Karibu tena katika makala ya leo ambayo nimekuandalia msomaji wangu ili wote kwa pamoja tupate kujifunza niliyokuandalia.
Mpendwa msomaji, inawezekana unapitia katika hali ngumu sana katika maisha lakini leo nataka nikwambie kitu kimoja, waweza kujishangaza mwenyewe, ndio waweza kujishangaza mwenyewe na magumu yako hayo uliyo nayo.
Jishangaze mwenyewe kwa kugeuza changamoto zako kuwa fursa, najua inawezekana ukifanya hivyo na utajishangaza sana kwa kuona nilikuwa wapi kipindi chote na sikufanya hivi.
Inawezekana umetengwa na wapendwa wako unao wapenda, waweza kujishangaza mwenyewe kwa kuwasamehe bure kabisa na kutua huo mzigo wa mawazo, tena sema kwa sauti kuu nawapenda nyinyi nyote mlio nitenga na ambao hamjanitenga, tamka upendo kwa sauti kubwa.
Inawezekana unamzigo wa mawazo kichwani mwako lakini leo hii waweza kujishangaza mwenyewe kwa kufikiri tofauti kabisa juu ya mawazo yako hasi unaweza kufikiri chanya sasa, kama kuna kitu au tabia inakusumbua kwa muda mrefu, sasa dhibiti mawazo yako kwa kukataa hicho kinachokusumbua, tamka kwa sauti mara mia hivi kwa siku, sitaki, sitaki, sitaki... Basi utajishangaza mwenyewe.
Mpendwa msomaji, kitu gani hicho kinachokutesa, au ni jambo lipi linalokutesa, kwa taarifa yako hakuna mtu anayeweza kukutesa wewe au kukuonea wewe, wewe mwenyewe unaweza kujitesa, sasa kwanini unajitesa, sasa leo waweza kujishangaza mwenyewe, igeuze na ithibiti kabisa dhamiri yako, angalia kwa jicho lingine kwa chochote kile ambacho ni mzigo kwako, vua kabisa hilo gamba la maumivu, jishangaze mwenyewe.
Mpendwa msomaji, jishangaze mwenyewe, usisubiri kushangazwa nje na wewe, jishangaze, jishangaze, jishangaze.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Washirikishe wengine ujumbe huu ili watoke kwenye vifungo vya mda mrefu na mizigo ambayo wameibeba.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment