Ni jambo la kumushukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii, Mungu tunakushuru kwaajiri ya siku hii asante kwa ktujalia, tunaomba siku hii ikawe siku ya mazuri kwetu kila tutakachofanya kikalete matokeo chanya, tusamehe makosa yetu.
Leo mpendwa rafiki yangu nimeona nikuulize swali wewe upo bize kitu gani? kitu gani kinakuchukulia mda wako kwa kiasi kikubwa? Nimi hasa unafanya wewe mpaka unakuwa bize? Usinijibu mimi wewe ndio ujijibu mwenyewe.
Imekuwa ni kawaida mtu akiulizwa vipi wewe mbona hupatikani? Mimi nipo bize na kazi. Je ni kweli upo bize na kazi au ndo unatuzuga? Ni kweli upo kazini lakini vipi mda wote unafanya kazi au mda mwingi unatumia kuchati tu kwenye mitandao ya kijamii. Vipi hupi stori maeneo ya kazi wewe na marafiki zako na kumasema bosi? Jijibu mwenyewe wewe ndio unaya jua.
Vipi masaa yako ishilini na nne unayapangiliaje? Mda wa kuingiza kipato chako unakuwa au mda wote unakuwa kanisani tu, umesahau kabisa mda huu wa kipato?
Vipi wewe sio mzee wa huku na huko unazulula tu, mara nipo Mbezi mara nipo Mbagara huna jambo la muhimu unalofanya, upo bize na mabo ambayo hayana umuhimu.
Rafiki yangu mpendwa mda ni mali sana na unapokuwa bize na kitu kifanye kwa uhakika na kikupe matokeo unayotaka ubize usio na maana hauna maana ni sawa na kusukuma ukuta harafu hausogei. Pangilia mda wako unapokuwa bize uwe bize kwelikweli usijidanganye mwenyewe na ukweli hauficha jambo mwisho sisi nje tutaona tu ulichokuwa unafanya.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment