Binafsi nafikiri ya kwamba Mungu alifanya hivi ili kuweza kuweka ubora wa kutosha katika mahusiano, ingekuwa watu wote wanafanana ubora usinge kuwepo kwasababu watu wote wa dunia hii wanamapungufu, mtu mwingine wa kuziba pengo la mwingine asingekuwepo.
Tumezaliwa duniani kuwezesha kitu ambacho mwingine hawezi kufanya hivo. Tunakamirisha pasipo kamirika, ili kufanya ubora uonekane, na hili ndilo jambo ambalo unatakiwa kulifikiria kila siku.
Imekuwa kawaida kwa watu kutofurahia mahala walipo na kufikiri kuna sehemu zaidi wangepaswa kuwepo, ni kweli inawezekana kabisa mahali ulipo sio penyewe, ukitambua hivo unapaswa kuchukua hatua haraka kugeuka na kupaendea mahala unapotaka wewe na unahisi patakupa furaha.
Mungu alipo tuumba kwa sura tofauti ilitaka, kila mmoja asababishe kadili ya uwepo na uwezo wake. Na hii ndiyo sababu pekee ya kuzaliwa, utafuta huku na huko lakini sehemu zote hizo ni funzo tu la maisha, kusababisha kwa wengine ndo maisha ya kweli.
Waweza ukawa na mali nyingi na utajiri mkubwa lakini zisikusaidie kwa lolote maana utakufa na utaacha mali hizo. Wenye mafanikio ya ukweli wanatambua ya kuwa wamebarikiwa kuwa baraka kwa wengine. Maisha ni mahusiano, ukifeli hapo maisha yatakuwa magumu sana.
Mpendwa msomaji, jambo la muhimu hapa ambalo unapaswa kutambua ni kwamba wewe ni muhimu sana kwa wengine na ndiomaana hakuna mtu unayefanana naye, utapaswa kutambua umezaliwa kusababisha kwa wengine, ondoa ubinafsi, kwa nafasi au wakati au hali yoyote ile uliyo nayo unaweza kufanya lolote lile la kumgusa mwingine kutokana na utofauti wako na huyo, usijishushe na kuona ya kwamba hufai hapana, lazima utambue ya kwamba unaweza kumfanya mwingine ajihisi na anafuraha, waweza hata kutabasamu tu, naye atatabasamu kwaajiri ya tabasamu lako.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Maoni yako ni muhimu sana pia washirikishe wengine ujumbe huu.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment