Wakati unafika kipindi ambacho hujui wapi ulipo, tambua umepotea, katika safari yoyote ile ikifika hatua onaona kila njia unayoiona ni njia tambua hapo umepotea. Hiki ni kipindi ambaco ni kigumu sana kwenye safari zetu, na kila kitu kinategemea maamuzi yako ukifika wakati kama huu, maamuzi utakayo fanya ndio yatakufanya uendelee kupotea zaidi au urudi katka njia kuu au njia sahihi maana unaona njia nyingi na hutambui ipi njia sahihi.
Vivyo hivyo kwenye maisha yetu, kupotea kupo, kipindi ambacho unona kiza tu yaani huoni sehemu ya kutokea tambua tayari mimi ni mpotevu. ni kipindi ambacho huwa tunaona kila fursa kwetu ni zaidi ya nyingine katika kufanya biashara, au ni kipindi ambacho tunaona ukuta mbele yetu kutokana labda tulikuwa tunataka kitu frani sasa tukifeli tunaona haiwezekani tena, huko ni kupotea, yaani usipo iona njia kwenye changamoto tambua umepotea. Wakati wote ukiwa umepotea kila kitu kinategemea maamuzi yako.
Maamuzi yako wakati ambao umepotea na wewe ukasema ngoja upoze au uondoe machungu kwa kujigunga madawa ya kulevya au kunywa pombe basi kaa na ujue unaendelea kupotea zaidi. Pombe haipunguzi mawazo , pombe inafanya ujione kama huna mawazo lakini unakuwa unayo na ndio maana mlevi huwa anakuwa kama anakatishakatisha hivi maneno yake yaani anazungumzia yale matatizo yake harafu anaacha.
Mwana mpotevu alipo potea, na alipo tambua ya kwamba nimepotea alirudi kwa baba yake kuomba msamaha, hii inatoka kwenye maandiko ya biblia. Ulipotea usijifanye wewe ndio wewe kwanza lazima ukili kwamba hapa nimepotea, Upotevu sio lazima uwe umepotea, njia hapana upotevu ni kutenda kosa, ukili kosa kama mwana mpotevu tayari unanjia ya kuanzia na hapa ndipo penye utu, mtu ambaye hawezi kukili makosa yake huyo ni mpotevu.
Kwahiyo jambo la msingi na la kutambua hapa ni kwamba, kupotea ni kuto kukili makosa yako, kuna watu hawezi hata kujisamehe wenyewe yaani hawezi kukili makosa yao. Mpendwa rafiki yangu jifunze kujishusha. kwani ajishushaye hupandishwa, ajipandishaye hushushwa.Ukifanya kosa omba samahani, sio kwamba wewe ndo zoba kabisa hapana huo ndio utu wenyewe.
Endelea kutembelea mtandao huu wa JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi, pia jiunge na mtandao huu kupata makala zaidi.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment