JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Saturday, March 31, 2018

Kipi Kinakusukuma Kukua?

 Sadick Kilasi     March 31, 2018     USHAURI, USWAZI TRICK     No comments   

Ukiweka mbegu sehemu duni, sehemu ambayo haina unyevunyevu wala udogo wa joto  hakika hiyo mbegu itabaki kama ilivyo haita ota kabisa.

Ili mbegu iote inahitaji unyevunyevu na joto, lakini ili ikue zaidi inahitaji udogo wa kutosha ambapo itaweza kusimama na kukua vizuri.

Mtu asiyesimama kwa chochote basi atadondoka kwa chochote. Malcon X. Ukweli ni kwamba tunahitaji kukua, kwa lolote lile tunalohitaji tunahitaji kukua, kutoka katika hatua moja kwenda nyingine.

Kama unataka kuwa mchezaji mzuri na mkubwa basi jipe muda na nafasi, fanya mazoezi utakua mpaka kufikia kiwango cha juu huko. Kikubwa ni kufanyia mazoezi kwa sana.

Ukitaka kupata chochote kile kinahitaji kumwagiliwa yaani mazoezi ya kutosha ili ukue vema. Ndiomaana mbegu inahitaji joto kuota lakini joto halitoshi kuikuza mbegu, udogo, unyevunyevu pamoja na joto vitasaidia mbegu kukua vema na kustawi zaidi.

Lazima kila mtu awe na kitu ambacho kinamsukuma kukua, ndoto yako ulioyonayo utaifikia kama kuna kitu kinakusukuma kukua.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

(SEHEMU YA PILI). Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu.(II).

 Sadick Kilasi     March 31, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Karibu tena mpendwa msomaji katika makala ya leo. Naendelea kukushirikisha sehemu ya pili ya mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu cha Bwana Wetu Aliyefanyika Haki Ya Mungu. Karibu karibu sana katika sehemu hii ya pili.
Soma SEHEMU YA KWANZA, kama bado hujasoma uchambuzi huu.

13.Mwili wangu ni kama pipa la taka taka, siwezi kuutegemea mwili. Ninamsifu Mungu wangu kwa moyo wangu, ninamwamini yeye.

14.Ukweli ni kwamba dhambi tunazofanya ni nyingi sana na hazihesabiki, kama tungekuwa tunafanya dhambi chache basi tungeomba toba na mambo yangeisha. Mungu ameturehemu kwa Kristo Yesu Bwana na Mokozi wetu kwa kutufanya huru siku zote za maisha yetu.

15.Hakuna kitu cha kukitegemea katika mwili vyote hivi vina ukomo lakini kwa Bwana kuna umilele tu. Lazima tutafute kitu ambacho ni cha milele.

16.Mioyo yetu siku zote inamtumikia Mungu lakini miili yetu siku zote hutenda dhambi siku zote kwa sheria ya dhambi. Bwana wetu amefutilia mbali dhambi zetu za zamani, sasa na baadae. Miili yetu haita acha kufuata dhambi. Tunamshukuru Mungu kwa hili ambalo haliwezi hata kuelezeka. Mwili hutumikia sheria ya dhambi.(warumi 7:24-25).

17. Watu ambao wanamtumikia Mungu hukosa furaha pale ambapo huhisi ya kwamba wametenda dhambi na tusije tukafikiri ya kwamba hatuwezi kutenda dhambi kamwe ili tuwe na furaha. Lakini ukweli ni kuwa hatuna ujasiri wa kuwa hatuta tenda dhambi kamwe au kabisa.

18.Tunaweza kumtumikia Mungu kwa kitambo kidogo tu kwa hamasa lakini hamasa hiyo huisha pale tu mwili unapotenda dhambi, hapa udhaifu huanza tena. Mwili hufuata dhambi na hii ni sheria ya dhambi. Ndo maana mtume Paulo anatenga mwili na roho. (warumi 7:24-25).

19.Usitegemee mengi kutoka katika mwili.

20.Mwili unapenda kukuza raha ya mwili, starehe, amani,  furaha na majivuno yake na si haki ya Mungu. Mwili unapenda vitu vyote vifanyike kama unavopenda. Mara nyingi mwili unapenda kujihesabia haki wenyewe. Hebu tuache kujihesabia haki wenyewe na tuuache mwili kama ulivo.

21.Tunaweza kufurahia maisha wakati wote ikiwa tutambua ya kwamba dhambi zetu zote zilikombolewa na kusamehewa, tukiokoka tunapaswa kutenda mema lakini mwili wetu huu wa mauti utaendelea kuishia katika dhambi. Basi tunapaswa kuomba toba, tusiishi kama watu wa kujitegemea wenyewe kwamba tukitenda dhambi tutaipoteza furaha yetu, hapana lazima tufurahie maisha.

22.Ikiwa tutatambua ya kwamba mwili wetu unatumikia sheria ya dhambi tu, basi tunaweza kukwepa dhambi kwa imani. Tukiishi kuamini kwa imani kwamba Bwana alituokoa dhambi zetu zote basi na tujengeke katika Neno lake. Hata kama tunatambua ya kwamba tunaweza kutenda dhambi tena lakini tunaamini kwa imani kwamba dhambi zetu zote zilikombolewa na Kristo Yesu na tudumu katika Neno.

Kwa leo ninafikia hapa mpendwa msomaji. Hongera kwa kuwa pamoja na katika mwendelezo huu wa uchambuzi. Ombi langu kwako wewe msomaji kutafakari mambo haya ninayo kushirikisha. Kama bado hujasoma sehemu ya kwanza basi hakikisha unaisoma, tafuta katika tafuta blogu hii utaipata.

Mtu hawezi kujengeka kama hakuna kitu ambacho kinamsukuma aweze kujengeka, mfanya nazoezi anajengeka kimwili kwa sababu ya mazoezi yake, wewe utajengeka kiakili kwa sababu ya kusoma na kutafakari. Maoni yako muhimu, toa maoni au nitumie meseji katika Mawasiliano yangu nitakujibu.

Nikutakie tafakari njema katika haya, tukutane tena katika mwendelezo ujao. Washirikishe wengine ujumbe huu uwasaidie wengi zaidi. Mungu awe nawe.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, March 30, 2018

Hiki Hapa Ndo Chanzo Kikuu Cha Msongo Wa Mawazo.

 Sadick Kilasi     March 30, 2018     MAHUSIANO     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeamka salama kabisa.

Adui mkubwa na anaye nyanyasa maisha ya watu ni msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni vita ambavyo vipo ndani ya watu na wakuvimaliza vita hivyo ni mhusika mwenyewe.

Anayepitia katika hali hii ndiye uwanja wa vita, ndani mwake mnapigana vita ambavyo si vyakawaida. Kuna wakati ambao mhusika huonyesha dhahili kabisa hali anayopitia. Msongo wa mawazo ni utumwa wa fikra.

Kuna chanzo kikuu kimoja cha msongo wa mawazo, mtazamo ndo chanzo kikuu cha msongo wa mawazo. Japokuwa kuna vyanzo vingine vya msongo wa mawazo lakini mtazamo ndo chanzo kikuu cha msongo wa mawazo.

Kukosa pesa inaweza kusababisha msongo wa mawazo lakini kama mhusika ukitambua namna ambavyo pesa inatakiwa hata lalamika ya kwamba sina pesa, wakati kuna mambo mengine ya muhimu yapo salama kama chakula, mavazi na sehemu ya kulala. Mtazamo utakusaidia namna ya kufikia katika hali fulani ya maisha bila ya kuwa na woga wowote wala masumbuko.

Mrundikano wa mawazo unaweza kusababisha msongo wa mawazo lakini kama mtazamo wako upo vizuri inamaana utajua namna ya kupangilia mambo yako muhimu na yasiyo muhimu.

Mtazamo ni uwezo wa kupambanua hali fulani au jambo fulani. Kuna mtazamo mzuri na mtazamo mbaya. Ukiwa na mtazamo wa hovyo kila kitu kwako kitakuwa ni tatizo na hapo ndipo chanzo cha msongo wa mawazo kwahiyo matatizo yote unayoyaona chanzo kikuu ni mtazamo wako.

Tatizo ambalo unaliona ni tatizo kwako kwa mwingine si tatizo. Mpendwa rafiki yangu kuwa tajiri wa mtazamo maisha yako yatakuwa bora kweli kweli. Jifunze kwa mapito yako, soma vitabu na kuwa msikivu.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 29, 2018

Neno Kutoka Kwa Sadick Kilasi....Kutaka Kunauumiza.

 Sadick Kilasi     March 29, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI     No comments   

Watu wengi wenye msongo wa mawazo ni watu ambao wanataka kitu. Kutaka kitu ni kama kujisababishia msongo wa mawazo. Ukipenda kitu rudi nyuma angalia na
weka mipango ambayo itakifikisha kwenye ndoto yako. Maisha ni kama maji ya mto, yanatiririka kutoka juu bila kuacha nafasi yoyote na kuifikia bahari.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, March 28, 2018

Hakuna Wakati Sawa Wakufanya Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     March 28, 2018     USHAURI     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai umeamka salama. Hongera kwa ushindi huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu katushindia mimi na wewe. Kuamka salama ni ushindi mkubwa sana. Wapo wengi ambao walitamani na kuiwekea malengo siku hii lakini hawajabahatika kuiona. Sisi tulio washindi hatuna budi kumtukuza yeye na kumshukuru Mungu.

Katika na mapito yetu, hakuna wakati sawa sawa wakufanya jambo ambalo sio sahihi wala hakuna wakati ambao sio sahihi kufanya jambo ambalo ni sawa.  Haijarishi tunapitia katika hali gani hatupaswi kugeuza sura zetu na kufanya mambo ambayo siyo.

Hakuna wakati sahihi wakufanya jambo ambalo ni sawa, wakati wote ni sawa kufanya jambo ambalo ni sawa. Kama tukiwa tunajaribu kufanya mema wakati tunaonekana tu ukweli ni kwamba tutakuwa tunajidanganya wenyewe, maisha yatakuwa magumu kwetu.

Kama ni kufanya jambo ambalo ni sawa basi yatupasa kuendelea kufanya haijarishi ya kwamba kunamtu anatuona au la, kwa sababu hakuna kitu ambacho kimejificha katika Ulimwengu huu, asipo kuona mtu ipo siku utaonekana tu huwezi kuiongopea dunia wakati wote, utaongopa kwa muda mwisho utaonekana tu. Mungu anakushuhudia rafiki yangu wakati wote.

Fanya kilicho bora rafiki yangu haijarishi upo katika hali ipi,  hali ngumu, peke yako, upo sawa au haupo sawa. Hatupaswi kufanya kilicho bora kwa kutegemea kupata kitu fulani, hapana, tunapaswa kufanya kilicho bora kwa sababu tunapaswa hivo.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

(SEHEMU YA KWANZA). Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu. (II).Kilicho Andikwa Na Paul C. Jong.

 Sadick Kilasi     March 28, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri. Karibu nikushirikishe mambo machache kati ya mengi ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu cha Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki Ya Mungu. (II). Hii ni sehemu ya kwanza ya uchambuzi.

Nimefanikiwa kupata kitabu hichi cha sehemu ya pili ikiwa ni mwendelezo wa kitabu cha kwanza lakini sijabahatika kukipata cha sehemu ya kwanza. Nimejifunza mengi sana kutoka kwenye kitabu hiki. Ni kitabu ambacho kimeanzia sura ya saba kutoka kwenye kitabu cha mwanzo yaani kitabu cha kwanza.  Kitabu hiki kina sura kumi na kurasa minne sabini na moja, kwahiyo pamoja na kuwa ni mwendelezo lakini ni kitabu kikubwa.

Kitabu hichi kinazungumzia maswala ya imani juu ya Mungu. Mwandishi amejaribu kuchambua vizuri kabisa juu ya imani kupitia kitabu cha Warumi. Mwandishi wa kitabu cha Warumi ambaye ni yule msomi Paulo ameonesha namna gani ambayo alipokea injili ya maji na roho. Mwandishi wa kitabu hiki cha Bwana Wetu Aliyefanyika Haki Ya Mungu ametuonyesha namna gani Paulo avyokuwa anaachilia mbali haki yake na badala yake kuamini katika Mungu.

Karibu nikushirikishe yale niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki.

1. Kila mtu ambaye anayaelekeza mawazo yake kwa kuamini katika haki ya Mungu basi anaweza kuipata haki hiyo na kuamini sasa hivi. (jifunze kutoka Warumi 1:17).

2.Haki ya Mungu tunaipata si kwa kuamini kwamba tunaifahamu bali tunapoiamini haki ya Mungu hakika tutafurahia baraka za kiroho.

3.Wale ambao wameifia dhambi hawapo tena chini ya himaya ya dhambi. Kama ambavyo mwanamke aliyefiwa na mume wake jinsi alivyo huru toka katika majukumu yake kwa mumewe. (Warumi 6:23).

4. Dhambi inadhihirika kwa sheria, sheria ndiyo inayofanya dhambi iwepo.

5.Mungu katuumba katika hali ya ukamirifu katika uhalisia wetu lakini tumezaliwa katika asili ya dhambi, asili yetu imejaa dhambi. Asili hii ni Wazazi wetu kutoka kwa Adam na Hawa.

6.Kuungana katika haki ya Mungu itatupasa kuamini kupitia Kristo Yesu na kujiunganisha naye kupitia maandiko matakatifu.

7. Mwanadamu ana sehemu mbili za uwepo. Moja ni mwili na nyingine ni moyo. Mwili hauwezi kuifikia haki ya Mungu hata kama ukijitaidi vipi na kwa kiasi gani. Pia hawezi kuitunza na kuishika sheria ya Mungu. Hata baaada ya kuzaliwa upya mwili hauwezi kuitunza sheria hii hata kama ukijitaidi kwa kiasi gani. (Warumi 4:15)

8.Ukweli ni kwamba hatuwezi kumtimikia Mungu kwa miili yetu hata baada ya kuzaliwa upya lakini kwa imani na tumpe shukrani Mungu kwa mioyo au moyo wako wote kwa upendo wake. Basi kwa kufanya hivyo mwili unakuwa kama chombo kinachofuata imani.

9.Pamoja na kuwa na miili yetu kuwa na mapungufu mengi sana lakini Mungu ametupenda na kutufanya sisi wenye haki.

10.Wakati mwingine huwa tinajikwa kwa miili yéti lakini Bwana wetu Mungu yeye hatuwazii mabaya na bado anatupenda. Anasema yeye ni mwokozi wetu tusifadhaike.

11. Ukweli ni kwamba wakati mwingine tunajikwaa na tunatenda dhambi na tunajikwaa tena basi sheria ya Mungu huinuka juu yetu na ndipo tunapovutwa zaidi kutenda dhambi na kujiona ni wadhaifu sana. Miili yetu inaenenda katika tamaa yake. Kwa hiyo mwili kamwe hauwezi kufuata Mungu.

12. Kufuata haki yako mwenyewe au tamaa yako ya mwili unaweza kupata furaha kwa muda na kisha furaha yako inaondoka mapema. Ohoooo !!  sasa hivi nilikuwa na furaha sasa furaha yangu iko wapi?  Mtu huyo anakuwa anajitegemea mwenyewe.

Mpendwa msomaji, unataka furaha ya kudumu katika maisha?  Je unapenda kubadilisha maisha yako?  Je umechoka kupata furaha kwa muda na kupoteza mara moja?  Usikose uchambuzi ambao nitakushirikisha mengi muno ju ya maisha yetu na imani. Watu wengi wanateseka katika maisha yao, wengi wao ni wale ambao wamesha ijua sheria ya Mungu, wanateseka kutokana na kutokujua haki yao na wanajitegemea wenyewe. Usikose sehemu ya pili ya uchambuzi huu.

Washirikishe wengine makala hii nzuri ili iwe msaada kwao. Toa maoni yako au nitumie ujumbe kwenye namba hii 0687000768 au tuma ujumbe kwa barua pepe sadikila65@gmail.com, nitakujibu rafiki yangu.

Ukawe na tafakari njema juu mafunzo haya na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 27, 2018

Usifanye Maamuzi Yoyote Unapokuwa Katika Hali Hii.

 Sadick Kilasi     March 27, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Wakati ambao shetani hutumia nafasi vizuri ni wakati ambao unafuraha sana na wakati ambao unahasila sana. Lakini shetani haishii hapo tu wakati ambao unauhitaji sana wa kitu shetani hutumia sana hizi fursa kutuingiza kwenye mtego.

Kumbuka shetani ni mwelevu sana, anajua ya kwamba ukiwa katika hali hizo huwezi kutumia fikra zako vizuri.

Leo nataka nikuambie rafiki yangu, usifanye maamuzi yoyote yale ukiwa na hasila. Nyakati hizi ambazo mtu anahasila huwa anajiona ya kwamba ameshushwa chini, halafu yeye mwenyewe huwa anajitaidi kwa kujitegemea mwenyewe anajipandisha kwa nguvu. Hasila maana yake ni kujiona ya kwamba umeshushwa chini halafu kwa kujitegemea mwenyewe ujajitahidi kujipandisha. Hasila ni ubinafsi. Mtu mwenye hasila ni mtu mbinafsi. Ajipandishaye hushushwa.

Sasa mara nyingi ukiwa katika hali hii ni ngumu sana mtu kuwaelewa wengine. Kaini sadaka yake iliposhindwa kupokelewa na Mungu, Kaini alikuwa na hasila sana, Mungu akamwambia Kaini, kwanini uso wako umekunjamana?  Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko,  inakuotea mlangoni,  nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Umeona dhambi ipo, wakati wote dhambi inakusubili ufanye kosa dogo hapo ndipo inapojipenyeza.
Lakini Kaini alishindwa kusikiliza sauti ya Mungu, akamwua ndugu yake.

Yatupasa kuwa makini sana tunapokuwa tumefanya makosa au tunahasila, huwa tunashindwa kujidhibiti wenyewe wakati huu, lakini sababu ya yote haya ni hali ya kuwa na umimi yaani ubinafsi.  Kosa dogo kwa ajili ya kujiona umekosewa sana inapelekea kufanya makosa makubwa kabisa kama Kaini alivyoenda kumwua nduguye kwa sababu ya wivu.

Wakati wowote ambao unakuwa na hasila kwanza kabisa lazima utambue hakuna mtu ambaye anaweza kukufanya wewe kuwa na hasila kwa hiyo wewe mwenyewe lazima ujiulize kwanini nipo katika hali hii, nimetafsiri vipi hii kauli au kitu hiki nilichokiona, ukiona unaona umekosewa tambua hiyo ni hali ya ubinafsi lakini ukiona unachukulia hilo kama funzo basi wewe ni mshindi. Kumbuka rafiki yangu dhambi ipo ndani yako imelala, inasubiri mtu wa kumwasha na lazima utambue hakuna mtu mwenye mwili ambaye hana kitu hiki kwahiyo wanao tambua kwamba miili yetu imejaa tamaa na ubinafsi hawawezi kufanya kosa hili na hata kama wakikosea basi hujitambua mapema.

Mpendwa msomaji, wewe ni mtu wa hasila basi nakupa mbinu hii hapa, tambua ya kwamba hakuna mtu mbaya duniani ila kuna mabaya. Ukiwa na mtazamo huu utakufanya usimchukie mtu na uchukie hali iliyopo pale. Hasila hupelekea kufanya dhambi zaidi ya dhambi, zaidi na zaidi. Kwa jinsi unavojiona unafaa zaidi ndivyo ambavyo unazidi kufanya makosa zaidi kwa hiyo wakati kama huu lazima ujifunze kujishusha.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, March 26, 2018

Wakati Ukifika Mambo Yanabadilika.

 Sadick Kilasi     March 26, 2018     UJASIRIAMALI, USHAURI, USWAZI TRICK     No comments   

Kila kitu ukikipa wakati na ukawa mvumilivu basi lazima utegemee utofauti kati ya kabla hapo mwanzo. Jambo lolote lile ukifika wakati wake lazima libadilike.

Unaweza ukawa unafanya biashara, kama unaweka kazi na juhudi kubwa kwenye biashara yako kama ukiipa muda lazima matokeo ya tofauti yatokee. Kama ni kupanda kwa biashara yako basi itapanda kutokana na juhudi yako.

Kama hupandi basi unashuka, kama biashara yako haipandi basi inashuka, wewe ni kuipa wakati tu na matokeo utayaona. Mambo huwa hayabaki kama yalivo mambo yote yanabadilika, wakati ukifika utaona matokeo.

Yawezekana unapitia katika kipindi kigumu basi huo ni wakati, na ndivyo ilivyo, simaanishi kwamba utakuja kufanikiwa sana, hapana, inategemea na hatua na gharama utakazolipa, ndivyo mambo yatakavyo badilika.

Kwa hiyo rafiki yangu kama sasa hivi imefanikiwa sana tambua wakati ukifika utashuka, dunia ndivyo ilivyo, inazidisha na kugawanya, kujumrisha na kutoa. Wakati ukifika.

Mpendwa msomaji, jipe muda mambo yote yatabadirika, uvumilivu ni jambo la muhimu sana, haijarishi munagombana vipi na mwenza wako lazima ujipe wakati mambo yote yataisha. Wakati, wakati jipe wakati.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 25, 2018

Neno Kutoka Kwa Sadick Kilasi...Tuumalize Ubaya Hivi.

 Sadick Kilasi     March 25, 2018     NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI     No comments   

Kama tukiendelea kuulinganisha ubaya na wema, basi ubaya hauna budi kuendelea kuwepo. Lakini kama hatutaki ubaya uwepo basi hatuna budi kuuongelea wema tu. Usicho kipenda usikiongelee kabisa.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, March 24, 2018

Huwezi Kubaki Salama Kabisa.

 Sadick Kilasi     March 24, 2018     USWAZI TRICK     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, kwanza hongera kwa ushindi mkubwa ambao mimi na wewe tumeshindiwa, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hili. Wapo wengi ambao walitamani kuiona siku hii lakini hawajaiona, wapo wengi ambao waliiwekea malengo siku hii lakini hawajaifikia, wapo wengi tena wenye pesa zao ambao walitamani kununua uhai lakini hawakuweza, lakini mimi na wewe tunapumua, ukweli ni kwamba kuna kusudi ambalo lipo na tuweza kufanya kitu ambacho kinaweza kubadili historia ya dunia hii. Haijarishi upo na hali gani, una pesa au huna pesa, upo kitandani unaumwa na unasoma hapa, unaweza kufanya kitu ambacho kitabadili kabisa historia ya maisha yako na dunia kwa ujumla.

Katika maisha chochote ambacho utasikia au kuangalia ukweli ni kwamba hakiwezi kukuacha salama. Unaweza kufanya kitu kidogo tu lakini ubongo wako hauachi kunasa sauti au picha ya kitu hicho.

Kuna vitu vitatu ambavyo vinaweza kuharibu maisha yako kabisa, ambavyo ni kuona kitu ambacho hukupaswa kuona, kusema kitu ambacho hukupaswa kusema na kisikia kitu ambacho hukupaswa kusikia. Kwa hiyo rafiki yangu angalia ni kitu gani ambacho unakipa muda sana maana hicho hakiwezi kukuacha kama ulivo kuwa.

Kama unatembea na walevi inamaana hata kama wewe sio mlevi huwezi kuachwa salama, lazima na wewe utakuwa mlevi tu.

Kama utatembea na watu wazuri basi huwezi kuachwa kama ulivo lazima watakuambukiza uzuri wao wa tabia zao.

Ukitembelea mitandao ya internet, huwezi huwezi, kuachwa kama ulivo lazima sehemu ya maisha yako itaathiliwa, kwahiyo ni muhimu kutambua ni mitandao ipi ambayo unatembelea ya kujenga au kubomoa.

Huwezi, huwezi kuachwa kama ulivo katika dunia hii ya matokeo, kila siku kuna vitu vinaingia vipya kwenye ubongo wetu haijarishi unataka au hutaki, ubongo kazi yake ni kunasa tu, kinachoonekana,  kinachosikika na kuhisiwa pia.

Huwezi kuachwa salama, muhimu ni kutambua tu mazingira yako, kumbuka ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi, ukitembea na watu wabaya na wewe utakuwa mbaya, kwanini?  Kwa sababu kila mtu anamabaya ndani yake yanasubili kuamshwa tu, yakipata mtu wa kuamsha yanaamka.

Endelea kitembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, March 23, 2018

Majaribu Hayana Budi Kuwepo.

 Sadick Kilasi     March 23, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Katika Tafakari roho ya leo:

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama. Hongera kwa ushindi mkubwa ambao mimi na wewe msomaji wangu tumeshindiwa. Kuiona siku hii mpya ni ushindi mkubwa sana, wapo ambao walikuwa watamani kuiona siku hii lakini hawajaiona, wapo ambao waliiwekea malengo siku hii lakini hawajaifikia, kwahiyo haijarishi wewe upo katika hali gani wewe ni mshindi mkubwa na unaweza kufanya lolote siku hii ya leo na ukabadili kabisa historia ya maisha yako. Hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetushindia.

Majaribu katika maisha yetu ni sehemu ya maisha yetu. Majaribu katika maisha yetu hayana budi kuwepo kwa sababu ni sehemu ya maisha. Adui yetu shetani ataendelea kutunyatia nyatia ili aweze kutunasa na kutupeleka katika maovu yake.

Ukisoma kwenye Biblia (Luka 4:1-13), 1.Na Yesu,  hali amejaa roho mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na roho muda wa siku arobaini nyikani, 2.akijaribiwa na ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu, na hata zilipotimia,  aliona njaa. 3.Ibilisi akamwambia, ikiwa ndiwe mwana wa Mungu, liambie jiwe hili ligeuke mkate. 4.Yesu akamjibu,  imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5.Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6.Ibilisi akamwambia, nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. 7.Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8.Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, msujudie Bwana Mungu wako,  mwabudu yeye pekee. 9.Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia,  ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, basi jitupe chini, 10.kwa maana imeandikwa, atakuagizia malaika zake wakulinde, 11.na ya kwamba, mikononi mwao watakichukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12.Yesu akajibu akamwambia, imenenwa usimjaribu Bwana Mungu wako. 13.Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaendazake kwa muda.

Ukisoma mstari huo wa pili utagundua ya kwamba, Ibilisi alikuwa anamjaribu hata kabla ya kujitokeza, akijaribiwa na Ibilisi, na ukisoma mstari wa nne, Yesu anamwambia Ibilisi, mtu hata ishi kwa mkate tu, kwa maneno haya tunajifunza ya kwamba majaribu lazima yawepo na hatuwezi kuishi kwa kutegemea mkate wa kula mda wote kwa hiyo lazima tupitie hali mbalimbali. Lakini pia ukisoma mstari wa kumi na tatu, Ibilisi alienda kwa muda, kwa sababu hiyo lazima atarudi tena. Atarudi tena kujaribu bahati yake kwa sababu yeye huwa hakati tamaa.

Mpendwa msomaji,  kesheni maana hatujui siku hata saa ambapo mjaribu wetu atakuja, maana yeye ni mwerevu na hutumia fursa vizuri sana. Wakati wa magumu, Ibilisi huja kukukatisha tamaa, wakati wa ushindi, Ibilisi huja kukujaza tamaa zaidi, wakati wote kwake ni fursa kwa kwahiyo lazima tukeshe vema kabisa.

Majaribu hayana budi kuja kukujenga ama kukubomoa kabisa, jiandae rafiki yangu kwa lolote lile katika kuifikia ndoto yako, mjaribu wako ni mwerevu sana.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 22, 2018

Mamlaka Juu Ya Mwingine, Kosa La Aibu La Kughushi.$#Hekima Na Chumvi Za Wazee Wetu.$#

 Sadick Kilasi     March 22, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri kabisa.

Karibu katika tafakari za wazee wetu, ambapo tumekuwa tukitafakari kwa umakini hekima ambazo wazee wetu na watu maarufu waliwahi kutamka na kusema. Leo tutatafakari nukuu mbili.

Hakuna taifa lenye mamlaka juu ya taifa jingine, wala mtu mwenye mamlaka ya kumwamulia mwenzake duniani, tunakoseana tu.
Mwalimu J. K. Nyerere. 

Yeyote anayeonekekana kwenye kosa la aibu la kughushi hawezi tena kuaminika hata kama anazungumuza ukweli.
Phaedrous.

Sina shaka kabisa namna ambavyo tunatambua michango mikubwa ambayo wazee wetu walituachia, wazee hawa walitengeneza misingi ambayo leo sisi tunasisimamia juu yake na kuendelea na maisha. Hekima hizi zilitamkwa katika mazungumzo yao mbalimbali lakini leo sisi tunatumia kama chumvi ya maisha.

Mwalimu Nyerere ni mtu ambaye hakuna hata Mtanzania ambaye hatambui mchango wake, ni mtu ambaye katengeneza mizizi ya Taifa letu la Tanzania. Mchango wake ni mkubwa muno katika taifa letu na Afrika katika kuleta amani.

Hakuna taifa ambalo linamamlaka juu ya taifa jingine wala mtu mwenye mamlaka juu ya kumwalia mwenzake duniani, tunakoseana tu.

Unaweza ukaona namna gani tamko hili au kauli hii ambavyo inavyojali utu, na hiki ndo kitu pekee Mwalimu ambacho alikuwa anakifanya, alikuwa anapenda sana sana kujali utu juu ya wengine.

Huwezi kujaribu kuthibiti kila mtu, huwezi kujaribu kuwa wewe tu katika kila jambo, huwezi kutumia kauli zako za vitisho kuwatisha wanyonge ni tunaoneana tu. Lazima tutambue mipaka yetu katika kuthibiti, sio kila mmoja unamwingilia tu bila hata ya kujali mwenzako anafikilia nini? Huo ni ughaidi wa uthibiti, ama kweli utaumiza wengi kwa tabia yako ya kumwingilia mtu maamuzi yake.

Ukweli ni kwamba, zawadi pekee ambayo mtu kapewa ya kwake binafsi, anamiriki yeye wenyewe ni kufanya maamuzi, vitu vingine vyote kapewa utawale tu lakini itafika wakati vitamponyoka yaani vinaukomo. Maamuzi ni kitu ambacho mwanadamu amepewa bure kabisa atumie na hakuna mtu ambaye anaweza kumwingilia katika kufanya maamuzi, japo kuwa unaweza kufikiri kwamba unaweza kumwamlia mtu lakini ukweli ni kwamba anakuwa ameamua mwenyewe. Ukijaribu kumlazimisha hamwezi kufika mbali mtagombana.

Siku zote kaa na utambue ya kwamba huna mamlaka juu ya mwingine, na ukijaribu kumwalia mwingine utakuwa unafanya kitendo cha kighaidi kwa wengine.

Yeyote anayeobekana kwenye kosa la aibu la kughushi, hawezi tena kuaminika hata kama anazungumza ukweli.

Katika hali ya kawaida ukiwa ulishawahi kufanya kosa na dunia ikatambua kwamba wewe ni mkosaji, kuja kuiaminisha dunia tena ni ngumu sana, watu ni wazuri sana wa kuangalia makosa ya wengine sio mazuri, ubaya unasambaa haraka kuliko wema. Watu wagumu sana kuutafuta ukweli lakini ni wepesi sana kuwa wajinga ndoomana watu wanapenda habari hasi zinazowaburudisha.

Ukweli hauwezi kumuburudisha mtu ila utampa uhuru, wengi tunapenda mashindano, sasa mtu akikughushia kitu cha uongo hakuna mtu atakaye kuamini tena ikizingatia watu wanapenda ujinga tu, sio kutafuta ukweli uko wapi. Ukijikuta kwenye hali kama hii usifanye chochote kaa kimya,  na ukipata muda sahihi basi ni vema kufanya jambo.

Watu wamejengeka katika mitazamo ya nje, watu wanapenda kuaminishwa kitu kwahiyo jipe muda na kuwa mvumilivu katika hali hiyo, ukweli lazima ushinde.

Nukuu hizi za wazee wetu ni chumvi kwetu, misingi ambayo tunasimamia, kwahiyo tuheshimu na tujipatie muda wa kutafakari.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, March 21, 2018

Dunia Na Mashindano, Upacha Ni Utofauti Tu.

 Sadick Kilasi     March 21, 2018     MAHUSIANO     No comments   

U hali gani mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI? Natumai unaendelea vizuri.

Kiasili vitu nyote vya dunia vipo katika hali ya upacha au uwili. Uwili huu upo katika kila kitu hapa duniani. Kuna uwongo na ukweli, mrefu na mfupi, mnene na mwembamba, mbali na jilani, kutaka na kutotaka, na mengine mengi yapo katika hali ya upacha.

Upacha huu una kazi moja kubwa, ni kutofautisha kati ya moja na nyingine, mfano unaweza kusema huyu ni mnene na huyu ni mwembamba, kule ni jilani na kule ni mbali.

Mashindano mengi katika dunia hii yanatokea kutokana na upacha huu, ukweli ni kwamba upacha huu ukianza kutumika kama mashindano huibui mambo mengine ya tofauti. Mungu aliuweka upacha au utofauti huu ili kuweka ubora tu. Mashindano mengi yanatokea kwa sababu ya utofauti, lakini wengi huwa tunasahau ya kwamba kila kitu kina ubora wake.

Mtu anaweza kuibua jambo ambalo si kweli, lauongo kabisa akalipeleka katika hali ya ukweli, akaaminisha watu kuwa jambo fulani ni kweli na wengine wakapokea kama ni kweli lakini bado kunawengine wakasimamia katika ukweli halisia. Mambo haya yanatokea sana katika jamii, kwamba mtu anaibua jambo kwa tamaa zake na kuwadanganya watu na kulipeleka katika hali ya ukweli kumbe si kweli, yeye anatafuta matakwa yake tu.

Hofu nyingi katika maisha ya watu zinatokea katika hali hii hii ya utofauti wa upacha huu,  tunaona ya kwamba wanaume sasa wanataka kuwa wanawake kitu ambacho hakiwezekani kabisa, wanawake weusi wanajikana wenyewe na kutaka kuwa weupe, mwanamke mweupe akijiunua na kusema mimi ni mzuri kuliko mweusi, mjinga mweusi anajiona kana kwamba yeye hafai kabisa na ndipo anaanza kujichubua na kuondoa asili yake ya zamani na kuweka ya kwake yote haya ni kwa sababu ya upacha wa utofauti.

Matumizi mabaya ya upacha huu huleta madhara makubwa sana katika jamii, lazima tutumie vizuri utofauti wetu ili kujenga ubora zaidi na tufanye dunia ni mahali salama, kubali mazingira yanayokuzunguka, kuwa jasili, kila kitu kina sababu zake.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, March 19, 2018

Tumeumbwa Kukua Kutoka Hatua Moja Kwenda Hatua Nyingine.

 Sadick Kilasi     March 19, 2018     TAFAKARI YA ROHO, USHAURI     No comments   

Ukweli ni kwamba tumeumbwa kuwa na uwezo mkubwa mno, uwezo wetu wa ndani ni wa ajabu. Ili mradi tu unakula chakula bora utakua kutoka hatua kwa hatua. Utajengeka namna wewe mwenyewe unavojijenga. Tumeumbwa kukua.

Mungu ni wa ajabu sana, katupa uwezo wa kujijenga wenyewe, kiakili tunajijenga wenyewe, kimwili tunajijenga wenyewe. Ukweli ni kwamba hii ni fursa ya kila mtu kujijenga kuwa bora, kujijenga katika hali ya utu. Rafiki yangu, hii ni nafasi nzuri sana kwa kila mmoja kubadilika kwani kifo hakina hodi wa kengele.

Yawezekana na ni kweli kabisa wewe ni mchoyo lakini waweza anza sasa kujiondoa katika hali hiyo na kujijenga katika hali ya upendo kwa wengine na kuwajali.

Yawezekana wewe una tabia ambayo wewe mwenyewe unayo na huipendi, anza sasa kujijenga katika hali ya kuipinga tabia hiyo, pole pole utajengeka katika kweli na upendo wa Mungu.

Ukweli ni kwamba tumezaliwa katika hali ya dhambi, mabaya yaliyo ndani yetu huwa yanaamka na kujikuta tunatumbukia huko, miili yetu imejaa tamaa na ubinafsi lakini pia kumbuka kiuhalisia sisi hatuna dhambi ila asili ndiyo inatutesa na dhambi lakini ili kushindinda lazima tuishi uhalisia wetu na tukue katika uhalisia huo.

Ukawe na siku bora na endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 18, 2018

Jihakikishie Kitu Hiki Siku Zote Katika Maisha Yako

 Sadick Kilasi     March 18, 2018     USHAURI     No comments   

Japo kuwa huwezi kukwepa kifo lakini wewe wenyewe unaweza kujihakikishia ya kwamba upo salama. Wewe mwenyewe unaweza kujua ya kwamba sasa nipo salama au la.

Mienendo yako lazima ikuhakikishie ya kwamba inakuweka salama, tabia yako lazima ikufanye uwe salama, huwezi kuwa salama kama unatabia mbaya ya kuwa na wapenzi wengi, kugombana na watu, ni mtu wa kuvunja sheria za barabarani, mwizi, utapeli, na mengine mengi ambayo ni hatari kwa wengine.

Wakati wowote jihakikishie upo salama, fanya kila kitu ambacho cha usalama kwako na kwa wengine pia, mdomo wako ni kitu hatari sana katika jamii, ulimi unaweza kubomoa au kujenga, wakati wowote jiulize maneno yangu yanawafanya watu kuwa salama, ukweli ni kwamba watu wakiwa hawana usalama na wewe pia hupo salama kabisa.

Mpendwa msomaji,  furaha unayoitafuta huwezi kuipata kama haupo salama, afya yako lazima iwe salama, kula kwa afya, kula kwa mpangilio, fanya mazoezi, fanya sala kuupa mwili nguvu, pata muda mzuri kabisa wa mapumziko, angalia mazingira uliyopo je yanakuweka salama kiafya? Kuwa salama siku zote.

Kuwa salama kiakili, watu gani ambao unawapa muda mwingi kimahusiano? mitandao ipi ya kijamii unayotembelea? Je unafanya nini ili kuijenga akili yako? Kuwa salama kiakili, akili yako ndo kila kitu, marafiki wanaweza kujenga au kubomoa akili yako, na mitandao ya kijamii pia hatari kwenye akili zetu. Pata muda wa kutafakari juu yako mwenyewe na maisha yako ili utumie akili yako vizuri.

Jihakikishie usalama rafiki yangu, usipo kuwa salama utakosa furaha na utashindwa kuzifikia ndoto zako, maisha yako yatakuwa magumu. Usalama wa maisha yako upo juu yako, kikubwa kuacha tabia mbaya zote ili kujihakikishia usalama.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, March 17, 2018

Hapa Ndipo Mwanzo Wa Matatizo Yote Ulimwenguni.

 Sadick Kilasi     March 17, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ukisoma kitabu cha Biblia utagundua kabisa mauti yalianza kuonekana au kutokea pale bwana Kaini alipomwua ndugu yake Habili. Hapa ndipo matatizo yanaonekana kuanza, mwanzo nne, (4).

Sasa waweza kujiuliza nini chanzo cha yote hayo, lakini ukweli ni kwamba TAMAA ndio chanzo cha matatizo hapa duniani. Kaini alikuwa na tamaa juu ya mazao yake, alikuwa analima anapata vizuri,  mazao yanastawi, lakini yeye alikuwa na tamaa akawa anatoa zaka mbovu au matoleo mabaya  kwa Mungu. Anachagua vile ambavyo ni vibovu ndivyo anamtolea Mungu.

Matatizo mengi hapa nyumbani Afrika, vita vingi, mauaji mengi yanatokea hii yote ni kwa sababu ya tamaa. Viongozi wanatamaa na uloho wa madaraka. Tunaona nchi nyingi zina vita vya wao kwa wao yote hiyo ni kwa sababu ya tamaa.

Mpendwa msomaji, mtu yeyote yule ukimkuta na mawazo mengi ni kwa sababu ya tamaa. Lazima kuna kitu anataka na hapo ndipo mwanzo wa mawazo ya mtu huyo. Tamaa ndiyo vita ambayo tunapaswa kupigana nayo, tamaa ndio mwanzo wa matatizo yote.

Leo hii vijana wengi wapo mitaani wameharika kwa madawa ya kulevya yote hiyo ni kwa sababu ya tamaa. Waliamani watakuwa matajiri lakini hawakutaka kulipa gharama ndipo wakajiingiza kwenye madawa ya kulenya kwa sababu ya msongo mawazo.

Tamaa huzaa mauti, ukitaka sana mwisho utakuwa takataka. Maisha yanahitaji utulivu, wacha kukuza matatizo na kujiona wewe ndiye mwenye matatizo sana, unataka kila kitu unakazana tu kukusanya tu bila kupunguzwa mwisho utakuja kupasuka. Ndio maana kuna kujumrisha na kutoa, hasi na chanya, zidisha na kugawanya, yote hii imekuja kwetu ili tutambue ya kwamba ukizishiwa kumbuka kugawa, ukiongezewa kumbuka kutoa. Toa zaka hata kama kipato chako ni kidogo au kikubwa, dunia huwa inatabia ya kujaza pale ambapo patupu na kupunguza palipo jaa. Anza kuishinda tamaa kwa kutoa zaka hata kama kipato chako ni kidogo kiasi gani.

Kutoa zaka ni kwaajili ya sisi wenyewe, Mungu kaweka sheria hii ili tuwe na shukrani. Shukrani ni uwezo wa kutambua mazuri juu ya mabaya. Kwa sababu hiyo Mungu kaweka zaka ili sisi tupate kuwa na furaha kwa shukrani.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, March 16, 2018

Kwa Vyovyote Ulivyo, Jitofautishe Kwa Jambo Zuri. $#Tafakari Chumvi Za Wazee Wetu.$#

 Sadick Kilasi     March 16, 2018     HEKIMA ZA WAZEE     No comments   

Abraham Lincoln,  raisi wa kumi na sita (16) wa Marekani alishawahi kusema, 'kwa vyovyote ulivyo, jitofautishe kwa jambo zuri'. Hii ni barua kwa kila mmoja na ni chumvi na hekima kutoka kwa mzee huyu.

Karibu mpendwa msomaji tutafakari kwa pamoja hekima hii, ambayo tumeachiwa itusaidie katika maisha yetu.

Kwa kawaida kila binadamu ameumbwa akiwa na uwezo mkubwa sana, kila mtu ameubwa akiwa bora katika maeneo fulani au na katika mambo yale ambayo hayupo bora anauwezo wa kufanya akuwe na awe bora pia. Kwa mfano, wewe unaweza ukawa na kipawa cha uimbaji, kumbuka kipawa ni zawadi ambayo mtu anazaliwa akiwa nacho, lakini pia licha ya kuwa na kipawa cha uimbaji unaweza ukafanya kitu kingine na ukawa bora pia, mfano, unaweza ukawa mkulima mzuri tu kutokana na kujiendeleza mwenyewe.

Kwa kawaida binadamu anamapungufu, na mapungufu huwa yanaonekana ni mengi kwa sababu kama unavojua dunia hii mabaya ndiyo huwa yanasambaa haraka sana. Kuna wakati unaweza ukajikuta kama wewe si lolote si chochote yaani unajiona kana kwamba wewe huwezi kitu, Si bora kwa chochote. Sasa Lincoln anatukumbusha ya kwamba kwa vyovyote vile ulivyo, jitofautishe kwa jambo zuri.

Wewe una jambo zuri unalo, unaweza kuwa unajua, harafu unadharau kwa sababu ya  kuambiwa au kukata tamaa na kuona huna jambo zuri ambalo unaweza kufanya na kuipa jamii kitu. Waweza pia ukawa hujui kwamba wewe upo bora maeneo yapi, lakini nakwambia rafiki yangu nikutie moyo tu kwamba wewe ni bora sana, hebu tafuta eneo ambalo ukifanya unaona kwako wewe ni bora au angalia jamii na ona mapungufu yako wapi na uwe na kiu ya kwamba jamii inependeza ingekuwa hivi hivi na hivi.

Mpendwa msomaji, kila mtu ni barua, barua ambayo jamii inahitaji isome, kumbuka tumezaliwa kuijaza dunia sehemu ambazo zinamapungufu, sasa hayo mapungufu uliyo nayo na sehemu ndogo unayoiona ni bora kwako basi hiyo ndiyo sehemu ambayo jamii inahitaji.

Una mengi mazuri ambayo jamii inahitaji kutoka kwako, usione mapungufu mengi kutoka kwako hayo ni sawa na maharage mabovu tu yanayojitokeza haraka lakini kuna mengi mazuri yapo chini anza sasa kutumika katika sehemu ndogo au uzuri ulionao.

Wewe ni tofauti na wengine, tuna vidole vitano kila kidole kinasaizi yake lakini ili ngumi iwe na nguvu vidole vyote vinahitajika na ubora unakuwepo. Wewe ni wa tofauti na wengine, utofauti wako ndiyo kitu pekee ambacho jamii inahitaji ili kutengeneza ubora, tafadhari, tafadhari usiinyime jamii ulichonacho na hapo ndipo mafanikio yalipo.

Endelea kutembelea blogu hii ili kijifunza zaidi.
Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 15, 2018

Kila Kitu Kinahitaji Subira, Je Unataka Kuwa Gaidi Wa Kila Kitu ?

 Sadick Kilasi     March 15, 2018     BIASHARA, KUFURAHIA MAISHA, NJOZI, UJASIRIAMALI     No comments   

Maisha ambayo hayana subira ni maisha ambayo yanakosa mwelekeo. Ukikosa subira utafanya vitu vingi kwa wakati mmoja na bado hutofikia malengo yako. Maisha kwako yatakuwa ni maumivu kila siku. Subira ni uwezo wa kuvumilia kwa kitambo na bila kuumizwa na jambo lolote.

Ugaidi ni kitendo cha kudhibiti au kukabili jambo kwa nguvu kwa matakwa yako bila ya kuwa na subira. Ugaidi huwa unajalibu kulazimisha jambo ambalo linahitaji kuwa na subira.

Ukweli ni kwamba zana hizi tumekosa subira na uvumilivu na tumekuwa magaidi wa kila kitu, kwetu maisha ni masumbuko ni kwaajili ya kufanya kila kitu kwa kujaribu kulazimisha, watu wamekuwa magaidi mpaka kwenye biashara zao, wanaanza leo kesho wanataka kupata faida, biashara inahitaji uvumilivu na muda lakini sisi tunataka mambo yawe haraka haraka kama sisi tunavotaka. 

Unaweza pia ukawa unafanya jambo ambalo linahitaji subira kidogo, kwa mfano, unahitaji kufungua chupa tu ya maji, sasa kutokana na kukosa subira chupa inakuwa imefungwa vizuri sasa unashindwa kufungua, ukikosa subira itakuwa ni maumivu kwako, utamlaumu weee aliyetengeneza chupa hiyo na wewe kupoteza furaha yako. Kukosa subira ni ugaidi, unapojaribu kukabili kila kitu kwa nguvu zako huo ni ugaidi.

Mpendwa msomaji, watu wengi kwa sasa tunachangamoto nyingi sana za kukosa subira. Kila jambo ambalo mtu anafanya anatafuta njia ya kumaliza hapohapo, watu tumekosa uvumilivu na subira, tunapendezwa na matokeo na hatutaki kulipa gharama, kila kitu kina gharama yake, lazima uwe tayari kulipa ili ufikie kule unakotaka kufika.

Acha kuwa gaidi wa kila kitu, kuwa na subira, lipa gharama, pata unachotaka. Kumbuka kuishi falsafa ya mti, mazizi yako lazima iende chini sana na ndio msingi wenyewe, shina ndio nguzo yenyewe na matawi ni mazao ya kazi yako. Usiache maneno yetu ya mwaka 2018, kuwa$fanya#pata.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com. 
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, March 14, 2018

Kama Unataka Maisha Yako Yawe Bora, Basi Yakupasa Utangaze Mambo Haya Katika Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     March 14, 2018     NJOZI, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Katika maisha kuna mambo mawili ambayo yana nguvu sana. Mambo haya ukiyatangaza katika maisha basi wewe lazima utakuwa mshindi siku zote. Vitu hivi viwili baadae husimama kama mshindi japo hufanyika polepole sana.

Upendo na ukweli, ndivyo vitu pekee ambayo msomaji wangu unapaswa kutangaza kama unataka maisha bora. Upendo ndio unaotawala dunia, penye upendo hapakosi furaha, upendo una nguvu sana.

Ukweli siku zote huibuka mshindi, Mpendwa msomaji, lazima utangaze katika maisha yako kwamba utaishi kweli katika maisha yako yote ili maisha yawe na furaha. Ukweli siku zote unakuweka huru, ukweli umeushinda uongo hata kabla ya kushinda, ndiomaana maisha ya ukweli ni ya furaha tupu.

Ukitaka kuwa mshindi zaidi ya mshindi, basi yakupasa utangaze kuishi vitu hivi viwili, ushindi zaidi ya ushindi ni kuishi imani ya ukweli kwamba utashinda na maisha yako yanatawaliwa na furaha tele.

Sasa waweza kujiuliza nawezaje kuishi ukweli na kuwa na upendo na watu, unapoenda kulala, tamka, mimi Sadick, au mimi mtu fulani, mimi ni ukweli, nitaishi kweli, nawapenda watu, nawapenda watu, tamka zaidi, zaidi na zaidi hayo maneno. Tabia hii itaanza kujengeka polepole ndani yako na utajikuta unaishi kweli na unakuwa na upendo na watu. Tamka hata wakati wa asubuhi.

Maisha yako yanapaswa kutawaliwa na furaha wakati wote, na hiyo furaha ipo ndani yako bado mwenyewe, hujaiamsha na kuanza kuitumia. Achana na furaha ya kutafuta nje kupitia vitu, hiyo siyo furaha ya kweli, hiyo ni ya muda mufupi, tafuta furaha ya kweli. Upendo na ukweli, vitakupa furaha ya kweli.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 13, 2018

Ushahidi Huu Hapa Unaonyesha Wewe Ni Mtaalamu Wa Kupalilia Matatizo.

 Sadick Kilasi     March 13, 2018     MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa ushindi mkubwa ambao Mwenyezi Mungu kakushindia, mimi na wewe mpendwa wangu tumebahatika kuifikia siku hii ya leo. Wapo wengi ambao waliiwekea malengo na mipango siku hii lakini hawajabahatika kuiona wala kuifikia.  Neema na rehema za Mwenyezi Mungu zimetufikisha hapa. Hatuna cha kumlipa Mungu sisi zaidi ya kukazana kuzifuata sheria zake na kumrudia yeye maana anatupenda kwelikweli. Pendo lake halina mipaka kwetu anatupenda tu sisi.

Mpendwa msomaji, katika hii dunia matatizo yapo kwaajili yetu, sisi ndiyo tumekuwa ni vyanzo vya matatizo. Tumeifanya dunia ni kwamba ni sehemu ya vurugu na kusababisha migogoro mbalimbali. Leo nataka nikuonyeshe namna gani unasababisha matatizo hata kama wewe unajiita mtu mwema, lazima ujitambue ya kwamba wewe ni chanzo cha migogoro.

-Kuna msemo unaosema dawa ya moto ni moto. Huu ni msemo ambao tumekuwa tunautumia kulipiza visasi, sasa ndungu yangu kama moto ukiendelea kuochochea unafikiri mwisho itakuwa nini? Si majanga matupu, kama ukikosewa jitafakari kwanza wewe mwenyewe, jihukumu kwanza wewe mwenyewe, usikimbilie kuangalia nje yako nani aliyekukosea, kumbuka wewe ndio chanzo, yaani uwepo wako tu haijalishi hukufanya lolote tayari wewe ndiyo chanzo, kwahiyo jihukumu kwanza wewe kisha ndo useme dawa ya moto ni moto. Leo naomba nikupe siri moja rafiki yangu wewe ambaye unapenda sana kulipa visasi, dawa ya moto ni kuuzima, ukipiga kelele penye kelele husikiki ng'o. Kumbuka hili siku zote.

-Unapotoroka changamoto. Katika hali ambayo siyo ya kawaida sisi ni wataalamu sana na kutoroka changamoto zetu, sasa kwa bahati mbaya au nzuri tupo kwenye kizazi cha neema, hiki ni kwamba ukikosea tu hukumu inaanza hapo hapo. Mpendwa wangu, hukumu imeanza tayari hapa hapa duniani, kama ulifikiri mpaka ufe ndio hukumu itaanza hapana, hapa hapa unakata tiketi na kujijua kabisa ya kwamba utaenda motoni. Ulishawahi kujiuliza hofu na woga vinasababishwa na nini? Ni kujaribu kutoroka matatizo, unaanza kuhukumiwa mapema na kusababisha maumivu kwenye maisha yako. Kutoroka matatizo ni kupalilia matatizo.

-Kupenda mambo ya anasa. Kuna watu ni wapaliliaji wazuri sana wa matatizo,  wanapenda burudani kuliko furaha, wanamapenzi sana kuliko upendo. Kupenda anasa ni kupalilia matatizo, tunaibua matatizo ambako yamejificha huko kwa tamaa zetu, tunapenda burudani ambazo siku zote zinabomoa, hakuna burudani inayojenga zaidi ya kubomoa tu, tafuta furaha, usitafute burudani.

-Tamaa na ubinafsi. Tamaa yako inakuonyesha wewe ni mtaalamu wa kupalilia matatizo. Kupenda mambo yawe kama wewe unavotaka ni kupalilia matatizo. Kuna mambo yapo na lazima ukubali kama yalivo huna haja ya kusumbuka nayo, utaumia bure kabisa, kutaka mwenzako afanye kama inavotaka wewe ni kupalilia matatizo, kusubili mwenzako ajishushe wakati amekukosea ni kupalilia matatizo, kwahiyo lazima ujiulize vizuri kabisa mpendwa wangu, ya kwamba hiki kitu kipo chini yangu au chini ya uwezo wangu, ndo ujue namna ya kufanyia kazi.

Mpendwa msomaji,  sisi ndio vyanzo vya matatizo, watu sio wabaya, ubaya upo kwako wewe unaye uona, Mwalimu Deo Kessy, ametuonya ya kwamba tuache kabisa kupenda mambo ya giza, mambo hayo ni mabaya, ni kupalilia matatizo, unajiweka kifungoni mwenywe, hukumu inaanza kwako mapema kabisa, tuache uongo ni kupalilia matatizo, ubinafsi, hiki ni kipindi cha neema, hukumu inaanza hapo hapo ukikosea na ndo unakuwa unajikatia tiketi ya kwenda motoni, ubinafsi wako usikupeleke motoni.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Nisaidie kuwashirikisha wengine ili ujumbe huu uwafikie wengi zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, March 12, 2018

Unanjaa Na Kiu Ya Kitu Gani?

 Sadick Kilasi     March 12, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Heri wao wenye njaa na kiu ya haki, maana wao watashibishwa. Ni mstari ambao unapatikana kwenye Biblia na unatupa mafunzo makubwa sana. (Mathayo 5-6).

Kitu chochote ambacho unakazana kufanya ndicho ambacho kitainuka na kuwa kikubwa sana. Jambo lolote lile ambalo unalipa kipaumbele sana litajengeka na kuwa kubwa sana.

Je wewe unanjaa na kiu ya kitu gani? Unafanya nini? Au unagusagusa tu mambo yako, Leo unafanya hiki, unaacha, kesho kile, unaacha, kesho kile, unaacha, hijaweka vipaumbele, utajazwa kwenye nini?

Chagua kitu kimoja ambacho unapaswa kukijengea misingi na kusimamisha kwa uhodari na ni jambo ambalo ndilo litakuwa legasi katika maisha yako. Jambo ambalo hata kizazi kijacho kitasema hii ni kazi ya mtu fulani, tunajivunia kwa kazi yake nzuri.

Tengeneza misingi, tengeneza uhodari, usiwe mtu wa kufanya kila kitu lazima uwe na njaa na kiu ya haki, Mwenyezi Mungu katuahidi kutujaza. Lazima uwe hodari katika mapito yako, Mungu alimwambia Joshua   uwe hodari, kuwa mkakamavu utashinda.

Njaa na kiu ya haki, mpendwa msomaji, hali ya uhitaji mkubwa sio kilele mama hapana, lazima uoneshe ushirikiano kweli kweli ndipo utapata unachokitaka. Mpendwa, sio lahisi kutengeneza misingi yako, lazima ufanye kwa bidii na ndipo utapata unachotaka.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 11, 2018

Kuna Watu Wanakupenda Wewe.

 Sadick Kilasi     March 11, 2018     No comments   

Katika maisha lazima utambue kuna watu wanakupenda, wapo watu watakao kukataa na kukuona hufai na huna maana kabisa lakini lazima ukumbuke kuna watu wanakupenda sana wewe. Wanakupenda pasipo chochote.

Kukataliwa na mmoja sio kukataliwa na wengine, kukataliwa na huyu sio kukataliwa na yule, kukataliwa na ndugu sio kukataliwa na rafiki, kuna watu wanakupenda wewe, tena sana kuliko wewe unavo fikilia, acha kukata tamaa, acha kuona kwamba dunia imekutenga, wewe ni wa muhimu sana lazima utambue hilo.

Usijinyonge kwa sababu ya mtu mmoja kuonyesha kwamba hakupendi, usijinyonge eti kwa sababu mwenzi wako anakuona wewe huna maana, Mpendwa msomaji, asiye jua umuhimu wako hajakujua wewe vizuri, kuna kundi kubwa sana la watu wanao kupenda wewe wapo nyuma yako. Je wewe huwapendi? Mbona sasa unawakana kwa kujiona hufai? Wao wanatambua thamani yako wewe kuliko huyo aliye kukataa, kuna watu wanakupenda sana wewe.

Wapende watu mpendwa wangu, wapende wanao kupenda, wapende zaidi na zaidi wasio kupenda maana hao hawajajua haswa umuhimu wako tena hawajui nini maana ya upendo, onyesha upendo pasipo pendeka utakuwa shujaa wa ukweli. Penda bila kutegemea chochote, maana wewe utakuwa kama mpanzi ambaye anapanda mbegu zake na kusubili mavuno makubwa huku akiwa na uhakika wa kuvuna baadae bila kuigombeza ardhi.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, March 10, 2018

Maisha Yanakuwa Magumu Kwa Maskini Na Matajiri Unapokuwa Na Kitu Hiki.

 Sadick Kilasi     March 10, 2018     NJOZI     No comments   

Natambua ya kwamba ushawahi kukutana na mtu ambaye anasema kwamba mimi siwezi kuwa tajiri kwa sababu maisha ya matajiri ni magumu sana. Inawezekana wewe mwenyewe unaamini hivyo ya kwamba maisha ya matajiri ni magumu sana. Je ni ukweli huo kwamba maisha ya matajiri ni magumu sana au yana matatizo mengi? Karibu sana ujifunze leo kwanini matajiri wengi hawaufurahii utajiri wao, na maskini nao pia kwanini maisha yao ni magumu.

Sasa waweza kujiuliza ya kwamba sasa inamaana gani kama nikiwa tajiri sifurahii utajitari wangu na nikiwa maskini nakosa furaha. Mpendwa msomaji kuna sababu ambazo huwa zinapelekea kukosa furaha hii, sio kila tajiri hana furaha na siyo kila maskini hana furaha. UBINAFSI  ndicho kitu ambacho hupelekea matajiri na maskini kukosa furaha.

Kwa hali ya kawaida ni kwamba ubinafsi hauchagui wa kutawala maskini na matajiri, ubinafsi ni pale ambapo unashindwa kujiweka nafasi ya wengine. Kwa kawaida ubinafsi unaumiza zaidi hata kuliko matatizo tuliyo nayo. Ukiwa na pesa na ukawa mbinafsi utateseka, ukiwa maskini na ukawa mbinafsi, ahaa wewe ndo kabisa maana utakuwa na kibuli cha kutosha, maisha yako yatakuwa magumu sana.

Hivi ushawahi kusikia hasa kwa maskini anakwambia, natafuta hela ya kula tu, katika maisha ukijikuta kila siku unatafuta, kwaajili ya mahitaji yako basi ni hatari sana, maisha yatakuwa magumu, unachokazana wewe ni kutatua matatizo yako binafsi na unashindwa kuangalia wengine na kusema natafuta hela ya kula tu. Mpendwa msomaji, tumezaliwa kuwasilisha tulicho nacho kwa wengine, kama sivyo haja ya kuzaliwa isingekuwepo kabisa. Tumezaliwa kutumika kwa wengine.

Kama wewe unafikiri kukusanya vitu vya dunia hii ndio utamaliza matatizo yako basi unafeli, utajiri sio wa pekee yako, umebarikiwa kuwa baraka kwa wengine. Kuwa na pesa sio njia ya kuwaonyesha watu kwamba wewe unazo lazima utakuwa na maisha magumu sana, kuna vitu ambavyo pesa hawezi kununua, utu wa mtu, na kama unaona ya kwamba mbona nawanyanyasa basi unawanyanyasa wenye tamaa kama wewe.

Kama wewe maskini unafikiri huna haja ya kufanikiwa basi wajipotodha mwenyewe, ukiushinda ubinafsi mafanikio kwako ni kitu rahisi sana na yatakufuata yenyewe. Kocha Makirita Amani anausemi wake unaosema, Mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa ni wewe tu uamue ufanikiwe au usifanikiwe. Sasa kama  wewe ni mwenye uamuzi, uteseke na ubinafsi wako maana kushindwa kufanikiwa pia ni ubinafsi, kuna kitu ambapo umeshindwa kuipa jamii na ndio maana umeshindwa kufanikiwa. Tajiri jali utu kuliko vitu na maskini hivo hivo.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, March 9, 2018

Je Ulipo Upo?

 Sadick Kilasi     March 09, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Habari za wakati huu mpendwa msomaji, natumai unaendelea vizuri.

Nina swali msomaji wangu, hivi ulipo upo?  Kama unapretend nafasi uliyopo je hiyo ni nafasi yako kweli? Unajua nini msomaji wangu, sisi ni wataalamu wa kuigiza sana. Rafiki yangu kuigiza maumivu sana.

Jiulize swali mwenyewe, wewe mwenyewe unatambua maeneo gani unawadanganya wenzako. Je ulipo upo?

Ishi kweli, ukweli utakuweka huru.

Wako Sadick kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Adhabu Tunayopewa Baada Ya Kuvunja Sheria Ya Asili Ya Dunia.

 Sadick Kilasi     March 09, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO  LA USHAURI, kama unasoma hapa hongera kwa ushindi ambao Mwenyezi Mungu katushindi, hatuna budi kumshukuru yeye ambaye katuamsha salama na kuiona siku hii mpya. Wapo wengi walio wekea malengo siku hii lakini wameshindwa kuiona. Je mimi na wewe mpendwa wangu, tumefanya jambo gani kama si neema za Mwenyezi Mungu?

Wakati tulipo zaliwa, tulizaliwa tukiwa tayari na tunapaswa kuenenda katika uhalisia wa asili ambao Mwenyezi Mungu alituandalia. Tulipaswa kutiririka kama maji ya mto katika safari yetu ya maisha. Ukivunja sheria ya asili ya dunia lazima utapewa adhabu. Yusuph aliyeandikwa katika kitabu cha biblia, alivunja sheria kwa kuwaambia ndugu zake habari za maisha yake na namna ndugu watakavo msujudia ilibidi apewe adhabu kwa kuuzwa na ndugu zake hao hao alio wambia ambao walikuwa hawana uwezo wa kuvumulia. Mungu alimwonesha maisha ya baadae lakini yeye akawaambia ndugu zake ikabidi apawe adhabu.

Mpendwa msomaji, kama unapitia changamoto kwa sasa, tambua ya kwamba unapitia katika adhabu yako, kuna sehemu umevunja sheria kidogo ndiomaana unaadhibiwa.  Mungu anataka utambue makosa yako mwenyewe ili utoke katika adhabu yako. Ndio maana si vizuri mtu anayepitia wakati mgumu kumsaidia ni vizuri yeye mwenyewe kujisaidia ili afikilie vizuri wapi alikosea? Na awe na majibu sahihi ili baadae isiwe changamoto tena kwake.

Je unapitia katika changamoto nzito? Basi yakupasa utubu makosa yako ili uanze tena, dunia haiwezi kukuacha ukawa unakosea na kutafuta mbinu zako za maisha lazima uadhibiwe. Ukishindwa kuchagua mwanamke mzuri wa kukufiti dunia lazima ikuadhibu, ukitafuta utajiri wa haraka dunia lazima ukuadhibu, haiwezi kukuacha salama katika mapito yako ya kuvunja sheria.

Lakini pamoja na adhabu unayopitia nikutie moyo ya kwamba ukitubu, furahia ukiwa katika adhabu hiyo maana ikitoka hapo si sawa na ambaye hajakosea, si sawa na ambaye hajapitia katika adhabu hiyo, utakuwa mkomavu haswa, huta tikiswa na hutatikisika kwa kitu rápido.  Upitiapo changamoto jifunze na ufurahi maana kwako ndio mwanzo wako wa ushindi.

Sheria ya asili ya dunia inakuadhibu ukishindwa kuifuata, huwezi kuachwa hivi hivi ukitafuta mbinu zako na kuvunja sheria lazima utapokea adhabu lazima ujifunze, unapotaka kitu bila kufanyia kazi dunia inakuadhibu kwa sheria yake kwa sababu ya tamaa yako. Ishi maisha, acha kutaka, tafuta, usitafute mbinu, tiririka, mbinu zitakuumiza.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 8, 2018

Tunapohisi Wengine Wanatutendea Ubaya.

 Sadick Kilasi     March 08, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa kujaliwa kuiona siku hii, mimi na wewe hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia siku hii mpya ya leo, ni ushindi mkubwa sana.

Moja kati ya sifa mwanadamu ni kujilinda na kujihami na chochote kile kinachotokea. Bila shaka ushawahi kujikuta unamhisi mtu anakuongelea ubaya kwa mwingine kisa kuna siku mligombana kidogo ama la! hampatani vizuri, ni tabia ambayo tunayo sisi, ni tabia ya mwanadamu kujiona mimi, nasemwa, mimi mnaniteta, mimi mnanitenga na tabia kama hizo za kibinafsi.

Kipindi kinakuwa ni kigumu sana kwa muhusika, asisimame mtu kuongea na mtu anaona ni kama yeye anasemwa, ni maumivu makali ambayo unajipa mwenyewe kwa kushindwa kupambabua nyakati.

Ni wakati wa kubadilika, ni wakati kufurahia maisha, huna sababu ya kuwaza hivo juu ya wengine, na njia pekee ya kujitibu na hilo ni kujiuluza mwenyewe hivi nipo sahihi? Au najistukia mwenyewe? Hata kama kuna mtu anakusema kwa ubaya, kitu gani kinapungua kwako, na kama unaamini hujafanya hivo basi lipa ubaya kwa wema. Furahia maisha, ondoa ubinafsi ndani yako, usipambane na watu pambana na hali, watu sio wabaya wewe ndiye unayeona ubaya. Kwahiyo wewe ndiye tatizo.

Endelea kujifunza kupitia blogu hii ya JIKO LA USHAURI.

Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, March 7, 2018

Tunaona, Tunasikia, Tunashuhudia, Tofauti.

 Sadick Kilasi     March 07, 2018     MAHUSIANO, USHAURI     No comments   

Ukisoma vitabu vya injili ya Yesu, kitabu cha cha Mathayo, kitabu cha Marko, kitabu cha Luka na kitabu cha Yohana ni vitabu ambavyo vinaelezea historia moja ya Yesu. Lakini vitabu hivi pamoja na kila mmoja alikuwa anaandika kitu kimoja wote, lakini kunautofauti ambao upo kwa sehemu kubwa mno. Kila mmoja alikuwa anaandika sawa sawa na alivosikia yeye na alivoona yeye.

Tunaweza kujifunza kupitia vitabu hivi, waliona tofauti jambo moja, na hiki ndio kipawa cha mtu.  Tunaona tofauti, tunasikia tofauti na kuwasirisha tofauti. tunawasirisha uhalisia uliopo ndani mwetu  sio kuongozwa na wengine.

Watu wengi zama hizi tumefungwa na wengine, tumekuwa tukifuata uelewa wa wengine na kushindwa kutumia uwezo wetu uliopo ndani mwetu. Mpendwa msomaji, kila mmoja anakipawa chake, tukijiamini na kuacha kufuata mikumbo lazima tutainua vipawa vyetu, tumeumbwa tukiwa na uwezo mkubwa sana lazima tuwasilishe ukweli wetu na uhalisi wetu.

Watu wengi wameshindwa kuwasirisha ukweli wao kwa sababu wanahisi wao hawafai, wanaogopa kukosolewa, wanajilinganisha na wengine, mwisho wanaona kwamba hawana uwezo wa kutoa maoni yao kutoka ndani mwao. Mpendwa msomaji,  kilicho ndani mwako ni kikubwa sana, Mwenyezi Mungu kakujalia hicho lazima ukiwasilishe kwa watu ili ulete ubora wa utofauti kama kwenye vitabu vya injiri. Waliandika kitu kimoja lakini kila mtu aliwasilisha kutokana na uwezo wake. Leo hii vitabu vyote ni vya muhimu japo ni historia moja, aliposhindwa kukazia mwingine vizuri, mwingine alionyesha vizuri na kazi ikaeleweka.

Mpendwa msomaji, imeandikwa alaaniwe tule amutemeaye mwanadamu kwenye biblia, hii ilikuwa inamaana kila mtu kampa uwezo wake lazima tutumie akili zetu vizuri,  uzuri ni kwamba akili zetu zinakua yaani tulivyo hivi tumekamilika kinachohitajika ni kuamsha akili zilizolala na kuzitumia vizuri kadili unavyotumika ndivyo nayo inaamka zaidi.

Mpendwa msomaji, tupo duniani kuwasilisha tulicho nacho, dunia inamaswali juu yetu lazima tuyajibu kupitia akili zetu, watu wanatutegemea lazima tutumie vizuri akili zetu, sisi ni zaidi ya tulivo sasa, wewe ni zaidi ya ulivo sasa, tumia akili yako vizuri kujisaidia mwenyewe na wengine pia, acha kumtegemea binadamu mwenzio,  tunaona tofauti, tunasikia tofauti na lazima tuwasilishe tulichoona na hapa tutakuwa tinajitendea haki wenyewe. Wewe ni mshindi, umezaliwa kushinda.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, March 6, 2018

Acha Kuteswa Na Mambo Yaliyopita.

 Sadick Kilasi     March 06, 2018     NJOZI     No comments   

Siku zote nimekuwa nikianza kuandika kwa kusema, "ni siku nyingine tena mpya", ni maneno ambayo nimekuwa nikianza nayo katika uandishi, ni maneno machache lakini huwa naamini ya kwamba, kila siku kwetu ni mpya ni zawadi kubwa sana kwetu.

Katika maisha tumekuwa tukipitia mapito mbalimbali lakini pale ulipo sasa ndipo penye thamani kubwa kuliko kwenye kumbukumbu ya mapito na siku ambayo unaitalajia kuifikia, siku ya kesho.

Mpendwa msomaji, inawezekana umepitia mapito mabaya ya kukuumiza na ya kukutesa lakini sasa unatakiwa kuanza siku mpya hii ya leo ukiwa tayari umejitangazia ushindi mkubwa na endelea kusonga mbele bila kujali mapito yako na changamoto ulizopitia huko nyuma.

Mpendwa msomaji, kama tayari umesha fanya maamuzi ya kusonga mbele lazima ukatae kabisa kuteswa na mapito yako, lazima ujitoe kikamirifu katika kusonga mbele na usigeuke nyuma. Mpendwa msomaji, mke wa Luthu aligeuka nyuma akawa jiwe, Yesu alimwambia mtu ambaye alitaka kwenda kumzika  baba yale ya kwamba wawaache wafu wajizike wenyewe. Mwalimu Nyerere alikuwa anawasimulia watu katika hotuba zake, stori moja, kuna mwanamke mmoja mzuri ambaye alikuwa sehemu moja ya mlima, na chini ya mlima kabla ya kuufikia mlima huo kulikuwa na bibi kizee, sasa wanaume wengi walitamani sana sana kumwona huyo mwanamke huyo mzuri, changamoto ilikuwa ni kwamba kabla hujamfikia huyo mwanamke kulikuwa na sauti kali sana ambazo zinakuzomea, huyo!! huyo!!!!!huyo!!!  auawe!!!, ni sauti ambazo ziliwatesa wengi sana ambao walitamani kumwona yule mwanamke mzuri na ukisikia sauti na ukigeuka nyuma basi wewe unageuka jiwe. Basi kulikuwa na kijana mmoja ambaye yeye alijitoa kweli kweli, akamwambia yule bibi kizee, bibi mimi nataka kwenda kumwona huyo nwanamke mzuri, bibi akamwambia we kijana mdogo wenzako wameenda huko wengi wamegeuka mawe na wewe unataka kugeuka jiwe? Kijana akamwambia akamwambia bibi nataka nikanwone huyo mwanamke, bibi akamwambia haya nenda lakini jilinde na sauti hizo na usigeuke nyuma, kijana akaenda, huyo!!! huyo!!!auawe!!!auawe!!! Sauti ilikuwa kali kadili anavyosonga mbele, lakini kijana hakugeuka nyuma na akamfikia mwanamke. Mwanamke akamwambia kwa sababu wewe ni wa kwanza kunifikia wengine waligeuka nyuma basi wewe utakuwa mme wangu.

Mpendwa msomaji, nimekuonyesha mifano mitatu, inayoonyesha namna gani mapito yalivo nauwezo wa kukufanya usiendelee mbele, mifano hii ni funzo kubwa sana, usirudi nyuma lazima kwa hiyali yako useme nitasonga mbele, NITASONGA  MBELE bila kujali nimepitia katika hali gani, ni kusudi lako tu kuamua kwenda mbele na kuyafikia mafikio unayotaka bila kipingamizi chochote.

Kelele ni nyingi, wapo ambao watasema huwezi, lakini wewe ishi sasa na kusema mimi ni mshindi, kunawakati wewe mwenyewe utasema, hapa siwezi lakini lazima ujipe moyo na kusema mimi ni mshindi. Anza siku mpya kwa ushindi mkumbwa,  kataa kuteswa na mapito yako, hiyo ni njia uliyopitia tu.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.



Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, March 5, 2018

Hizi Ndizo Sababu Zinazopelekea Kuwa Na Chuki Na Watu.

 Sadick Kilasi     March 05, 2018     MAHUSIANO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama. Kama unasoma hapa  basi hongera  kwa ushindi wako wa kuamka salama. Hatuna  budi mimi na wewe kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuamsha na kuiona siku hii ya leo. Wengi waliiwekea malengo na vipaumbele lakini wameshindwa kuamka. Mimi  na wewe ambao tumebahatika kuiona siku hii lazima tuiwajibikie vizuri siku hii.

Mpendwa msomaji,  kumekuwepo na watu ambao wanasumu kubwa sana ya chuki dhidi ya wengine. Yaani mtu anaishi na chuki kama mafuta ambayo yanasubiliwa kulipuliwa na moto au gesi ambayo inataka kupasuka. Watu wamekuwa na chuki ndani yao, watu wamekuwa wanasumu kali ndani yao, kitu ambacho ni hatari sana kwao na kwa wanao wachukia pia.

Kuna sababu ambazo hupelekea wengine wawachukie wengine. Japokuwa kuna sababu ambazo zipo, isiwe sababu kwako wewe msomaji wangu kuwachukia wengine, wewe ni mwanaharakati wa ukweli na upendo, lazima usimamie ukweli na upendo na usiwe na sababu yoyote ile ya kumchukia mtu.  Sasa hizi ni sababu ambazo zinapelekea wengine kuwachukia wengine.

1.Kumwangalia kwa mtazamo wa ubaya tu.  Hii ni sababu kubwa sana ambayo inapelekea wengine kuwa na chuki na wengine. Sisi binadamu kwa kawaida tunatabia ya kuangalia mabaya tu kwa wengine lakini hatuwezi kuangalia kwa jicho la uzuri. Mpendwa msomaji, ukiona mtu ni mbaya kwa wengine usimchukie yeye bali chukia mabaya ambayo yapo hapa duniani, chukia macho yako na fikra zako ambazo zinaona mabaya, acha kuhukumu mtu mwingine msome mtu kwa mzuri tu, jicho lako lijifunze kuangalia mazuri badala ya mabaya. Wote tulizaliwa tukiwa safi,  Mwenyezi Mungu anatupenda sisi sote na mabaya yetu, upendo wake hauna mipaka, anataka sisi tubadilike na tuwe na upendo kama yeye. Mpendwa msomaji, kuna mtu unamchukia, usiendelee kumchukia, kuendelea kumchukia ni kama mtu ambaye yupo kwenye giza umpeleke kwenye giza zito zaidi, mwoneshe upendo jinsi ulivo na hiyo ndiyo nuru ambayo anatakiwa kuipata mtu ambaye yupo kwenye giza.

2. Sababu ya pili ni ubinafsi. Mpendwa msomaji, ubinafsi ni kitu kibaya sana, ubinafsi unapelekea magomvi kwa watu. Ubinafsi ni hali kujiona wewe unastahili kulingo wengine. Ubinafsi ni kitu kibaya sana, ubinafsi unapelekea kuwa na maisha magumu sana. Mpendwa msomaji, unapokuwa mbinafsi unashindwa kuona thamani ya wengine, kila kitu ambacho unafanyiwa utaona hakifai kwako.  Tabia hii si nzuri na itakutesa sana mwenyewe  lazima utambue thamani ya wengine na kuwajali.

Upendo ndio hali pekee ambayo imeshinda haya yote. Ukweli ni jambo ambalo litaondoa hofu na maumivi. Ishi kweli na upendo, maisha yako yatakuwa mazuri.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, March 4, 2018

Fanya Kitu Hiki Unapokutana Na Upinzani Wakati Unafanya Jambo Ambalo Misingi Yake Ni Ukweli.

 Sadick Kilasi     March 04, 2018     MAHUSIANO, TAFAKARI YA ROHO, USHAURI     No comments   

Endelea kusonga mbele na ziba masikio yako kabisa unaposimamisha ukweli. Hivi ndivyo nataka kukwambia msomaji wangu, ukweli haujawahi kumuangusha yeyote yule, hata kama ni maskini, hata kama ni tajiri, hata kama ni mfupi, hata kama ni mrefu, ukweli siku zote hujipatia ushindi tu, simama na endelea kupambana katika kufikisha ukweli, kuwa wakili mzuri katika kuufikisha ukweli mahali pake.

Mpendwa msomaji,  siku zote ukweli hukutana na upinzani mkali dhidi ya uongo. Uongo ni kama maharage mabovu dani ya maji, hupanda haraka na huacha ukweli chini. Sifa uongo ni kusambaa haraka sana, ukweli misingi yake ni pole pole ili uwajenge watu vizuri na wauelewe.

Mpendwa msomaji, kama unafanya jambo ambalo misingi yake ni ukweli basi jiandae kuchelewa kufika unakotaka, lakini pia jiandae kuwa mshindi, maisha yametawaliwa na giza kuu, uongo zama hizi ni kitu cha kawaida tu kwa watu, tafadhali, tafadhali, tafadhali, kuwa balozi mzuri wa ukweli, dunia inahitaji nuru hiyo, giza limekuwa jingi sana. Mpendwa msomaji,  usiache kufanya jambo hilo kama tu misingi yake ni ya ukweli na wewe ni mshindi.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: Nisaidie kuwashirikisha wengine ujumbe huu ili uwafikie wengi zaidi. Maoni yako ni muhimu pia.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, March 3, 2018

Hiki Ndicho Kitu Ambacho Huwa Kinakunyima Furaha Siku Zote.

 Sadick Kilasi     March 03, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA ISHAURI,  natumai umeamka salama. Hongera kwa ajiri ya siku hii ambayo Mwenyezi Mungu katujalia kuiona. Ni ushindi mkubwa sana ambao amekuwa anatupatia na ametupatia leo pia.

Karibu katika makala ya leo ambayo mimi nimekuandalia ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Furaha ni kitu ambacho kimekuwa kikitafutwa kwa gharama kubwa. Furaha imekuwa ikitafutwa kwa gharama kubwa kwa kutambua au kutokutambua, lakini mara zote imekuwa ikitafutwa furaha.

Shughuli zote ambazo zimekuwa zikitendeka chini ya jua, kinachotafutwa ni furaha, unaoa au kuolewa ili upate furaha, unatafuta pesa ili upate furaha, unaenda shule ufaulu vizuri ili upate furaha, unaona kitu ambacho unacho na unakipenda na unapata furaha. Kwahiyo shughuli zote ambazo zinafanyika chini ya jua tunachotafuta ni furaha.

Kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kikiwanyima watu kupata furaha, kitu hicho ni, kutaka. Kutaka kumekuwa sababu kubwa ya watu kukosa furaha. Mpendwa msomaji wangu, maisha ni kutiririka kama maji ya mto. Unapokuwa unataka kitu kwa nguvu ndipo mwenyewe unapojinyima furaha yako.

Mpendwa msomaji ndio maana katika maisha unapaswa kuwa mhusika mwenyewe na uwe mtendaji mkuu. Kuna kitu kikubwa sana ambacho watu hawakitambui, unachokitaka sicho ambacho kitakupa furaha, kumbuka unapotaka kitu, unashindwa kutiririka kuna nafasi fulani unairuka na hapo ndipo kwenye tamaa na furaha yako itakuondoka. Ukitamani kitu lazima utambue miongozo ambayo itakupelekea kupata kile ambacho unakitamani.

Matendo ni muhimu sana katika safari ya kuipata furaha. Furaha ipo na itaendelea kuwepo, huta ipata baada ya kupata kitu furaha na kamwe kama unategemea hivi huwezi kufurahia maisha. Tiririka kama maji ya mto nawe utajazwa furaha.

Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: nisaidie kuwashirikisha ujumbe huu wengine ili upate kuwasaidia wengi zaidi. Maoni yako ni ya muhimu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, March 2, 2018

Hawa Ndio Watu Ambao Tunaweza Kujifunza Kutoka Kwao.

 Sadick Kilasi     March 02, 2018     NJOZI     No comments   

Wazee ni hazina kubwa sana kwenye jamii, vijana tunaweza kujifunza mengi sana kutoka kwa wazee. Wazee wanadata nyingi sana ambazo zinaweza kuwa msaada mkubwa kwa sisi vijana.

Sifa kubwa ya wazee ni kwamba wanekula chumvi nyingi sana, lakini pia wamepitia mambo mengi sana ambayo yamekuwa funzo kwao. Wazee ni hazina kubwa sana.

Sifa nyingine kubwa ya wazee ni kwamba wao huishi kwa kuweka vipaumbele. Wao hawafanyi mambo mengi sana, wao huishi kwa kufuata vipaumbele vyao. Kutokana na kufanya mambo mengi sana katika ujana wao na maisha yao ya nyuma kwa ujumla wametambua hawana haja ya kufanya mambo mengi wakati mda wao wa kuishi umebaki mchache, kwahiyo wao huangalia mambo yao ya muhimu tu na kuyafanya.

Mpendwa msomaji, vijana tunaweza kujifunza kutoka kwao sasa, tunaweza kupata data zao za nyuma kwa kuwauliza maswali, lakini pia tunaweza kuanza kuishi kwa kufanya mambo ya muhimu tu, kwa kufuata vipaumbele vyetu. Lazima tufanye mambo machache yanayotupa matokeo makubwa kuliko kufanya mambo mengi na tusipate matokeo yoyote.

Mpendwa msomaji, sio wazee wote wamefanikiwa kwa hili, kama wameshindwa kujifunza kutoka katika mapito yao basi mapito yao yamekuwa mapigo kwao. Usipo jifunza kutokana na mapito yako basi yatakuwa hatari kubwa sana kwenye maisha yako.

Vijana wakati tilionao ni sasa ili kujenga maisha bora, tusigeuze mapito yetu kuwa mapigo kwetu. Kanuni ya kuishi maisha yenye mafanikio ni kuishi utoto kwa uzingativu, kuishi ujana kwa kutumia vizuri nguvu zetu na kuishi uzee kwa kuweka vipaumbele. Haya ndio maisha bora yasiyo na kharaha.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, March 1, 2018

Maisha Bado Yanaendelea Na Hayasikii Kelele Zako.

 Sadick Kilasi     March 01, 2018     USHAURI     No comments   

Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, hongera kwa siku hii mpya ya leo ambayo Mwenyezi Mungu katujalia mimi na wewe kuiona siku hii leo. Ni ushindi mkubwa sana kuifikia siku hii. Wapo wengi walio iwekea malengo siku hii na kuipangilia lakini wameshindwa kuifikia siku hii. Mimi na wewe tumeiona, ni kwa neema za Mwenyezi Mungu.

Ni kawaida kwa watu, tunapo pitia katika changamoto zetu kulalamika na kuwa na lawama nyingi sana. Tunapopitia katika changamoto huwa lazima minung'uniko itasikika. Misemo mbalimbali itaanzishwa na watu ili tu, kuonyesha ya kwamba tunapitia hali ngumu. Misemo kama vyuma vimebana, hali ngumu na lugha  za malalamishi kwa watu kuonyesha tunapitia katika changamoto.

Wengine huimba nyimbo hizo hali wakiwa nyumbani tu na kusema, hali ngumu. Kwa bahati mbaya ni kwamba hata ukiimba kwa nguvu vipi kama wewe binafsi huta kuwa na makusudi ya kuchukua hatua ili kufanya vyuma vilegee, huo utakuwa wimbo wako wa kila siku. Maisha hayakusikii wala hayakuelewi, mambo yanakwenda mbele.

Mpendwa msomaji, ni wakati  wa kuacha kulalamika sana, ni wakati sasa wakutumia maamuzi zaidi na sio malalamishi. Ukiona mambo hayapo vizuri, tafuta njia ya kuondoka hapo penye ugumu. Weka kazi na sio kulalamika sana. Kwa chochote unachopitia tafuta suluhu na sio kulalamika.

Mara nyingi sana watu tunalalamika kwa sababu tunahisi ya kwamba sisi hatuhusiki katika jambo hilo. Tunawapa lawama wengine na kusema wao ndio wamesababisha na kutufikisha hapo tulipofika, lakini ukweli haupo hivo kabisa, tupo tulipo kwa sababu ya hatua tulizo chukua huko nyuma. Mpendwa msomaji, tatua matizo yako acha kupiga kelele, na kulalamika, maisha hayakusikii yenyewe yanasonga mbele.

Tuache kuwa walalamishi sana katika hali mbalimbali tunazopitia, mbona mambo yakiwa mazuri tupo kimya? Basi vivo hivyo na tuwe katika hali ngumu tuwe kimya.

Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. Maoni yako ni muhimu.

Wako Sadick Kilasi wa jikolaushairi.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ▼  March (33)
      • Kipi Kinakusukuma Kukua?
      • (SEHEMU YA PILI). Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwen...
      • Hiki Hapa Ndo Chanzo Kikuu Cha Msongo Wa Mawazo.
      • Neno Kutoka Kwa Sadick Kilasi....Kutaka Kunauumiza.
      • Hakuna Wakati Sawa Wakufanya Kitu Hiki.
      • (SEHEMU YA KWANZA). Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwe...
      • Usifanye Maamuzi Yoyote Unapokuwa Katika Hali Hii.
      • Wakati Ukifika Mambo Yanabadilika.
      • Neno Kutoka Kwa Sadick Kilasi...Tuumalize Ubaya Hivi.
      • Huwezi Kubaki Salama Kabisa.
      • Majaribu Hayana Budi Kuwepo.
      • Mamlaka Juu Ya Mwingine, Kosa La Aibu La Kughushi....
      • Dunia Na Mashindano, Upacha Ni Utofauti Tu.
      • Tumeumbwa Kukua Kutoka Hatua Moja Kwenda Hatua Nyi...
      • Jihakikishie Kitu Hiki Siku Zote Katika Maisha Yako
      • Hapa Ndipo Mwanzo Wa Matatizo Yote Ulimwenguni.
      • Kwa Vyovyote Ulivyo, Jitofautishe Kwa Jambo Zuri....
      • Kila Kitu Kinahitaji Subira, Je Unataka Kuwa Gaidi...
      • Kama Unataka Maisha Yako Yawe Bora, Basi Yakupasa...
      • Ushahidi Huu Hapa Unaonyesha Wewe Ni Mtaalamu Wa K...
      • Unanjaa Na Kiu Ya Kitu Gani?
      • Kuna Watu Wanakupenda Wewe.
      • Maisha Yanakuwa Magumu Kwa Maskini Na Matajiri Una...
      • Je Ulipo Upo?
      • Adhabu Tunayopewa Baada Ya Kuvunja Sheria Ya Asili...
      • Tunapohisi Wengine Wanatutendea Ubaya.
      • Tunaona, Tunasikia, Tunashuhudia, Tofauti.
      • Acha Kuteswa Na Mambo Yaliyopita.
      • Hizi Ndizo Sababu Zinazopelekea Kuwa Na Chuki Na ...
      • Fanya Kitu Hiki Unapokutana Na Upinzani Wakati Una...
      • Hiki Ndicho Kitu Ambacho Huwa Kinakunyima Furaha S...
      • Hawa Ndio Watu Ambao Tunaweza Kujifunza Kutoka Kwao.
      • Maisha Bado Yanaendelea Na Hayasikii Kelele Zako.
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates