Karibu katika makala ya leo msomaji wangu, nikushirikishe yale ambayo ni muhimu kuyajua na tujifunze kwa pamoja.
Katika dunia hii hapa ya matokeo chochote ambacho unakiona kwa macho yako au kukisikia basi kuna sehemu ambayo imejificha. Sehemu ambayo imejificha ni sehemu ambayo inapelekea matokeo ambayo tunayaona. Tukio lolote ambalo unaliona linasababu iliyopelekea tukio kuonekana, na hiyo ndo sehemu iliyo jificha.
Unaweza ukajiona upo sehemu fulani ambayo umeifikia haijarishi ni sehemu nzuri au mbaya, kumbuka kuna hatua kadhaa ndogo ndogo ambazo ulizipiga ambazo zimepelekea uwe pale ulipo. Hizi hatua ndogo ndogo inawezekana ukawa ulikuwa unaziona kwa kujali au kwa kutojali. Mapito yako ni sehemu iliyojificha.
Kila kitu hapa dunia kinasemu iliyo jificha, kuna sababu zilizo pelekea kuwa pale kilipo. Ukiuona mti umesimama vema basi tambua ya kwamba kuna mizizi ambayo imefanya mti ukasimama. Basi si mizizi tu lakini kuna kitu ambacho kimefanya huo mti na umekuwa vema.
Sasa unaweza kujiuliza kwanini tujifunze sababu? kwanini tujifunze sahemu iliyo jificha? Kwa sababu tulio wengi tunastukia maisha. Mpendwa msomaji, katika maisha kuna aina mbili za mitazamo wapo watu ambao wanapambana na matokeo na wapo watu ambao wanapambana na sababu, sehemu iliyo jificha. Ukiwa unapambana na matokeo ukweli ni kwamba maisha kwako yatakuwa magumu sana kwa sababu hujui ni kipi ambacho kimepelekea yale matokeo. Ni sawa sawa na kukazana kuziba chemichemi ya maji yanayo bubujika kutoka chini ya ardhi yatakusumbua kweli kweli.
Sasa wana Jiko La Ushauri tunatakiwa kapambana na sehemu iliyo jificha. Sababu zilizopelekea kitu hicho kuwepo. Mfano mzuri ambao naweza kukuonyesha ni kwamba, mnaweza mkakutana na mti akakutukana au kutoa kauli ambayo hujaielewa vizuri, ukiwa na mtazamo wa sehemu iliyo jificha hutapambana na ile kauli utambana na kipi kimepelekea atowe haya maneno makali, hapa utakuwa unapambana na sababu labda mwisho unaweza kugundua ya kwamba huyu alikotoka si salama, kwa hiyo utamsamehe bure. Lakini ukiwa ni wa kupambana na matokeo, kauli ya kwanza ambayo utamwambia ni, unanitukana mimi, kwanini unanitukana na hapo ndipo utakuwa uwanja wa vita.
Hatuwezi tukawa tunastukia maisha. Chochote tunachopitia lazima kiwe na ubora tukipe nidhamu kubwa. Matatizo mengi sana yanasababishwa na mtazamo wa kupambana na matokeo. Ukiangalia nchi ambazo zinapambana vita, wanapigana kwa mtutu kutafuta amani. Sio lahisi kupata amani.
Pambana na hali sio mtu.
Ukawe na siku bora rafiki yangu, nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment