Rafiki yangu kuna maeneo manne ambayo unatakiwa kuyaimarisha ili kuweza kuwa bora katika maisha yako na kuweza kupata mafanikio makubwa. Maeneo yote manne yanatakiwa kuwa bora sana na ni muhimu bila kuacha hata eneo moja na hapo ndipo utakuwa bora mafanikio yatakuwa ni yako. Maeneo hayo ni kama yafuatavyo;
Eneo la kwanza ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiroho. Eneo la kiroho ni eneo ambalo ni la muhimu sana, hapa tunazungumzia imani yako lazima uwe na imani na Mungu kwa dini yoyote bila misingi na falsafa za kidini huwezi kufanikiwa na hata kama ukifanikiwa utakuwa bado hujapa mafanikio ya kweli. Ukiishi na kuimarika katika falsafa za kidini utakuwa mtu mwenye amani na furaha na utakuwa na imani na Mungu ambaye yeye ndiye aliye tuumba sisi.
Eneo la pili ambalo unatakiwa kuwa bora ni eneo la kiakili. Rafiki eneo hili ni la muhimu sana, ni eneo ambalo kila siku uwe unaimarika ubongo wako unahitaji kupata chakula chake kila siku. Kama bado hujaanza kuurisha ubongo wako chakula basi anza leo jifunze kwa bidii sana. Kuna wengine huwa wanasema mimi nishasoma shuleni siwezi kusoma tena, elimu haina mipaka na elimu ya shuleni ni kipande kidogo sana kwenye maisha elimu kubwa ipo mitaani anza leo soma vitabu, kuwa makini na watu unao kutana nao wasikilize kwa umakini ulio makinika, tembelea mitandao kama huu wa JIKO LA USHAURI na mitandao mingine, soma vitabu vya dini na zama hizi za taarifa kujifunza ni rahisi sana ukiwa na simu janja tayari utakuwa bora.
Eneo la tatu ambalo unatakiwa kuawa bora ni eneo la kiafya. Mwili wako ndio nyumba yako, ukishindwa kuwa na afya bora maeneo yote utaferi. Hakikisha unawekeza kwenye afya yko kwa kufanya mazoezi, kula kwa afya, fanya tahajudi au kusali na usafi kwa ujumla.
Eneo la nne na la mwisho ni eneo la kimahusiano. Watu ambao unahusiana nao hakikisha unauza kwao. hakikisha unauza kipawa chako, unauza tabasamu, unauza tabia zako na hayo maeneo yote hapo juu hakikisha watu wanajifunza kutoka kwako. Huwezi kubadirisha watu kwa maneno bali kwa matendo yako. Ukiuza kwa matendo lazima utafanikiwa kazana kujenga mahusiano mazuri na watu wanao kuzunguka kwa matendo yako.
Kwa kumalizia ntasema hivi , dunia inakuhitaji sana rafiki yangu, hivyo ulivyo umekamirika unachohitaji ni kujiendeleza tu na kujitambua, rafiki yangu Mungu alituumba kila mtu kwa nafasi yake aangaze na kama wewe huwa unaangalia nyota za juu ndio sisi tulivo simama katika nafasi yako toa ulicho nacho acha kuiga kutoka kwa wengine, kuna mwanafalsafa mmoja alishawahi kusema siku hizi watu hawafungwi na mapepo ila wanafungwa na watu wanaowazunguka, watu watano wanao kuzunguka ndio wastani wa maisha yako. Hatua ya kuchukua sasa hakikisha unakuwa bora kwenye maeneo hayo yote manne lazima utapata mafanikio ya kweli.
Endele kutembelea blogu hii ya jiko la ushauri ili kujifunza zaidi pia jiunge na mtandao huu ili kupata makala mpya kila itakapo toka.
Maisha ni KUWA+KUFANYA=KUPATA
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment