Sasa rafiki yangu mpendwa leo nimekutayarishia maada hii ambayo inasema 'kama bado unasubiri kitu hiki kutoka kwa wengine huwezi kukipata kamwe' je ni kitu gani hichi? Basi kuwa na mimi mpaka mwisho na tutiririke wote kwa pamoja utajua maana chochote kwa taratibu kinakujengea utaratibu.
HESHIMA ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu, kama bado wewe unasubiri heshima kutoka kwa wengine ili na wewe uweze kuwaheshimu wao utasubiri sana na huwezi kupata hiyo heshima kamwe.
Unajua kwanini? kwa sababu wote mnasubiri kitu kimoja mwenzako anasubiri wewe umuheshimu na wewe unasubiri heshima kutoka kwake. Mpendwa rafiki yangu hebu fikiria kitu kimoja ukichukua sumaku mbili halafu ukazielekezea ule upande unao fanana vipi huwa zinagusana? Nafikiri huwa hazigusani na ndivyo ilivyo kwenye mmoja asipokuwa tofauti hanuwezi kutengeneza kitu kipya.
Mpendwa rafiki yangu hii ni asili ya dunia hebu fikiria kwanini kusingekuwa na matajiri tu dunia nzima, labda niseme vipi dunia ingekuwa ya matajiri pekee? au ya masikini pekee? Nafikiri kitu hicho haakiwezekani lazima kuwe na tajiri na maskini, jumulisha na kutoa, positive and nagative haya sasa mambo ya umeme.
Mpendwa rafiki yangu anza sasa kuwahaimu watu, wewe uwe wa kwanza kuwaheshimu wao na mambo yataenda sawa kama wewe ulivokuwa unataka. Heshima sio kuwa fedha au kuwa na kitu fulani hapana huo ni woga wala sio heshima. Watu wanawaogopa wenye pesa sio wanawahesimu. Hebu fikiria jambo hili yule mtu aliyekuwa anamuheshimu boss wake kwa sababu anapesa na yeye akipata pesa unafikiri atamuheshimu tena?
Neno langu kwako mpendwa rafiki yangu ni wape heshima wengine nao watakuheshimu kumbuka wao wanasubiri kutoka kwako.
Yote juu yako.
Makala hii imeandikwa na Sadick Kilasi
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment