Inawezekana wewe ni mtu ambaye ni moja kati ya watu wanaotamani kufanya jambo fuluni lakini sasa kuna mambo fulani fulani yanakutatiza.
Inawezekana ukawa ni mtu mwenye kipaji fulani lakini unashindwa kufanya na kuonyesha kipaji chako kwa sababu ya kujiona wewe hujakamirika peke yako unahitaji wanagrupu au mdhamini atakaye kufikisha mahali fulani unapotaka wewe kufika.
Lakini pia inawezekana wewe ni moja kati ya watu ambao wanatakiwa kutimiza jambo fulani lakini unaona bado wewe hujakamirika bado. Unaweza ukawa unatakiwa kutoa fungu la kumi lakini bado unaona kwamba kipato chako ni kidogo sana kwahiyo huwezi kutoa mpaka ufikishe kiasi fulani.
Mpendwa ndugu msomaji, kama bado unasubili kukamirika au kukamirisha vitu au wakati fulani unachelewa bure, huwezi kukamirika, walio kamirika wanapatokana makabulini. Kama bado wewe ni mzima wa afya, basi yakupasa uchukue hatua sasa hivi.
Moja kati ya sifa ya ukamirifu, hapa duniani, hapana ukamirifu, chochote utakacho fanya hapa duniani ukimaliza unahitaji kuboresha zaidi na zaidi la sivyo unarudi nyuma zaidi.
Jambo ambalo naweza kukushauri sasa hivi chukua hatua, anza kufanya, kadili utakavyo kuwa unafanya ndivyo utakavyo kuwa unajiboresha zaidi na zaidi ila usitegemee ukamirifu.
Endelea kutembelea blogu hii ili kukifunza zaidi. OMBI LANGU, nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako yanakuhusu.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment