Mungu tunakushukuru kwaajili ya siku hii mpya ya leo, hii ni siku ambayo ni yakipekee kwetu, maana siku hii sisi tunaenda kufanya kwa ukubwa na kupata mafanikio, asante kwaajili kutupendelea na tunaomba utusamehe dhambi zetu.
Rafiki yangu karibu katika maada ya leo ambayo nitaigusia kwa ufupi kabisa ili mengine nikuuachie wewe mwenyewe ukiwa unatafakari juu ya jinsi tunavyotazamaau kuchukulia juu ya mambo mema na mabaya. Rafiki yangu hii maada ni pana na ndio maana nimekwaambia nitasema kwa uchache lakini mengi wewe mwenyewe rafiki yangu ni wa kwenda kutafakari.
Unajua rafiki yangu wakati fulani mtu anweza akfanya jambo ambalo hatupendezwi nalo kabisa na kwa harakaharaka tukaona ya kwamba yule mtu tukaona hafai kabisa kwenye jamii au hatufai kabisa, wakati mwingine huwa tunaona ya kwamba jambo ambalo wanafanya kundi la watu fulani ya kwamba ni baya na halifai kabisa kufanya na mtu na tunachukulia ya kwamba ya kwetu ndio ya muhimu sana. Mfano; katika dini zetu hizihizi wapo watu ambao wanaona ya kwamba waislamu hawafai kabisa na wengine wanaona wakisto hawafai kabisa, tunaona kama wengine wanafanya makosa makubwa sana. Swali je wewe ndiye unaye hukumu?
Rafiki yangu kutambua mema na mabaya ni kujipa mzigo mkubwa sana, kwanini utambue wema na ubaya? je wajua hilo jambo kwanini linafanyika? kwanini unajipa mamlaka ya Mungu? je vipi Mungu angetambua mema na mabaya kwako vipi umetenda mema kiasi gani na ubaya kiasi gani?
Mpendwa rafiki yangu kabla kuanza kumhukumu mtu jiulize swali je hivi Mungu angekuwa ananihukumu saizi hapa mimi ningeonekanaje? Mambo unayo yatazama kwa ubaya saizi wakati ukifika unaweza kutazama kwa uzuri, na mambo ambayo unatazam kwa uzuri saizi wakati ukifika unaweza kutazama kwa ubaya. Rafiki yangu vya mwili havijakamirika bado kumbuka YESU alianza kwa kupendwa lakini akaja kupingwa na walewale walio mpenda mpaka jogoo akawika mara tatu bado mtu aliendelea kumkana.
Ujumbe wangu ni usitoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio wakati wewe unaboliti ndani yako.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment