwa haki na kutakaswa mara moja tu,  unapoamini injili ya maji na Roho. Moyo wako haubadiliki kwa hatua. Moyo wako unafanyika huna dhambi mara moja na ni imani yako ndiyo inayoweza kukua hatua kwa hatua kadiri unavyoliamini Neno la Mungu na kanisa lake.  (warumi 8:29-30).

7.Walio hesabiwa haki ni akina nani?
Kwa kweli Mungu hajachagua au kufanya chaguo katika kuwaita walio wake. (Yohana 1:29).

Kwa kweli wengi tunatambua ya kwamba Mungu alimchagua Yakobo na akasema Esau nimemchukia, aliwachagua tangu wakiwa tumboni mwa mama yao. Kwa kusema mkubwa atamtumikia mdogo. Je Mungu ana watu wake tayari alio wachagua? Tafadhari usikose uchambuzi ujao, tutajua vema walio hesabiwa haki ni akina nani.

Mpendwa msomaji, nisaidie kuwashirikisha wengine uchambuzi huu, ili ukawafikie wengi zaidi na tujifunze kwa pamoja. Mungu awe nawe.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, April 23, 2018

Sababu Hii Moja Tu Inatosha Kwako Wewe Kuanza Kusoma Vitabu.

 Sadick Kilasi     April 23, 2018     USHAURI     No comments   

Japokuwa usomaji wa vitabu unamanufaa mengi sana lakini mimi nataka nikupe sababu moja tu, kwanini na wewe uanze kusoma vitabu.

Kwa kweli Watanzania hatuna desturi kabisa ya kusoma vitabu, yaani hatusomi vitabu kabisa. Ukweli ni kwamba hata kama tunasoma basi tunapitisha macho kwenye maandishi kwa mara moja na kutupa huko. Desturi ya kusoma vitabu haipo kabisa katika jamii yetu ya Kitanzania.

Kuna uhuru mkubwa sana wa kiakili ambao unaupata wakati unasoma vitabu. Hii ndo sababu kubwa na ya kipekee kwanini uanze kusoma vitabu. Najua huwezi kunielewa namaanisha nini lakini kama ukianza kusoma vitabu basi utaanza kuyaona mabadiliko ndani yako.

Kwa kweli uhuru wa nchi kutoka kwa wakoloni tayari tulisha pata lakini uhuru wa fikra kwa mtu mmoja moja bado sana. Naweza kusema walio pata uhuru wa fikra ndio wale walio tuletea uhuru wa nchi.

Watu tunapenda sana kushikiwa mambo, watu hatupendi kabisa kujiongoza wenyewe ndo maana ni rahisi kabisa kuwa na lawama juu ya mwingine kwa sababu kila kitu tumeshikiwa na wengine. Hatuna uhuru wa kifikra.

SOMA:Mazingira Uliopo Yanakupa Tafsiri Gani? Dunia Imejaa Kitu Hiki.

Anza kusoma vitabu rafiki yangu, hakuna mtu ambaye anaweza kuongoza fikra zako na usipokuwa na taarifa sahihi lazina utakuwa mtumwa wa fikra za wengine kwa sababu huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani na undani wa jambo lenyewe lipo na mtu mwingine na wewe huna chochote. Malcon X alishawahi kunukuliwa akisema mtu asiyesimama kwa chochote ataanguka kwa chochote. Kwa kweli kila mmoja yampasa kuanza kutengeneza misingi yake. Usiseme mimi nimesoma sana shuleni nina diploma sijui vyuo huko, rafiki yangu hiyo ni elimu ya shuleni lakini elimu ya mitaani ni bora zaidi maana haya ndo maisha yenyewe. Ukweli ni kwamba usiache elimu ya darasani ikupe kiburi, anza kusoma vitabu. Mimi ninayekushauri hivi nimeona faida kubwa kwanini ni vizuri zaidi kusoma vitabu.

Soma vitabu upate uhuru wa mazingira, soma vitabu vya dini upate uhuru wa kiroho, soma vitabu upate uhuru wako. Soma vitabu vya dini mwenyewe na siyo kusomewa kuna siri nzito sana humo na zishuhudie mwenyewe.

Uhuru wa ndani ndo uhuru wenyewe, jijenge akili yako, jijenge katika maandiko, lisha akili yako chakula, amsha akili iliyolala.

Ukawe na siku bora kabisa na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, April 22, 2018

Mazingira Uliyopo Yanakupa Tafsiri Gani? Dunia Imejaa Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     April 22, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Tabia ya watu kuwa na mtazamo wa mema na mabaya kwa kweli imeleta mkanganyiko mkubwa sana katika maisha. Kutokana na asili ya binadamu kuwa mbinafsi hilo limekuwa tatizo kubwa sana katika maisha.

Kila mtu amekuwa akivutia kwake na kuona ya kwamba anachokiona yeye ni sawa kabisa lakini kwa mtazamo wa mwingine imekuwa ni changamoto. Anacho kiamini yeye anataka kila mmoja aamini. Anamini kwamba yeye yupo sahihi zaidi ya mwingine.

SOMA:Tatizo Sio Wao, Tatizo Ni Wewe Na Hapo Ndipo Migogoro Inapoanzia.

Kulinganisha mambo pia imeleta changamoto kwa sababu ukisha linganisha utapata utofauti na mwisho utaona kingine kizuri na kingine ni kibaya. Utauona uzuri wa kingine kwa uzuri wake na utaona ubaya wa kingine kwa ubaya wake.

Mpendwa msomaji, kwangu mimi kila kitu ni kizuri kwenye hii dunia, kila kitu poa hasa ukiwa mvumilivu. Kwa kweli unapokimbizwa lazima usifu na anayekukimbiza. Usije kusema unambio sana wakati unakimbizwa na kinyonga.

Dunia ni nzuri kwa kweli, vyote vinavyotokea ni kwa ajili yetu, kama si kutujenga basi kutukomaza, kama kutukomaza basi kutukumbusha. Lolote ambalo unaliona kwa ubaya kwa kweli hilo ndilo lililolifanya zuri kuonekana.

Shukrani kwa kila kitu, Mungu katupatia kila kitu, katupa tutawale. Mpendwa msomaji, usiishi kwa makundi, pata wakati na wewe halafu iangalie dunia ilivyo nzuri, sauti za ndege, wanyama, wadudu kwa kweli kila kitu ni poa. Fikiria kwamba ungekuwa sehemu fulani hivi upweke, sehemu ambayo upo peke yako, kwa kweli ingekuwa mbaya sana hii.

Ukawe na siku bora kabisa na ufurahie uzuri wa dunia.

Wako Sadick Kilasi

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, April 21, 2018

Thamani Ya Binadamu Haitokani Na Utajiri Alionao. #$ Tafakari Chumvi Za Wazee Wetu$#

 Sadick Kilasi     April 21, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, NJOZI     No comments   

Thamani ya mwanadamu haitokani na utajiri alionao, bali uaminifu wake na uwezo wa kuwabadili wanaomzunguka katika mienendo chanya.  BOB MARLEY. 

Karibu mpendwa msomaji katika tafakari ya chumvi wazee wetu ambazo wametuachia katika maisha yetu ili iwe misingi ya maisha yetu.

Katika zama hizi za taarifa, zama za matokeo, zama za internet ukiwa huna pesa huwezi kusikika hata kama unapiga kelele kiasi gani. Watu hawasikii maneno, watu wanaangalia matokeo ya kile unachofanya.

Ukitaka watu wathamini unachokifanya basi waambie ya kwamba mimi napata mahela kiasi fulani, basi ukitaja mahela mengi basi utawavutia wengi sana.

Watu wanapenda sana miugiza katika maisha, wapo tayari kufanya lolote lile ilimradi wasikie ya kwamba flani aliingiza mamilioni kupitia hapa. Ni rahisi sana kuwavuta wengi njia hiyo.  Hivyo ndivyo hata watu huwatapeli watu pesa zao kwa tamaa yao.

SOMA:Sehemu Iliyo Jificha.

Mpendwa msomaji, thamani ya binadamu ni uwezo wa kubadili wanao mzunguka, haijarishi ni tajiri au maskini. Kumbuka kila mmoja ni barua ambayo inasomwa na jamii inayomzunguka. Nguvu ya sauti ya mtu ipo kwenye upekee wake na sio pesa.

Kama unauweza wa kufanya kitu na ukabadili matokeo hasi kuwa chanya basi hiyo ndo itakumbukwa sana na watu.

Katika jamii unaweza kukumbukwa kwa mambo mawili, matatizo uliyoyatatua na kwa jinsi ambavyo uliigusa jamii. Matatizo uliyoyatatua kwa mfano barabara, madaraja na mengine ambayo utayatatua katika jamii basi utabaki katika historia.

SOMA:Tunaona, Tunasikia, Tunashuhudia Tofauti.

Utakumbukwa kwa jinsi ambavyo umeigusa jamii ni pale ambapo itafanya vitu vya tofauti, kugundua kitu ambacho hakipo kabisa, utaigusa jamii kwa namna ambavyo umefanya. Upekee wako ndo unakufanya kuwa tofauti na wengine.

Wewe ni barua na mimi ni barua lazima tusomeke vizuri katika jamii, lazima tutumie vizuri uwezo wetu ili dunia iwe sehemu salama.

Endelea kutambelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, April 20, 2018

Binadamu Ameumbwa Akiwa Na Tabia Hizi.

 Sadick Kilasi     April 20, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji? Natumai upo salama kabisa. Hongera kwa ajili ya siku hii ya leo ambayo Mwenyezi Mungu katushindia mimi na wewe. Kuamka salama tukiwa hai yaani tunapumua basi kwetu ni ushindi mkubwa sana. Hongera sana.

Kwa kawaida kwenye maswala ya kiroho na vitabu vya dini wamemzungumzia mtu katika sehemu tatu, mwili, nafsi na roho. Haya ni maeneo matatu ambayo mtu huwa anayo. Wengi tunatambua mwili ni nini lakini changamoto ipo kwenye nafsi na roho. Vitu hivi vyote viwili vipo katika mfumo wa software na siyo hardware kama mwili ulivo.

Mwili ni sehemu ya mtu ambayo humwuvutia mtu katika mazingira ya mwilini. Mambo ya mwilini ni kama vitu vyote ambavyo unaweza kuona kwa macho. Tabia ya mwili ni kama raha, burudani, tamaa na mambo mengine ya kujiburudisha.

Nafsi ni sehemu ambayo imejaa mtu mwenyewe. Nafsi ndio asili ya mtu. Nafsi humuvutia mtu katika mambo ya ubinafsi wenyewe, ubinafsi, majigambo maarifa na mengine ya mtu.

SOMA:(SEHEMU YA KWANZA) Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu. (II) Kilichoandikwa Na Paulo C. Jong.

Roho yenyewe ipo tu inakutegemea wewe kwa sababu ya matendo yako. Roho inategemea tabia yako ipate uamusho. Kwenye roho kumejaa vipawa mbalimbali. Kila aina ya ushindi umejaa kwenye roho kwahiyo sisi hatuna budi kutafuta mambo ya rohoni.

Sasa kwa asili mtu anazaliwa katika hali ya ubinafsi anakuwa na tabia ya kuvuta kwake. Tabia hii inakuwa ndani, inamaana anazaliwa nayo. Mazingira ambayo anayakuta sasa baada ya kuwa na mwili ndio yanaanza kumjenga kimwilini.

Sasa mara nyingi mtu akipata kitu fulani ama pesa anaanza kuonyesha tabia fulani za ubinafsi, hizo ni tabia ambazo kila mmoja anazo kwa sababu kama una nafsi basi lazima tabia hii uwenayo. Vitabu vya dini vinasema hakuna mkamirifu.

Cha muhimu ni kuishi kiroho, kwenye roho ndio kwenye ukomavu.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Wakati ujao tutachambua vema juu ya mambo ya rohoni.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, April 19, 2018

Wakati, Kila Jambo Wakati Wake.

 Sadick Kilasi     April 19, 2018     USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeamka salama kabisa. Kama unasoma hapa basi sina budi kukupa hongera ya ushindi wa uhai ambao Mwenyezi Mungu katushindia mimi na wewe. Haijarishi upo katika hali gani kama unaweza kusoma japa,  basi tambua ya kwamba unaweza kubadilisha historia ya maisha yako au na jamii kwa ujumla. Wakati ndo huu sasa wa kubadilisha historia ya maisha yako. Wewe ni mshindi zaidi mshindi.

Kila jambo kwa wakati wake.

Kuna wakati jambo la faa lakini kuna wakati jambo hilo hilo halitafaa kutokana na wakati wake. Wakati wakati wakati,  fanya kwa wakati, kwa kuwa una wakati, utafika wakati, hutokuwa na wakati wa kufanya kwa wakati. Kauli ambayo niliinukuu kutoka kwa Mwalimu wangu wakati nikiwa darasa la saba.

Mpendwa msomaji, kuna wakati wa kupanda, kunawakati wa kuvuna, kuna wakati wa kusifia na kunawakati wa kutosifia, kuna wakati kufaliji na kunowakati wa kutofaliji. Kuna wakati wa kusikiliza na kunawakati wa kusema. Kuna wakati wa kuona na kuna wakati wa kutoona.

Ama kweli kusikia jambo ambalo hukupaswa kusikia ni hatari katika maisha. Kusema jambo ambalo hukupaswa kusema unaweza kuharibu kabisa jamii au maisha yako. Kusikia je? Ndiyo, kusikia jambo ambalo hukupaswa kusikia unaweza kuharibu maisha yako kabisa.

SOMA:Hivi Ndivyo Ambayo Unapaswa Kuendelea Kufanya Haijarishi Upo Katika Hali Gani.

Zawadi pekee ambayo tumepewa bure kabisa kila mmoja wetu katika maisha basi ni wakati lakini wakati unatakiwa kutumika vema kabisa, kimatendo, kimaneno, kufaliji, na kila jambo kwa wakati wake.

Unapowapa kitu watu kwa wakati husika basi unakuwa umefanya kwa wakati. Kila neno lazima litolewe kwa wakati na kila jambo kwa wakati.

Narudia tena mpendwa msomaji, fanya kwa wakati, kwa kuwa una wakati, utafika wakati, hutokuwa na wakati wa kufanya kwa wakati.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, April 18, 2018

Fanya Hivi Ili Ukusanye Vizuri Unachokusanya.

 Sadick Kilasi     April 18, 2018     NJOZI     No comments   

Moja kati zawadi nzuri ambayo tunayo katika zama hizi basi vyakukusanya ni vingi sana. Lakini moja kati ya changamoto tuliyonayo katika zama hizi ni kwamba vya kukusanya ni vingi kuliko muda tulionao.

Zama hizi huwezi kuishi bila kufanya chochote, lazima kuna kitu ambacho uwe unakifanya. Changamoto kubwa zaidi ya tamaa ya mwili ni kwamba mazuri ni mengi zaidi kuliko ulicho nacho. Kila unachikiona kinakuwa kizuri kuliko ulichoshikilia.

Hapa ndipo changamoto na matatizo yanapoanza. Kila kitu ni kizuri kuliko nilicho shikilia. Muda ni mchache wa kufanya kila kitu, kila kitu tunakitamani tukusanye, hatujui nini tufanye na nini tuache. Fursa ni nyingi kuliko kawaida, mambo ni mengi kuliko kawaida hatujui nini tukusanye na nini tuache.

SOMA:Falsafa Ya Kuishi Nayo Mwaka 2018.

Tunacho fanya sasa ni kugusa hiki na kuacha kile na kuacha. Mambo ni mengi ya kufanya kuliko kawaida, mpaka inafika jioni tumefanya mambo mengi sana kuliko kawaida. Hakuna kitu ambacho tumekipa kipaumbele na kusema hiki ndicho cha muhimu zaidi, hapana, kila kitu ni sawa maana naona napitwa na wakati.

Ya kukusanya ni mengi muno na tumebaki njia panda. Mpendwa msomaji, muda wa kuishi hapa duniani ni mchache sana. Kelele ni nyingi, ukitaka kuigiza kila kelele inayopigwa hutasikika, piga kelele yako katika maisha yako, kusanya kinachokuhusu achana na visivyo kuhusu.

Kila kona fursa, kila jambo linaonekana ni la muhimu machoni pako lakini siyo. Kwenye hii dunia sasa ni bora kukusanya kile ambacho ni cha muhimu na siyo kile ambacho unaona wewe ni ya muhimu. Machoni pa macho ya mtu kila kitu ni cha muhimu, sasa muda tulionao ni mchache, mambo ni mengi. Bora kuchagua machache na kufanya kuliko kukimbizana na kila kitu. Mshika mawili moja humuponyoka, je mengi? Atapoteza yote.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, April 17, 2018

Kumbuka Mambo Haya Kama Tabia Ya Mtu Wako Wa Karibu Huipendi.

 Sadick Kilasi     April 17, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Moja kati ya shida kubwa ambayo inawasumbua wengi katika maisha basi ni mahusiano. Mahusiano kati ya mtu na mtu imekuwa changamoto kubwa sana. Watu wengi kwa sasa wanakosa furaha tu eti kwa sababu ya ndugu yake au mtu wake wa karibu.

Changamoto inaanza tu pale mtu akifanya tofauti na ilivyo tarajiwa. Waajili wengi sasa wanapata shida kubwa kwa sababu hili tatizo la kupata majibu au utendakazi tofauti nje ya alivyo taraji. Unakuta anayeajiliwa mwanzo anaonyesha tabia njema lakini baadae unao kama anabadilika vile, tofauti na mwanzo. Ndugu kunakitu ambacho kinakuwa fumbo kubwa kwao kwa maana wanachoona si ulichotegemea kukiona. Alichokuwa anategemea ni utendakazi mzuri ambao utaleta matokeo mazuri. Kumwamini mtu kupita kiasi.

SOMA:Usiwanyanyapae Watu Kwa Sababu Wanayofanya Ni Maovu.

Changamoto hii imewakuta hata watu wa kawaida ambao ni ndugu wa damu. Muda mwingine anaweza akawa mzazi kabisa, labda kuna watoto wawili wanaosoma mwingine anafanya vizuri darasani na mwingine hafanyani vizuri darasani, hapo inakuwa changamoto. Mzazi anampenda anayefanya vizuri darasani na mwingine anakosa upendo. Utofauti wetu wa tabia umekuwa changamoto kubwa sana katika maisha. Tumekuwa tukiishi kama sukari badala ya kuwa kama chumvi.

SOMA:Tunataka Kuwa Kama Sukari Kwa Watu Si Kama Chumvi.

Tatizo kubwa ni kwamba tunavutia watu badala ya kuwa halisia. Watu hatujitambui sisi akina nani. Wengi tumekosa kuwa na upendo na watu badala yake tumekuwa na mapenzi na watu au kazi zetu.

Mpendwa msomaji, watu hawa wawili wangetambuana vema, changamoto kama hizo zisingekuwepo kabisa. Hata wale wanao ajili bado hawachukui muda wa kujifunza namna tabia ya watu walivyo. Mwisho wanaishia kulaumu ya kwamba watu hawa hawabadiliki tabia zao. Wanachoka kabisa na kuona kwamba wafanyakazi wote hawafai kabisa.

Ndugu, tumelelewa tofauti, tunaahiba tofauti, tabia tofauti, uelewa tofauti, kila kitu tofauti. Usitake kila mmoja awe kama wewe ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Chukua muda kumchunguza mtu kabla ya kumpa nafasi, kwa sababu  wakati mwingi sana tunatumia hisia na wakati mdogo sana tunatumia akili. Wakati mtu anashida anatumia akili lakini mwisho anajikuta anaangukia kwenye hisia za mwili. Mwili unapenda kujifurahisha wenyewe. Moyo u radhi na mwili ni dhaifu.

Punguza kila kitu kutaka kiwe kama unavotaka wewe. Tumia falsafa ya chumvi yaani usawa. Kubali matokeo na uache kuhukumu wengine haraka. Mtoto asipo fanya vizuri darasani sio mbaya hajafeli kuishi anaishi maana elimu ya shuleni nayo ni kujitaidi tu kuishi. Maisha ni kuishi.

Mpendwa msomaji, kumbuka kila mmoja anaweza kubadilika, usihukumu usije ukahukumiwa.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano 0687000768 au sadikila65@gmail.com.



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, April 16, 2018

(SEHEMU YA TATU) Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa HaKi Ya Mungu (II).

 Sadick Kilasi     April 16, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Moja kati ya eneo ambalo watu wengi wanekuwa wakipata shida sana katika maisha haya ni eneo la kiroho. Wale ambao tayari wamegeuka, na wapo makanisani wanapata shida sana kwa sababu hawaelewi vizuri namna ya kupata haki ya Mungu.

Kitabu hichi cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu, ni kitabu ambacho kinatoa msaada namna injili ya Kristo Yesu inaweza kuwa msaada katika hali kama hii. Mwandishi amejaribu kuchambua vema kabisa kitabu cha Warumi ambacho kimeelezea namna ya kupokea injili ya Maji na Roho.

Karibu Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa mambo haya ninayokushirikisha niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hichi. Ombi langu kwako rafiki yangu msomaji, mambo haya ya kiroho yanahitaji utulivu sana, kwahiyo unaposoma unapaswa kuwa makini na mchambuzi mzuri ukitumia BĂ­blia.
Soma Hapa sehemu ya pili ya uchambuzi huu.

Karibu nikushirikishe mambo hayo niliyojifinza katika seheme ya tatu.

1.Sisi hatuna dhambi japokuwa tunaonekana japokuwa tunaonekana ni wenye dhambi. Sisi hatuna dhambi ingawa tunatenda dhambi. Kwa hiyo tunaweza kuwasaidia watu wengi sana kwa injili ya Maji na Roho. Hili ni fumbo la Kristo na siri ya Ufalme wa mbinguni.

2.Wanadamu wote waliridhi dhambi kutoka kwa Adam na Hawa. Kwa asili tulizaliwa kama uzao wa dhambi. Asili ya dhambi inalidhiwa kutoka kwa wazazi wetu.

3.Kuna aina kumi na mbili za dhambi ambazo tunaziridhi kutoka kwa Adam na Hawa, uzinifu, umalaya,  uuaji, jicho ovu, wizi, tamaa, ubaya, uovu, ufisadi, chukizo, majivuno na ujinga. Dhambi hizi zipo ndani ya miili yetu tangu tunazaliwa.

4.Kuna wakristo wa aina mbili kanisani wale ambao wanafuata mambo ya mwili na wale wanaofuata mambo ya rogo.
  (Warumi 8:9)

5.Mkristo aliyekombolewa hakika anafuata mambo ya roho na si mwili.
   Warumi 8:9$10-11).

6.Tumefanyika wenye haki mara mija na wala si kwa hatua baada ya hatua. Mungu ametufanya wenye haki. Hata kama tkijitaidi kwa matendo yetu hatuwezi kwa miili yetu hii.
  (Warumi 8:29-30).

7.Hakuna anayeweza kututenganisha na upando wa Mungu. Ikiwa Mungu yupo upande wetu nani ambaye anaweza kwenda kinyume nasi. Yeye asiye mwachilia  mwana  wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote.
   (Warumi 8:31-39).

8.Ukombozi ambao Mungu ametupatia ni lazima tukili kwa Yesu Kristo alitumwa kuja ulimwenguni kwa mujibu ya mapenzi ya Mungu Baba, lakini pia lazima tikili kuwa Yesu Kristo alichikua dhambi zetu zote katika mwili wake kupitia ubatizo wake katika mto Yordani na lazima tukili kuwa Yesu alisurubiwa kwa ajili yetu na kisha akafa akafufuka

9.Tunapokuwa tunaumia mioyoni mwetu ni Roho ambaye huwa anaugulia kwa sababu ya matendo yetu na mawazo yetu.

10. Tunapokuwa katika sara Roho Mtakatifu hutisaidia kuomba, maana yeye anafahamu kila kitu katika akili zetu. Kwa hiyo Roho Mtakatifu anafanya maombi kwaajili ya watakatifu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.

11.Tunapopokea injili ya maji na Roho na kwa kuamini, tunapokea katika injili ya maji na Roho na Roho Mtakatifu kama kalama au kipawa.
   (Matendo 2:28).

12.Mungu anatupatia kalama ya Roho Mtakatifu ili kwamba aweze kutiongoza sisi kuishi kwa mujibu wa mapenzi yake. Haya ni mapenzi ya Mungu Baba yetu.

13.Roho Mtakatifu na maandiko hayawezi kutenganishwa na Roho Mtakatifu na Mwamini hawawe kutenganishwa. Hii ndio sababu ya mahusiano ya Roho Mtakatifu wa kanisa na mwamini wa Mungu. Na Mungu utatu ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

14.Ikiwa utakuwa upokea haki ya Mungu, Roho Mtakatifu atakuongoza katika maisha yako. Roho Mtakatifu ananás ndani ya mioyo yetu. Tutapewa kuongozwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu.

Asante sana mpendwa wangu na rafiki yangu unayefutilia uchambizi huu mzuri. Ninatalaji kwamba mambo haya yatakuwa ni msingi mpya na mwongozo katika maisha yako hasa ukienenda katika kuyatafakari. Roho Mtakatifu ataendelea kukufunulia zaidi na zaidi.

Karibu tena katika mwendelezo ujao na kama unaswali lolote usisite kuniuliza kwa kutoa maoni au kunitumia ujumbe katika Mawasiliano yangu. Hakika ninakuwa na furaha sana ukiniuliza chochote au kunishirikisha zaidi ulichojifunza zaidi.
Asante sana.

Wako Sadick Jilani.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, April 15, 2018

Hii Hapa Ni Njia Nzuri Ya Kujifunza Zaidi na Zaidi.

 Sadick Kilasi     April 15, 2018     NJOZI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI?  Natumai umeamka salama kabisa. Hongera kwa ushindi mkubwa wa kuiona siku hii ya leo, siku mpya, mimi na wewe hatuna budi kushukuru Mwenyezi Mungu aliyetujalia kuiona siku hii ya leo. Hakika sisi ni washindi zaidi ya washindi.

Karibu katika makala haya ya leo ili tujifunze kwa pamoja lile nililo kuandalia rafiki yangu.

Kati ya watu ambao unawajua vizuri sana na uhakika unamjua vizuri basi mtu huyo ni wewe mwenyewe. Waweza ukawa hujijui kiundani sana sana lakini sidhani kama unawajua watu wengine zaidi unavojijua wewe mwenyewe. Kujijua maanake nini? Ni kufahamu vema wapi upo bora na wapi haupo bora. Sasa ukisema namjua mtu fulani kuliko unavojijua wewe mwenyewe, wajidanganya rafiki yangu, kila mtu anajitambua mwenyewe vizuri kabisa. Hasa unapokuwa bafuni unaoga, wajitambua vizuri sana wewe.

Siku zote ukitaka kujengeka vizuri kama unataka kuwa bora zaidi ya hapo basi tafuta udhaifu wako uko wapi na mapungufu yako ili ujijenge vema. Kama wewe ni mbinafsi na ukajitambua ya kwamba mimi ni mbinafsi basi hilo kwako si tatizo tena, cha muhimu ni kujifunza tabia mpya na kuondoa ubinafsi.

Watu wengi hawalitambui hili na ndo toba yenyewe. Mwenyezi Mungu katuwekea sheria juu yetu ili tuijue dhambi yetu ikisha tutubu kwa kugeuka moja kwa moja sio kila siku kufanya dhambi hiyo hiyo na kuomba toba, hapana. Sheria imewekwa ili tujitambue sisi ni akina nani na ikisha tugeuke upande mwingine.

Hivi ndivyo tunaweza kukua na kuwa bora zaidi na zaidi, kutumia udhaifu na kujiboresha zaidi na zaidi. Watu wano jiona wamekamirika basi hao wana kiburi na majivuno. Kila mtu anampungufu yake, tunatumia mapungufu ili kuweka ubora na tunatumia mapungufu ili kuwa bora zaidi. Walio kamirika wanapatikana makabulini.

Fikiria kitu kimoja kama kila kitu kingekuwa sawa ubora usinge kuwepo wala tusingekuwa na haja ya kujiboresha.

Ukawe na siku bora rafiki na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Nguvu Ya Matamshi.

 Sadick Kilasi     April 15, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Mara nyingi kuna maneno ambayo huwa tunajinenea wenyewe ama kuwasemea wengine maneno ambayo hayafai kabisa. Maneno kama natafuta pesa ya kula, mimi ndivyo nilivyo, sisi ndo asili yetu na kauli nyingine mbalimbali huwa zinatuharibu kwa kiasi kikubwa sana bila ya sisi wenyewe kujijua.
Soma:Huu Hapa  uwanja Ambao unaweza Kufanya Utakalo.
Mabaliko ambayo yanatokea pole pole sio rahisi kuyaona haraka kwani ni kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa macho. Kadili muda unavokwenda mabadiliko haya hujitokeza nje kimwili, ambayo unaweza kuyaona kwa macho yako mwenyewe. Ukweli ni kwamba mabadliko yanayotokea ndani sio rahisi kuelewa kwa haraka, eti kwa sababu nimesema, hivo hivo tu mambo yanakwenda, inawezekana kuathiri afya yangu? Ndiyo, matamshi yana nguvu sana, akili ndiyo ya kwanza kabisa kuathirika harafu baadae mwili huonyesha udhaifu huo. Kwa sababu, mwili sio hali (software) ni kitu au mata (hardware) matokeo yatakuja kama ugonjwa. Tunaanza kukimbizana huku na huko kwa sababu ya maneno tu uliyo jinenea mwenyewe. Ukienda kupima kwa wataalamu wa afya watakwambia unaumwa kansa au ugonjwa mwingine kwa sababu wao hawajui ulicho kifanya huko nyuma watakwambia kula chakula hiki na hicho, wewe unajua tatizo ni chakula kumbe maneno.

Maneno huwa yanaonekana yananguvu sana yanapotoka kwako na kwenda kwa mwingine au yatoka kwa mwingine na kuja kwako lakini unapojinenea mwenyewe nguvu yake huwa haionekani. Ukitaka kujifunza hili vizuri jifunze kupitia laana, laana ni maneno ambayo yanaweza kuharibu maisha yako kabisa ni mwisho ukapatwa na magonjwa ambayo hayaeleweki kwa sababu ya maneno tu.

Mpendwa msomaji, kusema kitu ambacho hukupaswa kusema kinaweza kuharibu maisha yako kabisa. Tatizo ni nini kutokujali vitu vidogo vidogo, tambua mipaka yako, usijinenee maneno ya hovyo mwenyewe na wala usiwanenee wengine maneno mabaya. Ukweli ni kwamba hatujui ni kwa kiasi gani maisha yao yanaharibikiwa. Tunene maneno ya USHINDI kila siku.

Ukawe na siku bora rafiki yangu na endelea kujifunza kupitia blogu hii tupo kwa ajili yako.

Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, April 13, 2018

Tunatakiwa Kuwa Kama Chumvi Si Kama Sukari.

 Sadick Kilasi     April 13, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Sukari na chumvi ni viungo ambavyo vinatumika kufanya kitu kama kilikosa ladha basi kiwe na ladha. Viungo hivi ni vya muhimu sana katika matuzi yetu.

Mpendwa  msomaji, tunatakiwa kuwa kama chumvi sio kama sukari. Maisha yetu tunatakiwa kuwa kama chumvi si kama sukari. Mbona sukari ni tamu kuliko chumvi? Ni kweli kabisa sukari ni tamu kuliko chumvi lakini kunautofauti kiutendaji.

Chumvi ni kiungo cha ajabu sana, pamoja na kwamba ukiweka kwenye mboga, chakula kinakuwa kitamu lakini huwezi kuila ikiwa peke yake, lazima uweke kwenye chakula ambacho kinahitaji kiungo hicho ndiyo utakula vizuri. Lakini sukari haipo hivo unaweza kulamba hata kama hujaweka kwenye chakula chake.

Katika maisha, mahusiano ni kitu cha muhimu hata kama wewe una hela kiasi, au unaakili kiasi gani lazima uhitaji wengine wenzako wenye utofauti na wewe ili uwasilishe ulicho nacho.

Ufanyaji kazi wa chumvi ni wa usawa lakini ufanyaji kazi wa sukari ni wa kuvutia zaidi. Ukizidisha chumvi kwenye chakula ukweli ni kwamba huwezi kula lakini sukari ni tofauti unaweza ukala hata kama umezidisha, kwa sababu hata kama ikiwa peke yake unailamba.

Dunia inaendeshwa kwa usawa kama chumvi, kuna sehemu unapaswa usizidi. Ukiona unatamani kufanya kila kitu, unataka kila mmoja akusikilize wewe basi tabua wewe unataka kuwa sukari, unavuta na visivyo vutika. Mpendwa rafiki, usawa ndo furaha yenyewe sasa, ukikosa furaha maisha yatakuwa magumu. Ubongo utafeli kufanya kazi kisawa sawa, hali yako itakuwa tete, utajitaidi kuishi tu maisha lakini hutaishi maisha. Cha ajabu ni kwamba mwili wote ni chumvi tupu yaani miili yetu hii. Pamoja na kwamba sukari ni tamu sana na kuvutia kwake kote sukari huleta magonjwa lakini chumvi haipo hivo.

Ukawe na siku bora ukitafakari ufanyaji kazi wa chumvi na sukari. Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, April 12, 2018

Huu Hapa Ni Uwanja Ambao Unaweza Kufanya Utakalo.

 Sadick Kilasi     April 12, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI     No comments   

Katika maisha yetu ya hapa duniani ambayo ni mapito yetu kitu peke ambacho tunaweza kumiliki moja kwa moja ni fikra tu. Fikra ni uwanja ambao ni mkubwa na mpana ambao unaweza ukafanya lolote bila kuzuiwa na yeyote.

Vitu vingine vyote tumepewa tutawale na tuendeleze lakini si vya kwetu, muda ukifika vikitaka kuondoka vinaondoka na huwezi kuzuia. Katika mazingira ya nje unaweza kuzuiwa na lolote, lakini kifikra hakuna kinachoweza kukuzuia kufanya unalotaka.

Mwili unaweza kukataa na ukasema mimi ninaumwa lakini fikra yako isipo kubali hutakuwa unaumwa. Uwanja mpana ambao unaweza kufanya lolote ambalo unataka ni uwanja wa fikra. Huko hakuna mtu ambaye anaweza kukuzuia maana haoni wala hasikii, ukitoka nje mwili unaweza kukataa, unaweza ukawa mwili wako au wa nwingine.

Mpendwa msomaji,  tumia fikra zako sahihi ndani mwako ili ukitoka nje uwe tunda ambalo linapaswa kuliwa na sio sumu.

Ukawe na siku bora kabisa rafiki yangu, endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, April 11, 2018

Usiwanyanyapae Watu Kwa Sababu Wanayofanya Ni Maovu.

 Sadick Kilasi     April 11, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Moja ya tabia ambayo watu wengi ni wa hanga wa tabia basi ni kuwanyanyapaa watu wenye tabia ambayo sio nzuri. Binadamu tumejaa ubaguzi sana, tukipata nuru basi tunaona ya kwamba walio kwenye giza si watu tena.

Watu wengi ambao wameokoka ni watu wa kuwanyanyapaa wengine wale ambao bado hawajamjua Mungu. Lakini je ni kweli ndivyo inavyotakiwa? Sio kweli kwa sababu kama wewe ulibadika basi na mwingine huyo anaweza kubadilika.

Hatuhitaji kuonyesha ya kwamba kufanya mema si jambo ambalo linapaswa kufanywa na kundi la watu wa aina fulani tu hapana, lazima tuwe mifano kwa wengine ambao bado hawajabadilika.

Mpendwa msomaji, usiwe kama yule mfarisayo dhidi ya yule mwandishi. Aliyemwambia Mungu wakati anasali ya kwamba mimi si sawa na huyo, mimi nafunga, natoa mafungu ya kumi na nawajiba katika maswala yote ya dini. Rafiki yangu, tukiwa hivi tutaangamia lazima tuwe barua njema kwa wengine.

Upendo ni swala la muhimu sana,  upendo utaondoa yote yaliyo ya giza kwetu, tuwapende walio gizani ili nao waige kutoka kwetu.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, April 10, 2018

Neno kutoka Kwa Sadick Kilasi.Kufikiri Kunaleta....

 Sadick Kilasi     April 10, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI     No comments   

Ukiwa unatumia akili vema kwa kufikiri ukweli ni kwamba utajisikia kuwa na furaha. Kunatofauti kati ya kufikiri na kuwa na mawazo, mawazo yanaondoa furaha.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, April 9, 2018

Sehemu Iliyo Jificha.

 Sadick Kilasi     April 09, 2018     USWAZI TRICK     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai upo salama kabisa. Hongera kwa kuiona siku hii ya leo, siku mpya ambayo mwenyezi Mungu katujalia kuiona, hatuna budi kushukuru yeye.

Karibu katika makala ya leo msomaji wangu, nikushirikishe yale ambayo ni muhimu kuyajua na tujifunze kwa pamoja.

Katika dunia hii hapa ya matokeo chochote ambacho unakiona kwa macho yako au kukisikia basi kuna sehemu ambayo imejificha. Sehemu ambayo imejificha ni sehemu ambayo inapelekea matokeo ambayo tunayaona. Tukio lolote ambalo unaliona linasababu iliyopelekea tukio kuonekana, na hiyo ndo sehemu iliyo jificha.

Unaweza ukajiona upo sehemu fulani ambayo umeifikia haijarishi ni sehemu nzuri au mbaya, kumbuka kuna hatua kadhaa ndogo ndogo ambazo ulizipiga ambazo zimepelekea uwe pale ulipo. Hizi hatua ndogo ndogo inawezekana ukawa ulikuwa unaziona kwa kujali au kwa kutojali. Mapito yako ni sehemu iliyojificha.

Kila kitu hapa dunia kinasemu iliyo jificha, kuna sababu zilizo pelekea kuwa pale kilipo. Ukiuona mti umesimama vema basi tambua ya kwamba kuna mizizi ambayo imefanya mti ukasimama. Basi si mizizi tu lakini kuna kitu ambacho kimefanya huo mti na umekuwa vema.

Sasa unaweza kujiuliza kwanini tujifunze sababu?  kwanini tujifunze sahemu iliyo jificha? Kwa sababu tulio wengi tunastukia maisha. Mpendwa msomaji, katika maisha kuna aina mbili za mitazamo wapo watu ambao wanapambana na matokeo na wapo watu ambao wanapambana na sababu, sehemu iliyo jificha.  Ukiwa unapambana na matokeo ukweli ni kwamba maisha kwako yatakuwa magumu sana kwa sababu hujui ni kipi ambacho kimepelekea yale matokeo. Ni sawa sawa na kukazana kuziba chemichemi ya maji yanayo bubujika kutoka chini ya ardhi yatakusumbua kweli kweli.

Sasa wana Jiko La Ushauri tunatakiwa kapambana na sehemu iliyo jificha. Sababu zilizopelekea kitu hicho kuwepo. Mfano mzuri ambao naweza kukuonyesha ni kwamba, mnaweza mkakutana na mti akakutukana au kutoa kauli ambayo hujaielewa vizuri, ukiwa na mtazamo wa sehemu iliyo jificha hutapambana na ile kauli utambana na kipi kimepelekea atowe haya maneno makali, hapa utakuwa unapambana na sababu labda mwisho unaweza kugundua ya kwamba huyu alikotoka si salama, kwa hiyo utamsamehe bure. Lakini ukiwa ni wa kupambana na matokeo, kauli ya kwanza ambayo utamwambia ni, unanitukana mimi, kwanini unanitukana na hapo ndipo utakuwa uwanja wa vita.

Hatuwezi tukawa tunastukia maisha. Chochote tunachopitia lazima kiwe na ubora tukipe nidhamu kubwa. Matatizo mengi sana yanasababishwa na mtazamo wa kupambana na matokeo. Ukiangalia nchi ambazo zinapambana vita, wanapigana kwa mtutu kutafuta amani. Sio lahisi kupata amani.

Pambana na hali sio mtu.

Ukawe na siku bora rafiki yangu, nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, April 8, 2018

Fanya Hivi Ili Maisha Yako Kuwa Bora Zaidi Na Zaidi.

 Sadick Kilasi     April 08, 2018     MAHUSIANO, NJOZI, USHAURI, USWAZI TRICK     No comments   

Mtu yeyote yule ambaye yupo sawsawa na anajitambua vizuri basi huyo anatambua tayari udhaifu wake. Kila mtu anaudhaifu wake. Ili maisha yako yawe bora basi lazima utambue udhaifu na uimala wako uko wapi.

Tumeumbwa namna hii ili kila mmoja awe msaada kwa mwenzie. Utofauti huu wa uimala na udhaifu ndiyo unaoleta ubora katika mahusiano yetu.

Ili mtu uwe bora zaidi na zaidi basi siyo mbaya sana ukawa mtu wa kujiangalia wapi udhaifu wako ulipo ikisha ukashughulikia vizuri. Udhaifu wako utakufanya kuwa mkomavu kama itaukubali na kuufanyia kazi.

Watu ambao hujiona wamekamilika huwa hawana tabia ya kujichunguza wenyewe, watu hawa hufikilia wenyewe tu na kujiona wapo sawa kwa kila kitu. Matatizo yakiotekea ni watu wa kuwalaumu wengine na kutafuta majibu ya matatizo yao nje yao. Watu hawa siku zote ni watu wa sababu tu.

Mpendwa msomaji, watu wale wenye mapungufu huendelea kusonga mbele kwa sababu wao wamejitambua kwamba wanamapungufu kwani walio wazima hawahitaji daktari na ili upande mlima sharti uwe bondeni, aliyopo kileleni amefika hahitaji kusonga mbele.

Maisha yatakuwa sawaswa kabisa, maisha yatakuwa bora kabisa, ukiwa mtu wa kuangalia wapi upo sawa na wapi haupo sawa, huwezi kuboresha kama huoni matatizo, unaona sawasawa tu.

Kila mmoja anampungufu, angalia mapungufu yako kwenye mahusiano, kwenye kazi, halafu boresha, utakuwa bora siku baada ya siku. Kwenye hii dunia hakuna ukamirifu, kila kitu kinahitaji kuboreshwa zaidi na zaidi na ndio maana Mungu alituumba ili tuendeleze na kutawala. Usije ukajiunua kwenye hii dunia, utashushwa haraka sana. Kama bado unapumua basi bado hujafika, kumbuka ya leo sio ya kesho.

Ukawe na siku bora rafiki yangu. Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, April 7, 2018

Dunia Inatufundisha Kutegemea.

 Sadick Kilasi     April 07, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa ushindi mkubwa ambao Mwenyezi Mungu kakushindia. Mimi na wewe rafiki yangu hatuna budi kumshukuru yeye na kurudishia sifa.

Katika mambo yote au vitu vyote ambavyo unaweza kuviona kwa macho ya kawaida ya nyama au vitu ambavyo unauwezo wa kuviona kwa macho yako siyo vya kwako. Mimi na wewe hatuna kitu ambacho tunamiliki moja kwa moja tumepewa tutawale, tuendeleze na kusimamia.

Labda nikufafanulie vizuri ni kwamba chochote ambacho unaweza kutamka kwamba hiki ni changu basi hicho siyo chako, umepewa utawale kwa muda tu. Sasa unaweza kusema, hata mwili wangu siyo wa kwangu, Ndiyo siyo wa kwako umepewa utawale kwa muda tu. Kwa sababu wewe huwezi kuzuia kifo chako mwenyewe na wakati wa kuondoka mwili unakufa na tunasema mwili wa marehemu fulani. Wakati nwingine waweza kujiuliza, hiki ni cha kwangu, mkono wangu, mwili wangu, Je mimi niko wapi?

Tulipoumbwa kwenye hii dunia, tuliumbwa kwa uwezo wa ajabu, tuliumbwa katika uhalisia na asili. Kiuhalisia sisi tumekamilika kabisa lakini katika asili yetu tunahitaji utegemezi. Mpendwa msomaji dunia inatufanya kuwa tegemezi.

Dunia inatufanya kuwa tegemezi sana kwa sababu katika asili tunamapungufu kwamba tunahitajiana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu hatujakamilika. Lazima mahusiano yawepo ndipo ubora uwepo. Huyu anamapungufu ya hiki na yule hiki na yule hicho.

Dunia inakufanya kuwa tegemezi kwa kwenda shuleni, kwenda kutibiwa mahali au hospitalini, kusoma vitabu, kusoma makala hizi ninaziandika na chochote kile ambacho unakinunua kwa fedha.

Mpendwa msomaji, tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, inamaana tunauwezo mkubwa sana wa kufanya lolote lile. Ni kweli tunahitaji msaada kutoka kwa wengine lakini inatupasa kufika wakati nasi au kila mmoja ajiwekee kikao chake peke yake ndani kwake akiwa na yeye. Kwa sababu chochote ambacho dunia inafanya usipokuwa makini ni kwamba inakufanya kuwa tegemezi zaidi na zaidi. Hatujaja kusavaivu au kujitaidi kuishi katika dunia hii tumekuja kuishi lazima tujiwekee vikao na sisi wakati wa jioni, ujiulize maswali peke yako na ujijibu mwenyewe.

Muhimu ambalo ninaweza kukwambia rafiki yangu, tumtafute Mungu, wapi? Kwenye vitabu vya dini. Vitabu vya dini vimeandikwa katika mfumo wa kila mtu kujitegemea, ni vitabu ambavyo vibahitaji utulivu kwenye kusoma. Tukazane kuutafuta uhalisia wetu badala ya kukazana kuishi nje kwenye asili. Mpendwa msomaji, vikao na sisi ni kitu cha muhimu sana, soma sana, fanya kila uliwezalo lakini mwisho uwe na wewe.

Endelea kujifunza kwa kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI na nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu uwafikie wengi maana naamini makala hii itakuwa msaada kwa wengi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, April 6, 2018

Acha Kufanya Kitu Hiki Mapema Kabisa Kama Unataka Kukua.

 Sadick Kilasi     April 06, 2018     HEKIMA ZA WAZEE, MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni lahisi kukwepa majukumu yako lakini ni ngumu sana kukwepa hatma yako. Kati ya tambia ambayo unapaswa kuiacha mapema basi ni tabia ya kusingizia. Unaweza ukafikiri unaposingizia unamtupia mzigo mtu mwingine lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kubeba mzigo wa mwingine.

Unaweza kukimbia sasa majukumu yako lakini hatma yako nini? Ni maisha magumu ya mateso na manung'uniko. Wanao bebeshwa mizigo ya watu siku zote wanaishia kuwa washindi na wenye furaha. Wangalie watu ambao wamefanikiwa kisawa sawa siku zote ni watu ambao wamebeba majukumu na hatma za watu wengi. Mwangalie mtu kama Raisi, amebeba majukumu ya watu wa nchi nzima na anategemewa na wananchi wake. Mwangalie mtu kama walinzi wa kulia wa viongozi, utakuta kiongozi mwoga kuliko mtu ambaye maisha yake yapo hatalini zaidi.

Mara nyingi tunajaribu kukimbia majukumu yetu kwa kuwatwika lawama watu wengine. Mfano mdogo tu, migogoro midogo midogo, mtu anaweza kukwambia umenikosea lakini ukakataa moja kwa moja kwamba mimi sijakukosea. Rafiki yangu, huko ni kukwepa majukumu, hata kama kwa mtazamo wako unaona ya kwamba hujamkosea. Mtu hawezi kabisa kugombana peke yake au kujihukumu peke yake bila mtu mwingine kuwepo, kwa hiyo lazima uwe tayari kukubali ya kwamba wewe ni chanzo cha yeye kujisikia vibaya. Ukiwa tayari kuchukua majukumu ya wengine utakuwa mkomavu haswa, wengi watafuta kuwa karibu na wewe tena watajifunza kutoka kwako.

Mpendwa msomaji, wengi tunapenda mafanikio makubwa, wengi tunapenda kuwa washindi kati yao, wengi tunataka kuwa wakubwa kati yao lakini hii tabia ya unyenyekevu hatuna kabisa, kukubari kuchukua matatizo ya wengine hatuwezi kabisa, tumekuwa walalamishi siku zote na watupia lawama, ubinafsi ni mbaya kwelikweli. Ukitaka kuwa mkubwa kwao lazima ukubali kubeba lawama na kutimika kwao, ukubwa ni shimo la jalala.

Wakati wote mtu anapokwambia ya kwamba wewe ni sababu lazima ukubali kuchukua majukumu, lazima uwe mtu wa kuuzima ubaya kwa wema. Nuru iliishinda giza,  ukweli uliushinda uongo tayari, kwahiyo hatma yako itakupa ushindi.

Usiwe mtu wa kutafutatafuta sababu siku zote, kuwa mtu wa kukubali makosa yako na majukumu yako. 

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, April 5, 2018

Hivi Ndivyo Ambayo Unatakiwa Kuendelea Kufanya Haijarishi Upo Katika Hali Gani.

 Sadick Kilasi     April 05, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Kuna msemo ambao unasema,  ni rahisi sana mwanadamu kurudia Mungu wakati ambao ana matatizo. Ni rahisi pia kwa mwanadamu kutolea Mungu matoleo wakati akiwa na vya ziada.

Tunatakiwa kuendelea kuwagusa wengine haswa wakati tukiwa na matatizo, tunatakiwa kufanya kilicho sahihi wakati ambao sio sahihi.

Kuna wakati ambao huwa tunajiona wanyonge sana, kuna wakati ambao huwa tunahisi kabisa sisi hatufai kumwinua mwingine kwa sababu ya mapito yetu lakini kwetu sisi huu ndo wakati mzuri kabisa. Ukiwa unamsaidia mtu kwenye pito ambalo wewe mwenyewe umepitia basi utamsaidia kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu sana.

Wakati ambao unahisi sio sahihi kuwashika mikono wengine ni wakati ambao ndio sahihi kuwashika mikono hao, haijarishi upo katika hali gani lazima uendelee na kazi ya kuwagusa na kuwa baraka kwa wengine. Usiseme sijisikii kufanya hivo endelea kusonga mbele si kwa sababu unajisikia ni kwa sababu ni lazima kufanya hivo.

Kuwa baraka kwa wengine katika wakati usio faa kabisa, kuwa baraka kwa wengine kwa wakati ambao unafaa kabisa. Kutenda kilicho sawa hakuna wakati, wakati ambao unafaa kutenda sawasawa ni wakati wote.

Usisubili wakati ambao unacho ndo utende sawasawa, hapana, watu wanasema heri mtu mmoja anayekusema mabaya wakati mgumu kuliko watu maelfu wanao kupigia makofi wakati umefanikiwa. Wakati ambao unafaa ni kuendelea kufanya kwa usahihi wakati wote.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Usimruhusu Adui Huyu Akutawale.

 Sadick Kilasi     April 05, 2018     USWAZI TRICK     No comments   

Kawaida kuna watu wa aina mbili, watu wa mtazamo chanya na watu wa mtazamo hasi. Watu wote hawa ni watu ambao wamechagua wenyewe mitazamo yao.

Sasa mimi naongea na watu wa mtazamo chanya, watu ambao hawataki kabisa kuishi mitazamo hasi hao ndo naongea nao sasa kupitia makala hii. Kama wewe ni mmoja wao basi endelea kusoma hapa au la kama ulikuwa hujui kama mtazamo ni kuchagua basi endelea kusoma hapa.

Moja kati ya adui mkubwa kwa watu wenye mtazamo chanya basi mtazamo hasi. Mtazamo hasi huja haraka sana na kuharibu kabisa mtazamo wako chanya. Mtazamo huu huja pale ambapo unahisi umefeli kufanya jambo fulani.

Unaendelea kuiharibu siku nzima kwa kitu kidogo tu. Unaweza ukawa unafanya kitu cha kawaida kabisa lakini ukiruhusu tu na kusema kwamba siwezi basi utajiona kwamba wewe hufai kabisa. Mungu anakuwazia mema, ajionavyo mtu ndani yake ndivyo alivyo. Hivyo ndivyo ilivyo.

Mpendwa msomaji, usiruhusu adui huyu awe kikwazo katika maisha, usimruhusu adui huyu akunyang'anye furaha yako, kuwa mjanja rafiki yangu, wewe ni mshindi. Lazima ujiambie mimi nina mtazamo chanya.

Mtazamo ni utajiri mkubwa sana katika maisha yako. Ishi mtazamo chanya, chagua huu utajiri.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, April 3, 2018

Fanya Kitu Hiki Ili Watu Wakuelewe Haraka.

 Sadick Kilasi     April 03, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ukitaka mtu akuelewe haraka kwenye kizazi hiki cha leo usimwambie maneno hata kuelewa kabisa. Watu hawaelewi kwa maneno watu wanataka matendo.

Watu wapo tayari kuiga hata kama jambo hilo ni la hovyo lakini hawapo tayari kufuata maelekezo mazuri. Kumbadilisha mtu huhitaji kumpa maelekezo bali anachotaka yeye ni kuiga kutoka kwako yaani akufwatishe wewe.

Watu wengi hatupendi kabisa kuchukua hatari, mara zote tunachotaka ni kuwa ni kuwa salama au tujihisi tupo salama. Yaani hata kama yupo mahali hayarishi lakini yeye anachotaka ajihisi yupo salama. Hakuna mtu ambaye anapenda kuwa katika eneo hatarishi na ndiomaana ni ngumu sana mtu kuanzisha jambo jipya kwa sababu ya watu wengi kuogopa kuchukua hatari na watapoteza usalama wao.

Ni vizuri zaidi kama unataka kumbadilisha mtu kutumia vitendo zaidi, mfano, umegombana na mtu, unajua kabisa hapa chanzo cha matatizo ni yeye na sio wewe, huhitaji kumwambia mimi mimi sijakosea hawezi kukuelewa kabisa, kitakachitokea ni mgongano baina ya nyinyi wawili, unachohitaji kufanya ni kuomba msamaha kabisa tena kwa unyenyekevu mkubwa. Ukweli ni kwamba hili litakuwa pigo kwake kwa sababu alichokitegemea yeye hajakipata na hata kuwa na sababu ya kuendelea kupiga kelele, ubaya unazimwa na wema wahenga walisema.

Mpendwa msomaji, watu tunachohitaji ni kujihisi tupo salama, mtu yupo tayari kumshirikisha mwingine tatizo lake ili wote muonekane wote mupo katika hali moja. Mtu akisikia tu na mwingine yupo kama yeye basi yeye anajihisi yupo salama.

Mara nyingi ukikuta watu wanazungumza katika kikundi jambo ambalo, wote wanaafikiana watu hawa huwa katika hali ya tabasamu sana, Je nini kinawafanya wawe na furaha?  Ni ule umoja ambao wameutengeneza kwa kuigana. Kwenye hii dunia hakuna mtu ambaye hampendi nwenzie, watu wanapenda kitu kiwe sawa kwa kila mtu. Haijarishi hilo jambo ni la hovyo kiasi gani au zuri.

Usitumie maneno kumbadilisha mtu hawezi kubadilika, sio kwamba hataki kubadilika bali hataki kuchukua hatari, fanya mema ili nao waige kutoka kwako. Watu  wanapenda matokeo na sio sababu zilizopelekea matokeo.

Jambo muhimu hapa la kuondoka nalo ni kwamba, watu hawapendi kuchukua hatari, ni vigumu sana mtu kumbadilisha kwa maneno. Ni ngumu sana kumbadilisha mtu ila ni rahisi sana mtu kubadilika. Hakuna mtu ambaye hampendi mwingine ila watu wanapenda hujihisi wapo salama.
Ukawe na siku bora na barua njema kwa watu.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, April 1, 2018

Wakati Usio Tarajiwa.

 Sadick Kilasi     April 01, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI     No comments   

Kuna wakati mambo huja bila kutalajiwa. Mambo ambayo hayakudhaniwa kutokea hutokea, wakati usio tarajiwa.

Wakati usio tarajiwa mambo yakitimia wengi huita bahati. Wengi wanasema ni bahati mambo yakitimia wakati usio taraji lakini je ni kweli ni bahati?  Hapana si bahati ila ni kutimia kwa mambo.

Umejiandaa vema kwa fursa? na wakati ukifika utaitumia vema fursa?  hiyo ni wakati taraji, wakati sahihi. Je wakati sahihi ni wakati gani? Wakati yanapotimia ndo wakati taraji.

Mpendwa msomaji, hakuna wakati mzuri kama wakati taraji, wakati wa sasa na ndo wakati wenyewe.

Fanya kila kitu kwa ubora wa hali ya katika wakati taraji, wakati usio tarajiwa utakuja kwako, haijarishi unaweza kuja na lolote zuri au baya.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.




Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ▼  April (31)
      • Mtu Anaweza Kukumbuka Kwa Hiki. $#Tafakari Hekima ...
      • Usitawanye Watu Kusanya Watu, Fanya Kitu Hiki Kuku...
      • Nyoosha Mikono Juu Iambie Jamii Nimeshindwa.
      • Kama Wewe Hujawahi Kuona Hata Kisogo Chako Ya Nini...
      • Hasira Ni Kama Maji Yanayochemka. Je Mwisho Wake H...
      • Hivi Ndivyo Vikwazo Katika Kuupata Ukweli Halisi.
      • Wengi Tunafanya Nusu Nusu Hatufanyi Kweli Kweli.
      • Ni Rahisi Sana Kuona Kitu Hiki Kwa Watu Wengine.
      • (SEHEMU YA NNE) Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye ...
      • Sababu Hii Moja Tu Inatosha Kwako Wewe Kuanza Kuso...
      • Mazingira Uliyopo Yanakupa Tafsiri Gani? Dunia Ime...
      • Thamani Ya Binadamu Haitokani Na Utajiri Alionao. ...
      • Binadamu Ameumbwa Akiwa Na Tabia Hizi.
      • Wakati, Kila Jambo Wakati Wake.
      • Fanya Hivi Ili Ukusanye Vizuri Unachokusanya.
      • Kumbuka Mambo Haya Kama Tabia Ya Mtu Wako Wa Karib...
      • (SEHEMU YA TATU) Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye...
      • Hii Hapa Ni Njia Nzuri Ya Kujifunza Zaidi na Zaidi.
      • Nguvu Ya Matamshi.
      • Tunatakiwa Kuwa Kama Chumvi Si Kama Sukari.
      • Huu Hapa Ni Uwanja Ambao Unaweza Kufanya Utakalo.
      • Usiwanyanyapae Watu Kwa Sababu Wanayofanya Ni Maovu.
      • Neno kutoka Kwa Sadick Kilasi.Kufikiri Kunaleta....
      • Sehemu Iliyo Jificha.
      • Fanya Hivi Ili Maisha Yako Kuwa Bora Zaidi Na Zaidi.
      • Dunia Inatufundisha Kutegemea.
      • Acha Kufanya Kitu Hiki Mapema Kabisa Kama Unataka ...
      • Hivi Ndivyo Ambayo Unatakiwa Kuendelea Kufanya Hai...
      • Usimruhusu Adui Huyu Akutawale.
      • Fanya Kitu Hiki Ili Watu Wakuelewe Haraka.
      • Wakati Usio Tarajiwa.
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates