Mpendwa wangu rafiki hinyo sasa ulivyo unavo jiona, unavo jitafsiri, hayo mafanikio uliyo nayo, hizo tabia unazozipenda au kuzichukia vyote hinyo vimesababishwa na wewe mwenyewe, wewe ndiye uliyejifikisha hapo ulipo sasa unaweza ukawa unapachukia hapo ulipo au unapapenda lakini wewe ndiye mhusika mkuu unaweza ukasema sasa nitoke hapa nilipo niende katika hatua nyingine nzuri zaidi au nzuri kutokana hapa ambapo sipapendi.
Mpendwa wangu kujenga tabia nzuri si jambo rahisi, kujenga tabia ya kukupereka kwenye mafanikio sio jambo rahisi. Kujenga tabia mbaya ni rahisi sana lakini ni vigumu kuacha ila kujenga tabia nzuri ni ngumu kujenga lakini ni rahisi kuacha. Kwa maana hiyo ili uwe na tabia nzuri ni lazima sasa ufanye maamuzi ni magumu na uanze kuyafanya na uyaendeleze. Na hii huwa inaanza pole pole sio kwa papala tabia murudio wa mambo kwahiyo jinsi unavorudiarudia baadae inakuwa ndo tabia yako.
Kama unataka kujenga tabia ambayo ni nzuri inabidi uanze kujenga vichocheo vya tabia yako ambayo unataka kuijenga mfano; wewe unataka kuamka kila siku asubuhi na mapama ila wewe huwa huwezi kuamka asubuhi na mapema kichocheo cha kwanza unaweka alamu, alamu ikipiga tu unaamka kwahiyo kupitia alamu umeaka asubuhi na mapema kinachofuata ni labda wewe unataka kuanza tabia ya kufanya mazoezi asubuhi kwahiyo kichocheo cha kufanya mazoezi kuamka mapema.
Sasa tayari baada ya hapo umemaliza mazoezi labda unasali au tahajudi baada hapo unaenda kuoga kwahiyo mazoezi ni kichocheo cha kusali ni kichocheo cha kwenda kuoga baaada ya kwenda kuoga labda unasoma au kuandika kwahiyo unajijengea hivo na inaendelea ratiba ya namna hiyo mpaka jioni kwa hiyo tayari unakuwa umeijenga siku katika hali ya ratiba labda kwa wakati mwingine unaweza kujiwekea vipaumbele vyako wakati wa kazi za mchana. Sasa mrudio wakila siku baadae inabadirika na kuwa tabia yako.
Ili kuwa karibu nami na kupata makala mpya na huduma nyingine hakikisha unajiunga nami kwa kujaza fomu ipo hapo palipo andikwa jingenasi tayari unakuwa unapokea makala moja kwa moja kwenye email yako.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment