Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii, Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii, tunaomba utujalie wakati wote wa siku nzima na utusamehe makosa yetu.
Hapo ulipo sasa hivi ni kwaajili ya maamuzi uliyo kuwa umeyafanya huko nyuma, kama ulikuwa unafanya maamzi ambayo ni mabovu najua hali yako sio nzuri kutokana maamuzi yako lakini kama maamuzi yako yalikuwa mazuri sasahivi unakula dodo. Siku zote maamuzi ndio hutupa matokeo ya uamuzi wako.
Binadamu sisi tunakitu kinachoitwa woga,ni kitu kibaya sana hichi japo wakati mwingine ni kitu kizuri sana lakini mimi naona kwa woga ni mbaya zaidi maana unaogopa jambo ambalo huna uhakika nalo yaani unaogopa kwa sababu hutaki kuingia kwenye hatari, hutaki kuingia kwenye hatari kwa sababu unataka vitu ambavyo tayari vimefanywa na wengine.
Unaogopa kuingia kwenye biashara kwa sababu unahofia kushindwa. Sasa hofu ya kushindwa inatoka wapi wakati kunaneno 'shindwa' hapo inamaana kushindwa kupo huwezi kushinda wakati wote, wewe ni nani ushinde wakati wote chukua hatua ukisndwa leo anza tena.
Unaogopa kuacha kazi yenye kipato kidogo na hulidhiki nayo kwa sababu hujui wapi pa kuanzia. Ni woga wako tu kwani hapo ulipo ulianzaje chukua hatua na jifunze juu yakujikwamua na kipato chako kidogo.
Kwanini unaogopa kwa sababu huna uhakika na matokeo yajayo na njia rahisi ya kuushinda woga wako ni kufanya lile jambo unnaloogopa. Na hata kama ukishindwa wewe ni wa kwanza kushindwa? Hivi unajua woga unaumiza zaidi kuliko matokeo hayohayo ya kushindwa. Wewe unafikiria nini kichwani mwako endapo utashindwa? Unaogopa kuchekwa? Je ukibaki hapo ulipo hutochekwa? Nani atajali zaidi unachofanya nafikiri ni wewe mwenyewe zaidi utajicheka mwenyewe, Je unafikiri watu wajari sana unachofanya wala hawana mpango na wewe na hata akiongea kitu sawasawa na kutoa maoni au like kwenye post ya facebook. Wacha woga kwa sababu ya watu wewe ndio wa muhimu zaidi.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
M
0 comments:
Post a Comment