Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii ya kipekee ambayo mimi na wewe rafiki yangu unaye soma hapa tumepewa. Bila kupoteza wakati nikukaribishe katika makala ya leo upate kujifunza yale ambayo nimekuandalia , na hichi ndicho chakula cha ubongo, twende sawa usome kwa umakini ulio makinika na sio kusoma tu.
Moja ya jambo ambalo ni la muhimu kujijengea katika maisha ya mtu ukiachana ubongo, roho yaani imani na afya basi ni mahusiano. Mahusiano yanaadhili maisha na ni jambo ambalo ni la muhimu sana katika maisha, Jambo hili halijaanzishwa na mtu bali na Mungu mwenyewe, pale Mungu alipo muumba Adam basi akamweka msaidizi wake ambaye ni Hawa. Haiba yako na tabia zako kwa kiasi kikubwa vimeathiliwa na mahusiano ya watu wanaokuzunguka.
Wastani wa watu watano ambao unaishi nao au kushinda nao ndio wamechangia haswa maisha yako kuwa hivo kwahiyo kwa namna hiyo kuna haja ya kuchagua watu sahihi wa kushirikiananao ili kujijenga vizuri kiujumla. Chukua hatu sasa kwani vitabu vya dini vimeandika usiketi balazani pa wenye mizaha. Japo kuwa unaweza kuchagua watu bora wa kushirikiana nao lakini bado unhitaji wewe mwenywe binafsi kuwa bora na kujitambua na hizi ndivyo jinsi unavotakiwa kuwa kwenye swala zima la mahusiano na watu wengine.
Tambua wewe ni wa muhimu katika jamii. Ukijitambua ya kuwa wewe ni wa muhimu katika jamii wewe mwenyewe utajisikia vizuri. Hapa sina maana ya kwamba sasa uanze kuwazalau wengine na kujiona wewe ndio wewe, sasa huo si ubinadamu, maana yangu ni kwamba kwenye umoja kuna mojamoja zaidi ya moja ambazo zinajenga umoja.
Tambua wewe ni tegemeo sio tegemezi. Ukisha jitambua ya kwamba wewe ni temeo na si tegemezi basi wewe utakuwa na msaada na jamii inayokuzunguka. Mtu anayetambua kwamba yeye ni tegemeo hawezi kubweteka hata siku moja kwahiyo jamii itakupenda kwa sababu utakuwa na msaada kwao. Utajikuta unaanzisha huduma yoyote kwenye jamii yako kwahiyo huduma ambayo ilikuwa haipo kwenye mtaa wako sasa itapatikana.
Jifunze kuwapenda watu wanao kuzunguka. Ukiipenda jamii inayo kuzunguka ni rahisi kufanya biashara palepale kwenye jamii yako. Kwa hali hiyo utajifunza ya kwamba chochote unachopata ni cha jamii kwahiyo unapaswa kuirudishia na hivi ndivyo matajiri wenye mafanikio makubwa wanavyofanya hii inaitwa shukrani.
Nimekuonyesha hayo mambo matatu tu lakini ukweli ni kwamba yapo mambomengi sana unachotakiwa kufahamu ni kwamba unatakiwa kuwa na utu ndani yako, unatakiwa kuwajibika katika hali yoyote ile wewe ndio wewe uko peke yako watu wanakuhitaji. Falsafa ya kumpenda mtu kama hutomwona tena, ni nzuri sana kuishi nayo kwenye jamii.
Endelea kujifunza na kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi. Usiache kujiunga na mtandao huu hakikisha unajaza fomu mahali pale palipo andikwa jiunge na mtangao huu. Jambo la msingi ambalo nakuomba kama umeupenda ujumbe huu usiache kushare kwa marafiki zako ili nao wanufaike. Asante
Wako SADICK KILASI wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment