Mpendwa msomaji, ni kiasi gani umekosewa na mwingine mpaka unafikia hatua hiyo ya kusema, nimekusamehe lakini sito kusahau, kwanini unamgawia maumivu mtu mwingine kama kweli umemsamehe? Je unafikiri hata ukimwambia hivo na yeye ataumia kama wewe unavyoumia?
Je huo mzani ulio uweka unafikiri nani atakula hasara zaidi? Inawezekana kabisa hujawahi kujiuliza au kuambiwa kwanini unapaswa kumsamehe mtu au nini maana ya msamaha, lakini leo nataka nikwambie kwanini utatakiwa kusamehe mtu.
Mpendwa msomaji, kila kitu tunachofanya hapa duniani ni kwaajili yetu wenyewe yaani kwaajili yako, unatakiwa kumsamehe mtu ili wewe uachilie mzigo ulioubeba wewe, kwani yeye haelewi mzigo ulionao wewe, mpendwa msomaji, hata ukiongea kwa uchungu kiasi gani aliyekukosea hayupo kama wewe, na mzigo wako hauelewi. Mpendwa msomaji, unaposema, nimekusamehe lakini sito kusahau ni kuendelea kujiumiza mwenyewe na aliyekukosea hatambui hilo.
Kila mtu anapokosewa, huwa tunachukua uzito tofauti wa lile kosa, na ndiomaana wengine wanajinyonga, mwingine atanuna sana, mwingine hata nuna kabisa. Mpendwa msomaji, chizi akikosea hutonuna, basi hata mtu mwenye akili timamu mchukulie hivohivo, sio kila mtu anachukulia uzito huo uliochukulia wewe, wengi ni machizi japo wanaonekana ni wazima, na usipo samehe utakuwa kama yeye, kusamehe ni kuonyesha tofauti kati yako na yeye.
Samehe, samehe, samehe, Acha kuweka kwenye mizani unapokosewa, achilia kila kitu kwa faida yako mwenyewe.
Kuna kitabu ambacho kimeandikwa na Mwandishi Deo Kessy, kitabu hicho kinaitwa Kwanini msamaha, ni kitabu kizuri sana na kitakufunza mengi juu ya msamaha, inawezekana umeumizwa sana, lakini mimi nakwambia tafuta kitabu hiki kitakusaidia sana, Wasiliana nae kwa namba hii 0717101505. Wapende wengine kwa kuwasamehe ili uwe mtu kamili na sio kichaa.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment