Watu wapo tayari kuiga hata kama jambo hilo ni la hovyo lakini hawapo tayari kufuata maelekezo mazuri. Kumbadilisha mtu huhitaji kumpa maelekezo bali anachotaka yeye ni kuiga kutoka kwako yaani akufwatishe wewe.
Watu wengi hatupendi kabisa kuchukua hatari, mara zote tunachotaka ni kuwa ni kuwa salama au tujihisi tupo salama. Yaani hata kama yupo mahali hayarishi lakini yeye anachotaka ajihisi yupo salama. Hakuna mtu ambaye anapenda kuwa katika eneo hatarishi na ndiomaana ni ngumu sana mtu kuanzisha jambo jipya kwa sababu ya watu wengi kuogopa kuchukua hatari na watapoteza usalama wao.
Ni vizuri zaidi kama unataka kumbadilisha mtu kutumia vitendo zaidi, mfano, umegombana na mtu, unajua kabisa hapa chanzo cha matatizo ni yeye na sio wewe, huhitaji kumwambia mimi mimi sijakosea hawezi kukuelewa kabisa, kitakachitokea ni mgongano baina ya nyinyi wawili, unachohitaji kufanya ni kuomba msamaha kabisa tena kwa unyenyekevu mkubwa. Ukweli ni kwamba hili litakuwa pigo kwake kwa sababu alichokitegemea yeye hajakipata na hata kuwa na sababu ya kuendelea kupiga kelele, ubaya unazimwa na wema wahenga walisema.
Mpendwa msomaji, watu tunachohitaji ni kujihisi tupo salama, mtu yupo tayari kumshirikisha mwingine tatizo lake ili wote muonekane wote mupo katika hali moja. Mtu akisikia tu na mwingine yupo kama yeye basi yeye anajihisi yupo salama.
Mara nyingi ukikuta watu wanazungumza katika kikundi jambo ambalo, wote wanaafikiana watu hawa huwa katika hali ya tabasamu sana, Je nini kinawafanya wawe na furaha? Ni ule umoja ambao wameutengeneza kwa kuigana. Kwenye hii dunia hakuna mtu ambaye hampendi nwenzie, watu wanapenda kitu kiwe sawa kwa kila mtu. Haijarishi hilo jambo ni la hovyo kiasi gani au zuri.
Usitumie maneno kumbadilisha mtu hawezi kubadilika, sio kwamba hataki kubadilika bali hataki kuchukua hatari, fanya mema ili nao waige kutoka kwako. Watu wanapenda matokeo na sio sababu zilizopelekea matokeo.
Jambo muhimu hapa la kuondoka nalo ni kwamba, watu hawapendi kuchukua hatari, ni vigumu sana mtu kumbadilisha kwa maneno. Ni ngumu sana kumbadilisha mtu ila ni rahisi sana mtu kubadilika. Hakuna mtu ambaye hampendi mwingine ila watu wanapenda hujihisi wapo salama.
Ukawe na siku bora na barua njema kwa watu.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment