Ni ukweli usiopingika kabisa maisha ni mahusiano, huwezi kuishi vema kama usipokuwa na mahusiano na mtu yeyote. Tunaishi tukiwa tunahusiana na watu mbalimbali, ambao tunawajua na wengine hatuwajui lakini yote haya ni mahusiano. Kuna mahusiano ya aina mbalimbali, mahusiano ya ndoa, mahusiano ya ndugu, mahusiano ya marafiki na mahusiano ya mwingiliano wa watu mbalimbali ambao hatuwajui.
Tunahusiana na watu kwa sababu mbalimbali, lakini ukweli ni kwamba wakati huohuo wa mahusiano ndipo na migogoro na matatizo na mafarakano huanza. Tukiwa tunakutana, kila mtu anawasirisha tabia na haiba yake, kwa mwingine. Ukweli ni kwamba kila mmoja amelelewa tofauti na mwingine lakini pia na haiba ni tofauti kabisa na mwingine. Watu wawili wanapokutana lazima wawe tofauti kabisa kutokana na tabia na haiba zao. Hata mapacha tu hawezi kufanya vitu vinavofanana.
Tofauti na migogoro huanzia hapa kwenye uwasirishaji wa tabia na haiba. Mtu anapowasirisha tabia yake mwingine anaona kero kwake na haifai kutokana na maadili yake. Lakini yote hii inategemea utambuzi na uelewa wa mtu juu ya hilo jambo aliloambiwa. Mafarakano yanaanza pale tunaposhindwa kuelewana watu wawili au makundi mawili.
Kuna siraha mbili ambazo wewe msomaji wangu unapaswa kutumia wakati wa migogoro inapotokea na ukajenga mahusiano bora kabisa na wengine. Migongano haina budi kutokea lazima itokee.
1. Wachukulie watu wote wanamapungufu. Hii ni siraha bora sana, utakapo wachukulia watu wote wanamapungufu kwako haita kuwa shida unapokutana na mtu mkashindwa kuelewana. Ukweli ni kwamba kila mmoja anamapungufu yake na udhaifu wake. Utakapochukulia kila binadamu anamapungufu haitakuwa tatizo sana kwako kwa sababu utakuwa umejiandaa kisaikolojia.
2. Chukulia ya kwamba hakuna mtu mbaya duniani, ila kuna mabaya duniani. Hii nayo ni siraha nzuri sana katika maisha. Ukweli ni kwamba hakuna mtu mbaya duniani lakini kuna mabaya duniani. Tulizaliwa tukiwa wazuri tu lakini yote haya tumeyakuta huku huku duniani kwahiyo sisi siyo wabaya ila kuna mabaya. Jambo muhimu unapoishi fuata njia njema tu, achana na mabaya, mabaya yapo na yataendelea kuwepo. Unapokutana na mtu kafanya makosa wewe unapaswa kuichukia ile hali iliyotokea pale na wewe utakuwa huna mgogoro na mtu yeyote na utaishi vema.
Siraha mbili hizi zinatosha kwako wewe rafiki yangu kuishi vema na watu na itapunguza kwako wewe mafarakano na wengine.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. OMBI: Nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu uwafikie wengi zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, maoni ni muhimu.
0 comments:
Post a Comment