Unaweza kukimbia sasa majukumu yako lakini hatma yako nini? Ni maisha magumu ya mateso na manung'uniko. Wanao bebeshwa mizigo ya watu siku zote wanaishia kuwa washindi na wenye furaha. Wangalie watu ambao wamefanikiwa kisawa sawa siku zote ni watu ambao wamebeba majukumu na hatma za watu wengi. Mwangalie mtu kama Raisi, amebeba majukumu ya watu wa nchi nzima na anategemewa na wananchi wake. Mwangalie mtu kama walinzi wa kulia wa viongozi, utakuta kiongozi mwoga kuliko mtu ambaye maisha yake yapo hatalini zaidi.
Mara nyingi tunajaribu kukimbia majukumu yetu kwa kuwatwika lawama watu wengine. Mfano mdogo tu, migogoro midogo midogo, mtu anaweza kukwambia umenikosea lakini ukakataa moja kwa moja kwamba mimi sijakukosea. Rafiki yangu, huko ni kukwepa majukumu, hata kama kwa mtazamo wako unaona ya kwamba hujamkosea. Mtu hawezi kabisa kugombana peke yake au kujihukumu peke yake bila mtu mwingine kuwepo, kwa hiyo lazima uwe tayari kukubali ya kwamba wewe ni chanzo cha yeye kujisikia vibaya. Ukiwa tayari kuchukua majukumu ya wengine utakuwa mkomavu haswa, wengi watafuta kuwa karibu na wewe tena watajifunza kutoka kwako.
Mpendwa msomaji, wengi tunapenda mafanikio makubwa, wengi tunapenda kuwa washindi kati yao, wengi tunataka kuwa wakubwa kati yao lakini hii tabia ya unyenyekevu hatuna kabisa, kukubari kuchukua matatizo ya wengine hatuwezi kabisa, tumekuwa walalamishi siku zote na watupia lawama, ubinafsi ni mbaya kwelikweli. Ukitaka kuwa mkubwa kwao lazima ukubali kubeba lawama na kutimika kwao, ukubwa ni shimo la jalala.
Wakati wote mtu anapokwambia ya kwamba wewe ni sababu lazima ukubali kuchukua majukumu, lazima uwe mtu wa kuuzima ubaya kwa wema. Nuru iliishinda giza, ukweli uliushinda uongo tayari, kwahiyo hatma yako itakupa ushindi.
Usiwe mtu wa kutafutatafuta sababu siku zote, kuwa mtu wa kukubali makosa yako na majukumu yako.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
0 comments:
Post a Comment