Katika maisha kila mtu anapitia hali mbalimbali, kuna wakati mgumu sana kwako na wakati ambao ni rahisi sana kwako. Hivi ni vipindi tofauti tofauti ambavyo kila mtu huwa anapitia.
Mpendwa msomaji, inawezekana kwa sasa unapitia wakati mgumu sana lakini leo nakutangazia huo ni wakati wa mapito, unapitia mapito ambayo yanapita, kwahiyo lazima utambue dunia ndivyo ilivyo kwamba lazima upitie hilo na hiyo ndiyo ladha yenyewe ya maisha. Kuna wakati utafika utapitia mazuri mpaka wewe mwenyewe utashangaa, kikubwa ni kutafuta njia ya kutokea ili kisiwe kipindi kirefu kwako.
Mpendwa msomaji, inawezekana kwa sasa unapitia wakati ambao ni mzuri sana, lakini naomba nikukumbushe ya kwamba, jua tu ndo linaangaza lakini dunia yote imejaa giza nene. Lazima utambue ya kwamba tunatawaliwa na changamoto zaidi kuliko furaha, lazima ujirinde na furaha isije ikawa burudani kwako.
Mpendwa msomaji, jambo lolote lile unalopitia ni darasa kwako na ni maandalizi ya baadae. Changamoto zipo na zitaendelea kuwepo.
Jambo la muhimu hapa kutambua hapa kama unapitia wakati mgumu tambua ya kwamba ni mapito na lazima upitie na kama unapitia wakati mzuri pia nayo hayo ni mapito tu lazima upitie, maisha ndivyo yatakavyokuwa siku zote na hiyo ndo ladha ya maisha.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.co.
0 comments:
Post a Comment