Kwa kweli Watanzania hatuna desturi kabisa ya kusoma vitabu, yaani hatusomi vitabu kabisa. Ukweli ni kwamba hata kama tunasoma basi tunapitisha macho kwenye maandishi kwa mara moja na kutupa huko. Desturi ya kusoma vitabu haipo kabisa katika jamii yetu ya Kitanzania.
Kuna uhuru mkubwa sana wa kiakili ambao unaupata wakati unasoma vitabu. Hii ndo sababu kubwa na ya kipekee kwanini uanze kusoma vitabu. Najua huwezi kunielewa namaanisha nini lakini kama ukianza kusoma vitabu basi utaanza kuyaona mabadiliko ndani yako.
Kwa kweli uhuru wa nchi kutoka kwa wakoloni tayari tulisha pata lakini uhuru wa fikra kwa mtu mmoja moja bado sana. Naweza kusema walio pata uhuru wa fikra ndio wale walio tuletea uhuru wa nchi.
Watu tunapenda sana kushikiwa mambo, watu hatupendi kabisa kujiongoza wenyewe ndo maana ni rahisi kabisa kuwa na lawama juu ya mwingine kwa sababu kila kitu tumeshikiwa na wengine. Hatuna uhuru wa kifikra.
SOMA:Mazingira Uliopo Yanakupa Tafsiri Gani? Dunia Imejaa Kitu Hiki.
Anza kusoma vitabu rafiki yangu, hakuna mtu ambaye anaweza kuongoza fikra zako na usipokuwa na taarifa sahihi lazina utakuwa mtumwa wa fikra za wengine kwa sababu huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani na undani wa jambo lenyewe lipo na mtu mwingine na wewe huna chochote. Malcon X alishawahi kunukuliwa akisema mtu asiyesimama kwa chochote ataanguka kwa chochote. Kwa kweli kila mmoja yampasa kuanza kutengeneza misingi yake. Usiseme mimi nimesoma sana shuleni nina diploma sijui vyuo huko, rafiki yangu hiyo ni elimu ya shuleni lakini elimu ya mitaani ni bora zaidi maana haya ndo maisha yenyewe. Ukweli ni kwamba usiache elimu ya darasani ikupe kiburi, anza kusoma vitabu. Mimi ninayekushauri hivi nimeona faida kubwa kwanini ni vizuri zaidi kusoma vitabu.
Soma vitabu upate uhuru wa mazingira, soma vitabu vya dini upate uhuru wa kiroho, soma vitabu upate uhuru wako. Soma vitabu vya dini mwenyewe na siyo kusomewa kuna siri nzito sana humo na zishuhudie mwenyewe.
Uhuru wa ndani ndo uhuru wenyewe, jijenge akili yako, jijenge katika maandiko, lisha akili yako chakula, amsha akili iliyolala.
Ukawe na siku bora kabisa na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment