Katika zama za zamani watu waliishi, kwa kuaminiana sana, watu walifanya mambo kwa uaminifu mkubwa, japokuwa uongo ulikuwepo lakini haukuwa umekithiri sana. Ni kweli kwamba maisha yao yalikuwa ya kumaanisha kuliko sasa hivi maisha yamekosa ladha yenyewe.
Zama hizi, zama za kizazi chetu, zama za intaneti na taarifa, ukweli ni kitu adimu. Kila kitu ambacho mtu amekuwa akifanya ni uongo mtupu. Mambo yamekuwa tofauti kabisa, ukweli umekuwa adimu sana na ni gharama kuupata.
Mwenye ukweli na taarifa sahihi zama hizi ndiye amekuwa akifanikiwa kimaisha. Wengi sana ambao hawana taarifa sahihi wamekuwa wakipata shida na kuishi maisha ya kuigiza tu.
Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ambayo watu wanafanyia uongo mkubwa, mtu anapiga picha yupo sehemu fulani nzuri na anaonekana anamaisha mazuri lakini huo ni uongo, kama tunavojua uongo ni mwendelezo ukiongopa mara moja inakulazimu uendelee kuongopa kila siku, uongo unambana anatakiwa kila anapotaka kipiga picha ajiweke vizuri aonekane anamaisha mazuri, kitu ambacho kwake ni usumbufu mkubwa na kutafuta gharama zisizo na maana.
Mpendwa msomaji, ukweli umekuwa kitu adimu sana, kila anafanya analojisikia yeye kufanya na kuababisha maumivu kwa wengine, biashara za utapeli zimekuwa nyingi, watu wamekosa kuishi maisha halisi sasa wanaishia maisha ya wengine, maarifa sahihi nayo yamekuwa adimu sana maana kila mtu anafanya analojisikia yeye kufanya. Mpendwa msomaji, kweli imekuwa kitu adimu sana kupatikana.
Mpendwa msomaji, tafuta kweli nayo kweli itakuweka, unaweza kujiuliza sasa nitafutie wapi, lakini cha muhimu anza wewe kuwa mkweli, nawe utauona ukweli na uongo kwa sababu wewe unaishi kweli, soma vitabu vya dini vitakusaidia.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Ombi: nisaidie kuwashieikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment