Katika zama hizi za mawasiliano kumekuwa na changamoto kubwa sana ya watu kujisahau wao wenyewe ni wakina nani? Na ndiomana leo rafiki yangu nimeona nikukumbushe ya kwamba badala ya kujaribu kumjua kila mtu nataka kukuonesha mtu ambaye wewe unatkiwa kumjua vizuri na kwa uhakika ili aweze kukupa mafanikio makubwa.
Kama nilivo kudonolea hapo juu ya kwamba zama hizi ni zama za mawasiliano sasa katka kufanya mawasiliano kumekuwa na tabia ya watu wamekuwa wanawajua watu wengine zaidi kuriko wanavojijua wao wenyewe. Na hii imekuwa tabia ya watu kutaka kumjua kila mtu anaye mzunguka lakini wao wenyewe wanajisahau kujijua.
Rafiki yangu ipo haja kubwa sana ya kujijua wewe mwenyewe na huna haja ya kumjua mtu mwimgine kwa sababu hata ufanye nini ili umjue huwezi kumjua uhalisia wake. Kama mzazi ameshindwa kumjua mwanaye wewe unawezaje kumjua? Mzazi angemjua mapema mwanae basi asingeacha mwanae awe mwizi au ghahidi.
Rafiki yangu unaarikwa kujitambua wewe mwenyewe kwanza na ni muhimu sana kujitambua. Unajitambua kwa kujiuliza maswali wewe mwenyewe na majibu utakayokuwa unapata basi ndo wewe. Jiulize swali wewe ni nani? Sasa usijipe jibu kwamba wewe labda Sadick hapana kuna utofauti kati ya wewe ni nani? na jina lako ni nani? rafiki yangu jiulize swali kwanini unafanya unachokifanya? jiulize maswali mengi kuhusu wewe na jijibu wewe mwenyewe.
Ishi wewe kama wewe.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment