Tukitambua tunaishi siku moja tutaijali siku, tukitambua kwamba leo ni moja kati ya siku tutaidhamini sana leo na tukitambua ipo siku tutakufa basi hatuna budi kufanya kila kitu ili kutimiza wajibu wetu ili tuache alama dunia. Kwahiyo hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajili ya siku hii tulio nayo ni siku ya dhamani sana na kesho anapanga yeye.
Karibu mpendwa rafiki yangu tujifunze kwa pamoja kwewnye maada ambayo nimekuandalia leo ambayo inasema, maeneo matatuambayo unatakiwa kuwa makini kama untaka kuwa mwekezaji wa maarifa.
Ni watu wachache sana ambao wanatambua ya kwamba tunatakiwa kuwekeza kwenye maarifa, wengi wetu tunachojua ni kuwa unatakiwa kuwekeza pesa tu au tunatambua ya pesa tu ndo huwa inawekezwa. Kama wewe ni mmoja kati ya waadhirika wa hilo basi leo tambua ya kwamba maari yanawekezwa. Maarifa ni uwezo wa kuona unafuu ndani ya changamoto.
Tukianza kuwekeza kwenye maarifa, kwenye uwekezaji mwingiune itakuwa ni rahisi kwetu kutokana maarifa yetu. Uwezekezaji wowote ule unachangamoto zake kwahiyo kama huna maarifa utashindwa kuwekeza. Ni maeneo mengi sana tunawekeza bila ya sisi wenyewe kutambua ya kwamba hapa tunawekeza, kwa mfano; tunaishi kwenye jamii, ili niwekeze kwenye jamii inatakiwa niwe na tabia njema kwahiyo ukiwekeza tabia njema watu watakuheshimu na hata ukianzisha kitu itakuwa rahisi kwako kukuunga mkono. Yafuatayo ni maeneo matatu ambayo tunatakiwa kuwa makini nayo ili kuwekeza vizuri kwenye maarifa.
Eneo la kwanza kabisa ni usikivu wakati wa mazungumzo. Hili ni eneo ambalo tunatakiwa kuwa makini sana kwani ndilo eneo linalotumika wakati wote, watu tumekuwa wajinga kwa sababu ya kukosa usikivu yaani mtu anzungumuza na wewe unataka kuzungumza, mtu anazungumza wewe unajishikashika au unachezea simu, huko ni kukosa usikivu. Kwenye usikivu kuna mengi utajifunza haijarishi unaongea na mtu wa aina gani lakini usikivu ni wa muhimu sana.
Eneo la pili ni kujifunza kupitia changamoto. Hili ni eneo la muhimu sana kwa sababu hili ndo maana halisi ya maarifa. Tumekuwa watu wakukimbia changamoto au kuwabebesha wengine bila kujua tunatupa dhahabu. Maisha changamoto, kuishi changamoto na changamoto maisha. Mara nyingi wanaotatua changamoto sana ndio wanao fanikiwa sana. Kwahiyo rafiki yangu usikimbie changamoto hiyo ni ladha ya maisha tu.
Eneo la tatu ni kusoma vitabu au kusoma kwa ujumla. Hili ni eneo ambalo tunajifunza mengi kutoka kwa wengine ambao sio rahisi kukutana nao sisi,wengine walisha kufa zamani, wengine wapo mbali na hali nyingine tofauti. Rafiki yangu kusoma vitabu ni kitu cha muhimu sana kwa sababu tumezaliwa kizazi hichi cha taalifa na zama hizi lakini hatujui miaka 5000 iliyopita huko nyuma yaani hatuna uelewa kabisa wahuko nyuma sasa lazima tujifunze kupitia mababu zetu walifanyaje fanyaje na sisi tujue tunafanyajefanyaje. Kwahiyotunatakiwa kuanza kusoma vitabu sasa hivi utaona mabadiliko akubwa sana.
Haya ndiyo maeneo matatu ambayo unatakiwa kuanza nayo rafiki yangu ili kujiwekeza kwenye maarifa, japo yapo maeneo mengi lakini hayo unaweza kuanza nayo halafu baadae ukaendelea kujiendeleza kwa namna tofauti.
Karibu ujiunge na mtandao huu kwa kujaza fomu ili kupata makala moja kwa moja kwenye emaili yako utatumiwa, pia usisahau kuwashirikisha wengine ujumbe huu na endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. Maisha ni kuwa+fanya=pata
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment