JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Monday, December 31, 2018

Jani Lilojiachilia.

 Sadick Kilasi     December 31, 2018     No comments   

Jani Lililojiashilia.

Mti hauwezi kulirudisha jani ambalo tayari limesha jiashilia na kudondoka kutoka kutika pale lilipokuwa.

Jani huusapoti mti kukua kwenda juu na kukua zaidi kwa kadili ambavyo lilikuwa tayari kuusapoti.

Ukweli ni kwamba, hatunauwezo wa kuwalipa watu ambao tayari wametufikisha hapa tulipofika. Hata tuwe na vipato gani hatuwezi kufanya chochote kwa wale ambao tayari wamefanya tufike hapa tulipofika.

Kila mtu kuna mtu amemsaidia kufikisha popote pale alipofika. Hatukufika tukiwa sisi wenyewe pekee yetu.  Na kwa sababu walisha tutendea hatuwezi kilipa gharama ambayo tayari tumefanyiwa. Nimefika hapa nilipofika ni kwa sababu watu wengine walikuja kama majani na kunisapoti licha ya jani kuwa ni sehemu ndoto ya mti lakini hao ndio walionipa chakula. Sijajua kama wasingekuwa wao leo ningekuwa wapi?

Haijarishi walikuja kwa picha gani ya ubaya ama uzuri lakini walinichonga hivi leo ninafurahia maisha.  Aliyekuja kwa ubaya ulibidi aje ili tuone na tuambatanishe na uzuri ili tupate nguvu. Aliyekuja kwa uzuri alikuja ili tuambatanishe na ubaya ili nguvu ipatikane. Basi, viungo haviwezi kufanya kazi bila joint ambayo sawa sawa na udhaifu.

Leo ninafurahia maisha kwa sababu walikuja kwangu kama zawadi yangu.  Naam, nimejiona kupitia wao.

Ninawashukuru nyinyi nyote ambao mlikuja kwangu na sasa hampo, kutokuwepo kwenu bado kunaniruhusu mimi nijione. Mungu awabariki. Majani yaliyodondoka nyinyi.

Basi, Adamu akasema, wewe ni mfupa wangu.

Nyinyi nyote ni zawadi yangu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, December 28, 2018

Je, Unaweza Kula Chakula Harafu Na Kufuta Mdomo Na Kusema Sijala Kabisa?

 Sadick Kilasi     December 28, 2018     No comments   

Je,  Waweza Kula Chakula Na Kufuta Mdomo Na Kusema Hujala?


Hivi ndivyo ambavyo tumezoea kuishi, kula chakula na kufuta mdomo na kusema kwamba mimi sijala kabisa.

Unafanya nini pale mtu anapokukosea? Wewe humsamehe? Kama unasubiri mtu akukosee harafu umsamehe ni sawa na kula chakula na kusema kwamba mimi sijala kabisa.

Kumsamehe mtu wakati ambao amekukosea ni sawa na kuweka jointi kwenye ubaya harafu ukasema sina ubaya ndani mwangu.

 Ufanye nini sasa wakati umekosewa?

Kuwa kama jua linalochomoza likipita giza linakimbia lenyewe. Samehe kabla ya kukosewa na hapo ndipo giza litakimbia lenyewe.

Kingiza giza na kulitoa ni jambo ambalo halileti maana. Vaa siraha za kiroho, uvae utayari miguuni mwako. Usitengeneze jointi.

Kila mwanadamu anamapungufu yake kwahiyo ukimtegemea binadamu ni sawa na kujiangamiza mwenyewe.

 Unaye Roho wa Mungu ambaye atakutia nguvu katika hili. Zaliwa upya katika hili uanze kuishi maisha tofauti.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, December 26, 2018

Je! Andazi Laweza Kupita Mikononi Mwako Harafu Lisikuachie Kitu?

 Sadick Kilasi     December 26, 2018     No comments   

Je! Andazi Laweza Kupita Mikononi Mwako Harafu Lisikuachie Kitu?

Ni andazi hili hili ambalo kila mmoja analijua. Ukilishika tu na kuliachia litakuachia mafutamafuta na harufu kwenye mikono yako.

Kama andazi laweza kukuachia kitu kama hichi basi chochote kila ambacho unakuona kwa macho kwa kutaka ama kutokutaka lazima ubakiwe na chochote ndani mwako.

Na lazima uelewe kuwa chochote kile ambacho umekifanya ipo siku kitakuja kuoza na kutoa harufu. Kinapokuja kubadilika nguvu ili kifanye kazi nyingine. Vitabu unacyosoma ipo siku vitatoa harufu, mazoezi unayofanya ipo siku utaona kazi yake. Ulevi wa pombe ipo siku utaona kazi. Hakuna kitu ambacho hufanyika na kisibadilike na kinapobadilika inamaana kinakubadilisha.

Kila mbegu ambayo inapandwa kwako zingatia ni mbegu ipi ambayo unapaswa kuimwagilia ili baadae uvune mavuno ya kufaa. Ukweli ni kwamba, hatuwezi kukwepa mambo ambayo hatuyataki lakini tuna nafasi ya kuvipa vipaumbele vile tunavyohitaji vikue ili vitupe mabadiliko. Mwagilia mbegu njema, acha kumwagilia yasiyofaa.

Ardhi ni kubwa lakini sisi tupo sehemu ndogo tu. Basi, zingatia kidogo kinachokujenga kuliko kuzingatia ubaya mwingi unakuharibu na kukubomoa baadae. Tai hutazama kitu anachohitaji akiwa juu, huona ardhi kwa ukubwa lakini huzingatia kile anachohitaji.

Pata muda kutafakari ili mambo yatakapobadilika kwako yasiwe muujiza.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, December 24, 2018

Je! Itapona?

 Sadick Kilasi     December 24, 2018     No comments   

Je! Itapona?

Ni miti ambayo ipo chini ya mti mkubwa wakati wa kuangamizwa mti mkubwa, je! hii inayojiburudisha chini yake itapona?

Wakati maalumu, wakati wa kutoweka mti mkubwa, hii ya chini itakuwaje?

Nakuuliza wewe ndugu Yangu, ni wapi ambapo unatumainia? Wewe wamtumania mwanadamu, wakati ukifika wa kuondoka huyo, wewe utakuwa katika hali gani?

Wewe ambayo matumaini yako yapo kwenye vitu, furaha yako hutegemea vitu, wakati vikiondoka utakuwa katika hali gani?

 Ndugu yangu, mtumainie Mwenyezi Mungu, jiweke chini ya kivuli chake, yeye ndiye mwanzo na mwisho. Kila kitu unachokiona kwa macho ukifika Wakati wa kuondoka vitaondoka. Hata sahani ikifika wakati wa kuondoka itaondoka.

Jiweke chini ya haki ya Mungu daima, ufurahie maisha daima. Alaaniwe amtumanie mwanadamu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Dalili Za Mabadiliko.

 Sadick Kilasi     December 24, 2018     No comments   

Dalili Ya Kuelekea Mabadiliko Ya Asili.

Dalili ya tawi kukauka ni jani kudondoka. Dalili ya tawi kukauka ni shina kukauka. Dalili ya shina kukauka ni mizizi kukauka na dalili ya mizizi kukauka ni mti kukauka.

Maisha yalikosa furaha, hutawaliwa na dalili kama hizi. Tunakufa mara nyingi zaidi kabla hatujakifikia kifo kamili.

Kwa kadili unavyokubali kuumizwa na watu, hiyo ni dalili ya mapema zaidi ya kuonyesha kwamba utakufa mapema. Kwa kadili ambavyo unakubali vitu vya dunia hii vikutawale hiyo ni dalili ya kifo.

Usikubali fikra zako zikandamizwe na zitengeneze bwawa yaani mkandamizo wa fikra. Kabla nguo haijachafuka ifue mapema, ifurahie kesho leo. Wakati wote kuwa mtu wa kitiririka.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 23, 2018

Sala Ya Shukrani.

 Sadick Kilasi     December 23, 2018     No comments   

Sala Ya Shukrani.

Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tunakushukuru kwa neema yako, asante kwa haki yako.

Tunakushukuru kwa hekima zako, maana kwa hekima zako sisi tunaishi. Umeifanya mbingu na nchi na ukaumba vyote vilivyomo ndani ya bahari na nchi kavu.

Kwa hekima zako uligawa mbingu na nchi ukagawa maji ya juu na chini. Ukaweka usiku na mchana, ukafanya jua na mwezi. Umetupa watoto wako gombo la chuo, kwa chuo hicho tupate kuzijua hekima zako.

Umejifua utukufu wako kupitia uumbaji wako, ukaweka kila kitu ndani ya chuo ili wana wako tupate kujifunza na kuona hekima zako humo.

Ni nani aliye mkuu kuliko Wewe? Umefanya makao ndani mwetu ili upate kutuongoza kwa usalama. Umewaweka watumishi wako ndani nchi ili watoto wako tusipate kupotea.

Umefanya mito kwa hekima zako na kuumba mti kwa ukuu wako. Ni nani ajuaye uhai wa sisimizi ulipo? Ni nani pekee yake ajuaye juu ya kesho? Basi, sisi watoto wako tutakutumainia wewe Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Tutayara matunda ya kesho leo maana tunalitia nanga tumaini letu kwako wewe uliye Mkuu mwenye enzi yote.

Tunasimama kwa ujasiri maana ndani mwetu umefanya makao na umeliweka neno ndani mwetu na chuo pia kipo kwaajili yetu.

Ukimbilieni usalama enyi watu wa dunia, jificheni ndani ya utukufu wake, maana Mwenyezi Mungu ndiye pumzi ya uhai wetu. Tuamanieni haki kwa Mwenyezi Mungu maana Mwanadamu ni kiumbe dhaifu sana.

Ee Mungu wetu, ndani yako usalama tele, ndani yako furaha tele.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, December 18, 2018

Ni Wapo Wewe Mwisho Wa Pumzi Yako?

 Sadick Kilasi     December 18, 2018     No comments   

Ni Wapi Wewe Mwisho Wa Pumzi Yako?

Mwaka huu nilianza mwaka kwa kuishi falsafa ya mti, ninashukuru nilianza kwa kuelewa mambo mchache lakini mpaka sasa kuna sehemu kubwa ambayo nimejifunza kutoka kwenye mti.

Yapo mengi sana ambayo unaweza kujifunza kutoka kwenye mti. Binafsi mimi nimejifunza kwa kiasi changu namna ambavyo mti unaweza kunielewasha nini maana halisi ya maisha. Kabla ya mwaka huu kuisha nitakushirikisha mambo ambayo nimejifunza kutoka kwenye mti lakini pia kwenye kitabu cha Dunia Mama Haimtupi Mwanae, nimeeleza mengi juu ya mti.

Unajua tunapoishi hapa duniani ni kama tumetupwa kwenye sehemu ambayo hatuijui. Na hata wale ambao wametumika kutuleta duniani wameendelea kuishi bila kutafuta uhalisi kamili wa maisha. Japokuwa wapo wengi ambao wamefanya kwa kiasi kikubwa ila nasi hatuna budi kujua zaidi na kuendeleza pale ambapo wamefikia wenzetu. Vipo vitabu vitakatifu ambavyo ndiyo msingi wa haya yote. Lakini yote kwa yote kuweka mambo wazi wazi, sifa za Mungu ni kuficha hekima na mwanadamu kufichua hekima za Mungu.

Wapi Mwisho Wa Pumzi Yako?

Ushawahi kuiona miti, miti ambayo inakuwa chini ya miti mingine? Bila shaka ushawahi kuona.

Tunachoishi duniani ni kukua na kukua huwa kunategemea utupu yaani anga. Sasa anga lako likiwa jilani ni wazi kwamba  hakuta kuwa na uwezekano wa kukua, kwa sababu utazuiwa kwa juu ili usiendelee mbele. Miti inafokasi kuelekea juu angani, inakuwa na pumzi kubwa kwa sababu ya utupu mkubwa.

Katika maisha ya kawaida kunauwezekano mkubwa sana wa kuzuia anga na kufanya pumzi yako isifanye kazi vizuri. Na hii hufanyika katika ubongo wako namna ambavyo unaendesha maisha. Tamaa ya mambo ya dunia fedha, wanawake inaweza kukuzuia usipumue vizuri katika maisha yako, watu wanaokuzunguka wanaweza kukuzuia usipumue vizuri. Jiulize namna ambavyo unaendesha maisha yako, je, wewe ni mti ambao upo chini ya mti mwingine? Unapaswa kuona anga likiwa wazi juu na sio kuwa chini ya kivuli kingine. Tunakuwa katika hali nne, ambazo tunapaswa kupata wakati wote, kwanza, Maji, pili udongo ama kitu, tatu mwanga na nne hewa. Sasa hapa leo tunazungumzia mwanga na hewa.

Ukiwa chini ya kivuli cha mti mwingine huwezi kupata mwanga vizuri. Ukiwa chini ya mti mwingine huwezi kupumua vizuri kwa sababu unazuiwa na aliyeko juu yako.

Kutawala sio kumiliki, kutawala ni utambuzi, kumiliki ni kujimilikisha na kuweka mipaka. Kumiliki huletaa tamaa, tamaa ambayo inasababisha kuwa mtumwa wa hicho ambacho unamiliki. Unachomiliki kinakuzuia usione mbele yako wewe kitu ambacho husababisha pumzi yako isiwe huru.

Ndugu, tumebarikiwa tuwe baraka. Vitu ambavyo ni vya dunia hii huzuia pumzi yetu isifanye kazi vizuri. Chunguza kile ambacho kinakunya kila siku uamke na kufanya kazi, je? kinakupa furaha ama kinazuia pumzi yako tu! pumzi inapotoka vizuri inakufanya ujiachilie vizuri.

Elewa maisha ili uishi maisha, ni kipindi cha hakati hiki, tunaweza kujikuta tunajiingiza katika mambo ambayo sio kisudi letu kuishi.

Elewa na uishi, ishi na uelewe.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 16, 2018

Ulipo Hapo.

 Sadick Kilasi     December 16, 2018     No comments   

Ulipo Hapo.


Hivi ulishawahi kujiuliza ni kitu gani kwa siku hiyo ambayo ulikuwepo ama kwa leo hapo ulipo kinakufanya uwe hai? Je, vipi kuhusu uzima? Je, ushawahi kujiuliza ni kitu gani ambacho kinakufanya uwe mzima?

Kama bado hujawahi kujiuliza maswali haya kuna haja ya kujiuliza ili kujitafuta mwenyewe na kujielewa mwenyewe.

Jambo kubwa zaidi ambalo kila mmoja anahitaji na ni la muhimu ni kujikomboa mwenyewe kutoka katika kifungo cha vitu mbalimbali ambavyo vipo nje ya wewe.

Jambo la muhimu zaidi katika maisha ni kuelewa ni wapi ulipo na ni kitu gani kinakufanya uwe jinsi ulivyo. Anza kujitazama ndani ya hema yako ikisha toka nje ya kambi yako na uone ni kitu gani kinakufanya uwe hai na uwe na uzima ama ukose uzima.

Kabla ya kutaka unachotaka elewa ni kitu gani kinakuzunguka.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, December 14, 2018

Kifanye Kivuli Kiwe Nyuma Yako.

 Sadick Kilasi     December 14, 2018     No comments   

Kifanye Kivuli Kiwe Nyuma  Yako.

Tukitanguliza mabaya katika mitazamo yetu kwenye mahusiano hatuwezi kuona uzuri wa mambo ambayo watu wanatufanyia.

Tukitanguliza kivuli katika mwendo kwenye maisha inatufanya tusione mambo mazuri ambayo Mungu katuandalia kwaajili yetu.

Siku zote unapoelekea kama mwanga upo mbele yako basi kivuli kitakuwa nyuma yako. Kama kivuli kikiwa mbele yako kitakuzuia usione vema. Wakati Mungu anafanya uumbaji kwanza alitanguliza nuru mbele kitu ambacho kilifanya giza liwe nyuma.

Hata macho yetu yanatufunza, kwa sababu rafiki wa macho ni mwanga, mwanga ukiwepo tunaona vyema. Nyuma yetu hakuna macho kwahiyo nyuma yetu ni giza hata kama kunamwanga.

Hata Nuhu wakati wa gharika ya maji alipomtanguliza kunguru kunguru hakurudi kwa sababu yeye asili yake ni mweusi lakini njiwa alienda na kurudi.

Kutanguliza ubaya katika maisha, ni bonge la kosa. Ni sawa na kufumba macho ili kujizuia usione mbele. Wakati umekosewa na mtu na ukatanguliza ubaya wa kumchukia ni sawa na kuwekewa sumu mbele yako, nawe unachukua harafu unainywa ukitegemea adui yako atadhurika.

Sio siri, hakuna kitu kizuri kama kuona wema kwenye kila jambo, maana ni sawa na kuchoma ubaya kwa wema.

Je, umeokosewa sana na mtu ambaye ulimwamini? Je, maisha yako hayana matumaini unahisi uchungu wakati wote?  Leo nataka uone, uone kwa kutumia ubongo na siyo macho. Uone namna gani ambavyo huwa inatanguliza mabaya mbele yako badala ya nuru ambayo ndiyo husafisha njia yako.

Unaweka kizuizi mbele harafu unataka kwenda mbele, je, hii inaleta maana? Ona wema kwenye kila jambo. Acha kutanguliza mabaya katika maisha yako. Mtumanie Mwenyezi Mungu yeye ndiye Mfalme wa nuru, jiweke chini ya haki yake, usihukumu kwani wewe sio Mungu.

Ni bora kuzingatia mazuri ambayo adui anakufanyia kuliko kuzingatia mabaya yake. Ni bora kuona mazuri ambayo mtu anafanya kuliko kukazana kuona mabaya.

Asante kwa kusoma makala hii, msambazie na mwingine. Kuchukua hatua ni muhimu zaidi na ndiomaana kuna Agano la kufanya tohara, (kuondoa govi).

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, December 12, 2018

Kilichofichwa Hufichuliwa. Je! Mwizi Tutamchukuliaje?

 Sadick Kilasi     December 12, 2018     No comments   


Kilichofichwa Hufichuliwa.
Je! Mwizi Tumchukuliaje?

Madini yaliyojificha chini ya ardhi hutafutwa kwa juhudi kubwa, watu huchimbua kwa juhudi kubwa ili kuyafichua chini kabisa ya ardhi. Thamani yake ni kubwa kutokana na jinsi ambavyo yanapatikana kwa ugumu.

Wezi hutia juhudi kuhakikisha kwamba nyumba ambayo imezungushiwa fenzi kubwa na yenye ulinzi mkubwa, vitu ambavyo vipo ndani ya nyumba hiyo vinafichuliwa.

Maswali magumu humfanya anayejibu kuwa mwenye akili kwa sababu ya jibu kuwa limefichwa sana.

Sehemu za siri huwa na thamani zaidi kwa sababu zimefichwa sana.

Fedha ambazo hazipatikani kiurahisi hutafutwa na kila mtu na dhamani yake ni kubwa ukilinganisha na vitu vya kawaida.

Nimekuonyesha haya yote ili nikuonyeshe dhana ya vitu vilivyojificha namna ambavyo vinakuwa na thamani kubwa sana. Lakini je, mwizi anakosa?

Tunaishi katika ulimwengu ambao tunapenda kuhukumiana kwa kuona kwamba wengine ni wabaya baada ya kuibiwa na walio waibia, tunasahau kuwa msababishi wa kwanza katika wizi ni yule ambaye anaficha. Mpanzi mkubwa wa mbegu ya wizi ni yule ambaye anaogopa kuibiwa lakini pia mtendaji mkuu wa wizi ni yule ambaye anaiba.

Ukificha kitu unamfanya mwingine atamani, usingeficha asingetamani. Kwa sababu unaubinafsi wa kutaka kujilimbikizia mali na ndiomaana unaficha. Lakini na mwizi naye, kwa sababu ya ubinafsi unaiba, unaiba ili kujilimbikizia wewe pekee lakini pia unapenda giza na ndiomaana unaiba. Unaiba na unaenda kuficha tena, bora ungeiba na kuweka wazi wazi lakini umeiba na kuficha.

Sisi sote ni watoto wa Mungu, sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Je! Tufanyaje katika hili?

USIHUKUMU, HURUMIA.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, December 11, 2018

Mungu Mfalme Wa Haki.

 Sadick Kilasi     December 11, 2018     No comments   



Mungu ndiye Mfalme wa haki, mizani yake ni ya haki. Ni nani aliye kama Mungu?

Mwanadamu ipoumbwa mawazo yake yalikuwa ni kukusudia uovu tu ndani ya moyo wake Mungu akaleta gharika ya maji lakini baadae Mungu akasema, sitaiangamiza tena dunia kwa maji kwa sababu mwadamu tangu utoto wake hujiwazia uovu tu. Ndugu, tupo tayari kufanya maamuzi kama haya ili tuushinde uovu kwa wema? Tumwige Mungu japo sisi si wakamirifu, tujitahidi katika hili.

Wakati Esau alipokuwa anataka kuchukua mibaraka yote kwa baba yake Isaka dhidi ya ndugu yake Yakobo, Mungu alifanya kwa haki, akambariki Yakobo kupitia kwa baba yake Isaka kwa sababu Isaka alikuwa kipofu  na baadae akambariki Esau wote wakawa watu wenye mali nyingi na matajiri. Tusifanye kwa upendeleo kwa sababu fulani bali tunapaswa kufanya kwa sababu tunapaswa kufanya. Tujitaidi katika hili.

Wakati Raheli alipokuwa mzuri machoni pa Yakobo na Lea alikuwa dhaifu, Mungu alimtia utasa kwa muda Raheli na kumjalia Lea watoto sita na mwisho akamjali Raheli watoto wawili. Mungu hufanya kwa haki, hakuna mwanadamu ambaye aweza kutambua mahesabu yake.

Ndugu yangu, inawezekana upo katika hali ambayo ipo nje ya uwezo wako, unapitia magumu kiasi ambacho kinakufanya ukate tamaa, usijiweke chini ya haki yako wewe mwenyewe binafsi bali jiweke chini ya haki ya Mungu. Mungu hufanya vitu vidhaifu kuwa vyenye   nguvu. Mungu humjalia kila mtu ambaye yupo tayari kumtumania .

Machoni pa mwanadamu kila kitu kinaweza kuwa sawa lakini machoni pa Mungu mambo huwa tofauti.

Yusuph aliyezaliwa wakati wa uzee kwa Raheli akiwa mtoto ambaye alikuwa na ndugu mmoja kwa mama  alipitia wakati mgumu lakini baadae alikuja kuwaokoa nduguze, huo nao ulikuwa mpango wa Mungu. Jina la Yusuph lilitukuka kwa sababu aliwaokoa ndugu zake, je! ni nani ni sawa mbele za Mungu? Ndugu zake pia wasingeokoka bila Yusuph.

Sisi wanadamu ni kitu kimoja, kila mmoja ni kwaajili ya mwingine na si kwaajili ya haki yake binafsi. Anayejua ni anajua kwa sababu ya yule asiyejua. Sisi sote kitu kimoja na tujiweke chini ya haki ya Mungu na tumwachie Mungu yeye pekee ahukumu kwa haki.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, December 10, 2018

Bubujiko lisilo isha.

 Sadick Kilasi     December 10, 2018     No comments   

Bubujiko  Lisilo Isha.

Akili ni nywele kila mtu ana zake. Unapotumia akili yako kama maarifa kwenye maisha yako ni kama nywele, hukua bila kuwa na kikomo na hata ukikata bado zitaota tu kwa sababu shina bado lipo. Hili ni bubujiko lisilo isha.

Unapotumia akili kwenye maisha kama maarifa ni kama kumimina mafuta ndani ya chombo hayaishi kirahisi. Hili nalo ni bubujiko lisilo isha.


Unapotumia akili yako kama maarifa kwenye maisha, ni kama chemichemi ya maji ambayo hububujika wakati wote. Hili nalo ni bubujiko lisilo isha.

Unapotumia akili yako kama maarifa kwenye maisha, ni kama mti kukua kuelekea mawinguni. Hili nalo ni bubujiko lisilo isha.

Bubujiko lisilo isha ni matumizi ya akili kwenye mbegu ndogo ya kitu na kuifanya kuwa kubwa zaidi na zaidi na zaidi. Bubujisha kila kitu kwenye maisha yako ili kiwe zaidi ya hivyo kilivyo.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, December 9, 2018

Wakati Wa Kujitokeza.

 Sadick Kilasi     December 09, 2018     No comments   




Tumeimaliza program yetu ya kuishi maisha yenye maana jumapili ya jana. Binafsi nimejifunza mengi namna ambavyo nililivyo na jinsi ninavyochukulia mambo. Natumai hata wewe kuna jipya umejifunza, kama tumekuwa wote katika program hii basi yawezekana umebaki kama ulivyo ama umekwenda mbele hatua kidogo. Kama umekwenda mbele hatua kidogo, hongera sana lakini kama hakuna matokeo yoyote ambayo hujapata bado hujachelewa unaweza kufanya lolote nangu sasa ili kuondoka katika hali hiyo ya mgando.

Tuna safari ndefu sana ambayo tunapaswa kwenda ili kuhakikisha injili inafika mbali. Tumeshiriki wiki hii ya kuishi maisha yenye maana tukifokasi katika tabia mbalimbali kwa wiki tofauti sasa ni wakati wa KUJITOKEZA.

Ndugu yangu, ukienda kulala usiku, usipotoka ndani ya chumba chako watu watajua umelala hata kama umeamka. Mbegu iliyopandwa chini ya ardhi isipojitokeza juu itaonekana imekufa hata kama haijafa. Martin Luther King Jr anasema, ukimya wa wapendwa wetu unaumiza sana kuliko kelele za maadui zetu. Albert Einstein anasema, dunia si mbaya kwa sababu ya watu wabaya ila ni mbaya kwa sababu ya watu wazuri ambao wamekaa kimya.

Wewe ni shaidi katika ulimwengu wa sasa kwa sababu sisi sote tunaishi katika ulimwengu huu. Matunda ya ulimwengu huu ni mabovu hayafai hata kuliwa. Tunasababu ya kuchukua hatua mimi na wewe kuhakikisha nuru inang'aa ulimwenguni.  Sisi ambao tunabahatika kusoma mafunzo mbalimbali ya kujenga tunapaswa kuenda hatua ya ziada, tunapaswa kuwa nuru ya ulimwengu.

Usifikiri wakati wote kuwa chini ya kivuli cha mti mkubwa eti kwa sababu muda wako haujafika bado.  Ukiangalia miti ambayo huwa inakuwa chini ya vivuli vya miti mikubwa huwa inaonekana kustawi wakati wote lakini huwa haifiki mbali kwa sababu haiwezi kujitegemea yenyewe. Badala ya kulishwa kila siku maarifa kanisani na kwenyeajukwaa mbalimbali ni wakati kufanyia kazi ambayo unajifunza kila siku. Usipokuwa makini kama ukijifunza kitu na usipokitendea kazi unakuwa mlevi, mlevi wa maarifa kitu ambacho kitakufanya kuona kwamba kila siku unahitaji maarifa zaidi ili kufanya jambo kumbe unapaswa kuanzia na pale ulipo. Kithamini kwanza ulichokipata ikisha kichofuata kiwe na thamani zaidi.

Ili kuweza kutumika na Mungu si jambo la ajabu sana ni jambo ambalo tunapaswa kukusudia kama tulivyokuwa tunakusudia kwenye mwezi wetu wa kuishi maisha yenye maana. Tunachopaswa kufanya ni kumrusu Mungu kutenda kazi ndani mwetu. Sisi tunafokasi katika matunda yake.
-UPENDO
-FURAHA
-UVUMILIVU
-UTU WEMA
-FADHILI
-UAMINIFU
-UPOLE na
-KIASI.

Tumesha jifunza namna ya kuendesha tabia mbalimbali kupitia program yetu ya mwezi na sasa hizi ndizo tabia ambazo ni matunda ya Roho wa Mungu ndani mwetu, inamaana kama kila siku tukiamka na kukusudia kuishi tabia hizi tutakuwa tunaishi kwa kutumika na Mungu.

Andika hizi tabia na uweke mahala peupe na kupitia kila siku. Ni mtu yeyote ambaye anapaswa kufanya hivi haijarishi ni mtumishi ama si mtumishi. Ikiwa tu unamwamini Yesu utapikea Roho yake na kwa mwongozo wake utaonyesha matunda hayo.

Jitokeze ili kuirutubisha dunia. Hata kama hupendi namna ambavyo dunia inafanya usipojitokeza hakuna lolote ambalo linaweza kubadilika. Siku zote mambo ya Mungu yapo automatic, mwanadamu ndiye haaminiki na ndiomaana meno ya juu hachezi lakini ya chini yanachezacheza. Ukitoka nje utakutana na jua. Chochote unachohitaji unahitaji kukiendea na kukifanya.

Anza sasa huu ndio wakati wako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sababu Nne (4) Kwanini Unapaswa Kusamehe Watu.

 Sadick Kilasi     December 09, 2018     No comments   



Moja ya kitu kikubwa zaidi ambacho nimekuwa napenda kuona mtu anajikwamua na kwenda hatua ya juu zaidi katika maisha yake kwenye mahusiano ni jinsi ya kuachilia msamaha kwa wale ambao wanamwumiza. Jinsi ambavyo unaweza kujiachilia wakati mgumu na kutokupoteza furaha yako hata kwenye jambo ambalo isingewezekana kabisa kuachilia msamaha.

Na kama tunavyojua, kinachotutesa watu wengi ni hali ya ubinafsi iliyopo ndani mwetu na hii ndio ilisababisha Kaini amwue ndugu yake, ilisababisha Mafarisayo na waalimu wa sheria wamkatae Yesu, na hii pia ndio inasababisha watu sasa hivi tuishi kama tunavyoishi. Kama kuna eneo ambalo halipo sawa basi chanzo kikubwa ni ubinafsi.

Ili kuishi maisha ya furaha na kutokurusu kuumizwa na wengine ipo sababu ya kujifunza namna ya kuachilia msamaha. Kuna kitabu ambacho Deo Kessy amekiandika kinaweza kukusaidia zaidi jinsi ya kuachilia msamaha, wasiliana naye kwa 0717101505. Jipatie kitabu hichi ni kizuri sana.

Lakini leo napenda tuangalie, kwanini unapaswa kuwasamehe watu walio kukosea. Unajua kwenye hii dunia utambuzi ndio unatufanya tuendeshe maisha na ndiomaana ni muhimu kujifunza hata jinsi ya kuwasamehe watu. Mtu hawezi kusamehe asipokuwa na Roho njema ambayo ni Roho ya Kristo ambayo tunaipata baada ya kujifunza neno la Mungu na kuua kabisa tabia za nafsi na tunabaki tukiendeshwa na Roho badala ya kuishi kawaida na kutafsiri mambo kimwili.

Sababu Kwanini Usamehe.


1.Uwepo wako mbele ya macho ya huyo ambaye amekukosea ni sababu ambayo imesababisha hiyo migogoro. Ni rahisi kuona makosa kwa wengine lakini ni ngumu kuona makosa yetu. Kila mgogoro unapokuja huwa unakuja kwa chanzo, kuna mbegu ambayo ilipandwa. Ikiwa upo katika eneo la migogoro basi hata wewe umeingilia ufalme wa mwingine. Usingekuwepo hakuna jambo ambalo lingetokea. Kuwa tayari kujiadhibu badala ya kuwasingizia wengine kwenye kila kitu.


2.Mbegu ya chuki inatoka wapi? Kama ukiona mwingine amekukisea, jiulize, nimejuaje kwamba amenikosea kama sio tafsiri ya uovu uliopo ndani mwangu? Mtu anayeweza kuonyesha uovu naye ni mwovu. Kila mtu anamakosa yake ambayo alishakosea, je! ulishawahi kujiuliza ni kwa kiasi gani yule uliye mkosea aliumia kiasi gani hapo nyuma? Kila mtu hupokea jambo kwa uzito wake. Hata kama uliomba msamaha, huwezi jua kovu ambalo umeliacha linamwumiza kiasi gani. Achilia msamaha kwa Sababu unajua kukosewa kwa sababu hata wewe umewakosea watu. Watoto wadogo hawana uovu ndani mwao na ndio maana utakuta mtoto mdogo haoni ubaya wowote, anapofanya jambo yeye hufanya tu, ila wanajua uovu utasikia huyu, mwizi, huyu ni mbaya, huyu ni malaya na mengine kama hayo. Usihukumu penda huruma.

3. Kila mtu yupo bize na hema yake. Kila mtu anamapungufu yake, kila mtu yupo bize na kile ambacho ataka kuwaza. Huwezi kumlazimisha mtu muendane kimawazo ni jambo ambalo haliwezekana. Kila mtu anamtazamo wake juu ya mambo fulani na ndio maana tumesema huwezi kusamehe kama hujui nini maana ya msamaha na kama huna Roho ya Mungu ndani mwako. Ikiwa mtu hajajifunza juu ya msamaha hawezi kusamehe kwa Sababu hana elimu hiyo. Hatuwasamehe wengine kwa sababu wametukosea tunawasamehe wengine ili tujisamehe wenyewe. Hakuna mtu anayeweza kumsame mwingine isipokuwa waweza kujisamehe mwenyewe. Kutokujisamehe mwenyewe ni sawa na kunywa sumu mwenyewe na kutegemea mwingine atakufa kwa sumu uliyokunywa wewe. Kwa hiyo anza kubadili mtazamo, toka nje ya hema yako na ndipo ulalamike mvua. Wakati mwingine unapaswa kujua nini mwenzako anafikiria, ingia ndani ya hema yake ili ujue ni kitu gani hakipo sawa.

4.Mtu siyo kosa, yeye ni tofauti na kosa. Mara nyingi kinachotuumiza ni kile ambacho tayari kimefanywa na wala si kile ambacho kinafanywa au ambacho hakijafanywa. Watu huwa wanabadilika, watu huwa wanajirekebisha. Sisi ni watu ambao tunamapungufu lakini sifa ya mwanadamu ni kwamba anauwezo mkubwa wa kubadilika na kukua kwa chochote kile. Ukiona unazingitia sana mambo ambayo umefanyiwa inamaana umekosa uwepo, huishi sasa hivi, mwili wako upo hapo lakini fikira zako bado zimetekwa na tukio la nyuma. Kunautofauti mkubwa kati ya kosa na mtu, kunautofauti mkubwa kati mtu na anachokifanya. Jitaidi kuishi sasa na kuyapa thamani mambo ambayo unafanya saizi.


Kujiondoa katika kila kifungo inahitaji utayari, utayari wa kufanya. Nimekupa harufu ya matumaini ya kuwasamehe watu ili uishi maisha ya furaha, unahitaji kufanya mchakato nawe utashiba amani na furaha.

Tafakari;
6:1, Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho  mrejezeni upya mtu huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.

Ndugu yangu, nisaidie kusambaza makala hii ili iwafikie wengi zaidi. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, December 8, 2018

Katika Wiki Ya Hamasa, Nakuandikia Wewe Uliye Mkubwa.

 Sadick Kilasi     December 08, 2018     No comments   



Mara nyingi tumezoea kufanya vitu kimazoea. Kama ni kusoma tumekuwa tukisoma kimazoea kama watu ambao tunajua kusoma. Kama ni kufanya jambo lolote tunafanya kama watu ambao tunajua. Na hii siku zote nimekuwa nikisema, kujiaminisha kuwa kivuli ndio uhalisi wenyewe. Tunatembea kama vivuli tukiwa tunajua ndio ukweli kumbe ni kivuli cha ukweli.

Na kwa hili nimeona nikuandikie wewe uliye mkubwa, ambaye unajiona mkubwa, unayetembea na vivuli ukijua ndio ukweli.

Inawezekana wewe ni mchezaji wa mchezo fulani, inawezekana wewe ni mwandishi kama mimi, inawezekana wewe ni msomaji wa vitabu, lakini yote kwa ujumla nataka nikwambie unaweza kufanya zaidi ya unavofanya saizi. Hakuna mipaka kwenye kufanya. Watu wazima sisi ambao tunajiita watu wazima ndio tumekuwa tunajidanganya sana, tukiwaangalia watoto wadogo tunaona ni kama sisi hatuwezi kukua zaidi na tumefika mwisho na hata watoto wetu wanapaswa kufikia angalau viwango vyetu, wakue kama sisi. Tunatengeneza mipaka ambayo inawaandaa watoto kuwa kama sisi, tunataka waige vivuli vyetu vya mambo. Mwisho utakuta ukoo ama jamii fulani wanafanana kwenye kila kitu, kimafanikio na hata kifikra. Yote hii ni kwa sababu ya watu wanaojiona wakubwa, watu ambao kufanya kila kitu kwa mazoea na kuona kana kwamba haiwezekani kufanya zaidi ama kwa njia ya tofauti na jinsi ambavyo hufanya.

Tunaweza kuwaangali watoto wadogo wanapokuwa huwa wanakuwaje?  Na hivi ndivyo inavyokuwa, inapaswa tuwe kama watoto wadogo, kuchukua hatari kama watoto wadogo, kupenda kujifunza kama watoto wadogo, kuwa watu wa haraka kuachilia msamaha kama watoto wadogo, ukishindwa kurudia kufanya kama watoto wadogo, unapaswa kukua kama watoto wadogo, kila kitu ambacho unakifanya fanya kama mtoto mdogo. Tunasafari ndefu sana, safari yetu ni kama kutoka chini ya ardhi kwenda mawinguni kwa miguu.

Usijione kama wewe ni mtu ambaye unaweza kila kitu, ujione kana kwamba unahitaji kufanya kitu bora. Usitundike kitu kwenye ubongo wako katika kufanya kitu. Kama nikikisea nikijua kwamba nimekosea na nikatubu basi ni bora kuliko kutokukosea harafu nikabaki katika hali ya kawaida na nisiadhiri chochote ama kuleta jambo jipya. Kufanya kawaida ni sawa na kubaki kawaida. Kawaida ni kitu ambacho tayari kimekufa.

Kama ni mtu mkubwa na unajiona kama ni mtu mkubwa acha kufikiri kimipaka. Anza kufikiri tofauti. Kile ambacho unapaswa kuishi tangu sasa ni kuipa thamani sasa kwa kufanya sasa kwa ubora wa hali ya juu.

Yesu Kristo alisema, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, hamwezi kuuuona ufalme wa Mungu.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, December 3, 2018

Katika Wiki Ya Hamasa

 Sadick Kilasi     December 03, 2018     No comments   




Kuna wakati mazingira yanayokuzunguka yanaweza kukufanya ukashusha hamasa yako na kujikuta upo katika hali ya kujiona huwezi lolote. Kuna wakati maneno ya mtu yanaweza kukufanya ukajihisi wewe si mtu wa kuzinguzia vitu vikubwa. Kuna wakati ukikumbuka mapito yako yanaweza kukufanya ukashusha hamasa yako ya kusonga mbele, baada ya kukumbuka tu udhaifu wako wa hapo nyuma.

 Usikubali, usikubali ndugu yangu, usikubali mazingira, maneno ya watu, kumbukumbu mbaya zikutoe katika mstari wa hamasa. Adui anakuja kiujanja kukuonea kiujanja lazima uwe mjanja. Ulicho kidhamiria hakikisha kinakupa matokeo makubwa hata kama unahisi nguvu hasi inaingia kwako. Ushinde ubaya kwa wema.


Wako akina Yezebeli mpaka sasa ambao hutishia maisha yako. Usikibali kukaa kwenye mti wa mretemu kama Elia ukajionea huruma mwenyewe.


Shetani hutumia watu kama alivyomtumia Petro kufanya Yesu asifikie malengo yake. Mara nyingine watu hutumiwa ili kukukatisha tamaa lakini wewe usikubali, baki katika njia kuu.

Sifa ya kwanza ya shetani ni mwelevu, sasa wewe kuwa mjanja zaidi, usikubali kudanganywa.

Tia juhudi, usijikinai, ushindi upo kwaajili yako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, December 1, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Unahitaji Kupalilia.

 Sadick Kilasi     December 01, 2018     NJOZI     No comments   



Mpanzi anayepanda mbegu na akaacha ikue yenyewe bila yeye kupalilia kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza tumaini lake ambalo alikuwa anatumainia kuvuna.

Inahitaji kupalilia, ndiyo palilia kile ambacho unahitaji kikupe na kilete mafanikio yako. Kile ambacho unataka kikupe matokeo makubwa na si ya kawaida. Unahitaji kupalilia.

Wakulima wa mahindi hupalilia mahindi ili yakue katika kiwango kikubwa ambacho wao wanataka kuvuna. Huweka mbolea na madawa na kila kitu ambacho kitafanya mazao yakue katika ubora na kuleta mavuno bora. Chochote kile ambacho unapenda kikupe matokeo makubwa unahitaji kupalilia.

Mungu alipotumba hakutuacha hivi hivi bali bado anaendelea kutupalilia kupitia neno lake na Roho Mtakatifu. Anataka tukue tufike kiwango cha juu kabisa na tulete matokeo ya juu kabisa duniani.

Palilia ndoto yako, wekeza muda katika ndoto yako, ongeza maarifa katika ndoto yako, palilia mahusiano yako, weka muda katika kuhusiano na watu, na uweke kipaumbele cha muda katika hilo.

Mbegu yoyote ile ambayo umeipanda na unataka ikue na ifike katika viwango vya juu, Unahitaji kupalilia, unapalilia kwa kuongeza viungo katika mbegu yako. Chochote kile ambacho unataka kiufikie upana mkubwa zaidi kinahitaji manjonjo ndani yake, asili ya dunia inaruhusu hivo, na ndivyo mambo yalivyo.

Kama ukipanda mbegu na ukaondoka zako bila kupalilia kuna hatari ya kuvuna magugu ama kuvuna kwa uchache ambao hukutarajia.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 30, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Wewe Umeachwa.

 Sadick Kilasi     November 30, 2018     NJOZI     No comments   



Jambo la kwanza kabisa ambalo ni muhimu zaidi katika maisha pale ambapo umepitia katika wakati mgumu ama unaona upo katika wakati mgumu ni kumshukuru Mungu kwa sababu ya ugumu huo ambao umekuacha salama. Kama kwa sasa unajihisi kutokuwa sawa na mambo yako, ni wazi kwamba wewe ni mzima na endelea kufanya maamuzi ya kukupa uzima zaidi.

Wakati fulani nilikuwa naangalia filamu ya King Kong, nilijifunza kwamba, hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani bado unapaswa kufanya maamuzi ya kuendelea kuwa mzima zaidi licha  ya mazingira kutokuruhusu kuwa hivo. Unajua nini? Kile ambacho kinatokea kwetu sisi ni tofauti kabisa na sisi, yale ambayo tunatenda, yale ambayo tunatendewa, huwa yanakosa nguvu kabisa endapo hatutaruhusu yaingilie maisha yetu.

Nilipokuwa naangalia filamu ya King Kong, mhusika kunawakati alikuwa katika hali ngumu sana, wakati anasogea mbele alimwona mnyama mbaya ambaye ni hatari katika maisha yake lakini wakati anageuka nyuma, kumbe alikuwa anaviziwa kwa nyuma. Lakini bado hakujikunyata alifanya maamuzi ya kuendelea kuwa mzima zaidi. Kila hatua ambayo alikuwa anapiga ilikuwa ni hatari kwake lakini bado aliendelea kufanya maamuzi ya kuwa mzima zaidi. Maamuzi ambayo alikuwa anafanya yalikuwa ni ya kijasiri. Leo hii naweza kujifunza kutokana na maamuzi yake.

Kunawakati unaweza ukawa haupo sawa, usimuumize mwingine kwa sababu wewe haupo sawa. Usijiumize mwenyewe eti kwa sababu haupo sawa. Kila wakati ni sawa kufanya maamuzi sahihi.

Ukigundua umefanya jambo lisilofaa, usiendelee kufanya jambo lisilofaa. Tubu anza kufanya jambo linalofaa.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 28, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Kama Hatua Unazopiga Unapoelekea Mahali.

 Sadick Kilasi     November 28, 2018     NJOZI     No comments   



Kama ilivyo katika maisha ya kila siku, maisha ni utayari wa kuishi matuini sasa kwa Imani. Kilicho cha thamani zaidi ni utayari wa kuchukua hatua sasa maana hicho ndicho kitakupeleka katika matumaini yako.

Wakati wa kutembea, mguu mmoja ukiusindilia chini mwingine unakupa uafadhali kwa kuwa unakupa unafuu katika tembea, unakupa hamasa ya kuendelea mbele. Kwa hiyo, hatua moja moja ambazo tunapiga ni kama, kufa na kufufuka, unakanyaga hatua ya kwanza unaipa thamani, unendelea mbele, ya pili nayo unaipa thamani, unaendelea mbele.

Kila hatua utakayopiga inathamani kubwa sana katika maisha yako. Mshukuru Mungu kwa hatua ndogo ndogo unazopiga kwani hizi ndizi zinakupeleka katika kusudi na shabaha yako.

Mungu alipikuwa anaumba, alikuwa anathamini kila alichokuwa anakifanya, nasi lazima tumwige Mungu.

Ukawe na hatua nzuri, kila hatua kwako ni ya thamani sana, thamani kila hatua.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 26, 2018

Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.

 Sadick Kilasi     November 26, 2018     NJOZI     No comments   

Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.


Kwa mtu ambaye bado hajaanza kuishi tabia za ndoto yake huyo ni njiti ambayo bado haijawashwa na siku zote haina nguvu yotote kwa sababu haifanyi kazi yoyote. Kila mtu ndani yake ana nguvu ambayo inasubiri kuchochewa.

Kwa mtu ambaye anajua nguvu yake ama ndoto yake harafu haifanyii kazi huyu ni sawa na mtu ambaye kapata jiti ya kiberiti na ganda lake Na yupo msituni harafu hataki kuwasha kwa sababu labda anafikiri kwamba kuna cha ziada ambacho anahitajika kufanya zaidi.

Kwa mtu ambaye anaishi ndoto yake, huyu sasa ni sawa na mtu ambaye kawasha moto ndani ya msitu wa paini ambao moto wake huwa unakuwa hatari sana.

Kama bado hujawasha moto wako, tafuta ganda lako ambalo ni Mungu, Mungu wa enzi yote mtumainie yeye pekee. Hakuna jambo ambalo linashindikana.

Kama tayari unakila kitu, washa moto wako, huna cha kusubiri kwani duniani hakuna ukamirifu ila tunaishi tabia za ukamirifu.

Kama tayari unewasha moto wako, hongera. Jambo la kujua zaidi ni kwamba moto unavichocheo vyake, usiweke maji kwenye moto.

Jiweke chini ya haki ya Mungu ili usiwe na lawama yoyote katika safari yako ya kuyaendea matumaini yako yeye ni tuzo lako.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 25, 2018

Katika Wiki Ya Kukua.

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   



Tumekuwa na wiki mbili, wiki moja ilikuwa ya shukrani na wiki ya pili ilikuwa wiki ya kutawala. Wiki hizi zote mbili zimekuwa wiki ambazi zimejenga misingi ya sisi kuendelea kuishi maisha yenye maana.

Kama umekuwa unachukua hatua kwa kile ambacho unajifunza, natumaini kwamba umeona mabadiliko kwa kiasi fulani katika maisha yako. Lengo letu kubaki na kuishi maisha ya kawaida, sisi kama washindi tulioushinda Ulimwengu tunaendeleza kile ambacho tumekianza na kuzidi kukua katika msingi huo.

Tumeingia katika wiki ya KUKUA, wiki ambayo inataka tuende hatua ya ziada kwenye vile ambavyo tunavifanya. Katika maisha kitu kizuri zaidi ni maamuzi bora ambayo yanaamuliwa kutoka katika msingi bora maana mbegu bora zimepandwa ndani mwetu zinahitaji kumwagiliwa ili kukua zaidi.

Unachiweza kufanya sasa ni kufikiri sahihi sasa na kufanya maamuzi ambayo yapo sahihi zaidi. Tunapaswa kukua kwenye kila kitu, tabia zetu binafsi, katika mahusiano, katika vile tunafanya na mengine zaidi.

Ninachoamini ni kwamba, si kile ambacho  umekifanya katika ubora mkubwa ndicho kilicho bora zaidi na wala si kile ambacho hujakifanya na unategemea kufanya ndicho kitu bora zaidi bali  kitu bora zaidi ambacho mimi naamini ni kile ambacho unakifanya kutokana na maamuzi yaliyo bora zaidi. Thamani ya maisha ni sasa, sasa inaweza kuharibu kabisa mambo yote mazuri uliyofanya nyuma na yale ambayo unatumai kufanya.

Biblia inatutaka wakati wote tuwashe taa, nuru iwe inang'aa.

Lengo letu si kuisha kawaida na kuishi kuwa wa kawaida bali kwa chochote kile ambacho kipo mbele yetu ama kinapita mbele yetu ama kufanywa nasi, kinatakiwa kipewe ubora wa kipekee ili kiwe bora zaidi. Boresha mahusiano yako, boresha shughuli zako, boresha ufikiri wako zaidi.

Kuwa zaidi, nenda viwango vya juu zaidi. Wiki ya kukua ndo imeanza leo, twende tukiwa tunataka kuwa na njizi kubwa zaidi. Natumai kwamba tayari una mbegu ya matumaini yako, mbegu ambayo inapaswa kuwa mti mkubwa.
 Asante sana

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Je! Ndege Hutegemea Tawi Alilotua?

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   

Katika Wiki Ya Kutawala, Je! Ndege Hutegemea Tawi Ambalo Amesimamia.

Ni ndege huyu, ndegu huyu kiumbe, ambaye hupaa katika miti, je! hutegemea tawi ambalo ametua?

Ndege hategemei sana tawi ambalo ametua lakini hutegemea zaidi mbawa zake lakini pia ni lazima atue kwani hawezi kupaa wakati wote.

Mpendwa somaji, je! umekuwa unaweka matarajio makubwa kwa watu? Tangu sasa usiweke matarajio mengi kwa watu bali uwe na kiasi ili usiumie. Lakini pia lazima uwe na matarajio kwa watu, ni lazima utue maana hupaswi kutokuwaamini watu kabisa, utashindwa kuishi mahusiano na watu.

Yote na yote, mtumainie Mwenyezi Mungu, tia nanga kwake ili tumaini lako lisiwe la kugonjagonja. Kumbuka maisha ni furaha, maisha yakikosa harufu yatakosa ladha. Usikate tamaa mwamini Mungu.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.


Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Katika Wiki Ya Kutawala, Mungu Ndiye Mfalme Wa Kila Kitu.

 Sadick Kilasi     November 25, 2018     NJOZI     No comments   



Kuna wakati ambao sisi kama wanadamu huwa hatuwezi kuwa na uhakika wa mambo yajayo. Yawezekana yawezekana ni ugonjwa ambao unatusumbua, ama matatizo fulani ya kiafya, ulemavu na mambo mengine. Hapa tunahitaji Mungu mwenyewe ajidhihirishe. Wakati mgumu ndio wakati mzuri zaidi wa Mungu kujidhihirisha na kuonyesha nguvu zake.


Badala ya kujitabilia mambo maovu, tunahitaji kumpa Mungu na kumwachia ugumu wa nyakati ngumu kwetu. Ni vema kuishi maisha ya furaha kuliko kubaki katika hema ya kuugulia huku ukiwa huna tumaini lolote.

Sara alijua kwamba hana uwezo wa kuzaa kwa jinsi alivyojitabiria yeye kwa macho ya uanadamu lakini Mungu alikuwa na mpango wake juu yake.

Waweza kujikuta unabaki katika wakati mgumu wa kuugulia na jambo fulani labda umeambiwa haiwezekani kupona, lakini kumbe Mungu anampango juu yako. Miaka mingi unaugulia, unajikuta umetumia miaka mingi kuugulia kwa hicho, wakati mwingine hata maamuzi ambayo unafanya yanakuwa katika hali ya kukata tamaa, yaani kwa sababu huoni tumaini unafanya maamuzi ambayo si yako. Sara alifikiri kwamba  hawezi kuzaa tena akafanya maamuzi ya kumruhu mmewe Ibrahim azae na mfanyakazi wake, kumbe Mungu alikuwa hawazi kwa namna hiyo, mwisho Mungu anampa mtoto lakini maamuzi ambayo amefanya nyuma yanakywa kikwazo kwake na yanamnyima furaha kwa sasa.

Mtumainie Mwenyezi Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa. Usifanye maamuzi ya hovyo eti kwa sababu ya kipindi cha mpito. Mungu ndiye anajua fungu lako, anajua wapi sahihi kwa wewe kusimama. Usikate tamaa.

Siku zote kinachotuumiza kwenye maisha ni kile ambacho hatutaki kukiamini na tunakiamini kidogo kidogo. Tumaini la kugonjagonja huumiza moyo.

Tumembiwa tuitawale dunia na tumaini letu litie nanga katika patakatifu pa huko mbinguni kwa yeye aliye mkuu, Mfalme wa mbingu na dunia, yeye anatawala kila kitu.

Usifanye maamuzi kwa sababu ya wakati wa mpito fanya maamuzi kwa sababu ya tumaini lako la mwisho. Matarajio madogomadogo yasikuumize kichwa kwani mtu akipotea njia anaweza kurudi ulikotoka na kuanza upya safari yako na kufanya mambo bora zaidi. Kujikwaa sio kudondoka, kudondoka sio kulala wala kulala sio kuamka. Bado unahitaji kukaza viungo vyako kwani viungo vyako hulegea ili vikazwe.

Jiweke chini ya haki ya Mungu, yeye ndiye mwanzo wako, ngao yako na tuzo lako. Yeye ndiye aliyekuumba.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 23, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Jiweke Nafasi Ya Wengine.

 Sadick Kilasi     November 23, 2018     NJOZI     No comments   



Mlango mojawapo wa kuingia katika Ufalme wa Mungu ni kujiweka nafasi ya wengine.  Licha ya mlango huu, mlango mwingine ni mlango wa shukrani. Kwa hiyo kuna milango miwili, shukrani na kujiweka nafasi ya wengine.

Wakati kuhani alipokuwa anafanya ibada ya upatanisho ili kuondoa dhambi za wana wa Israeli, ilimbidi kwanza ajitakase yeye mwenyewe kwanza pamoja na jamaa zake yaani familia harafu baada ya yeye kuwa safi atafanya ibada kwaajili ya jumuiya yote ya wana wa Israeli. Ikisha ataingia mahali watakatifu na makaa ya moto na ubani na kuvukizia moshi ilikufunika kifuniko cha Sanduku la Agano.  Kumbuka, katika wiki ya shukrani tumejifunza kuwa, shukrani ni bayana ya mambo yasiyoonekana kwa macho, tukasema harufu. Lengo la kufunika kifuniko cha Sanduku la Agano, inamaanisha kutokujiangalia kimwili, yaani Sanduku ni miili yetu, sisi ni hekalu la Mungu.

Ndugu yangu, kujiweka nafasi ya wengine ndicho kitu ambacho kuhani alikuwa anafanya. Amri zetu kuu ni mbili tu, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote na mpende jilani yako kama nafsi yako.

Nini kilichopo hapa, sisi sote tunamadhaifu, kuhani alikuwa anajitakasa yeye kwanza ikisha anawatakasa wengine. Je! wewe ukisamehewa huwezi kusamehe wengine? Ni rahisi kuwasamehe wengine kama hata wewe unajitambua na kujiona wewe ni mtu mwenye makosa, ulishakosa sana.


Ndugu yangu, watu hujiuliza ni kwa namna hani wanaweza kuachilia uchungu ambao unawaumiza, njia ni moja, ubongo wako unafanya kazi, je! wewe hujawahi kumuumiza mtu? Je! wewe hujawahi kumdanganya mtu? Usiseme huyu ameniumiza sana, Ndugu, chochote kile ambacho umemfanyia mtu mwingine kama hakifai huwezi kujua ni kwa kiasi gani kinaweza kuharibu maisha yake. Donge dogo la chachu huharibu chachu nzima.

Kama unaomizwa na uchungu ambao watu wamekufanyia, achilia kwa kukumbuka namna hata wewe ulivyowafanyia wengine, hii itakufanya ujione hata wewe hufai kitu na itakuwa rahisi kwako kusamehe. Kumbuka, ajikwezaye, hushushwa.

Kama mtu amefanya kosa usikimbilie kuhukumu bali angalia kwa jicho la upendo, hurumia, angalia mazingira ambayo yamesababisha kuwa katika hali hiyo. Hakuna jambo ambalo hutukia pasipokuwa na mbegu ya jambo hilo. Mara nyingi kila jambo ambalo kila jambo huwa linakuwa na nguvu hasi, nguvu hasi hii ndio husababisha ajali.

 Kwa hiyo mpendwa, siku hii ya leo, jiweke katika nafasi ya wengine na kuwa na shukrani bayana na mambo ambayo huwezi kuona kwa macho yako. Siku zote huwa kunakuwaga na dalili na dalili ndiyo inakupa furaha. Shukrani huleta furaha na kujiweka nafasi kwa wengine huleta raha. Raha ya kuwa pamoja ambayo husabishwa na upendo. Upendo ni kuwa tayari kuchukua madhaifu ya wengine.

Katika maisha yako, vipe vipaumbele zaidi vitu hivi viwili. Kujiweka nafasi ya wengine na shukrani.

Kajifunze kutoka;
Walawi 16.
1Yohana 5.

Tunaendela na tabia ya zetu nne za kutoongoza kuishi maisha yenye maana. Ikiwa ni wiki ya Kutawala, leo tunaongozwa na kujiweka nafasi ya wengine. Jipe thamani, wape thamani wale ambao  wamefanya makosa, warutubishe kwa sababu wewe umesharijua hili. Kuhani aliingia patakatifu wakati anajipatanisha mwenyewe akitoka anawapatanisha wenzake. Sisi sote ni kitu kimoja, haijarishi mtu amefanya kosa kubwa kiasi gani, kosa ni kosa yeye si kosa.

Kilicho ndani ya mwili huwa kinahitaji kutoka, kinatoka kwaajili ya wengine.

Kitu ambacho napenda katika maisha yangu, ni kuona wewe unatabasamu na tabasamu huja kwa kujitambua, madhaifu yako na maeneo ambayo upo bora. Na hapo marumaini ya kujiboresha huwa yanaanza ili kuhakikisha unafika katika viwango fulani baada ya kujiona. Wengi tunajitazama lakini hatujioni kwa sababu tupo bize kuwahukumu wengine, luwashabikia wengine na kujisahau kwa ajili yetu. Anza kujisoma.

Karibu kwa maswali juu ya hii program ya mwezi, nitumie ujumbe 0687000768. Tupo pamoja.


Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 22, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Moyo Huwa Unakubali.

 Sadick Kilasi     November 22, 2018     NJOZI     No comments   



Ushawahi kuwa unafanya kitu harafu ukajikuta umeangukia katika kupenda zaidi kile ambacho unakifanya? Ni moyo, moyo huwa unakubali. Kwa kadili ambavyo akili yako unaipa jambo fulani kuwaza zaidi, moyo unakubali na hauoni namna nyingine unaona hicho ndicho kitu pekee cha kufanya.

Kipindi cha nyuma nikikumbuka, nilikuwa nakwenda mahala fulani kukaa na kupiga stori kila siku, nisipokwenda naona kana kwamba siku haijakwenda vizuri lakini hii yote ni kwa sababu ya moyo.

Sasa kwa hili ni muhimu zaidi kutambua, ni maeneo yapi na tabia zipi ambazo unapaswa kuwekeza zaidi ili moyo wako ukubali, sehemu ambayo unapaswa kuwekeza zaidi ni sehemu ambayo inakujenga ama inawajenga wengine.

Chagua tabia ambazo unataka kufanya na moyo uzikubali, rudia zaidi na zaidi ili moyo ukubali. Moyo ukishakubali utakuwa umefika kiwango cha uraibu ama uteja.  Ukifika kiwango hichi utajisikia kwenye kila ambacho unakifanya ni burudani kwako yaani utamu, haijatishi kwa wengine hiyo kazi watu wanaichukuliaje? Kwako wewe kwa sababu umekuwa mteja wa hilo, kwako ni utamu tu.

Kitu kigumu katika maisha, ni kukifanya kile ambacho kinanukia kuwa kitamu, mchakato, moyo unapokubali tunasema mwili umekubali.

Yesu alisema, ingieni kwa mlango mwembamba, maana huo ndio mlango wa uzima. Ikiwa kuna mlango basi ndani yake kuna uwazi, ikiwa kuna uwazi basi kuna sehemu ngumu ya kutokea.  Mambo ya kujenga huanza kwa ugumu lakini mambo ya kubomoa huanza kwa raha. Yesu anatuasa tuingie kwa mlango mwembamba maana huo ndio wenye uzima.

Ndugu yangu, kila mtu anauwezo wa kujenga tabia ambayo unapaswa kujenga ikiwa tu tayari umelijua hili. Na tabia njema za kujenga ni luangalia matunda ya Roho Mtakatifu ni yapi ili kuishi kwa hayo, uvumilivu, upendo, haki, huruma, shukrani na mengine. Ni muhimu zaidi kukuza tabia njema ambayo unahitaji kuwa nayo, unapaswa kuitawala tabia ambayo unataka kwa kukusudia kabisa.

Ili kujenga kitu chochote ambacho unahitaji ni wewe kuvaa viatu, utayari. Mungu atakusaidia kwenye hilo unalofanya ukimwomba msaada na kumpa moyo wako. Patanisha kile unachofanya na Mungu, patanisha meno yako ya chini na ya juu. Siku zote Mungu anasubiri wewe uchukue hatua ili kupatanisha. Kama yalivyo meno ya juu yanasubili ya chini ili kupatanisha.

Jitoe hapo ulipo, jitoe katika hema yako ambayo umejizungushia kwa muda mrefu, chagua hema mpya ambayo inakujenga na kukufanya kuwa bora zaidi ya leo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 21, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Inahitaji Utambuzi Na Akili Kumkichwa.

 Sadick Kilasi     November 21, 2018     NJOZI     No comments   



Njaa kubwa ya watu wa Ulimwengu huu ni kukosa utayari wa kutambua utofauti. Ili utambue utofauti inahitaji utulivu na akili kumkichwa.

Mtawala yeyote ambaye hawezi kutambua utofauti wa viwango mbalimbali vya watu anaowatawala, atafeli kutawala. Lazima atambue kwamba kuna maskini, watu wa kati na matajiri wakubwa. Ni muhimu kuyatambua madaraja haya kwa mtawala yeyote ambaye anatawala nchi. Si hali za kiuchumi tu, bali hata tabia za watu wa asili fulani (makabila) na dini kwa ujumla.

Siku zote ili uweze kutawala inapaswa angalau uwe na utambuzi wa taarifa fulani hata kama hujui kwa undani kuhusu watu hao.  Unapokuwa na utambuzi, unakuwa na malengo ni kipi cha kupaki na ni kipi cha kutanguliza katika maamuzi yako. Kwa mtawala kujua makundi ya watu ni muhimu zaidi, kwa mfano, utambua kwamba kabila la watu wa aina fulani wanapaswa kufanyiwa kitu fulani mapema zaidi kuliko makabila mengine, hii ni kutokana na tabia zao zilivyo, ama ni watu wa kuongeo na wenye ushawishi mkubwa. Nyerere alitumia mfumo huu kuongoza nchi lakini pia wakati Mungu anawaondoa wana wa Israeli Misri ilibidi aangamize uzao wa kwanza wa watoto wa Misri ili kuondoa utawala.

Katika maisha yetu tunatawala, kila mmoja ni mtawala. Kwanza kabisa tunaanza kujitawala wenyewe mpaka kuwatawala wengine. Ukifeli kujitawala mwenyewe utatawaliwa na hisia zako na ukifeli kuwatawala watu, utatawaliwa na watu.

Sasa unaweza kujiuliza, yaaani mimi niwe mtawala wa kila mtu? Niwe juu ya kila mtu? Huwi juu ya kila mtu lakini unakuwa na utambuzi wa kutambua tofauti. Kama tulivyosema hapo mwanzo, ukifeli kujitawala mwenyewe utatawaliwa na hisia zako na kama ukiweza kujitawala mwenyewe unaweza kuwatawala wengine pia.

Watu wengi tunaumizwa katika maisha yetu kwa kufeli kutawala (kutambua tofauti). Tunaumizwa na wengine kwa sababu tumefeli kutawala, tunaumizwa na mapito yetu kwa sababu tumefeli kutawala.

Utambuzi wa kuelewa kuwa mimi na mwingine tunawaza tofauti, tunafikiri tofauti na hisia zetu ni tofauti. Kila mmoja wakati wote huwa anakuwa yupo katika hema yake ya kipekee uliyojizungushia. Unapomwendea mtu usishangae anakuona kama wewe ni adui kwani hafikiri namna yako. Na mara nyingi watu huwa tunakazana kujilinda kwa ubinafsi bila kutambua utofauti.

Ndugu yangu, anza kuwa mtawala sahihi kwa kutofautisha utofauti. Usiangalie na kung'ang'ania mapito yako bali angalia ni namna gani ambavyo unaweza kuboresha kila kitu, unaweza kuboresha maneno mabaya uliyoambiwa na mwingine kuwa kama Mwalimu kwako badala ya kuumia, jielewe kwamba wewe ni tofauti na yeye na hata maneno yake anayosema wewe hayakuhusu kama hayaendani na wewe. Ushawahi kujiuliza kwanini mwanzilishi wetu Yesu Kristo alipoambiwa maneno yasiyomhusu alisema, WEWE WASEMA? Kuna maneno ambayo hayapaswi kuingia ndani mwako na mengine yanapaswa kuingia ndani mwako.

Mapito yako ni zawadi yako, usiumizwe na mapito yako, kama ulishawahi kumkosea mtu basi sasa fanya vizuri kwani hapo mwanzo ulikuwa huna utambuzi na kama ulikosewa sana basi sasa ishi kwa kutambua utofauti wa tabia za watu.

Basi, hii ndio thamani ya leo, fikira zetu zinapaswa kuvaa utayari wa kujenga na amani, usiwe kama watu wa kimwili ambao hutafsiri maneno kimwili na kuishi kuumizwa. Unapaswa kuwa mtu wa kiroho, ambaye unatawala kiroho.

Tawala, tawala kishukrani, tawala kiutambuzi, uona wema kwenye kila jambo. Kitu ambacho unapaswa kuishi ndugu yangu ni hiki, kuona wema kwenye kila jambo, ndani ya ubaya uzuri hauwezi kukosekana. Chakula kilichotumika kujenga mwili kinyesi chake hutumika kuritubisha ardhi. Nikupe siri nyingine,  watu wote waliozaliwa upya, miili yao ni zawadi kwa wale ambao hawajazaliwa upya, ni kinyesi kinachorutubisha kwa sababu wao si watu wa mwilini. Unapokuwa unaruhusu kuumizwa na mwingine  unajiweka katika viwango vya chini vya kutawaliwa na hisia zako, yaani kipande kidogo cha wewe badala ya wewe kutawala hisia zako.

Ukawe na siku ya kutawala, anza kujitafakari mwenyewe, anza kuishi na wewe ndani yako, jihimili ili uweze kuhimili mazingira yako. Ishi maisha yenye maana zaidi kwa kuboresha maisha yako.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 19, 2018

Katika Wiki Ya Kutawala, Toka Nje Ya Hema Yako.

 Sadick Kilasi     November 19, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ulishawahi kukutana na mtu ambaye hashauriki kwa lolote like? Ulishawahi kukutana na mtu ambaye anamwambia hivi na hivi harafu akakwambia kwamba mimi ndivyo nilivyo maana hata ukoo wetu ndivyo tulivyo.

Hizi ni hema ambazo watu huwa wanajizungushia katika maisha yao. Itikadi kali ambazo watu wanakuwanazo. Mara nyingi watu wa namna hii huona kwa njia moja tu bila kufikiri nje ya boksi, kufikiri zaidi ya kufikiri.

Naam, siku ujikijizubgushia hema yako huwezi kutawala mazingira yanayokuzunguka ni lazima utoke nje ya hema yako. Toka nje ya hema hiyo uone utofauti wa mambo.

Kama upo ndani ya hema ya kuwalaumu wengine na umezoea kufanya hivyo, kuanzia leo, toka nje ya hema yako na kufikiri tofauti kwa njia tofauti.

Kama unapitia wakati mgumu katika maisha yako, hata kama unaona kwamba hamna njia ya tofauti, giza limetanda katika mazingira yako, toka nje ya hema yako na kufikiri zaidi ya unavyofikiri siku zote.

Wakati Wana wa Israeli walipokuwa wanakombelewa kutoka Misri, waliokuwa wamejizungushia hema yao ambayo walifikiri kana kwamba haiwezekani kutoka katika hali hiyo ya mateso, lakini Mungu alisema, nataka niondoe kwanza nira za Wamisri walizo lishwa. Bila kuondoa nira hizo hawezi kuona kitu ama unafuu mwingine zaidi ya kuona mateso yao pekee.

Toka nje ya hema uliyojizungushia, usiangalie kambi inayokuzunguka, mwangalie Mungu aliyekuumba, yeye anaweza kufanya lolote ambalo utamwomba.

Ili uweze kutawala unatakiwa uwe mtu ambaye huna itikadi yoyote, unatakiwa kuwa wazi katika akili yako. Unatakiwa kuwa msikilizaji unayesikia, ukisikia unabainisha kati ya wema na ubaya, unauchukua wema na ubaya unauacha kama ulivyo. Unapaswa kuishi kama mtoto ila uwe na utambuzi wa kutambua tofauti.

Toka nje ya hema uliyojizungushia kwa chochote kile, usifanye kwa mazoea, fikiri kwa utofauti. Boresha zaidi ulichonacho.

Ukawe na siku njema ya kuishi maisha yenye maana na kuchagua fungu sahihi kwenye kila jambo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 18, 2018

Ndani Ya Wiki Ya Kujitawala, Jitambue Wewe Mwenyewe.

 Sadick Kilasi     November 18, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ili uwe na uwezo wa kutawala vingine ama wengine kwanza wewe mwenyewe lazima uwe na uwezo wa kujitawala kwanza.

Kujitambua, nguvu yako iko maeneo gani yaani kitu ambacho unaweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu, ama wakati mwingine inaweza ikawa kiafya, ni maeneo gani upo bora zaidi lakini pia kimadhaifu lazima utambue kwamba ni maeneo yapi wewe ni dhaifu, huwezi kufanya vizuri na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu kiafya.

Eneo la kutawala linahitaji utambuzi na uelewa mzuri. Hii inasaidia kujijua wewe ni nani na unahitaji kufanya nini na mipaka yako ni ipi. Lakini yote hii ni kuhakikisha kwamba tunaishi maisha yenye weledi, furaha na amani.

Unapokuwa na uwezo wa kujitambua mwenyewe unauwezo pia wa kuwatambua wengine pia. Lengo pia ni wewe uweze kujihimili ili uwahimili wengine pia. Kila mtu anaubora wake na udhaifu wake. Vyote hivi viwili kwa mtu mwenye uwezo wa kujihimili havimtii tatizo kwani hatari kubwa katika maisha kwenye udhaifu ni kutanguliza woga badala ya shukrani.

Paulo pamoja na kuwa alikuwa ni msomi mkubwa na Mungu alimmiminia hekima nyingi na kuhubiri injili kwa kiasi kikubwa, inasemekana alikuwa na madhaifu yake ndani ya mwili wake, alikuwa anatembea huku ameinama kidogo mgongo wake. Lakini Paulo hajawahi kulalamika, kuna mahala kwenye vitabu Paulo alikiri kuhusu hili lakini hakuchukulia kama tatizo. Ukweli ni kwamba, udhaifu wetu ukiunganisha na maeneo ambayo ni bora ndiyo nguvu yetu.

Kwahiyo jichunguze ni maeneo yapi upo bora ili uyabireshe zaidi na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu ili ubadilishe kuwa nguvu yako. Pale ambapo huwa tunapatanisha sehemu dhaifu na zenye uimara na ndipo huwa tunapata nguvu na ndiomaana maneno matakatifu yatwambia, kaza viungo vyako usilegee.

Uwezo wa kutajitawala mwenyewe ni jambo la muhimu zaidi. Ukiweza kujihendo mwenyewe, unaweza kuwahendo wengine. Mungu  hutaka nibadilike mimi kwanza ili niwabadilishe wengine lakini na wewe pia hilo linakuhusu. Badilika wewe ili uwabadilishe wengine pia. Kwa chochote kile unachofanya lazima iwe hivyo.

Nikukalibishe katika wiki hii ya kutawala, mwanzo wetu ndio huu na kitu cha kuangalia leo ni kuangalia wewe mwenyewe ni wapi upo bora na ni wapi dhaifu. Dunia ilianza katika hali hiyo, Mungu aliona ukiwa na utupu, giza likiwa juu ya vilindi vya maji lakini Roho alikuwa juu ya uso wa maji. Mungu akasema na iwe Nuru, ikawa nuru, uwepo wa Roho wake  ndio ulisababisha Mungu atamke nuru ndani ya giza.  Mungu akasema nuru ni njema kwenye giza. Kwahiyo wema wa nuru ni ulitokana na giza. Huku ndiko kutawala kutambua  tofauti.

Karibu sana, yapo mengi ya kujifunza na kubadili mitazamo juu ya mambo mengi ambayo wewe huchukulia kama mzigo lakini kumbe kwa sababu ya mtazamo wako tu.

Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Saturday, November 17, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Itazame Wiki Yako Imekwendaje.

 Sadick Kilasi     November 17, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Kila jambo huwa linakuwa na ufunuo wake. Katika kumalizia wiki ya shukrani leo hii tangu tuanze jumatatu ya wiki hii, itazame wiki yako ili uone wapi ambapo umekwenda hatua ya zaidi na ni wapi umefeli.

Leo ifunue wiki yako, kwa kuitazama jicho la kujifunza zaidi. Ukweli ni kwamba, wakati umejizungushia hema kwenye mambo unayofanya huwezi kuona vizuri lakini pale utakapita ndipo utaona vizuri, na ndiomaana utakuta wengi tukitazama na kuzifunua historia za maisha tunajikuta kama tulikuwa bora sana, maisha ya zamani ni afadhari kuliko leo. Ushawahi kukaa na mtu ukawa unamchukulia kawaida lakini akiondoka ukajisikia kuwa kunautofauti kubwa na pengo lake laonekana sasa. Hivi ndivyo ambavyo kila kitu kilivyo. Unapopitia ile hali unayopitia inaweza kuchukuliwa ni kawaida lakini si kawaida kiroho. Na kwa kuishi maisha ya shukrani na kukipa thamani kila kitu, tunakuwa tunapandisha thamani ya kila kitu na ubora unakuwa mkubwa zaidi.

Leo ifunue wiki yako, kwa kutumia kanuni ya ndani, nje, kuwa mchezaji na mtazamaji, leo kuwa mtazamaji wa mechi uliyocheza wiki hii. Angalia ni maeneo yapi ulikuwa bora ili uboreshe zaidi na ni maeneo gani umefali ili uyarekebishe na kubaresha tena.

Haijarishi unaona umepiga hatua chache lakini ukweli unabaki kwamba umepiga hatua, endelea kuendelea tabia hiii ya shukrani ili kuwa bora zaidi kwa uvumilivu. Yape thamani maisha yako na kila kitu ulichonacho.

Asante kwa kuwa pamoja na mwanzo wetu wa kuishi maisha yenye maana na yenye weledi. Tuendelee kuwa pamoja ili kusonga mbele zaidi.
Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Friday, November 16, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Ni Nani Aliyempanzi Wa Tumaini Lako?

 Sadick Kilasi     November 16, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   




Siku zote mfumo wa maisha ni ule ule, IMANI, UTAYARI NA MATUMAINI.

Japokuwa wengi hufikiri kwamba watu ambao hawajihusishi na mambo ya kiroho ( dini) hawana imani, lakini ukweli ni kwamba wote tunaishi kwa mfumo huo huo. Utofauti ni kwamba, wengine hutumainia kifo na wengine hutumainia uhai wa milele.

Wale ambao hawasimamii chochote huongozwa na mwili, na wale ambao husimamia ukweli na upendo hawaongozwi na mwili bali na Roho.

Swali langu kwako wewe rafiki yangu? Ni nani aliyempanzi wa mbegu ya matumaini yako? Ni nani anayekuoza na kukutia nguvu kuendelea mbele? Wapi umetia nanga ili kuhakikisha meli yako haiendi mahali?

Ndugu Yangu, umtumainie Mwenyezi Mungu, wote ambao humwani Yesu, mpanzi wa tumaini lao ni Mwenyezi Mungu mwenyewe. Hufanya mambo yao kwa imani, kwani yeye ndiye aliye ngao yao.

Mungu alimwambia Abraham;
Mwanzo 15:1,Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likanena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na dhawabu yako kubwa sana.

 Kwa imani Abramu alitimiza maneno ya Mungu kwani Mungu alijitokeza kwake, akambia kwamba yeye ni ngao yako lakini pia akamwambia kwamba yeye ni tuzo lake. Mbegu ya matumaini ilipandwa ndani ya Abramu, alinza kuishi kama mtu mwenye matumaini, nanga yake ikiwa imetiwa kwa Mungu.

Ndugu, kuwa na matumaini yasiyo na shaka, mtumainie Mwenyezi Mungu, kuwa katika njia zake na pokea tuzo lake.

Mbegu ya matumaini yako lazima iwe Mungu mwenyewe, ikiwa ukitia malighafi kwenye kiwanda, bidhaa itakayotoka lazima iwe sawa na malighafi japokuwa hazita kuwa na sura sawa.

Ndugu yangu, Mtupe Paulo anasema, msijidanganye, marafiki wabaya huhatibu tabia njema, nasi twasema, kiwanda kibovu hakitoi bidhaa njema. Umtumainie Mwenyezi Mungu, ukitia juhudi na kujua kwa Mungu ndiye ngao yako. Usiogope, ukidondoka amka, maana umepewa udhaifu ili viungo vyako vikilegea uvikaze.

Mwamini Mungu, mpokee Kristo Yesu, tumaini lako litie nanga patakatifu huko mbinguni, Kristo Yesu amefanyika kuhani wetu akituombea mambo  mema kwa mfano wa ukuhani wa Melkizedeki ambaye alikuwa mfalme wa amani na hali.

Litie nanga tumaini lako huko, ili lisiteteleke, naam, meli ikitia nanga mahali pasipofaa itayumbayumba na haiwezi kutulia. Usijiamini peke yako. Watu husema, mtu asiyesimamia kwa lolote hudondoka kwa lolote.

Aliye kuumba umtumainie huyo. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com.


Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Thursday, November 15, 2018

Mshukuru Mungu Kwa Kila Kitu.

 Sadick Kilasi     November 15, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Habari Ndugu yangu? Katika wiki ya shukrani, tunaendelea kuyapa thamani kubwa maisha yetu.

Leo hii tunaiendea siku yetu kwa kumshukuru Mungu kwa kila kitu. Unaposhukuru kwa kila kitu, unashukuru kwa sababu unaelewa ni kitu gani unashukuru.

Mpendwa Ndugu yangu, tunasema mapito ni zawadi yetu, kilichopo ni jibu ya changamoto yetu, naam, tumaini ni nguvu yetu. Ukweli ni kwamba hatuna cha kupoteza katika maisha yetu.


Sisi ambao tumechagua kuishi Nuru, neno ningeli halitutawali. Kama tulifanya makosa hapo mwanzo iliikuwa ni sababu ya kufanya maamuzi bora hivi sasa.

Tunapo mshukuru Mungu kwa kila kitu, hii inafanya tuthamini kile ambacho Mungu amekupa. Nenda leo kwa shukrani, mshukuru Mungu kwa chochote ambacho inakiona mbele yako, mshukuru Mungu kwa historia unazopata lakini pia tumaini letu linapenya patakatifu pa mbinguni, tumetia nanga huko ili tumaini letu liwe lenye nguvu.

Mshukuru Mungu kwa neno lake ambalo umekuwa unalisoma, mshukuru Mungu kwa watu waliokufa kwenye historia zao kwa kuingia katika hatari kubwa ili wewe upate kuishi maisha mema. Wapo wengi waliokufa katika biblia, ili wewe uwasome na uishi maisha yenye maana sasa.

Mshukuru Mungu kwa watu watumishi ambao wanakufundisha na unasoma vitabu vyao, usije ukafikiri huwa unasoma kwa nguvu zako.

Mshukuru Mungu kwa hali ya hewa hivi sasa ili ikichafuka usije ukajutia. Japokuwa itaonekana mjinga ama utajiona wewe mwenyewe mjinga ukimshukuru Mungu kwa ndege, wadudu na wanyama unaowaona, lakini nikwambie ukweli kila kitu cha asili ni zawadi kwa wenye mwili.

Angalia ndege, sauti zao zinakufariji, angalia wanyama pambo la ulimwengu, angalia miti huleta harufu nzuri na kusababisha mvua kunyesha, angalia watu wako wa karibu, ni zawadi yako hao. Usijali kama sasa wapo bize lakini ukweli ni kwamba ukisukwa na jambo zito hapo ndio wa kwanza kukuinua. Mshukuru Mungu kwa kila kitu, usiache chochote.

Unapomshukuru Mungu kwa kila kitu, ni sawa na kupokea kila kitu ambacho Mungu amekupa. Na zaidi ya yote, Mungu ataendelea kukupa zaidi kwa sababu akikupa unapokea.

Je! Ushawahi kumshukuru Mungu kwa ardhi uliyoikanyaga, thamani ya maisha yetu ni pale tulipo. Angalia kwa macho yako jinsi ulivyo hai, gusa mkono wako kwenye moyo uone moyo wako unavodunda, cheki macho yako yanavoona mengi, sikiliza ndugu yangu, akili yako ipo vizuri na ndiomaana unasoma hapa, masikio yako yapo sawa na ndiomaana unasikia, kinywa chako kipo sawa na ndiomaana unasema. Wapo wengi wenye mapungufu ya hivyo vitu, ijapokuwa ni kimoja tu kati ya hivyo, lakini vinawanyima furaha kwa sababu hawana.

Mpendwa Ndugu yangu, inawezekana maisha yako ni magumu, ni magumu kwa sababu hutimizi ndoto zako na huna furaha kwa hilo. Lakini nataka nikwambie kitu kimoja, kuna watu wanapigania maisha ya familia zao, hawajawahi kufikiria juu ya familia zao. Watoto wao kila siku wanahitaji ada na chakula. Kuna wengine wamekosa furaha kwa sababu hata mtoto wa kumlipia ada hana.

Ninachotaka ni nini Ndugu yangu, ni wewe kuangalia ulichonacho na ukione kwa macho yako ikisha mshukuru Mungu. Mungu ametupa kila kitu, lakini hatutaki kukubali kile Mungu ametupa,  Mungu hatupi kile ambacho tunataka bali anatupa kile ambacho tunahitaji.

Siku hii ya leo, ipe thamani kubwa sana, ukiipa leo thamani kubwa itafanya vizuri sana kwenye kile unachofanya, zaidi kesho itakuwa siku ya thamani zaidi ya leo. Ipe leo thamani kubwa tumia kila kitu ambacho umepewa na Mungu  ulichonacho kuhakikisha, maisha yako na ya wengine pia yanakuwa bora zaidi ya ulivyofikiri.

Usiangalie udogo wa jambo, bali tumia vizuri kama zawadi yako. Ndugu yangu, miili yetu ni mikubwa, na ipo kwa sababu ya cell za mwili ambazo ni ndogo ndogo sana kiasi kwamba hata kwa macho huzioni. Usiangalie ni kitu gani huna, bali angalia ni namna gani unavyoweza kubooresha maisha yako zaidi kwa vile vidogo ulivyonavyo ili vifanye kikubwa kiwe hai.

Siku ya leo na vyote unavyoviona ni zawadi yako. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Wednesday, November 14, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani, Tambua Kitu Kikuongoze Katika Maisha Yako.

 Sadick Kilasi     November 14, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ukipita nje ya nyumba ambayo wanapika chakula kizuri, utasikia harufu nzuri ya chakula hicho ambacho kinapikwa ndani. Lakini pia kama chakula kinachopikwa si vizuri, utasikia harufu ya ubaya wa chakula.

Katika maisha ndivyo ilivyo, kila jambo huwa lina dalili ya kujiliwa yaani harufu ya kujiliwa na jambo jipya. Kama ndio harufu hiyo unaisikia maeneo ya nyumbani, basis utasema, leo inaonekana kuna chakula kizuri kinapikwa, lakini kutoka na harufu pia waweza kusema leo kuna chakula kibaya kinaandaliwa. Harufu hii haihitaji ukione chakula, bali ni manukato tu yanatosha wewe kukutambulisha.

Unajua mara nyingi kwa sababu ya kukosa umakini, huwa hatuwezi kuona jambo hili la kujiliwa na jambo jipya, dalili.  Kama upo makini unaweza kujiandaa na jambo lolote ambalo linatokea ikiwa upo makini na dalili hata kama linakuja kukuumiza lakini dalili itakulinda. Ukweli ni kwamba, mambo mengi ambayo hutuumiza si ugumu wa mambo hayo ila matarajio ambayo tulikuwa yumejiwekea yakienda tofauti na jinsi tulivyokuwa tunataka ndiyo hufanya tuumie. Moyo wetu unauwezo wa kukubali jambo lolote lile kama tayari tumelifanyia maandalizi kabla halijatokea, hata kama ni maumivu makali, kama uliuandaa moyo wako kupokea maumivu, maumivu hayo hayatakuwa sawa ukilinganisha kama hukujiandaa.

Itambue dalili, itambue harufu ya kujiliwa na jambo jipya, ili kama jambo linalokujilia ni baya ucheze mchezo wa ndani, nje, kujitoa katika mchezo ama kujiingiza katika mchezo.

Wakati mwingine unaweza ukawa unazungumza na mtu, lakini jinsi maongezi yetu yanavyokwenda wakati mwingine huanza harufu ya kumsengenya mtu, cheza mchezo wa kutoka nje ya mazungumzo, wakati mwingine unaweza ukawa unabishana na mtu kiutani tu, ila ukaisikia harufu ya ugomvi, toka nje ya mchezo. Usitake jambo baya likufikie, lakini pia hata kama hamuna uwezekano wa kuyafanya mazungumzo yenu yawe mazuri, usiruhusu matokeo ya dalili yakuumize wewe kihisia.

Yesu alifundisha juu ya jambo hili;  Mathayo 16:1-3, Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Akajibu, akawambia, (kukiwa jiona, mwasema, kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. Na asubuhi mwasema, leo kitakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kutambua uso mbingu; lakini je! ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?

Ndugu yangu, Yesu hakuishia tu katika hilo, bali alifundisha juu ya kupana na adui kabla hajakupeleka mahakamani. Lakini yote hii alikuwa anazungumzia harufu ya kujiliwa na jambo jipya na mtu aweze kupatana na jambo jipya.

Hakuna kitu ambacho hakina dalili, hakuna kitu ambacho hakina harufu ya jambo jipya. Dalili ama harufu ni kiungo ambacho kinakuunganisha kutoka jambo ulilokuwa na unalokwenda.

Mpendwa msomaji, katika wiki ya shukrani, mshukuru Mungu kwa kila jambo, naam, dunia huendeshwa kwa majira na wakati wake, lakini tunayozawadi ya pekee ambayo ni harufu, harufu ambayo inatuandaa kuishi jambo jipya.

Mshukuru Mungu leo kwa hali uliyopo, mshukuru Mungu leo kwa yale ambayo unayopia, kwamaana kama unapitia magumu sana hiyo ishara kwamba kunaunafuu unakuja katika maisha yako. Usiku menene sana katika maisha, husababisha pambazuko, ikifika saa nane usiku majira huanza kupambazuka.

Harufu ya maisha yako ni pale ulipo wewe, kila saa, kila wakati tunaingia jambo jipya lakini kila jambo jipya huwa na dalili, harufu. Kwa jinsi maisha yetu yalivyo ni kama mifupa yetu ilivyojipanga. Kwa wale ambao humwamini Yesu hawana usiku wala giza, Paulo anasema, ndani ya nyumba kubwa huwa kunakuwa na vyombo vya aina mbalimbali, vya thamani na visivyo vya thamani, Lakini sisi tunathamini vya thamani pekee. Ndiyo, sisi watu wa nuru, hatuangalii magumu, tunaangalia ni nini tutajifunza kupitia ugumu ule.

Endelea kusoma biblia kwa bidii ufikie uhuru wako wa kimazingira. Hamna namna, lazima tufurahie maisha wakati. Ishi maisha yenye maana na weledi.

Ukawe na shukrani juu yako na wakati wako, na mazingira unayopitia, kubali mazingira, chagua jambo jema kwenye mazingira yako, songa mbele.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Tuesday, November 13, 2018

Katika Wiki Ya Shukrani; Anza Na Chochote.

 Sadick Kilasi     November 13, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Habari Ndugu yangu?

Katika kuendelea na wiki yetu ya shukrani, ndani ya program yetu ya tabia nne za kuishi kwa mwezi, ili kuishi maisha yenye maana, leo tuangalie, anza na kidogo ulichonacho.

Badala ya kuendelea kulalamika kwamba maisha ni magumu, angalia kwanza, je! hakuna namna ambayo unaweza kuanza na chochote? Mara nyingi ukiendelea kulalamika mika bila ya kuwa na jicho la shukrani huwezi kuona vile ambayo Mungu amekupa.


Badala ya kujiona kwamba wewe ni mtu thaifu na huwezi kufanya lolote na ni mtu ambaye usiye na kipawa chochote, jikubali na kwa kumtumainia Mungu aliyekuumba. Mungu alimwambia Musa, mimi ndiye niliyekuumba nitatia maneno yangu kinywani mwako.

Jikubali, chunguza chochote kile, ili mradi upo hai una chochote kile cha kuanza nacho. Mungu anasema katika kitabu cha ufunuo, wewe unayekiita upo hai kumbe imekufa, tafuta chochote kile ambacho kimebaki kwako na kua kwa hicho ukikesha usiku na mchana.

Mungu anachotaka ni wewe kujikubalia, jikibali pokea vyote ambavyo Mungu kakupa. Lugha ya Mungu ni moja, una nini mkononi mwako? Una nini pembeni yako? Anachotaka ni sisi kukua kwenye vyote ambavyo ametupa. Hakuna kitu amnacho Mungu kakiuumba ambacho huwezi kuanza nacho kuwa fursa kwenye maisha, kila kitu ni jibu la matatizo yetu.

Jikubali, kubali mazingira yanayokuzunguka kwa kupokea kwa shukrani kila ambacho Mungu amekupa. Chochote ambacho unaweza kukibooresha, hata kama kinaonekana ni takataka kwa wengine ukiboresha huwa na thamani kubwa sana. Hakuna kitu ambacho si jibu la changamoto zetu, hakuna kitu ambacho si kiungo kwenye maisha yetu. Kuwa na moyo wa shukrani, yathamini mazingira kwa kuona ni zawadi yako na kiungo cha maisha yako. Kama yalivyo macho yako na ndivyo kila unachokiona ni kiungo mwako, kuna wakati unatumia, kuna wakati hutumii, kila kiungo hufanya kazi kulingana na mazingira.

Anza na chochote, kua Na hicho. Thamani ya chochote kile inategemea mtazamo wako, kuwa na mtazamo chanya wa kugeuza mazingira hasi kuwa chanya. Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Monday, November 12, 2018

Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha Ili Kuwa Na Furaha Zaidi.

 Sadick Kilasi     November 12, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   

Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha  Ili Uweze Kuwa Na Furaha Zaidi.

Ni wiki ya shukrani, ambayo imeanza leo. Binafsi ninafuraha kubwa sana ninapokuqndia makala haya,  jambo ninaloweza kushukuru zaidi ni wewe kuendelea kuwa pamoja nasi.

Wiki ya shukrani katika program ya kuishi maisha ya maana kwa mwezi, binafsi ninafuraha sana na naendelea kufurahia maisha.

Katika wiki hii ya shukrani kuna mitazamo ambayo unapaswa kudumisha ili kuendelea kufurahia maisha. Mitazamo hiyo ni yale mafundisho ambayo yalifundishwa na Yesu maarufu kama mafundisho ya mlimani.


Mathayo 5:3-4, Heri walio maskini wa roho;  Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

Mpendwa wangu ili kuendelea kudumisha furaha yako ni kwamba lazima uishi mtazamo chanya.

Usiangalie tatizo lako bali angalia ni kitu gani kitatokea baada ya kudumisha mtazamo wako chanya. Unajua mara nyingi sana watu tumekuwa tunafanya makosa, tunahuzunika tukitegemea kupata furaha, ni jambo ambalo haliwezekani kabisa.


Endelea kudumisha mtazamo wako chanya hata kwa wakati mgumu. Mambo mabaya hayana budi kuwepo lakini wewe kwa sababu ni mtu wa shukrani angalia tumaini lako la baadae. Haijarishi upo katika hali gani, zingatia kile kizuri wakati wote kwa sababu wakati unakuja utapokea tuzo lako. Ugumu unapita baada ya ugumu ulaini.


Usiangalie tatizo lako angalia tuzo lako. Endelea kufanya unachopaswa kufanya kwa sababu kila japo humtukia kwa wakati wake.

Una heri wewe ambaye ni maskini kwa sababu unaenda kuwa tajiri ukichukua hatua na kudumisha mtazamo wako chanya. Unaheri wewe ambaye unajisikia kuumwa kwa sababu kuumwa sio kifo bali ni mapito. Una heri wewe ambaye umeachwa kwa sababu huna lawama na mtu. Una heri wewe ambaye unasoma hapa na kufanya kazi lile ambalo unalisoma hapa kwa sababu harufu nzuri ya matumaini inanukia ya kuendelea kufurahia maisha.

Chochote kile ambacho ni kidogo, andelea kukipa thamani kitakupa majibu makubwa zaidi ya hayo.

Ishi kwa shukrani, usisahau ulikotoka ambako Mungu kakutoa, thamani kile ulichonacho sasa, furahia kile ambacho unatarajia kupokea.

Yape maisha yako thamani zaidi kwa shukrani, boresha zaidi maisha yako.

Sadick Kilasi wa
jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg

Sunday, November 11, 2018

Wiki Ya Shukrani.

 Sadick Kilasi     November 11, 2018     KUFURAHIA MAISHA     No comments   



Ni jumatatu ya tarehe 12/11/2018 siku ambayo tunaenda kuipa thamani kubwa sana. Siku ambayo tunaenda kuishi maisha ya maana zaidi yenye weledi, tukiongozwa na wiki ya shukrani. Tunakwenda kuyapa thamani maisha yetu kwa kuishi maisha yenye maana.

Unaanzaje kuishi shukrani pamoja na misukosuko mingi ambayo inakuzunguka?

 Kwanza kabisa, jambo la kwanza la kuiendea siku hii ya leo ni kuyakubali mazingira ambayo upo. Kama ndo unaamka basi mshukuru Mungu kwanza kwa uwepo wako, lakini pia angalia ni nani ambaye yupo jilani na wewe, mshukuru Mungu kwaajili ya huyo uwepo wake ni faraja kubwa sana kwako hata kama hajakufanyia lolote. Angalia kila kitu ambacho unakiona mshukuru Mungu. Hii unafanya kabla hujatoka nje. Unapofanya hivi unaanza kuishi matumaini kwa kuipa siku yako thamani yake na pia unakuwa unaipokea siku ambayo Mungu kakujalia na vyote ambavyo Mungu kakupa kwa siku hii ya leo. Tuliza mawazo yako hakikisha unafili mazingira na kila kinachokuzunguka. Ikubali siku kwa kuamka kiakili badala ya kuamka kimwili.

Baada ya kutoka nje, kubali kila kitu unacho kutana nacho kwa kusema, asante. Kila kitu kipo chini yako kitimie kama zawadi yako kwa wakati huo. Usikubali mambo ambayo ni ya tamaa yako yaiingilie siku ya leo.

Katika kuhusiana na wengine, mkubali kila mmoja. Tanguliza mapatano badala ya kuhukumu. Mwambie Mungu asante kwaajili huyu ayepo mbele yangu. Mpe thamani kubwa, mwangalie jinsi alivyo kwa jicho la wema. Mtazame harafu mwambie uvohisi juu yake. Kama kunautofauti, ufanye uso wako, uwe kioo kwake chenye kumfanya ajihi kwamba anahitaji kuendelea kuishi. Tumia maneno asante, nashukuru, samahani, kwa wingi usio na mipaka. Msifie pale anapofanya vizuri, mwombe samahani pale unapotia ushauri. Shauri kwa kiasi, ili thamani ya Ushauri wako iwe kubwa zaidi. Aliyeko mbele yako ni zawadi yako. Kila unachofanya tanguliza shukrani. Neno la lawama lisitoke kwako wala hukumu.

Leo ni siku yako ya kipekee, itumie leo kama ni siku yako ya mwisho kuishi leo. Kila jambo unalofanya, fanya kama hutapata nafasi tena ya kufanya.

Mungu atakuti nguvu, anachotaka kwako ni maandalizi ya moyo wako ili nguvu yake itawale moyo wako na akili zako. Shukrani ndiyo nguvu ya kuingia patakatifu yaani amani na furaha isiyoelezeka.

Siku njema yenye thamani zaidi.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
Read More
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Newer Posts Older Posts Home

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ▼  December (17)
      • Jani Lilojiachilia.
      • Je, Unaweza Kula Chakula Harafu Na Kufuta Mdomo Na...
      • Je! Andazi Laweza Kupita Mikononi Mwako Harafu Lis...
      • Je! Itapona?
      • Dalili Za Mabadiliko.
      • Sala Ya Shukrani.
      • Ni Wapo Wewe Mwisho Wa Pumzi Yako?
      • Ulipo Hapo.
      • Kifanye Kivuli Kiwe Nyuma Yako.
      • Kilichofichwa Hufichuliwa. Je! Mwizi Tutamchukuliaje?
      • Mungu Mfalme Wa Haki.
      • Bubujiko lisilo isha.
      • Wakati Wa Kujitokeza.
      • Sababu Nne (4) Kwanini Unapaswa Kusamehe Watu.
      • Katika Wiki Ya Hamasa, Nakuandikia Wewe Uliye Mkubwa.
      • Katika Wiki Ya Hamasa
      • Katika Wiki Ya Kukua, Unahitaji Kupalilia.
    • ►  November (25)
      • Katika Wiki Ya Kukua, Wewe Umeachwa.
      • Katika Wiki Ya Kukua, Kama Hatua Unazopiga Unapoel...
      • Katika Wiki Ya Kukua, Washa Njiti Yako.
      • Katika Wiki Ya Kukua.
      • Je! Ndege Hutegemea Tawi Alilotua?
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Mungu Ndiye Mfalme Wa Kil...
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Jiweke Nafasi Ya Wengine.
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Moyo Huwa Unakubali.
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Inahitaji Utambuzi Na Aki...
      • Katika Wiki Ya Kutawala, Toka Nje Ya Hema Yako.
      • Ndani Ya Wiki Ya Kujitawala, Jitambue Wewe Mwenyewe.
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Itazame Wiki Yako Imekwen...
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Ni Nani Aliyempanzi Wa Tu...
      • Mshukuru Mungu Kwa Kila Kitu.
      • Katika Wiki Ya Shukrani, Tambua Kitu Kikuongoze Ka...
      • Katika Wiki Ya Shukrani; Anza Na Chochote.
      • Ndani Ya Wiki Ya Shukrani, Mtazamo Wa Kudumisha Il...
      • Wiki Ya Shukrani.
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
All Comments
Atom
All Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates