Karibu katika makala haya ya leo ili uweze kujinza nami jambo ambalo mimi rafiki yako nimeingia jikoni ili nilipike tule kwa pamoja. Karibu sana tujifunze kwa pamoja.
Katika mahusiano ni rahisi sana kumwambia mwingine hafai, ni rahisi sana kuona mapungufu ya wengine, ni rahisi sana kuona ya kwamba huyu mtu sio mtu sahihi wa kuhusiana nami. Haijarishi ni mahusiano ya aina gani lakini wengi tukiona mambo fulani fulani hayapo huwa tunakata tamaa kabisa na kusema ya kwamba mimi siwezi kabisa kuishi na huyu mtu.
Je ishawahi kujiuliza kwanini mahusiano mengi yanavunjika? Najua unatambua vizuri kabisa ya kwamba ni nini kinasababisha. Haijarishi ni mahusiano ya aina gani, lakini mahusiano mengi, au yote yanavinjika kwa sababu ya maslahi. Wengi wanao vunja mahusiano ni kwa sababu ya matakwa yao binafsi.
Mtu anaweza kukuelezea sababu nyingi sana za kuvunja mahusiano, lakini sababu kubwa ni kutafuta matakwa yake binafsi. Yawe mahusiano ya ndoa au mahusiano mengine ya kawaida.
Utakuta mtu anajielezea vizuri sana, ohoo mimi siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu huyu mtu anapenda sana hela, siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu alinidanganya, siwezi kuishi na huyu mtu kwa sababu anatoka nje ya ndoa. Sasa unaona, sababu zote hizi ni nzuri lakini, zote ni za kibinafsi. Mtu anavunja mahusiano na mtu kwa sababu zake binafsi, kwa sababu hataki yeye kuumizwa na jambo lolote.
Mahusiano ni kitu cha ajabu sana, ubinafsi ukizidi waweza kujikuta hata wewe mwenyewe ukajivunja. Unaposhindwa kuhusiana na watu wa nje inamaana ya kwamba huwezi kujiongoza ndani mwako, utawatenga wengine mwisho utajitenga na wewe mwenyewe. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kwamba, dhambi ya kuwatenga watu, haiwezi kukuacha salama. Ni kweli kabisa, ukianza kumkana mwenzako mwisho utajikana hata wewe mwenyewe. Na sababu nyingi za kujinyonga ni sababu kama hizihizi.
Mahusiano ni kitu kipana na ni muhimu sana katika maisha yetu, lazima tukazane kujenga mahusiano mazuri na wengine. Jambo la muhimu la kuzingatia ni kuweka mipaka yako katika mahusiano yako. Kama inavotamburika zama hizi hata mahusiano yamekuwa changamoto, muda umekuwa ni mchache sana kwahiyo lazima utambue ni wakati gani unapaswa kuwa na watu fulani na wa aina gani.
Jambo la muhimu hapa mpendwa msomaji, siku zote wewe usiwe chanzo cha mahusiano kuvunjika yaani bora kuachwa kuliko kuacha, kikubwa ni kujitaidi na kuje. Jitaidi sana isije dhambi ya kumtenga mtu ikakuadhibu. Waweza kujitadhimi mwenyewe wale wote ambao waliacha makaenda kuolewa kwingine mpaka leo wanatangatanga na wanaona kila mtu hafai. Hii yote ni kwa sababu ya ubinafsi na kutafuta vitu na matakwa yao.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment