Lakini wakati mwingine unaweza ukawa unapitia wakati mgumu, na ukaona hamna kabisa njia ya kutokea, unaona kote kumefungwa giza tupu hamna njia. Je kweli njia inakuwaga haipo?
Mpendwa msomaji, ukisoma Biblia, mwanzo 1, mstari wa nne, maneno yanasema, Mungu akaiona Nuru ya kuwa ni njema, ikaitenga nuru na giza.
Mpendwa msomaji, giza lipo mahali pale palipo kosa nuru, ubaya upo mahali palipo kosa wema, na hata kama wema ukijaa bado chembechembe za ubaya zipo. Wakati wote lazima utambue ya kuwa, unapopata Mafanikio makubwa lazima pia uwe makini sana na kushindwa kwasababu hivi vyote vinaenda kwa pamoja.
Unapo pitia magumu lazima utambue kuna wema, lazima uangalie tu, ya kuwa uafadhari wangu uko wapi hapa penye magumu. Usilaumu sana unaposhindwa, tazama na uone ni wapi pa kupitia wewe.
Mpendwa msomaji, dunia nzima imejaa giza, jua linapopita basi giza linafifia, lakini bado linakuwepo, jua linapopotea ndivyo na giza linapoongezeka. Rafiki yangu, jiandae kwa yote hayo, unapokuwa na wema tambua kuna ubaya, unapokuwa na ubaya tambua kuna wema.
Endelea kukifunza kupitia blogu hii. Pia nisaidie kisambaza ujumbe huu uwafikie wengi zaidi, maoni yako ni ya muhimu sana rafiki yangu.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment