Unaweza usinielewe nini namaanisha, ila yapaswa kujiuliza mwenyewe. Fikiria ya kwamba mwanzo ulikuwa na pesa za kujikimu mwenyewe au na familia lakini ukatumia pesa tofauti na matumizi yako ya kawaida na ukawa huna pesa, Je hapo utakuwa katika hali ngumu au mwenyewe umeamua kufanya hivo.
Ulimwamini mtu, ukajenga imani kubwa juu yake ukategemea msaada juu yake, akashindwa kukusaidia kama ulivyotegemea, unaona hafai, kakukosea, ni mchoyo, hutomsamehe, je ndivo ilivyo?
Jiulize swali hili unapokutana na migogoro mbalimbali lakini jiulize swali hili wakati wa raha na burudani. Hofu kubwa tuliyo nayo kizazi hiki ni kuchukulia mambo kwa ukubwa mkubwa, tunazidi viwango vya kawaida. Mpendwa msomaji chochote unachokiangalia chini ya jua, kiangalie kwa ukawaida. Mtukuze Mungu na umutegemee yeye.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment