Mpendwa msomaji, tunatakiwa kuwa kama chumvi sio kama sukari. Maisha yetu tunatakiwa kuwa kama chumvi si kama sukari. Mbona sukari ni tamu kuliko chumvi? Ni kweli kabisa sukari ni tamu kuliko chumvi lakini kunautofauti kiutendaji.
Chumvi ni kiungo cha ajabu sana, pamoja na kwamba ukiweka kwenye mboga, chakula kinakuwa kitamu lakini huwezi kuila ikiwa peke yake, lazima uweke kwenye chakula ambacho kinahitaji kiungo hicho ndiyo utakula vizuri. Lakini sukari haipo hivo unaweza kulamba hata kama hujaweka kwenye chakula chake.
Katika maisha, mahusiano ni kitu cha muhimu hata kama wewe una hela kiasi, au unaakili kiasi gani lazima uhitaji wengine wenzako wenye utofauti na wewe ili uwasilishe ulicho nacho.
Ufanyaji kazi wa chumvi ni wa usawa lakini ufanyaji kazi wa sukari ni wa kuvutia zaidi. Ukizidisha chumvi kwenye chakula ukweli ni kwamba huwezi kula lakini sukari ni tofauti unaweza ukala hata kama umezidisha, kwa sababu hata kama ikiwa peke yake unailamba.
Dunia inaendeshwa kwa usawa kama chumvi, kuna sehemu unapaswa usizidi. Ukiona unatamani kufanya kila kitu, unataka kila mmoja akusikilize wewe basi tabua wewe unataka kuwa sukari, unavuta na visivyo vutika. Mpendwa rafiki, usawa ndo furaha yenyewe sasa, ukikosa furaha maisha yatakuwa magumu. Ubongo utafeli kufanya kazi kisawa sawa, hali yako itakuwa tete, utajitaidi kuishi tu maisha lakini hutaishi maisha. Cha ajabu ni kwamba mwili wote ni chumvi tupu yaani miili yetu hii. Pamoja na kwamba sukari ni tamu sana na kuvutia kwake kote sukari huleta magonjwa lakini chumvi haipo hivo.
Ukawe na siku bora ukitafakari ufanyaji kazi wa chumvi na sukari. Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment