Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwaajiri ya siku hii mpya, tunakushukuru Mungu kwaajiri ya siku hii mpya ulio tujalia, hii ni hatua mojawapo kubwa na dhamani sana ambayo umetupeleka, tunajua wapo wengi walitamani kuifikia siku hii lakini washindwa na sisi kuifikia siku hii si kwasababu sisi ni wazuri sana bali ni upendo wako tu, tunakuomba siku ya leo ikawe siku ya furaha na mafanikio na kila tutakachokwenda kugusa wewe ukakibariki. Tunaomba utusamehe dhambi zetu.
Mpendwa wangu karibu ujifunze makala hii ya leo.Yupo mpinzani ambae huwa anatusumbua sana sisi binadamu na yeye huyu ndiye anaye tuendesha mara nyingi, ukimshinda huyu ni rahisi sana kukamirisha malengo yako madogomadogo na hata badae kuyafikia malengo makubwa.
Mpinzani huyu ni nani? hisia za mwili wako, mambo yote tunayofanya kama sio zuri basi tu ni hisia ndizo zinazo tuendesha wala sio kitu kingine. Mwili unaendeshwa kwa hisia zako ndio maana unashindwa kukamirisha malengo yako na hii ni mbaya sana.
Tunasema hisia zetu ni mpinzani mkubwa kwa sababu unaweza ukawa umeweka malengo yako madogamadogo kwa mfano; kuamka asubuhi na mapema na kufanya mazoezi lakini mwili wako ukakataa kabisa kuna kitu kinakujia, wewe unasema ngoja nifanye lakini mwili unakukatalia kabisa mwili unakwamba hapana wew rudi kulala kwanza wewe huna shida yoyote na wewe unakubali unarudi kitandani unalala tena. Mimi nakupa pole hayo sio maamuzi yako maamuzi yako ni malengo yako likini huyo ndo mpinzani wako inatakiwa umushinde.
Unatembea barabarani ukaona kanguo kazuri ukanunua bila malengo yako. Huyo ni mpinzani wako kanunua sio wewe ila anatumia pesa yako vibaya inatakiwa umushinde asikuendeshe kabisa kabisakabisa ni mbaya huyo.
Huna sababu ya kuwatafuta wapinzani wako wa mbali wakati huyu wajilani yako ujamshinda, ni vigumu kuyafikia malengo yako. Sasa kivipi utashinda hili ni lazima ulazimishe kwa sababu ni kitu ambacho kipo ndani yako sema tu 'HAPANA SIWEZI KUFANYA HIVI HAYA SIYO MALENGO YANGU'. Huna sababu ya kwenda mbali huyu ndiye adui yako mkuu wa mafanikio yako.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0659639168, 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment