Watu wengi ambao wameokoka ni watu wa kuwanyanyapaa wengine wale ambao bado hawajamjua Mungu. Lakini je ni kweli ndivyo inavyotakiwa? Sio kweli kwa sababu kama wewe ulibadika basi na mwingine huyo anaweza kubadilika.
Hatuhitaji kuonyesha ya kwamba kufanya mema si jambo ambalo linapaswa kufanywa na kundi la watu wa aina fulani tu hapana, lazima tuwe mifano kwa wengine ambao bado hawajabadilika.
Mpendwa msomaji, usiwe kama yule mfarisayo dhidi ya yule mwandishi. Aliyemwambia Mungu wakati anasali ya kwamba mimi si sawa na huyo, mimi nafunga, natoa mafungu ya kumi na nawajiba katika maswala yote ya dini. Rafiki yangu, tukiwa hivi tutaangamia lazima tuwe barua njema kwa wengine.
Upendo ni swala la muhimu sana, upendo utaondoa yote yaliyo ya giza kwetu, tuwapende walio gizani ili nao waige kutoka kwetu.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
0 comments:
Post a Comment