Mpendwa wangu karibu kwenye makala hii ya leo ambayo dunia inavyokuendesha bila wewe kujua. Makala hii inamlenga kila mtu ambaye bado hajajua hili ya kwamba yeye anaendeshwa na dunia.
Ni ukweli usio pingika dinia kila siku inabadilika na dunia inavobadilika ndani yake kuna mambo mengi sana yanayo tokea. Mambo hayo hutokea kila siku yapo mambo mazuri na yapo mambo ambayo si mazuri, yote haya atokea kwenye hii dunia.
Mara nyingi yale mambo mabaya yanapo tokea huwa hayawi mabaya ila sisi ndo tunafanya yawe mabaya kwa siku hizi kila siku kuna fashion mpya za nguo zinatoka na wewe kila fashion unataka kuivaa unasema hutaki kupitwa na wakati tayari hapo unaendeshwa na hisia zako, tayari hapo jambo zuri linageuka kuwa baya maana wewe unaadhirika unataka kila kitu uwe nacho kitu ambacho hakiwezekani.
Tumeona wenyewe miaka kama minne huko nyma mambo yalivokuwa kwa vijana wakiume, suluali walikuwa wanavalia kwenye magoti milegezo ya kufa mtu wanajiita wahuni kwa kiga tabia za watu na kwa wenzetu wakina dada wao nao wanakangamoko sijui, sasa hivi wao wana mfumo mpya wa uvaji wa madela ambayo madela ni vazi la kuhemika wao sasa wamegeuza wanavaa wanavo jua wao.
Yote hii ni kuiga mambo ambayo hayana maana kabisa, na yanakuondolea heshima yako. Mambo haya yanapokuja ni vyema kujiuliza mara mbili hivi jambo hili ni zuri kweli kulifanya? Linanipa faida gani? Kwanini nafanya? Hapo utajua ufanye au usifanye ila ukumbuke usikubali kuendeshwa na dunia mambo mengine wacha yapi.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0659639168 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment