Hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii, siku mpya kwetu na mara nyingi huwa napenda kusema ni kama tumefufuliwa tena kwa sababu tulikuwa tumelala na hatujitambui miili yetu imekufa, nafsi yetu ndiye aliye kuwa hai lakini miili ilikuwa imekufa kabisa.
Leo rafiki yangu nimekuandalia mbinu bora ya kuwa na afya bora katika maisha yako na ili uyafikie yale malengo ambayo umejiwekea.
Kufanya mazoezi, kulisha ubongo chakula chake, kula kwa afya, kulala kwa wakati, haya ni mambo yanayoeleweka kwa kila mtu, toka enzi tumekuwa tukishauliwa kufanya mambo haya na watalamu wa afya ili kulinda afya zetu.
Mpendwa rafiki yangu kuishi wewe ndio mbinu kubwa zaidi ambayo itakufanya kuwa na afya bora kabisa kabla hata hizo zingine. Maana ya kuishi wewe ni hali ambayo inatakiwa wewe uwepo katika wakati husika, kama upo nyumbani basi uwe nyumba, kama upo ofisini basi uwe ofisini yaani uwepo wako kihali na kimawazo uwe mahali pale ulipo wewe. Zama hizi za mawasiliano kumekuwa na tabia ya watu kushindwa kujenga mahusiano mazuri na wengine. mfano anaweza akawa nyumbani na familia lakini anakuwa yupo mbali kabisa kuchati na magroup ya whatsapp na matokeo yake ni kukosa kuonyesha mihemuko mizuri na watu wako wa karibu.
Mambo madogo madogo madogo tunayo dhalau ndiyo haswa yanayo haribu kabisa maisha yetu tunaalikwa kuishi maisha yale ambayo tuliopo, ukiwa nyumbani kuwanyumbani, ukiwa unasoma soma yaani kila kitu kipe umuhimu kutokana na wakati wake, tujifunze kutoka kwa wazee wetu wa zamani walivokuwa wanaishi hawakukimbizana na kitu chochote na afya zao zilikuwa bora sana na waliishi miaka mingi.
Endelea kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI kujifunza zaidi.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 068700068 au sadikla65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment