JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Tuesday, December 26, 2017

Kitu gani kipo nyuma ya hili? Kitu gani kitafuata baada ya hili?

 Sadick Kilasi     December 26, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Habari rafiki? Ni siku nyingine tena, natumai umeamka salama na unaendelea vizuri. Leo ni tarehe 25/12/2017, kwa maana hiyo sikuu ya krismas imekwisha. Natumai imekuwa krismas bora sana kwako na umesherekea vema. Lakini rafiki ya ngu kama krismas hii haikuwa bora kwako lakini hilo si jambo ambalo la kulichukulia maanane sana, jaapo unaweza ukajifunza kupitia krismas ya jana lakini wakati ulio nao sasa ndio wakati  bora zaidi kuliko wakati wowote kuwahi kutokea katika maisha yako. Dakika na sekunde ulio nayo sasa waweza kupanda mbegu na baadae ukaja ukavuna matunda baadae lakini pia waweza kupanda mbegu ukaja kuvuna mabaya baadae.

Karibu rafiki yangu ujifunze na kutafakari mwenyewe kuhusu haya maswali; Kitu gani kipo nyuma ya hili? kitu gani kinafuata baada ya hili? Haya ni maswali nyeti sana katika maisha yetu, kama tungekuwa tunajipa nafasi ya kujiuliza au tungetambua moja kwa moja kinachofuata kwetu sisi tungejiandaa.

Tumekuwa watu ambao tunakosa japo kujipa nafasi hata kidogo kufikiria, tumekuwa tukianzisha mambo hata kujiuliza maswali haya mawili tumeshindwa, sisi tunachokitafuta ni kitu kizuri tu, tumesahau kabisa ule msemo usemao heri mateso ujanani kuliko kuliko mateso uzeeni, msemo huu unamaana kubwa sana katika maisha yetu.

Wakati mwingine tamaa zetu zimetupeleka mbali sana na kujipa maumivu ambayo huwezi kulinganisha kabisa na kale kastalehe kadogo tuliko kafanya kwa mda mfupi, lakini yote hiyo inasababishwa na tamaa zetu na ubinafsi mkubwa tulio nao. Hebu fikiria kitu hiki, mvuta sigara alianza kwa tamaa zake za starehena kufuata mikumbo lakini yeye alisahau kabisa matokeo yake na majuto ya uzeeni na alisahau kabisa ya kwamba atakuja kuwasumbua watu ambao hawana hatia kwa kuanza kuwapeleka huku na huko kutibiwa.

Rafiki yangu maamuzi unayo toa leo ni matokeo ya kesho na ndio maana siku zote nimekuwa nasisitiza ya kuwa hakuna kitu bora kwenye maisha kama mdahuu ulio nao, kama unajiingiza kwenye mahusiano usijaribu, chochote kinachaanza kwa starehe lazima uwenacho makini sana. Hapo ulipo sasa ni matokeo ya jana  sasa jiulize jana ulifanya nini? Siku zoete uwe mtu wa kujiuliza haya maswali kabla ya kuanza kufanya jambo.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii daima tupo pamoja.
Wako Sadick Kilasi wa JIKO LA USHAURI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
jipatie kitabu hichi kwa kutembelea mtaalamu.net/kessydeo
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, December 25, 2017

Maeneo matatu ambayo unatakiwa kuwa makini kama unataka kuwa mwekezaji kwenye maarifa

 Sadick Kilasi     December 25, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu siku mpya, hongera kwaajili ya siku hii kwa sababu tukijali kila siku inayopita mbele yetu kupata mafanikio litakuwa sio jambo la kushangaza. Tunaishi siku moja yaliyopita yamepita na yajayo ni matarajio lakini maisha ya kweli ni sasa na ni leo, tunaishi siku moja, leo ni siku na siku moja tutakufa.

Tukitambua tunaishi siku moja tutaijali siku, tukitambua kwamba leo ni moja kati ya siku tutaidhamini sana leo na tukitambua ipo siku tutakufa basi hatuna budi kufanya kila kitu ili kutimiza wajibu wetu ili tuache alama dunia. Kwahiyo hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii tulio nayo ni siku ya dhamani sana na kesho anapanga yeye.

Karibu mpendwa rafiki yangu tujifunze kwa pamoja kwewnye maada ambayo nimekuandalia leo ambayo inasema, maeneo matatuambayo unatakiwa kuwa makini kama untaka kuwa mwekezaji  wa maarifa.

Ni watu wachache sana ambao wanatambua ya kwamba tunatakiwa kuwekeza kwenye maarifa, wengi wetu tunachojua ni kuwa unatakiwa kuwekeza pesa tu au tunatambua ya pesa tu ndo huwa inawekezwa. Kama wewe ni mmoja kati ya waadhirika wa hilo basi leo tambua ya kwamba  maari yanawekezwa. Maarifa ni uwezo wa kuona unafuu ndani ya changamoto.

Tukianza kuwekeza kwenye maarifa, kwenye uwekezaji mwingiune itakuwa ni rahisi kwetu kutokana maarifa yetu. Uwezekezaji wowote ule unachangamoto zake kwahiyo kama huna maarifa utashindwa kuwekeza. Ni maeneo mengi sana tunawekeza bila ya sisi wenyewe kutambua ya kwamba hapa tunawekeza, kwa mfano; tunaishi kwenye jamii, ili niwekeze kwenye jamii inatakiwa niwe na tabia njema kwahiyo ukiwekeza tabia njema watu watakuheshimu na hata ukianzisha kitu itakuwa rahisi kwako kukuunga mkono. Yafuatayo ni maeneo matatu ambayo tunatakiwa kuwa makini nayo ili kuwekeza vizuri kwenye maarifa.

Eneo la kwanza kabisa ni usikivu wakati wa mazungumzo. Hili ni eneo ambalo tunatakiwa kuwa makini sana kwani ndilo eneo linalotumika wakati wote, watu tumekuwa wajinga kwa sababu ya kukosa usikivu yaani mtu anzungumuza na wewe unataka kuzungumza, mtu anazungumza wewe unajishikashika au unachezea simu, huko ni kukosa usikivu. Kwenye usikivu kuna mengi utajifunza haijarishi unaongea na mtu wa aina gani lakini usikivu ni wa muhimu sana.

Eneo la pili ni kujifunza kupitia changamoto. Hili ni eneo la muhimu sana kwa sababu hili ndo maana halisi ya maarifa. Tumekuwa watu wakukimbia changamoto au kuwabebesha wengine bila kujua tunatupa dhahabu. Maisha changamoto, kuishi changamoto na changamoto maisha. Mara nyingi wanaotatua changamoto sana ndio wanao fanikiwa sana. Kwahiyo rafiki yangu usikimbie changamoto hiyo ni ladha ya maisha tu.

Eneo la tatu ni kusoma vitabu au kusoma kwa ujumla. Hili ni eneo ambalo tunajifunza mengi kutoka kwa  wengine ambao sio rahisi kukutana nao sisi,wengine walisha kufa zamani, wengine wapo mbali na hali nyingine tofauti. Rafiki yangu kusoma vitabu ni kitu cha muhimu sana kwa sababu tumezaliwa kizazi hichi cha taalifa na zama hizi lakini hatujui miaka 5000 iliyopita huko nyuma yaani hatuna uelewa kabisa wahuko nyuma sasa lazima tujifunze kupitia mababu zetu walifanyaje fanyaje na sisi tujue tunafanyajefanyaje. Kwahiyotunatakiwa kuanza kusoma vitabu sasa hivi utaona mabadiliko akubwa  sana.

Haya ndiyo maeneo matatu ambayo unatakiwa kuanza nayo rafiki yangu ili kujiwekeza kwenye maarifa, japo yapo maeneo mengi lakini hayo unaweza kuanza nayo halafu baadae ukaendelea kujiendeleza kwa namna tofauti.

Karibu ujiunge na mtandao huu kwa kujaza fomu  ili kupata makala moja kwa moja kwenye emaili yako utatumiwa, pia usisahau kuwashirikisha wengine ujumbe huu na endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Maisha ni kuwa+fanya=pata

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 24, 2017

Mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha ONGEA LUGHA YAKO [sikiliza sauti yako ya ndani ndio mafanikio yako].

 Sadick Kilasi     December 24, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, natumai umeamka salama, hongera kwaajili ya siku hii ya leo. Karibu nikushirikishe mambo ambayo nilijifunza kutoka kwenye kitabu cha Ongea lugha yako, kitabu ambacho kimeandikwa na Deogratius S Kessy. Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika kitabu hichi, lakini yafuatayo ni baadhi ya mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki.

1.Katika zama hizi za taarifa kumekuwa na changamoto kubwa ya watu kushindwa kuishi maisha ya uhalisia na yenye maana, na hii ndo sababu ya mwandishi aliliona hilo na ndio maana akatuletea kitabu hiki. Tupo zama za taarifa, zama ambazo ni nzuri kuishi lakini ni zama ambazo zina changamoto nyingi sana. Jina la kitabu linaitwa ONGEA LUGHA YAKO [sikiliza sauti yako ya ndani ndio mafanikio yako], jina la kitabu ndilo lililo nifanya ninunue kitabu, na yafuatayo ni mambo niliyojifunza kutoka kwenye jina la kitabu.
-Kila mtu anauelewa wake katika jambo lolote, kwahiyo huwezi kuelewa kama mwingine anavoelewa
-Tumezaliwa kwa sababu kwahiyo tunapaswa kusababisha
-Tunaweza kujisikiliza wenyewe kabla ya kuwasikiliza wengine
-Vipawa vyetu vipo ndani mwetu
-Kuongea vitu vilivyo ndani mwetu bila kujali hisia za wengi yaani tutoe tulicho nacho.
Na mwisho naweza kusema akiwa na maana ya kwamba ndani ya miili yetu tuna usisi yaani unachotoa ni matokeo ya ndani mwetu. Haya ndiyo niliyo jifunza kutoka kwenye jina la kitabu na jina la kitabu linasanifu yaliyopo ndani.

2.Kuishi maisha yenye maana. Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo muhusika anatambua na kuelewa nini au jambo gani ana paswa kufanya na ndilo lilomfanya azaliwe hapa duniani. Deo Kessy anatuarika ya kwamba kama wewe ni mwandishi basi andika maandiko yatakayosaidia jamii kizazi hadi kizazi na mwisho tambua dhumuni lako na timiza dhumuni. Haya ndiyo maisha ya ukuu.

3.Katika swala la kujifunza na kuongeza maarifa, Mwandishi anatuonyesha namna gani tunapoteza mda wetu kwa kuangalia tv na kwenda sehemu mbalimbali za burudani badala ya kuongeza maarifa. Watu wengi tumekuwa watu wa kujali mambo ambayo hayana maana badala ya kujifunza na kuongeza maarifa yaani tupo tayari kujibomaa sisi na kuwajenga wengine na mwisho tunakosa kuishi maisha yenye maana.

4.Mambo ya kuzingztia kabla ya kufunga ndoa,
-Badili mtazamo wako
-Usisubiri upewe ruhusa
-Kubali cghangamoto na uzikabili
-Hakuna mafanikio ya haraka
-Uwe mtu wa kupanda kujifunza
-Kubali kulipa ghalama
-Acha ushabiki wa vitu visivyokuwa na ulazima au msingi
-Uwe na nidhamu
-Uishi katika falsafa ya kutokuwa na hofu
- Uwe mtu wa kujali afya.
Haya mambo unatakiwa kuyazingatia na kuyaishi kabla ya kufunga ndoa.

5.Staa mkubwa unayetakiwa kumfatilia sana ni wewe mwenyewe. Kuna mtu mmoja alishawahi kusema siku hizi watu hawafungwi na mapepo ila wanajifunga wao kwa wao, yaani mtu anashindwa kuishi maisha yake anaishi maisha ya mtu mwingine halafu baadae unajipoteza wewe mwenyewe. mwandishi antuasa kwa kusema jifunze kuwa wewemwenyewe, usisubili  mpaka ufukuzwe bali jifunze kwanza wewe mwenyewe ili uweze kuwa bora zaidi.

6. Katika malezi ya watotowazazi ndio wenye jukumu lao na ndio kioo, na ili tuwe na jamii bora lazima tuwe na misingi bora katika malezi ya watoto na wazazi ndio jukumu lao kubwa.

7.Kuna sehemu kumi za kuchota baraka katika maisha
-Mungu
-Wazazi
-Watu wengine
-Familia
Kwahiyo lazima tutambue nini wajibu wetu katika sehemu hizo ili tuchote baraka.

8. Falsafa ya ufagio katika maisha. Falsafa ya ufagio ni falsatfa ya unyenyekevu. Maisha ni mahusiano kwahiyo tunapaswa kujenga mahusiano bora na wengine.

Haya ni machache kati ya mengi ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu hiki, kikubwa ninachokuomba rafiki yangu jipatie kitabu hiki ili kujifunza mengi yaliyomo humo, labda nikwambie haya niliyokuandikia hapa ni machache sana kati ya mengi niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki, hakikisha unajipatia nakala yako ya kitabu.  Kukipata kitabu hichi tembelea mtaalamu.net/kessydeo.

Maisha ni kuwa+fanya=kupata.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com, Usiache kujiunga na mtandao huu na kushare kwa wengine ili uwafikie wengi zaidi.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, December 22, 2017

Hii ndio maana halisi ya kupotea

 Sadick Kilasi     December 22, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Kama wewe unaishi mjini na mtu wa kutembea hasa kwa miguu utakuwa unatambua maana halisi ya kupotea lakini pia kama wewe umezaliwa vijijini utakuwa unatambua pia dhana hii tena vizuri ya kupotea. Kupotea kupo kwa aina mbalimbali, inategea mazingira kwa jinsi yalivo.

Wakati unafika kipindi ambacho hujui wapi ulipo, tambua umepotea, katika safari yoyote ile ikifika hatua onaona kila njia unayoiona ni njia tambua hapo umepotea. Hiki ni kipindi ambaco ni kigumu sana kwenye safari zetu, na kila kitu kinategemea maamuzi yako ukifika wakati kama huu,  maamuzi utakayo fanya ndio yatakufanya uendelee kupotea zaidi au urudi katka njia kuu au njia sahihi maana unaona njia nyingi na hutambui ipi njia sahihi.

Vivyo hivyo kwenye maisha yetu, kupotea kupo, kipindi ambacho unona kiza tu yaani huoni sehemu ya kutokea tambua tayari mimi ni mpotevu. ni kipindi ambacho huwa tunaona kila fursa kwetu ni zaidi ya nyingine katika kufanya biashara, au ni kipindi ambacho tunaona ukuta mbele yetu kutokana labda tulikuwa tunataka kitu frani sasa tukifeli tunaona haiwezekani tena, huko ni kupotea, yaani usipo iona njia kwenye changamoto tambua umepotea. Wakati wote ukiwa umepotea kila kitu kinategemea maamuzi yako.

Maamuzi yako wakati ambao umepotea na wewe ukasema ngoja upoze au uondoe machungu kwa kujigunga madawa ya kulevya au kunywa pombe basi kaa na ujue unaendelea kupotea zaidi. Pombe haipunguzi mawazo , pombe inafanya ujione kama huna mawazo lakini unakuwa unayo na ndio maana mlevi huwa anakuwa kama anakatishakatisha hivi maneno yake yaani anazungumzia yale matatizo yake harafu anaacha.

Mwana mpotevu alipo potea, na alipo tambua ya kwamba nimepotea alirudi kwa baba yake kuomba msamaha, hii inatoka kwenye maandiko ya biblia. Ulipotea usijifanye wewe ndio wewe kwanza lazima ukili kwamba hapa nimepotea, Upotevu sio lazima uwe umepotea, njia hapana upotevu ni kutenda kosa, ukili kosa kama mwana mpotevu tayari unanjia ya kuanzia na hapa ndipo penye utu, mtu ambaye hawezi kukili makosa yake huyo ni mpotevu.

Kwahiyo jambo la msingi na la kutambua hapa ni kwamba, kupotea ni kuto kukili makosa yako, kuna watu hawezi hata kujisamehe wenyewe yaani hawezi kukili makosa yao. Mpendwa rafiki yangu jifunze kujishusha. kwani ajishushaye hupandishwa, ajipandishaye hushushwa.Ukifanya kosa omba samahani, sio kwamba wewe ndo zoba kabisa hapana huo ndio utu wenyewe.

Endelea kutembelea mtandao huu wa JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi, pia jiunge na mtandao huu kupata makala zaidi.

Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, December 19, 2017

Mbinu bora ya kuwa na afya bora ni hii hapa

 Sadick Kilasi     December 19, 2017     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu, natumai umeamka salama na upo tayari kwenda kutoa dhamani na kuwagusa wengine kwa namna ya kipekee kabisa kupitia kalama na vipawa ulivyo navyo, Yaweza kuwa unatumia elimu uliyo nayo kutoa thamani kwa wengine, yaweza kuwa unatumia kipawa chako kutoa dhamani kwa wengine au na wakati mwingine unatumia uzowefu ulio nao kutoa thamani kwa wengine lakini kikubwa ambacho mwenyezi Mungu anataka tuangaze kwa nafasi zetu tulizo nazo, sisi ni nuru katika giza.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii, siku mpya kwetu na mara nyingi huwa napenda kusema ni kama tumefufuliwa tena  kwa sababu tulikuwa tumelala na hatujitambui miili yetu imekufa, nafsi yetu ndiye aliye kuwa hai lakini miili ilikuwa imekufa kabisa.

Leo rafiki yangu nimekuandalia mbinu bora ya kuwa na afya bora katika maisha yako na ili uyafikie yale malengo ambayo umejiwekea.

Kufanya mazoezi, kulisha ubongo chakula chake, kula kwa afya, kulala kwa wakati, haya ni mambo yanayoeleweka kwa kila mtu, toka enzi tumekuwa tukishauliwa kufanya mambo haya na watalamu wa afya ili kulinda afya zetu.

Mpendwa rafiki yangu kuishi wewe ndio mbinu kubwa zaidi ambayo itakufanya kuwa na afya bora kabisa kabla hata hizo zingine. Maana ya kuishi wewe ni hali ambayo inatakiwa wewe uwepo katika wakati husika, kama upo nyumbani basi uwe nyumba, kama upo ofisini basi uwe ofisini yaani uwepo wako kihali na kimawazo uwe mahali pale ulipo wewe. Zama hizi za mawasiliano kumekuwa na tabia ya watu kushindwa kujenga mahusiano mazuri na wengine. mfano anaweza akawa nyumbani na familia lakini anakuwa yupo mbali kabisa kuchati na magroup ya whatsapp na matokeo yake ni kukosa kuonyesha mihemuko mizuri na watu wako wa karibu.

Mambo madogo madogo madogo tunayo dhalau ndiyo haswa yanayo haribu kabisa maisha yetu tunaalikwa kuishi maisha yale ambayo tuliopo, ukiwa nyumbani kuwanyumbani, ukiwa unasoma soma yaani kila kitu kipe umuhimu kutokana na wakati wake, tujifunze kutoka kwa wazee wetu wa zamani walivokuwa wanaishi hawakukimbizana na kitu chochote na afya zao zilikuwa bora sana na waliishi miaka mingi.

Endelea kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 068700068 au sadikla65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Haya ndiyo maumivu ambayo tunajitengenezea wenyewe

 Sadick Kilasi     December 19, 2017     MAHUSIANO     No comments   

Habari za wakati huu rafiki yangu natumai unaendelea vizuri na umekuwa una siku bora kabisa, hongera kwaajiri ya siku hii ya leo.

Kuna wakati mwingine huwa tunajitengenezea maumivu sisi wenyewe kwa kujua kabisa ya kwamba haba nitendalo si sahihi lakini utakuta bado tu utakuwa unaendelea kufanya ubaya ili hali unjua kabisa kwamba huu ni ubaya. Mara nyingi huwa tunatenda hivi tukiwa tunasababu za kujitukuza mbele za macho ya wengine ili tu uonekane upo katika nafasi fulani, mfano mtu unaweza ukawa unataka kununua gari ili uwaonyeshe wengine ya kwamba wewe unapesa wakati unajua kabisa mimi siwezi kufanya vitu kama hivi bado sijatosha.

Wakati mwingine inaweza ikawa unajaribu kumridhisha mwenzako hali ukijua kabisa hapa haiwezekani yaani hapana lakini unamwambia unaweza. Yaani unashindwa kutumia vizuri maneno haya mawili NDIYO au HAPANA, unafanya ili kujaribu kumridhisha mwenzako yaani mwili unaenda lakini nafsi inakataa, na hapo  ndipo unapojitengenezea maumivu mwnyewe. Mfano unaambiwa twende sehemu fulani unajua kabisa huna muda wakutosha unakubali tu ili kumridhisha na mwisho unajuta.

Kujaribu kumridhisha kila mtu ghalama yake ni maumivu makali ndani ya moyo wako, na matokeo yake si mazuri  mara nyingi ni ya kujuto. Na ili kulikwepa hili inatakiwa kufanya vitu kutokana na mihemuko yetu ila si kwa kulazimishwa au kujilazimisha. Kwepa ghalama hizi rafiki yangu zisizo na ulazima huo ni unafiki.

Wako SADICK KILASI wa JIKO LA UASHAURI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadkila65@gmail.com. Pia hakikisha unajiunga na matandao huu ili kupata makala mpya kila itakapo toka. 



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 17, 2017

Jinsi ya kujenga mahusiano bora na watu wako wa karibu

 Sadick Kilasi     December 17, 2017     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu siku mpya kwaajiri ya kwenda kuweka kazi katika maeneo yetu ya kazi kwa misingi ya nidhamu na kujituma. Leo ni siku ya juma tatu natumai itakuwa siku bora sana kwako kwa sababu una nguvu mpya kabisa baada ya mapumziko ya wikiendi. Rafiki yangu unapokuwa unapokea siku mpya kama hii lazima uwe na shukrani kwasababu ndio nafasi ya kipekee ya wewe kuendelea kusonga mbele. Kwahiyo shukrani inakufanya uone ya kwamba unaziada ya hapo ulipo na utaendelea kusonga mbele kwa jambo unalofanya.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii ya kipekee ambayo mimi na wewe rafiki yangu unaye soma hapa tumepewa. Bila kupoteza wakati nikukaribishe katika makala ya leo upate kujifunza yale ambayo nimekuandalia , na hichi ndicho chakula cha ubongo, twende sawa usome kwa umakini ulio makinika na sio kusoma tu.

Moja ya jambo ambalo ni la muhimu kujijengea katika maisha ya mtu ukiachana ubongo, roho yaani imani na afya basi ni mahusiano. Mahusiano yanaadhili maisha na ni jambo ambalo ni la muhimu sana katika maisha, Jambo hili halijaanzishwa na mtu bali na Mungu mwenyewe, pale Mungu alipo muumba Adam basi akamweka msaidizi wake ambaye ni Hawa. Haiba yako na tabia zako kwa kiasi kikubwa vimeathiliwa na mahusiano ya watu wanaokuzunguka.

Wastani wa watu watano ambao unaishi nao au kushinda nao ndio wamechangia haswa maisha yako kuwa hivo kwahiyo kwa namna hiyo kuna haja ya kuchagua watu sahihi wa kushirikiananao ili kujijenga vizuri kiujumla. Chukua hatu sasa kwani vitabu vya dini vimeandika usiketi balazani pa wenye mizaha. Japo kuwa unaweza kuchagua watu bora wa kushirikiana nao lakini bado unhitaji wewe mwenywe binafsi kuwa bora na kujitambua na hizi ndivyo jinsi unavotakiwa kuwa kwenye swala zima la mahusiano na watu wengine.

Tambua wewe ni wa muhimu katika jamii. Ukijitambua ya kuwa wewe ni wa muhimu katika jamii wewe mwenyewe utajisikia vizuri. Hapa sina maana ya kwamba sasa uanze kuwazalau wengine na kujiona wewe ndio wewe, sasa huo si ubinadamu, maana yangu ni kwamba kwenye umoja kuna mojamoja zaidi ya moja ambazo zinajenga umoja.

Tambua wewe ni tegemeo sio tegemezi. Ukisha jitambua ya kwamba wewe ni temeo na si tegemezi basi wewe utakuwa na msaada na jamii inayokuzunguka. Mtu anayetambua kwamba yeye ni tegemeo hawezi kubweteka hata siku moja kwahiyo jamii itakupenda kwa sababu utakuwa na msaada kwao. Utajikuta unaanzisha huduma yoyote kwenye jamii yako kwahiyo huduma ambayo ilikuwa haipo kwenye mtaa wako sasa itapatikana.

Jifunze kuwapenda watu wanao kuzunguka. Ukiipenda jamii inayo kuzunguka ni rahisi kufanya biashara palepale kwenye jamii yako. Kwa hali hiyo utajifunza ya kwamba chochote unachopata ni cha jamii kwahiyo unapaswa kuirudishia  na hivi ndivyo matajiri wenye mafanikio makubwa wanavyofanya hii inaitwa shukrani.

Nimekuonyesha hayo mambo matatu tu lakini ukweli ni kwamba yapo mambomengi sana unachotakiwa kufahamu ni kwamba unatakiwa kuwa na utu ndani yako, unatakiwa kuwajibika katika hali yoyote ile wewe ndio wewe uko peke yako watu wanakuhitaji. Falsafa ya kumpenda mtu kama hutomwona tena, ni nzuri sana kuishi nayo kwenye jamii.

Endelea kujifunza na kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi. Usiache kujiunga na mtandao huu hakikisha unajaza fomu mahali pale palipo andikwa jiunge na mtangao huu. Jambo la msingi ambalo nakuomba kama umeupenda ujumbe huu usiache kushare kwa marafiki zako ili nao wanufaike. Asante

Wako SADICK KILASI wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Maeneo manne ya kuimarisha ili kuweza kupata mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     December 17, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu tunakutana tena hapa JIKO LA USHAURI ili kuweza kujifunza yale mazuri ambayo mimi rafiki yako nimekupikia hapa na kukuletea wewe uyale maana maarifa ndicho chakula cha ubongo. Rafiki yangu hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutujalia siku hii ya leo ambayo ni siku bora sana kwetu kuliko siku zote maana maisha ni sasa yaliyopita ni kumbukumbu na ya mbele ni ya kufikirika. Kwahiyo rafiki yangu siku  ya leo ni ya muhimu sana maana kesho maandlizi yake ni leo na leo maandalizi yake yalikuwa jana. Rafiki yangu jinsi unavojiona leo ni kwasababu ya jana kwahiyo itengeneze leo kuwa siku bora ili kesho yako kuwa bora zaidi.


Rafiki yangu kuna maeneo manne ambayo unatakiwa kuyaimarisha ili kuweza  kuwa bora katika maisha yako na kuweza kupata mafanikio makubwa. Maeneo yote manne yanatakiwa kuwa bora sana na ni muhimu bila kuacha hata eneo moja na hapo ndipo utakuwa bora mafanikio yatakuwa ni yako. Maeneo hayo ni kama yafuatavyo;

Eneo la kwanza ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiroho. Eneo la kiroho ni eneo ambalo ni la muhimu sana, hapa tunazungumzia imani yako lazima uwe na imani na Mungu kwa dini yoyote bila misingi na falsafa za kidini huwezi kufanikiwa na hata kama ukifanikiwa utakuwa bado hujapa mafanikio ya kweli. Ukiishi na kuimarika katika falsafa za kidini utakuwa mtu mwenye amani na furaha na utakuwa na imani na Mungu ambaye yeye ndiye aliye tuumba sisi.

Eneo la pili ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiakili. Rafiki eneo hili ni la muhimu sana, ni eneo ambalo kila siku uwe unaimarika ubongo wako unahitaji kupata chakula chake kila siku. Kama bado hujaanza kuurisha ubongo wako chakula basi anza leo jifunze kwa bidii sana. Kuna wengine huwa wanasema mimi nishasoma shuleni siwezi kusoma tena, elimu haina mipaka na elimu ya shuleni ni kipande kidogo sana kwenye maisha elimu kubwa ipo mitaani anza leo soma vitabu, kuwa makini na watu unao kutana nao wasikilize kwa umakini ulio makinika, tembelea mitandao kama huu wa JIKO LA USHAURI na mitandao mingine, soma vitabu vya dini na zama hizi za taarifa kujifunza ni rahisi sana ukiwa na simu janja tayari utakuwa bora.

Eneo la tatu ambalo unatakiwa kuawa bora ni eneo la kiafya. Mwili wako ndio nyumba yako, ukishindwa kuwa na afya bora maeneo yote utaferi. Hakikisha unawekeza kwenye afya yko kwa kufanya mazoezi, kula kwa afya, fanya tahajudi au kusali na usafi kwa ujumla.

Eneo la nne na la mwisho ni eneo la kimahusiano. Watu ambao unahusiana nao hakikisha unauza kwao. hakikisha unauza kipawa chako, unauza tabasamu, unauza tabia zako na hayo maeneo yote hapo juu hakikisha watu wanajifunza kutoka kwako. Huwezi kubadirisha watu kwa maneno bali kwa matendo yako. Ukiuza kwa matendo lazima utafanikiwa kazana kujenga mahusiano mazuri na watu wanao kuzunguka kwa matendo yako.

Kwa kumalizia ntasema hivi , dunia inakuhitaji sana rafiki yangu, hivyo ulivyo umekamirika unachohitaji ni kujiendeleza tu na kujitambua, rafiki yangu Mungu alituumba kila mtu kwa nafasi yake aangaze na kama wewe huwa unaangalia nyota za juu ndio sisi tulivo simama katika nafasi yako toa ulicho nacho acha kuiga kutoka kwa wengine, kuna mwanafalsafa mmoja alishawahi kusema siku hizi watu hawafungwi na mapepo ila wanafungwa na watu wanaowazunguka, watu watano wanao kuzunguka ndio wastani wa maisha yako. Hatua ya kuchukua sasa hakikisha unakuwa bora kwenye maeneo hayo yote manne lazima utapata mafanikio ya kweli.

Endele kutembelea blogu hii ya jiko la ushauri ili kujifunza zaidi pia jiunge na mtandao huu ili kupata makala mpya kila itakapo toka.

Maisha ni KUWA+KUFANYA=KUPATA
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, December 15, 2017

Huyu ndiye mtu ambaye unatakiwa kuwa naye makini kwenye mahusiano yako

 Sadick Kilasi     December 15, 2017     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu natumai umeamka salama na tayari kwenda kutoa dhamani katika eneo lako la kazi na kama wewe leo ni siku ya mapumziko basi utaenda kutoa dhamani kutokana na hali yako ilivo na matendo yako. Rafiki yangu kila siku ni siku mpya kama ambavyo nimekuwa nasema siku zote unapo uona mchana hakikisha unaishi kwani kila siku tunakufa na kufufuka na ndio maana siku ikienda hairudi yaani huwezi kusema kesho itajirudia kamwe kitu hicho hakiwezi kutokea. Maisha ni sasa unapokuwa umepata fursa ya sasa tumia vizuri fursa ya wakati. Katika hali ya kuukomboa wakati tumia msemo huu kujikumbusha ; Fanya kwa wakati, kwa kuwa una wakati, utafika wakati, hutokuwa na wakati wa kufanya kwa wakati. Jambo jingine na muhimu ambalo nataka nikukumbushe ni kwamba maisha ni mwili, roho na akili.

Nisikupeleke mbali sana na karibu tujifunze katika makala ya leo na uwe umakini ulio makinika upate kuelewa vizuri kabisa  na maarifa haya yakakusaidie katika maisha yako kwa ujumla.

Mara nyingi katika maisha yetu kwenye mahusiano baina ya mtu na mtu tumekuwa tuna kutana na watu wa aina mbalimbali kwenye kazi zetu, kwenye ibada na katika mizunguko yetu kwa ujumla. Katika kukutana nao unajikuta unatengeneza mahusiano na mtu ambaye humjui vizuri ni wa aina gani kwa sababu kila mtu anatabia zake na haiba zake.

 Leo nataka kukuonyesha mtu ambaye hutakiwi kutengeneza uhusiano nae kwa haraka na mtu huyu ni mtu ambaye anataka kuwa karibu nawe kwa haraka sana.

Rafiki yangu ukikutana na mtu ambaye anataka kuwa karibu na wewe wakati wote na hana mipaka achana naye kwa lugha nyingine tunasema 'mteme'. Mimi binfi huwa sijui hii huwa inatoka wapi unakuta mtu hamjuani lakini anakupapatia kama mnajuana vile na wewe unamkaribisha mpaka nyumbani, humjui anatoka wapi, anatabia gani wewe hujali mwisho wa siku anakuibia na unaanza kulalamika nimeibiwa nimeibiwa unaulizwa na nani rafiki yangu, rafiki yako wakati hamjuani kuwa makini.

Mtu ambaye hana sababu ya kukusaidia, unatakiwa kuwa makini na watu ambao wanataka kukusaidia wala hamjuani anaonesha hali ya kukusaidia. Unatakiwa kuwa makini kwasababu utaingia kwenye mtego bila ya wewe mwenyewe kujijua, wengine wanaonesha hali ya kukusaidia ili akutapeli vizuri. Siku zote kumbuka kila apandae huvuna.

Mtu ambaye anakuazima pesa wakati hamjuani. Rafiki yangu kuwa makini unapomkopesha mtu na sio kila mtu wa kumkopesha na kusema wewe ndo una moyo mzuri unajidanganya  bure. Ngoja nikupe kisa kimoja ambacho nilisimuliwa, kuna mtu alikuwa na duka lake sasa akatokea mtu  kama mteja tu siku ya kwanza alikuja na gari  na siku ya pili hakuja na gari ukimwona kapendeza sasa akawa anatengeneza ukaribu na yule jamaa mwenye duka wakazoeana wanakaa kupiga stori jamaa kila siku ananunua vitu halafu anaacha chenji akinunua vitu vya 6000 chenji ya 4000 kwenye 10000 anaacha na siku nyingine 3000 hivohivo na mwenye duka akawa akimwuliza vipi chenji yako jamaa anasemaa acha tu, sasa yule jamaa kama baada ya siku ya  nane hivi baada ya kujenga urafiki akaja akasema bwana mimi nataka uniazime kama milioni tatu kesho nakurejeshea. mwenye duka akaona isiwe tabu jamaa mwenyewe anaonekana anazo huyu  kwasababu alikuwa anaacha chenji na anagari ataleta tu akampa. kwani hiyo kesho alimwona uliziaulizia watu wakasema hawamjui huyo mtu. Kwahiyo alitapeliwa kwanjia hiyo kwahiyo tunatakiwa kuwa makini sana. Tuache tamaa na vitu vidogovidogo.

Siku zote rafiki yangu tambua hili mahusiano hayaanzishwi kwani ni lahisi kuvujwa, mambo yanayoanzishwa yanavunjwaga, bali mahusiano yanaanza baina ya watu wawili. Tafakari hilo.

Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, December 14, 2017

Haya ndiyo mambo ambayo wewe unatakiwa uyaache yapite katika zama hizi za mabadiliko.

 Sadick Kilasi     December 14, 2017     MAHUSIANO, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na upo tayari kwenda kuweka kazi na kuwagusa wengine kwa namna moja au nyingine kutokana na shughuli zako unazofanya. Hongera rafiki yangu kwa siku hii, hebu itumie siku hii vizuri kuwapa dhamani wengine na hapo ndipo utakapokuwa umekamirisha utu mbele za wengine kwani ukitambua ya kwamba wewe unategenewa na wengine tangu hapo utakuwa umekomaa na utaweka kazi katika eneo lako la kazi.

Rafiki yangu si jambo dogo kuiona siku hii ya leo, ni jambo kubwa mno kwa sababu hii ni siku ya kipekee katika maisha yako na hivyo hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa ajili ya siku ya leo. Na popote ulipo nakusihi umshukuru mwenyezi Mungu.

Katika zama hizi za internet na taarifa yaani mawasiliano mabadiriko yamekuwa yakitokea kila siku, japo mabadiliko katika dunia hii yalianza toka hapo dunia ilipoumbwa mambo yalikuwa yanachukua  kipindi kirefu yaani mambo yalikuwa hayaendi haraka kama zama hizi.

Mabadiliko katika dunia yapo ya aina mbili, mabadiliko makubwa mfano; zama za mawe, zama za chuma,zama za viwnda na sasa tupo hizi zama za mawasiliano.lakini kuna mabadiliko madogo haya ni mabadiliko yanayopita mfano; fasheni za nguo, simu na kadharika.

Rafiki yangu katika mabadiliko haya mabadiliko ya kupita ndiyo yanayoadhiri maisha ya watu kwa kiasi kikubwa na katika mabadiliko haya ndipo mimi nilipo palenga haswa. Yanapotokea mabadiliko kunamambo ambayo huwa yanatokea ambayo ni mazuri na mabaya. Unachotakiwa ni kuwa makini na mabadiliko haya.

Yafuatayo ni mabadiliko ambyo wewe utakiwa uyaache yapite mbali na wewe yaani usihangaike nayo kwenda nayo sambamba kwa sababu sio kila mabadiliko yanayotokea ni mabaya laha sha mengine ni mazuri na unatakiwa kuwa makini sana.

Fasheni za nguo zisizo faa.Kuna nguo ambazo hazina maadili ambazo wewe mwenyewe ukivaa unajua kabisa ya kwamba hii nguo haifai kuvaliwa. vinguo vifupi viache vipite,nguo zinazo bana ziache zipite.

Misemo mibovu. Kuna misemo ambayo huwa inazuka ambayo sio rafiki katika familia zetu na hata kwa watu wetu wa karibu, misemo michafu kabisa, lugha za kihuni na kauli mbalimbali ambazo hazina maadili, tunazijua lakini mimi nashindwa kuzitaja kwa sababu ni mbaya kuzungumzia sana maneno mabaya.

Mwenendo wako yani tembea yako. Rafiki yangu mwendo unaotembea uwe na maadili sio unatembe unanyodokanyodoka hiyo haifai kabisa. Tembea mwendo wa kawaida. Kuna tembea zingine mitaani hazifai kabisa inatakiwa kuwa makini unakuta wavaa nguo zinazobana harafu wanatembea mwendo fulani ambao sio mzuri kimaadili. tuwe makini na hii ni kwa wote waume na wake.

Tabia yako kiujumla. Wewe ni mtu mkamilifu kabisa kwahiyo kiujula hutakiwi kuwa na mambo ya ajabuajabu tabia yako kiujumla iwe nzuri mpka kwenye fasheni za nywele lazima uwe makini.

Kwa kumalizi ni kwamba  mabadiliko yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo lakini pamoja na kuwa yana hasala lakini mabadiliko ni ya muhimu sana katika dunia hii. Rafiki yangu ili kunufaika na mabadiliko yanayotokea kila siku inatakiwa kuwa makini na kuwa na watu sahihi wanao kuzunguka. Jiandae na mabadiliko unafaike nayo.


Endelea kutembelea blogu hii ya jiko la ushauri kujifunza zaidi, ili kupata makala mpya zinazotoka kila siku tafadhari jiunge na nasi,utapokea makala moja kwa moja kwenye email yako. HAKIKISHA UNAJAZA HIYO FOMU HAPO CHINI  YA BLOGU HII PALIPOANDIKWA JIUNGE NAMI AU BONYEZA REGISTRETOR. Pia kama umeipenda makala hii naomba unisaidie kushare kwa watu wengine unaopenda ujumbe huu uwafikie na wanufaike nao pia.

Ni mmi mwenye kukujali SADICK KILASI 
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com. Tafadhari wasiliana nami kwa changamoto yoyote ile tutashilikiana.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, December 13, 2017

Huyu ndiye mtu pekee ambaye wewe unatakiwa kumjua vizuri katika maisha yako.

 Sadick Kilasi     December 13, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena rafiki yangu tunakutana tena ili tuweze kushirikiana kwa namna moja au nyingine na kuweza kujifunza zaidi. Hongera rafiki yangu kwa ajiri ya siku hii mpya ambayo mwenyezi Mungu kakujalia lakini hata mimi pia sina budi kumshukuru mwenyezi Mungu aliye nijalia siku hii. Kikubwa ni kutambua ya kwamba upo duniani kufanya nini na nini kusudi lako la maisha.

Katika zama hizi za mawasiliano kumekuwa na changamoto kubwa sana ya watu kujisahau wao wenyewe ni wakina nani? Na ndiomana leo rafiki yangu nimeona nikukumbushe ya kwamba badala ya kujaribu kumjua kila mtu nataka kukuonesha mtu ambaye wewe unatkiwa kumjua vizuri na kwa uhakika ili aweze kukupa mafanikio makubwa.


Kama nilivo kudonolea hapo juu ya kwamba zama hizi ni zama za mawasiliano sasa katka kufanya mawasiliano kumekuwa na tabia ya watu wamekuwa wanawajua watu wengine zaidi kuriko wanavojijua wao wenyewe. Na hii imekuwa tabia ya watu kutaka kumjua kila mtu anaye mzunguka lakini wao wenyewe wanajisahau kujijua.

Rafiki yangu ipo haja kubwa sana ya kujijua wewe mwenyewe na huna haja ya kumjua mtu mwimgine kwa sababu hata ufanye nini ili umjue huwezi kumjua uhalisia wake. Kama mzazi ameshindwa kumjua mwanaye wewe unawezaje kumjua? Mzazi angemjua mapema mwanae basi asingeacha mwanae awe mwizi au ghahidi.

Rafiki yangu unaarikwa kujitambua wewe mwenyewe kwanza na  ni muhimu sana kujitambua. Unajitambua kwa kujiuliza maswali wewe mwenyewe na majibu utakayokuwa unapata basi ndo wewe. Jiulize swali wewe ni nani? Sasa usijipe jibu kwamba wewe labda Sadick hapana kuna utofauti kati ya wewe ni nani? na jina lako ni nani? rafiki yangu jiulize swali kwanini unafanya unachokifanya? jiulize maswali mengi kuhusu wewe na jijibu wewe mwenyewe.

Ishi wewe kama wewe.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, December 12, 2017

Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya wakati unapo taka kumaliza tabia hizi ambazo zinakuzuia kufikia mafanikio.

 Sadick Kilasi     December 12, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Habari za leo rafiki yangu? Natumai umeianza siku yako vizuri na kwa hamasa kubwa kabisa. Hongera rafiki yangu kwaajiri ya siku hii ya leo ambayo mwenyezi Mungu kakujalia sasa ni wewe kwenda kuweka kazi ili kutimiza kusudi lako.

Karibu ujifunze kwenye makala hii ya leo ambayo leo nimeona nikushirikishe wewe rafiki yangu yenye kichwa kinachosema 'Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya wakati unapokutana kitu hiki kizuricha kukupa mafanikio'. 

Katika maisha kuna vitu ambavyo huwa tunafanya lakini hatuvipendi kabisa. Vitu hivi vinaweza kuwa ni kazi au katabia fulani ambacho wewe mwenyewe unachukia kukifanya lakini unakuta umwefanya tu bila mwenyewe kuelewa na wakati mwingine unaelewa lakini unakuta unafanya tu kwa sababu ya mazoea.


Mara nyingi kama ni tabia unaweza kukuta uliijenga bila wewe mwenyewe kuijua kwamba hii ni tabia mbaya lakini baadae ukajua kumbe hii tabia hafai sasa unataka kuibadilisha lakini unajikuta unashindwa, mfano; kuongea sana mbele za watu, labda kula harakaharaka, sasa unajikuta unatamani kubadilisha tabia kama hizi lakini unashindwa kabisa.

Binafsi kitu ambacho ni kigumu kukibadili jua hicho ni kitu kizuri. Nasema ni kitu kizuli endapo wewe mwenyewe ukichukulia kama changamoto kwako na siku zote vitu kama hivi matokeo yaliyajificha nyuma yake huwa yanakuwa ni mazuri sana.Kwa mfan wewe ni muongeaji sana mbele za watu inamaana wewe sio msikivu lakini ukivuka hiyo changamoto tayali utakuwa msikivu na utajifunza mengi sana.

Kuna mbinu ambazo unaweza kutumia kubadili tabia kama hizi, unachotakiwa kukifanya unatakiwa kujiuliza imekuwajekuwaje mpaka nimefikia hapa? mchakato mzima ulio kupelekea pale ulipo yaani matokeo hayo yanayo kusumbua halafu mwenyewe sema nimekosea. Ndio lazima ukili mwenyewe kwamba nimekosea hata kama kuna mtu alisababisha uwe hivo hata kama ni mzazi ila kwasababu wewe ndiye unayefanya inatakiwa ukili sasa na baada hapo usimpe lawama mwingine hata shetani usimpe lawama, hata Mungu usimpe lawama na mtuyeyote wa karibu yako ila wewe na wewe na sema mimi sitaki tena kufanya jambo hili.

Ni bora kupona ugonjwa bila kutumia dawa kuriko kupona kwa kutumia dawa.
Wako SADICK KILASI
Mawsiliano ni 068700768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, December 11, 2017

Hii ndio falsafa ambayo kila mtu inatakiwa kuiishi.

 Sadick Kilasi     December 11, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku ngingine tena ambayo ni siku mpya, natumai umeamka salama na upo tayari kwenda kuongeza ufanisi katika maeneo yako ya kazi hongera sana rafiki yangu kwa sababu wewe ni mmoja wa watu wa kipee ambaye mwenyezi Mungu kakuchagua kuiona siku hii ya leo. Rafiki yangu kuamka na kuona siku mpya si jambo la kulichukulia kawaida na ndiomaana tunapo iona siku mpya ni sawa na mtu aliye kufa na kufufuka tena maana ukilalala unakuwa hujielewi miili yetu inakuwa imekufa na jambo lolote linaweza kufanyika na usijue kitu gani kimetokea.

Mungu tunakushukuru kwaajili ya upendo wako wa kutupa kibali cha kuiona siku hii ya leo, katika dunia hii iliyo jaa kiza kinene mbaraka wako unatenda kazi kila siku kwahilo tunakushukuru na siku zote wewe watufanya kuwa washindi katika maisha yetu na kwahilo pia tunakushukuru. tunaomba utusamehe dhambi zetu.

Rafiki yangu karibu tujifunze katika makala na maada ya leo ili uweze kujengeka katika maisha yako. Maisha ni safari ndefu sana kwahiyo kila siku unatakiwa kujifunza na kupata jambo jipya ili kuwa bora katika kukabiliana na changamoto za maisha.


Tafuta kama hutokufa milele lakini mtumikie Mungu kama utakufa kesho, hii ndio falsafa ambayo kila mmoja wetu anatakiwa kuiishi katika maisha yake. Unatakiwa uishi katika kusimamia kitu ili usije ukadondoka kwa chochote na ndio maana ya maisha.

Tunajua kabisa katika swala la utafutaji hakuna mipaka ya kutafuta, huwezi ukasema sasa nishapata nilichokuwa natafuta sasa ngoja nilale ndani tayari nimetosheka hicho kitu hakipo ila kuna kupumzika na ndio maana Mungu alisema fanya kazi siku sita pumzika siku moja. Rafiki yangu utafutaji hauna mipaka kabisa kama dunia ilivyokuwa haina mipaka , tafuta uwezavyo ili upate kuwasaidia watu wengi zaidi na Mungu atakubariki zaidi.

Katika kumtumikia Mungu hili ni jambi la muhimu sana unatakiwa kujua ya kwamba pasipo yeye wewe huna mafanikio. Katika kufanya mambo yako lazima utambue MUNGU wakati wote anakuona kwahiyo lazima uwe na hofu juu yake na mafanikio yako yatakuwa katika mstari ulio nyooka.

Tafuta kama hutokufa milele lakini mtumikie Mungu kama utakufa kesho. Endelea kutembelea mtandao huu wa JIKO LA USHAURI ili kujifunza zaidi.

Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 10, 2017

Hivi ndivyo ambavyo tunavyotakiwa kutazama juu ya mambo mema na mabaya.

 Sadick Kilasi     December 10, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, siku mpya kabisa ya kwenda kuweka kazi na alama katika maisha na kumbukumbu zetu za baadae. Katika hali hii ya kuiona siku mpya hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii maana pasipo yeye sisi hatuwezi sikuzote sisi tukilala tu kama wafu lakini yeye huja kutuasha tena, wapo watu ambao wamelala na hawajaamka, wapo watu ambao waliiwekea vipaumbele vikubwa sana siku hii ya leo lakini hawajaiona sisi ni akina nani mpaka tuione siku hii, hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya upendeleo huu aliotupa haijalishi tupo katika wakati mgumu kiasi gani kwasababu kakupa siku na nafasi basi ujue wakati wowote makubwa yanaweza kutokea.

Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii mpya ya leo, hii ni siku ambayo ni yakipekee kwetu, maana siku hii sisi tunaenda kufanya kwa ukubwa na kupata mafanikio, asante kwaajili kutupendelea na tunaomba utusamehe dhambi zetu.

Rafiki yangu karibu katika maada ya leo ambayo nitaigusia kwa ufupi kabisa ili mengine nikuuachie wewe mwenyewe ukiwa unatafakari juu ya jinsi tunavyotazamaau kuchukulia juu ya mambo mema na mabaya. Rafiki yangu hii maada ni pana na ndio maana nimekwaambia nitasema kwa uchache lakini mengi wewe mwenyewe rafiki yangu ni wa kwenda kutafakari.


Unajua rafiki yangu wakati fulani mtu anweza akfanya jambo ambalo hatupendezwi nalo kabisa na kwa harakaharaka tukaona ya kwamba yule mtu tukaona hafai kabisa kwenye jamii au hatufai kabisa, wakati mwingine huwa tunaona ya kwamba jambo ambalo wanafanya kundi la watu fulani ya kwamba ni baya na halifai kabisa kufanya na mtu na tunachukulia ya kwamba ya kwetu ndio ya muhimu sana. Mfano; katika dini zetu hizihizi wapo watu ambao wanaona ya kwamba waislamu hawafai kabisa na wengine wanaona wakisto hawafai kabisa, tunaona kama wengine wanafanya makosa makubwa sana. Swali je wewe ndiye unaye hukumu?

Rafiki yangu kutambua mema na mabaya ni kujipa mzigo mkubwa sana, kwanini utambue wema na ubaya? je wajua hilo jambo kwanini linafanyika? kwanini unajipa mamlaka ya Mungu? je vipi Mungu angetambua mema na mabaya kwako vipi umetenda mema kiasi gani na ubaya kiasi gani?

Mpendwa rafiki yangu kabla kuanza kumhukumu mtu jiulize swali je hivi Mungu angekuwa ananihukumu saizi hapa mimi ningeonekanaje? Mambo unayo yatazama kwa ubaya saizi wakati ukifika unaweza kutazama kwa uzuri, na mambo ambayo unatazam kwa uzuri saizi wakati ukifika unaweza kutazama kwa ubaya. Rafiki yangu vya mwili havijakamirika bado kumbuka YESU alianza kwa kupendwa lakini akaja kupingwa na walewale walio mpenda mpaka jogoo akawika mara tatu bado mtu aliendelea kumkana.

Ujumbe wangu ni usitoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio wakati wewe unaboliti ndani yako.

Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, December 8, 2017

Huyu ndiye mtu pekee ambaye wakati wote wewe unatakiwa kumfanyia wema.

 Sadick Kilasi     December 08, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, siku mpya na ya kipekee kwewtu sisi mimi na wewe rafiki yangu msomaji wa blogu yetu ya JIKO LA USHAURI natumai umeamka salama na upo tayari kwenda kuweka juhudi katika maeneo yako ya kazi, pamoja hayo yote rafiki yangu hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa utujalia siku hii mpya ambayo ni siku ya kipekee kwetu kwa sababu hakuna siku kama hii maishani mwetu, kwahiyo hili si jambo la kuchukulia kawaida katika maisha yetu. Mungu tunakushukuru kwa kutujalia kuiona siku hii mpya, sio kwa sababu ya uwezo wetu bali ni kwaajili ya upendo wako kwetu sisi, tunaomba utubariki siku hii ikawe siku ya mafanikio kwetu na kila mmoja akapate kumgusa mwingine kwa namna utavyombariki, tunaomba utusamehe dhambi zetu.

Karibu rafiki yangu ujifunze jambo ambalo mimi rafiki yako nimeona nikushirikishe ili kwa pamoja tuifanye dunia ni mahala salama na pa furaha katika maisha ywtu.'Huyu ndiye mtu pekee ambaye wakati wote wewe unatakiwa kumfanyia wema', na hii ndio maada ambayo nimeamua nikushirikishe .

Mpendwa rafiki yangu kama kuna mtu ambaye wewe huwa unafikiria kumtendea mambo mazuri na kumpa furaha basi mtu asiye kufaa ndiye mtu pekee kwako ambaye wewe unatakiwa kumtendea wema. Inawezekana ukawa unajiuliza nitamtendeaje wema mtu asiye nifaa? Lakini ukweli ni kwamba wema kwake ndiyo haki yake.


Najua siyo jambo rahisi kumpa wema mtu ambaye unamchukia, mtu ambaye anakuchukia, mtu ambaye kakufanyia mambo mabaya lakini yeye ndiye anayestahili wema wako. Rafiki yangu haijalishi yeye unamchukia kiasi gani lakini wewe unatakiwa usimchukie na umlipe wema wakati inawezekana wewe unachukia anavyo fanya lakini njia pekee ya kubadirisha tabia yake ni kumpa wema mtu huyo ambaye hastahili kupata wema kabisa kwani ndio haki yake.

Binadamu huwa tunawapenda wanao tupenda, lakini vipi yule ambaye hapendwi atapendwa na nani maana huyu ndiye anaye stahili kupata upendo kwa sababu hana upendo na siku zote dunia ndiyo inavyotaka mjazie ambaye hana ila punguza kwa mwenye kingi.

Kila mtu anastahili hapa duniani kwahiyo rafki yangu mtu ambaye humpendi ndio daraja lako la mafanikio kiroho na hata kiwmili. Je hivi unajua ukimtendea wema mtu ambaye hastahili kitu gani kitatokea? Ukweli ni kwamba hata kusahau kamwe na tayari wewe mwenyewe binafsi utakuwa katika mazingira mazuri katika maisha yako.Wakati wote atakuona wewe ni mtu wa tofauti unaye stahili kwenye jamii na atakuheshimu. Yesu alilitambua hilo ndio maana hata wanafunzi wake aliowachagui ni watu ambao walikuwa hawafai kwa matendo yao wengi walikuwa ni wanyang'anyi na wauwaji na leo hii ndiye mtu pekee anayekumbukwa zaidi duniani.

Rafiki yangu unachotakiwa kukikumbuka kila siku ni kwamba lipa wema kwa ubaya kwa faida yako na sio kwamba unafaidisha yeye hapana. Kwasababu kila jambo tunalolifanya hapa duniani kwa fadayetu binafsi hata kama unamfanyia mtu mwingine.
Shida za wengine sio furaha kwako na wewe inakuhusu.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 3, 2017

Nyeusi na nyeupe si rangi

 Sadick Kilasi     December 03, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Habari mpendwa rafiki yangu? natumai umeamka salama . Ni siku nyingine tena rafiki yangu ambayo ni siku mpya kabisa kama rafiki yangu umebahatika kuiona siku hii basi huna budi kumshukuru mwenyezi Mungu aliye kujalia siku mpya.

Rafiki yangu dunia hii imejaa giza nene sana si mchana si usiku bali kuna giza nene sana na ndio maana mara nyingi tunajikwaa katika changamoto mbalimbali. Giza hili nene kuna mambo ambayo limeficha rafiki yangu sasa ni wajibu mimi na wewe rafiki yangu kufichua hayo mambo. Na kila mmoja katika giza hili anawajibu wake na nafasi yake ya kuangaza katika sehemu ambayo yupo.

Wakati unatoa kile kitu ambacho kimejificha ndani yako basi hapo unaondoa giza ambalo limejificha ndani yako na hiyo ndio dunia yako. Wakati unaangaza na kutoa mwanga kwa wengine kwa kutoa huduma ya kipekee basi hapo umeleta mwangaza kwa wengine na wewe unakuwa unang'aa. Inasemekana kuwa nyota unazoziona kule juu wale ni binadamu.

Giza unaloliona angani na unaona nyota inaangaza katika nafasi yake hivyo ndivyo maisha yalivyo kwahiyo dunia imejaa giza lakini kila mmoja anaangaza kwa nafasi yake. Rafiki yangu angalia kwa umakini namna nyota zilivo jipanga na kisha jitadhimini wewe ni nani katika hizo nyota nyota iliyo fifia  au nyota inayo ng'aa? Giza lile ni jamii, jamii inakuhitaji wewe uangaze kwa nafasi uliyopo na kama hutoangaza kwa nafasi yako giza litatanda.

Rafiki yangu wewe upo kwenye dunia kwaajili ya wengine acha kuwa mbinafsi kilicho ndani yako wape wengine wanufaike. Ukweli ni kwamba hakuna rangi nyeusi wala nyeupe  ila  ni kwamba penye weusi [giza] panahitaji weupe [mwanga] ili pawe peupe na ndio maana huwezi kuwasha taa wakati wa mchana.

Washa taa kwenye giza yako watu wanahitaji mwanga wako. Endelea kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI ili kujifunza zaidi.
Kanuni ya maisha ni KUWA+FANYA=POKEA.
Wako SADICK KILASI 
Mawasiliano ni 068700768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 28, 2017

Huu ndio wakati ambao unaweza kujenga fikra zako na ukajengeka na baadae kuyafikia mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 28, 2017     UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu yetu ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeshinda vizuri upo salama kabisa. Bila shaka siku yako imekuwa bora sana. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye katufikisha wakati huu wa usiku na hatuna budi kumshukuru, Mungu wetu muumba mbingu na nchi tunakushukuru kwaajiri ya siku hii ya leo asante kuturinda siku nzima, tazama sasa ni wakati wa usiku huu na tunenda kulala, wakati huu nyama zetu zinaenda kufa, ehe Mungu wetu ukawe pamoja nasi na ukatuamshe salama katika siku ya kesho, tunaomba utusamehe dhambi zetu tulizofanya leo na hata sasa.

Mpendwa rafiki yangu kuna wakati ambao ni mzuri kwetu sisi kujifunza na kujenga fikra zetu kwa usahihi. Wakati huu mtu huwa anajengeka kwa ubora sana na hasa unapokuwa unajirudiarudia akili huwa inafanya kazi kubwa sana. Wakati wenyewe ni wakati wa changamoto. Changamoto ndizo huwa zinamjenga mtu nakuwa bora sana.

Mpendwa rafiki yangu kama unataka kujengeka kiakili na hekima basi huu ndio wakati wake hakuna sehemu nyingine ambayo unaweza kujengeka kiakili kama wakati huu. Watu wengi wenye mafanikio makubwa duniani hao ndio wametatua changamoto nyingi sana na ndozo zili waweka pale walipo.

Ukweli ni kwamba maisha bila ya changamoto si maisha, fikiria ya kwamba tungekuwa tunaishi bila ya changamoto vipi ingekuwaje? maisha yangekuwa wapi? vipi tungekuwa hapa tulipo au tungekuwa huko tulikokuwa zama za mawe?  Ukweli ni kwamba maisha bila changamoto tungekuwa tumekufa kabisa maana vitu ambavyo vimekufa havina changamoto.

Mpendwa rafiki yangu wakati changamoto inapotokea hakikisha unaiangalia kwa jicho la upana, ipe wakati wakufikiria wewe mwenyewe bila ya kukimbilia kwa watu kuomba msaada na hapa ndipo mantiki yako itakapo kuwa kubwa. Unaweza ukapata jibu la kukosea lakini ukishajua ya kwamba hapa nimekosea na ukarudia tena ukafanya vizuri ni wazi kabisa ya kwamba hutokosea tena.

Sisi binadamu tunapenda mambo yetu yawe laini na wakati tunakutana na changamoto tunaona kuwa pale ndio ukomo wa mambo lakini kumbe haipo hivo. Changamoto yako ni yako huna haja ya kumpa mtu mwingi lakini ukishindwa mwambie akupe maelwkezo sio maelezo. Maelekezo yatakujenga inamaana kwa hali hiyo huwezi kufanya makosa tena.

Mpendwa rafiki yangu jambo la kufanya saizi ni kuepuka zile hamasa sizo na maana, mtu unachangamoto unaambiwa tulia tu mambo yatakaa sawa, ukweli ni kwamba unatakiwa kufikiria siyo kusema utafanikiwa pasipo njia. Chukua hatua saizi jiulize uliambiwa ya kwamba utafanikiwa tu leo uko wapi? Hamasa inatakiwa ukipe wewe mwenyewe sio mtu mwingine kwani maisha ni wewe, hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuchukua jukumu la maisha yako.

Kama wewe huwa unakuwaga na mawazo yale ya kusaidiwa na mtu mwingine yaani kuwa tegemezi basi umepotea sana kwa sababu huwezi ukajijenga wewe mwenyewe binafsi. Changamoto ni ladha ya maisha na utamu wake anujua muhusika.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi lakini pia unaweza kujiunga nami kwa kujaza fomu ambayo inamaelezo ya kwamba jiunge nami. 

Utatu wa maisha ni KUWA+FANYA=SUBIRI MATOKEO.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
WWWW
W
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 27, 2017

Hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi kwenye jamii inayokuzunguka ili kupata mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 27, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa rafiki yangu, natumai umeamka salama na upo na mwenye nguvu tele. Kitu pekee ambacho ni cha dhamani sana ni wewe kuwa na pumzi hiyo uliyo nayo haijarishi upo katika hali gani, ukuwa na pumzi na unaweza kusoma tayari wewe unaweza kufanya kitu chochote na kikawagusa wengine na kuleta matokeo ulio talajia. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu katika hili kwasababu bila yeye tusingeweza kufanya kitu chochote maana kwa usiku ambao tulikuwa tumelala ni sawa mtu mfu. Kwa hili tumshukuru mwenyezi Mungu, tunakushukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii mpya na uzima huu tulio nao, tunakuomba katika siku hii ya leo kila tutakapo kwenda kukanyaga ukatubariki na uwepo wako ukadhihirike, tunakuomba utusamehe hdambi zetu.

Mpendwa rafiuki yangu katika maisha hasa ya sasa kumekuwa na changamoto nyingi sana. Ajira na mahusiano vimekuwa vitu vinavo wapa watu wakati mgumu katika maisha yao. Rafiki yangu tukizungumzia kwenye swala la ajira kwa sasa limekuwamni tatizo kubwa sana, watu ambao walikuwa na uhakika wa ajira lakini lakini sasa   hawana uhakika tena katika ajira zao. Ukweli ni kwamba mambo yamebadirika haswa katika nyanza hizi za ajira.

Tukizungumzia kwenye swala la mahusiano nalo pia limeadhirika sana katika zama hizi za mawasiliano. Ukweli ni kwamba mawasiliano yamekuja kuleta tofauti kubwa sana kwenye uhusiano wetu na watu wetu wa karibu. Zamani mtu wa mbali akitaka kuwasiliana na wewe alikuwa anaandika barua na inakufikia wewe kwa hali hiyo barua zilikua zinatugusa sana wakati tunasoma unajisikia muhemuko fulani. Lakini sasa haipo kabisa.

Kwenye swala zima la kazi na mahusiano zamani mtu ukipata kibarua unaenda kumfuata mtuwako wa karibu na kumwambia bwana e kuna kibarua sehemu flanitwende tukafanye tupate ridhiki lakini kwa sasa haipo hiyo. Watu ambao walikuwa na uhakika na ajira na kazi zao kwenye makampuni na katika sehemu mbalimbali  lakini kwa saizi unaweza ukaamka asubuhi na ukaambiwa tumempata mtu wa nafasi yako kwa sababu ana uwezo zaidi yako.

Ndoa zimekuwa zikivunjika kwa sababu watu wanaoana kwa sababu wanategemea matarajio fulani kutoka kwa wenza wao wanapokosa hivo vitu basi ndoa imeisha.

Hvi ndivyo unavyotakiwa kujiweka na kuishi kwenye jamii yako, kuwa MUHIMU na sio kuwa wa dhamani. Unapokuwa wamuhimu katika jamii yako kamwe hakuna mtu ambaye atachukua nafasi yako inamaana pasipo wewe hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika. Mpendwa wangu mambo yanabadirika unaweza ukaamka asubuhi unaenda kazini unafika kazini unaambiwa hamna kazi hapa na kazi hauna. Rafiki yangu unaweza ukaamka asubuhi akaambiawa na mwenza wako wewe hunifai huna pesa na sababu zingine mbalimbali.

Unapokuwa wa dhamani kumbuka wewe unapanda na kushuka na kwa zama hizi za mabadiriko mbona kesho dhamano yako inaisha, hapo ndipo unapoanza kujiuliza nimelogwa nini? Hujalogwa tatizo ni wewe umejiweka katika dhamani na kwa hali hio watu wamepanda dhamani na hapo ndipo unaanza kukimbizana na ajira.

Wewe ni mtu wa muhimu sana kwenye jamii na ni wakipekee sana, ipo njia ya wewe kuwa mtuwa muhimu katika jamii inayokuzunguka, jiulize swali hili darasani bila mwalimu inawezekana? Na hapo utajua kwanini unatakiwa kuwa wa muhimu.

Endelea kutembelea JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi.
Fomula ya maisha ni kuwa+fanya=matokeo
Wako SADICK KILASI.
Mawasiliano 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 24, 2017

Hii ndio sheria ya dunia

 Sadick Kilasi     November 24, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena,  natumai umeamka salama kabisa na Mungu ni mwema aliyetuamsha kutoka kwenye kifo cha mwili maana mwili wetu ukiwa umelala ni sawasawa  na mtu aliyekufa, hata mtu akija kukufanyia lolote wewe huwezi kujua kwahiyo Mungu mweyewe ndio anajua. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya hili, Mungu tunakushukuru kwa ajiri ya kutuamsha salama, unatupenda zaidi ya kawaida kwa hili tunakushukuru siku zote upo na sisi kwaajili ya kuturinda na sisi hatuna kitu cha kukulipa wewe asante sana, tunaomba katika siku hii ukawe nasi pioa tunaomba utusamehe makosa yetu.


Mpendwa rafiki yangu leo sitaandika lolote zaidi ya haya kukwambia ya kwamba sheria ya dunia ni kwamba toa kwanza harafu suburi matokeo yatakayo toka.

Naomba uende ukatafakari juu ya hili je watu wanaotoa wapoje? Kumbuka ya kwamba kwa neema yake sisi tulipona kwahiyo uzima tulionao hatukupata bure.

Uwe wewe kama wewe.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 23, 2017

Kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine huwezi kukipata kamwe

 Sadick Kilasi     November 23, 2017     MAHUSIANO, NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena, hongera kwa kuamshwa salama natumai umuzima kwa sababu aliye kuasha kakuamsha akiwa anatambua ya kwamba wewe ni mazima. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye katuamsha kutoka kwenye hali ambayo kimwili tunakuwa tumekufa baki nafsi zetu tu ndo zinakuwa zinaishi, hongera sana rafiki yangu mpendwa ni jambo zuri kutoka kwenye hali hiyo ya kifo cha mda.


Sasa rafiki yangu mpendwa leo nimekutayarishia maada hii ambayo inasema 'kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine huwezi kukipata kamwe' je ni kitu gani hichi? Basi kuwa na mimi mpaka mwisho na tutiririke wote kwa pamoja utajua maana chochote kwa taratibu kinakujengea utaratibu.

HESHIMA ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu, kama bado wewe unasubiri heshima kutoka kwa wengine ili na wewe uweze kuwaheshimu wao utasubiri sana na huwezi kupata hiyo heshima kamwe. 

Unajua kwanini? kwa sababu wote mnasubiri kitu kimoja mwenzako anasubiri wewe umuheshimu na wewe unasubiri heshima kutoka kwake. Mpendwa rafiki yangu hebu fikiria kitu kimoja ukichukua sumaku mbili halafu ukazielekezea ule upande unao fanana vipi huwa zinagusana? Nafikiri huwa hazigusani  na ndivyo ilivyo kwenye mmoja asipokuwa tofauti hanuwezi kutengeneza kitu kipya.

Mpendwa rafiki yangu hii ni asili ya dunia hebu fikiria kwanini kusingekuwa na matajiri tu dunia nzima, labda niseme vipi dunia ingekuwa ya matajiri pekee? au ya masikini pekee? Nafikiri kitu hicho haakiwezekani lazima kuwe na tajiri na maskini, jumulisha na kutoa, positive and nagative haya sasa mambo ya umeme.

Mpendwa rafiki yangu anza sasa kuwahaimu watu, wewe uwe wa kwanza kuwaheshimu wao na mambo yataenda sawa kama wewe ulivokuwa unataka. Heshima sio kuwa fedha au kuwa na kitu fulani hapana huo  ni woga wala sio heshima. Watu wanawaogopa wenye pesa sio wanawahesimu. Hebu fikiria jambo hili yule mtu aliyekuwa anamuheshimu boss wake kwa sababu anapesa na yeye akipata pesa unafikiri atamuheshimu tena?

Neno langu kwako mpendwa rafiki yangu ni wape heshima wengine nao watakuheshimu kumbuka wao wanasubiri kutoka kwako.

Yote juu yako.
Makala hii imeandikwa na Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 22, 2017

Ijenge tabia ikisha nayo itakujenga wewe

 Sadick Kilasi     November 22, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa rafiki yangu natumai umeamka salama na upo tayari kwaajili ya siku hii ya leo. Ni jambo la jema na kufurahisha kuiona siku hii ukiwa na pumzi  njema kwa sababu hicho ndicho kiashiria  pekee kinacho kutamburisha ya kwamba bado unanafasi ya kufanya jambo fulani ambalo litakupeleka katika hatua fulani na mwisho kuifikia ndoto yako. Mwili ambao hauna pumzi haufanyi jambo lolote ni kama gogo tu kwahiyo weweambaye una hekalu lenye pumzi huna budi kumshukuru mwenyezi Mungu; Mungu tunashukuru kwa ajili ya siku hii ya leo ambayo umetuamsha salama tunaomba utubariki siku hii ikawe siku ya ukuu kwetu yenye furaha na mafanikio katika mambo tutakayoenda kuyafanya uwepo wako ukadhihirike, tunaomba urtusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu rafiki hinyo sasa ulivyo unavo jiona, unavo jitafsiri, hayo mafanikio uliyo nayo, hizo tabia unazozipenda au kuzichukia vyote hinyo vimesababishwa na wewe mwenyewe, wewe ndiye uliyejifikisha hapo ulipo sasa unaweza ukawa unapachukia hapo ulipo au unapapenda lakini wewe ndiye mhusika mkuu unaweza ukasema sasa nitoke hapa nilipo niende katika hatua nyingine nzuri zaidi au nzuri kutokana hapa ambapo sipapendi.

Mpendwa wangu kujenga tabia nzuri si jambo rahisi, kujenga tabia ya kukupereka kwenye mafanikio sio jambo rahisi. Kujenga tabia mbaya ni rahisi sana lakini ni vigumu kuacha ila kujenga tabia nzuri ni ngumu kujenga lakini ni rahisi kuacha. Kwa maana hiyo ili uwe na tabia nzuri ni lazima sasa ufanye maamuzi ni magumu na uanze kuyafanya na uyaendeleze. Na hii huwa inaanza pole pole sio kwa papala tabia murudio wa mambo kwahiyo jinsi unavorudiarudia baadae inakuwa ndo tabia yako.

Kama unataka kujenga tabia ambayo ni nzuri inabidi uanze kujenga vichocheo vya tabia yako ambayo unataka kuijenga  mfano; wewe unataka kuamka kila siku asubuhi na mapama ila wewe huwa huwezi kuamka asubuhi na mapema kichocheo cha kwanza unaweka alamu, alamu ikipiga tu unaamka kwahiyo kupitia alamu umeaka asubuhi na mapema kinachofuata ni labda wewe unataka kuanza tabia ya kufanya mazoezi asubuhi kwahiyo kichocheo cha kufanya mazoezi kuamka mapema.

Sasa tayari baada ya hapo umemaliza mazoezi labda unasali au tahajudi baada hapo unaenda kuoga kwahiyo mazoezi ni kichocheo cha kusali ni kichocheo cha kwenda kuoga baaada ya kwenda kuoga labda unasoma au kuandika kwahiyo unajijengea hivo na inaendelea ratiba ya namna hiyo mpaka jioni kwa hiyo tayari unakuwa umeijenga siku katika hali ya ratiba labda kwa wakati mwingine unaweza kujiwekea vipaumbele vyako wakati wa kazi za mchana. Sasa mrudio wakila siku baadae inabadirika na kuwa tabia yako.

Ili kuwa karibu nami na kupata makala mpya na huduma nyingine hakikisha unajiunga nami kwa kujaza fomu ipo hapo palipo andikwa jingenasi tayari unakuwa unapokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 21, 2017

Mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa kwenye maisha

 Sadick Kilasi     November 21, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamuka salama kabisa na upo tayari kwenda kuongeza dhamani katika shughuli zako. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii maana bila yeye tusingeweza sisi peke yetu. Wapo watu ambao wameshindwa kuiona siku hii ya leo kwahiyo sisi tulio iona hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kusema asante Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo, ambayo ni siku ya kipee kwetu na tunakushukuru kwa kutusaidia kuiona siku hii ya leo tunaomba ukawe pamoja nasi katika siku hii yote na ikalete matokeo mazuri na tunaomba utusamehe makosa yetu.

Mpendwa wangu rafiki yangu karibu sana kwenye makala hii ya leo ambayo mimi rafiki yako nimekuandalia ambapo nitakuonyesha mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa kwenye maisha yako.

Kwanza naomba nikutaarifu ya kwamba sisi watu wa ngozi nyeusi hatupendi kujifunza kabisa yaani mtu kujifunza anaona ni kitu cha ajabu sana yaani tunapenda kila kitu kwetu kiwe rahisi tu kama kuangalia TV maana kuangalia sio kazi ila kazi ipo kwenye kulichukulia lile jambo ambalo umeliangalia yaani wewe binafsi unamutazamo gani juu ya kitu ambacho umekiangalia.

Wakati tulipo hitimu ngazi mbalimbali, tujua tumesha maliza kila kitu lakini ukweli ni kwamba hujamaliza na huwezi maliza kwa  sababu mambo yanabadilika sasa kama mambo yanabadilika wewe usipo jifunza si utaachwa pale na mawazo yako ya zamani unaweza ukasema mbona mimi naona poa tu mambo yanaenda, kiuhalisia yanaenda lakini lazima ujue wewe unaendeshwa mara huku mara huku kwa sababu huna upekee uliopo ndani yako. Kwahiyo kujifunza kunakupa wewe upekee wako binafsi.

Sasa nisikuchoshe sana mpendwa wangu ngoja tuende mojakwamoja katika mbinu mbalimbali za kujifunza kwenye maisha.

Mbinu ya kwanza ni kujifunza kupitia mazungumzo yako na mtu mwingine au kikundi fulani. Sasa hapo kila neno linalozungumzwa lazima ulichukulie kwa uzito kiasi na uliangalie kwa mtazamo wako binafsi na ili kujifunza zaidi lazima uwape nafasi zaidi kuriko wewe kuwa mzungumzaji zaidi na wewe unakuwa msikilizaji sana kuriko kuzungumza. Haijarishi yuho mtu anazungumza kitu gani hata kama ni pumba anaongea lazima usikilize itakusaidia kitu fulani. Kama wewe unataka mambo mazuri kila siku sasa mabaya utayajuaje? Kuwa msikilizaji.

Penda sana kujisomea vitabu mbalimbali. Hii mbinu kwangu mimi naichulia kama mbinu kuu katika kujifunza, usomaji wa vitabu una raha yake bwana na hapa ndipo kwenye maarifa ya watu chanya, kwa sababu mtu anayeandika kitabu huwa anatoa kitu kilichopo ndani yake kwahiyo kama wewe ukikisoma kile kitabu tayari unachukua upekee wa mtu mwingine. Sasa ukisoma vitabu vingi utatengeneza kitu kipya kutoka kwenye vitu mbalimbali. Mpiganaji BLUES LEE alijifunza style mbalimbali za mapigano halafu akaja kutengeneza kitu ambacho kipya kabisa na ndicho kilicho mpa jina kubwa.

Jifunze kupitia internet. Saizi mambo yamerahizishwa yaani mda wote unaweza kujifunza yaani kila kitu kipo poa tu unacho taka unakipata.

Jifunze kupitia mikanda mbalimbali ya cd. Ndio unaweza kujifunza kupitia mbinu hii kwa kuangali tv ukajifunza.

Zipo mbinu mbalimbali za kujifunza ni nyingi sana kama luenda kwenye semina  kwahiyo ni nyingi sana lakini kujifunza ni jukumu lako wewe lazima uongeze maarifa kwa namna yoyote ile na kujifunza ndiko kunawapa watu mafanikio pia kunawapa watu uhuru wa maisha.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 20, 2017

Kila kitu kipo tayari unasubiri nini rafiki yangu kupuliza kipyenga?

 Sadick Kilasi     November 20, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu, karibu katika makala hii ya leo ili uweze kujifunza na kuongeza maarifa. Natumai unaendelea vizuri na upo tayari kwa ajiri ya siku hii ya leo katika shuguli zako za maendeleo au kuongeza dhamani katika maeneo mbalimbali. Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii ya leo, huwezi kusema ni kwaajiri ya uwezo wangu utakuwa unaongopa sana. Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii.

Mpendwa rafiki yangu kati ya kipindi ambacho mambo yote yapo sawa basi zama hizi mambo yote yapo tayari, ni kila nyanja mambo yapo sawa na tunainjoi sana kuishi zama hizi ambazo ni zama za mawasiliano. Chochote unachotaka kipo tayari ni wewe kukamirisha tu ratiba yako, kitu gani unataka? puliza kipyenga sasa.

Je unataka kuanza biashara na hauna mtaji? Huwezi kusema siwezi kuanza biashara kwa sabababu sina mtaji wa kuanzia utakua unakosea sana japo hukosei kwa namna moja au nyingine unakosea, zipo biashara ambazo unaweza kuanza hivyohivyo ulivyo na ukaendelea mbele. Biashara kama network marketing[biashara ya mtandao] ni biashara ambazo unawza kuanza bila ha mtaji.

Je unataka kuanza mazoezi na unashindwa namna ya kunza? Tayari kila kitu kipo cha kukuongoza ni wewe tu sasa kusema sasa nataka kuanza mazoezi download alamu aplication ambazo zitakuamsha asubuhina jifunze namna kuanza mazoezi, zipo aplication ambazo zina sound ambazo zitakupa hamasa ya kuendelea kufanya mazoezi.

Unataka kuandika na kuacha alama kwenye maisha yako kila kitu kipo sawa, blogu ni jukwaa zuri sana la kuandika na unakuwa unaandika mafunzo au habari yoyote ile unayotaka kutoa cha msingi uwe unatoa kitu cha dhamani kwenye jamii na inafaidika kutoka kwako na hapa ndipo unapoweza kuanza kutengeneza kipato chako kwa kutumia tu simu hiyohiyo uliyo nayo, kwahiyo tayari biashara bila mtaji.

Je wewe unataka marafiki wa ukweli wa kusafiri nao katika ndoto yako unaona kama huna watu sahihi? Mpendwa wangu kama wewe upo tayari basi wapo wengine nao wapo hivohivo  sasa wewe anza kuwaonesha watu hao ya kwamba wewe ni mtu sahihi sasa kama hivi kama wewe unataka kwa rafiki yangu au mtu wangu wa nguvu basi jaza form hapo chini tayari unakuwa rafiki yangu tutakuwa wote.

Kila kitu kipo sawa ila wewe haupo sawa na wewe ndio refa wa maisha yako, na kila kitu kina mda wake kama ulivyo mpira wa miguu  ni dakika tisini tu kwahiyo ndio maana tuliwekewa masaa, kama huchukui hatua shauri yako. Mchezo dakika tisini tu unaweza ukaishi kwa mfumo huo tu kwa kuchukulia maisha yapo ndani ya dakika tisini, ukipoteza dakika moja inakula kwako.

Puliza kipyenga sasa wakati ni sasa hili ndilo jambo la msingi kwenye maisha yako na chukua hatua.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com


Subscribe to our mailing list

* indicates required
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 17, 2017

Hii ndio silaha pekee uliyonayo wewe ukiitumia vizuri lazima itakupa mafanikio makubwa

 Sadick Kilasi     November 17, 2017     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI, USHAURI     No comments   

Wakati mwingine unaweza ukawa unajiuliza nitafanya nini kwenye hii dunia mbona kila kitu ambacho nataka kufanya kinafanywa na wengine? Wakati bado hujaingia kwenye hilo jambo ulikuwa unaona kama wafanyaji ni wachache lakini baada ya kuingia unaona wanaofanya ni wengi na tayari unaanza kukata tamaa nakuona ya kwamba huwezi kushinda nao.

Ni kweli kama unataka kushindana nao hutoweza utashindwa lakini nikutie moyo ya kwamba wewe unayo silaha pekee ambayo silaha yenyewe ni wewe kama wewe. Ikiwa kwenye shughuli hiyo utasimama wewe kama wewe lazima utapenya kwenye kundi kubwa  ambalo linawashindani wengi.

Utasimamama wewe kama wewe kwa kutoa kile kitu ambacho kipo ndani yako. Unajua binadamu kabla hujatoa hiyo sauti ya nje huwa unajiongelesha ndani kwanza yaani unaweza ukajiuliza swali harafu ukajijibu mwenyewe halafu ndipo unamuuliza mtu mwingine sasa ile sauti yako ya ndani ndiyo uitumie kama silaha ya mafanikio yako.

Kitu ambacho unatakiwa kukitambua mpendwa wangu ni kwamba binadamu hatufanani kwa kila kitu hata muwe mapacha wa kufanana bado kuna vitu vinatofautiana. Ukisimama wewe kama wewe lazima uoneshe uhalisia wako watu watakupenda wewe kama Sadick Kilasi hiyo kopi watu hawata ipenda.

Ukijitofautisha na washindani wako kwa jia hii ni lazima utafanikiwa tu haijarishi mnafanya kitu kimoja mpo wangapi kumbuka unatakiwa kufanya sauti yako ya ndani, mawazo yako ya ndani na ikisha fanya kwa ubunifu mkubwa tayari wewe utatengeneza chako.

Kitu cha kukumbuka hapa lazima utambue ya kwamba sio kila mtu ni wakwako bado kuna watu wengine sio wa kwako, watu wanao mpenda Sadick sio wote watakao mpenda Juma na huo ndio upekee wenyewe na ukitaka watu wasio kukubali wakukubali basi ongeza ubunifu lakini sio wote watakukubali.

Kama wewe ni mwimbaji anza kuimba wape watu ujumbe mzuri na wakipekee  na watu waseme ladha kama hizi nitazipata wapi. Kama wewe unapenda kuandika andika kwa ubunifu mkubwa.

Fanya kazi kwa ugmu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 16, 2017

Woga wako ndio umaskini wako

 Sadick Kilasi     November 16, 2017     NJOZI, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa wangu msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na upo tayari kwaajiri ya siku hii ya leo na kupambana ili kuzifikia ndoto zako. Nikupe hongera mpendwa wangu na nikutie moyo ya kwamba kuiona siku hii ya leo ni ushindi mkubwa sana, wewe waweza ukawa umekata tamaa ya kwamba mimi siwezi kwasababu nipo kitandani miaka kumi sijaamka naumwa kwahiyo mimi ni wa kusubili kufa tu lakini ukweli haupo hivo kuumwa ni hali tu na bado hivyo ulivyo kuna jambo kubwa unaweza ukalifanya  na hata yule mzima wa afya bado naye hana galanti ya maisha yake lolote linaweza kutokea kwa hapo ulio kuanzia sasa hebu fanya kitu ukiamini maisha bado yanaendelea.

Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii, Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii, tunaomba utujalie wakati wote wa siku nzima na utusamehe makosa yetu.

Hapo ulipo sasa hivi ni kwaajili ya maamuzi uliyo kuwa umeyafanya huko nyuma, kama ulikuwa unafanya maamzi ambayo ni mabovu najua hali yako sio nzuri kutokana maamuzi yako lakini kama maamuzi yako yalikuwa mazuri sasahivi unakula dodo. Siku zote maamuzi ndio hutupa matokeo ya uamuzi wako.

Binadamu sisi tunakitu kinachoitwa woga,ni kitu kibaya sana hichi japo wakati mwingine ni kitu kizuri sana lakini mimi naona kwa woga ni mbaya zaidi maana unaogopa jambo ambalo huna uhakika nalo yaani unaogopa kwa sababu hutaki kuingia kwenye hatari, hutaki kuingia kwenye hatari kwa sababu unataka vitu ambavyo tayari vimefanywa na wengine.

Unaogopa kuingia kwenye biashara kwa sababu unahofia kushindwa. Sasa hofu ya kushindwa inatoka wapi wakati kunaneno 'shindwa' hapo inamaana kushindwa kupo huwezi kushinda wakati wote, wewe ni nani ushinde wakati wote chukua hatua ukisndwa leo anza tena.

Unaogopa kuacha kazi yenye kipato kidogo na hulidhiki nayo kwa sababu hujui wapi pa kuanzia. Ni woga wako tu kwani hapo ulipo ulianzaje chukua hatua na jifunze juu yakujikwamua na kipato chako kidogo.

Kwanini unaogopa kwa sababu huna uhakika na matokeo yajayo na njia rahisi ya kuushinda woga wako ni kufanya lile jambo unnaloogopa. Na hata kama ukishindwa wewe ni wa kwanza kushindwa? Hivi unajua woga unaumiza zaidi kuliko matokeo hayohayo ya kushindwa. Wewe unafikiria nini kichwani mwako endapo utashindwa? Unaogopa kuchekwa? Je ukibaki hapo ulipo hutochekwa? Nani atajali zaidi unachofanya nafikiri ni wewe mwenyewe zaidi utajicheka mwenyewe, Je unafikiri watu wajari sana unachofanya wala hawana mpango na wewe na hata akiongea kitu sawasawa na kutoa maoni au like kwenye post ya facebook. Wacha woga kwa sababu ya watu wewe ndio wa muhimu zaidi.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com

M
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 15, 2017

Jiulize, mimi nipo bize na nini?

 Sadick Kilasi     November 15, 2017     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama na unaendelea vizuri. Najua upotari kwa mapambano ya wajibu wetu wa kutafuta mafanikio ali kuzifikia ndoto ni jambo zuri. Kitu cha muhimu siku mpya unapoianza na lazima kujitafakari wewe umetoka wapi, uko wapi, na unaenda wapi? Siku hazigandi huwezi kuifidia ikitoka imetoka hata uew vipi mda hauzuiriki.

Ni jambo la kumushukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii, Mungu tunakushuru kwaajiri ya siku hii asante kwa ktujalia, tunaomba siku hii ikawe siku ya mazuri kwetu kila tutakachofanya kikalete matokeo chanya, tusamehe makosa yetu.

Leo mpendwa rafiki yangu nimeona nikuulize swali wewe upo bize kitu gani? kitu gani kinakuchukulia mda wako kwa kiasi kikubwa? Nimi hasa unafanya  wewe mpaka unakuwa bize? Usinijibu mimi wewe ndio ujijibu mwenyewe.

Imekuwa ni kawaida mtu akiulizwa vipi wewe mbona hupatikani? Mimi nipo bize na kazi. Je ni kweli upo bize na kazi au ndo unatuzuga? Ni kweli upo kazini lakini vipi mda wote unafanya kazi au mda mwingi unatumia kuchati tu kwenye mitandao ya kijamii. Vipi hupi stori maeneo ya kazi wewe na marafiki zako na kumasema bosi? Jijibu mwenyewe wewe ndio unaya jua.

Vipi masaa yako ishilini na nne unayapangiliaje? Mda wa kuingiza kipato chako unakuwa au mda wote unakuwa kanisani tu, umesahau kabisa mda huu wa kipato?

Vipi wewe sio mzee wa huku na huko unazulula tu, mara nipo Mbezi mara nipo Mbagara huna jambo la muhimu unalofanya, upo bize na mabo ambayo hayana umuhimu.

Rafiki yangu mpendwa mda ni mali sana na unapokuwa bize na kitu kifanye kwa uhakika na kikupe matokeo unayotaka ubize usio na maana hauna maana  ni sawa na kusukuma ukuta harafu hausogei. Pangilia mda wako unapokuwa bize uwe bize kwelikweli usijidanganye mwenyewe na ukweli hauficha jambo mwisho sisi nje tutaona tu ulichokuwa unafanya.

Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ▼  2017 (58)
    • ▼  December (16)
      • Kitu gani kipo nyuma ya hili? Kitu gani kitafuata ...
      • Maeneo matatu ambayo unatakiwa kuwa makini kama un...
      • Mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha ONGEA...
      • Hii ndio maana halisi ya kupotea
      • Mbinu bora ya kuwa na afya bora ni hii hapa
      • Haya ndiyo maumivu ambayo tunajitengenezea wenyewe
      • Jinsi ya kujenga mahusiano bora na watu wako wa k...
      • Maeneo manne ya kuimarisha ili kuweza kupata mafan...
      • Huyu ndiye mtu ambaye unatakiwa kuwa naye makini k...
      • Haya ndiyo mambo ambayo wewe unatakiwa uyaache yap...
      • Huyu ndiye mtu pekee ambaye wewe unatakiwa kumjua ...
      • Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya wakati unapo taka...
      • Hii ndio falsafa ambayo kila mtu inatakiwa kuiishi.
      • Hivi ndivyo ambavyo tunavyotakiwa kutazama juu ya...
      • Huyu ndiye mtu pekee ambaye wakati wote wewe unata...
      • Nyeusi na nyeupe si rangi
    • ►  November (22)
      • Huu ndio wakati ambao unaweza kujenga fikra zako n...
      • Hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi kwenye jamii inayo...
      • Hii ndio sheria ya dunia
      • Kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine h...
      • Ijenge tabia ikisha nayo itakujenga wewe
      • Mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa...
      • Kila kitu kipo tayari unasubiri nini rafiki yangu ...
      • Hii ndio silaha pekee uliyonayo wewe ukiitumia viz...
      • Woga wako ndio umaskini wako
      • Jiulize, mimi nipo bize na nini?
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates