Karibu mpendwa msomaji katika tafakari ya chumvi wazee wetu ambazo wametuachia katika maisha yetu ili iwe misingi ya maisha yetu.
Katika zama hizi za taarifa, zama za matokeo, zama za internet ukiwa huna pesa huwezi kusikika hata kama unapiga kelele kiasi gani. Watu hawasikii maneno, watu wanaangalia matokeo ya kile unachofanya.
Ukitaka watu wathamini unachokifanya basi waambie ya kwamba mimi napata mahela kiasi fulani, basi ukitaja mahela mengi basi utawavutia wengi sana.
Watu wanapenda sana miugiza katika maisha, wapo tayari kufanya lolote lile ilimradi wasikie ya kwamba flani aliingiza mamilioni kupitia hapa. Ni rahisi sana kuwavuta wengi njia hiyo. Hivyo ndivyo hata watu huwatapeli watu pesa zao kwa tamaa yao.
SOMA:Sehemu Iliyo Jificha.
Mpendwa msomaji, thamani ya binadamu ni uwezo wa kubadili wanao mzunguka, haijarishi ni tajiri au maskini. Kumbuka kila mmoja ni barua ambayo inasomwa na jamii inayomzunguka. Nguvu ya sauti ya mtu ipo kwenye upekee wake na sio pesa.
Kama unauweza wa kufanya kitu na ukabadili matokeo hasi kuwa chanya basi hiyo ndo itakumbukwa sana na watu.
Katika jamii unaweza kukumbukwa kwa mambo mawili, matatizo uliyoyatatua na kwa jinsi ambavyo uliigusa jamii. Matatizo uliyoyatatua kwa mfano barabara, madaraja na mengine ambayo utayatatua katika jamii basi utabaki katika historia.
SOMA:Tunaona, Tunasikia, Tunashuhudia Tofauti.
Utakumbukwa kwa jinsi ambavyo umeigusa jamii ni pale ambapo itafanya vitu vya tofauti, kugundua kitu ambacho hakipo kabisa, utaigusa jamii kwa namna ambavyo umefanya. Upekee wako ndo unakufanya kuwa tofauti na wengine.
Wewe ni barua na mimi ni barua lazima tusomeke vizuri katika jamii, lazima tutumie vizuri uwezo wetu ili dunia iwe sehemu salama.
Endelea kutambelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment