Vitu vingine vyote tumepewa tutawale na tuendeleze lakini si vya kwetu, muda ukifika vikitaka kuondoka vinaondoka na huwezi kuzuia. Katika mazingira ya nje unaweza kuzuiwa na lolote, lakini kifikra hakuna kinachoweza kukuzuia kufanya unalotaka.
Mwili unaweza kukataa na ukasema mimi ninaumwa lakini fikra yako isipo kubali hutakuwa unaumwa. Uwanja mpana ambao unaweza kufanya lolote ambalo unataka ni uwanja wa fikra. Huko hakuna mtu ambaye anaweza kukuzuia maana haoni wala hasikii, ukitoka nje mwili unaweza kukataa, unaweza ukawa mwili wako au wa nwingine.
Mpendwa msomaji, tumia fikra zako sahihi ndani mwako ili ukitoka nje uwe tunda ambalo linapaswa kuliwa na sio sumu.
Ukawe na siku bora kabisa rafiki yangu, endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment