Sasa mimi naongea na watu wa mtazamo chanya, watu ambao hawataki kabisa kuishi mitazamo hasi hao ndo naongea nao sasa kupitia makala hii. Kama wewe ni mmoja wao basi endelea kusoma hapa au la kama ulikuwa hujui kama mtazamo ni kuchagua basi endelea kusoma hapa.
Moja kati ya adui mkubwa kwa watu wenye mtazamo chanya basi mtazamo hasi. Mtazamo hasi huja haraka sana na kuharibu kabisa mtazamo wako chanya. Mtazamo huu huja pale ambapo unahisi umefeli kufanya jambo fulani.
Unaendelea kuiharibu siku nzima kwa kitu kidogo tu. Unaweza ukawa unafanya kitu cha kawaida kabisa lakini ukiruhusu tu na kusema kwamba siwezi basi utajiona kwamba wewe hufai kabisa. Mungu anakuwazia mema, ajionavyo mtu ndani yake ndivyo alivyo. Hivyo ndivyo ilivyo.
Mpendwa msomaji, usiruhusu adui huyu awe kikwazo katika maisha, usimruhusu adui huyu akunyang'anye furaha yako, kuwa mjanja rafiki yangu, wewe ni mshindi. Lazima ujiambie mimi nina mtazamo chanya.
Mtazamo ni utajiri mkubwa sana katika maisha yako. Ishi mtazamo chanya, chagua huu utajiri.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment