Mpendwa msomaji, karibu katika makala hii ya leo ili tupate kujifunza kwa pamoja mimi na wewe msomaji wangu.
Moja kati ya sifa kubwa ya dunia hii ni kwamba kila kitu kimeumbwa pande mbili, dunia imewekwa katika mfumo wa kuchagua, chochote unachohitaji kipo katika machajiguzi hii ndio asili ya dunia yetu tunayoishi.
Wakati wote binadamu tumekuwa tukikazana kuyaangalia mazuri yako wapi, haswa hiki ndo kitu ambacho tunakihitaji, lakini kwa dunia ilivo lazima upate maumivu kwanza, lazima kwanza mabaya, usiyo yapenda yakutokee harafu yale mazuri yaje.
Mpendwa msomaji, ndivyo jinsi dunia ilivyo sio wewe unayosababisha au mimi au mtu fulani kakuloga, hapana, hii ni asili ya dunia. Tutajivunia matunda tunayoyachuma sasa lakini kwa mda mrefu tumekuwa wavumilivu wa hali ngumu tukitumainia tunachotaka, na sasa tunafurahi tumepata tunachotaka baada ya maumivu mda mrefu.
Mpendwa msomaji, kitu gani unakiona kwa mwenzio ni kizuri na unakitamani, Juan tayari alipata maumivu, kitu gani unakitaka kwenye hii dunia? Basi lazima ujiandae kwa maumivu makali, ili upate unachotaka, na ukiona unaanza kwa kutokupokea maumivu hayo basi yakupasa utazame kwa umakini, yaweza kuwa umepotea au kuna maumivu yanakuja mbele yako, ambayo yameandaliwa kwa ajili yako. Hii ndio asili ya dunia, sio mimi, hapana.
Mpendwa msomaji, mabaya unayopitia yamewekwa na dunia hii kwa sababu ya kukuonyesha wewe, unachokitaka ni cha thamani kiasi gani, kama maumivu yake ni madogo basi na mazuri nayo ni madogo, unapata jinsi ulivyo pokea. Maumivu yanakuonesha thamani ya kile kitu, maumivu yanakupa tumaini, maumivu yanakujenga kuwa mtu wa uvumilivu. Mpendwa msomaji lazima ujifunze hilo.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Naomba unisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako pia ni ya muhimu.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment