Mara nyingi tumezoea kufanya vitu kimazoea. Kama ni kusoma tumekuwa tukisoma kimazoea kama watu ambao tunajua kusoma. Kama ni kufanya jambo lolote tunafanya kama watu ambao tunajua. Na hii siku zote nimekuwa nikisema, kujiaminisha kuwa kivuli ndio uhalisi wenyewe. Tunatembea kama vivuli tukiwa tunajua ndio ukweli kumbe ni kivuli cha ukweli.
Na kwa hili nimeona nikuandikie wewe uliye mkubwa, ambaye unajiona mkubwa, unayetembea na vivuli ukijua ndio ukweli.
Inawezekana wewe ni mchezaji wa mchezo fulani, inawezekana wewe ni mwandishi kama mimi, inawezekana wewe ni msomaji wa vitabu, lakini yote kwa ujumla nataka nikwambie unaweza kufanya zaidi ya unavofanya saizi. Hakuna mipaka kwenye kufanya. Watu wazima sisi ambao tunajiita watu wazima ndio tumekuwa tunajidanganya sana, tukiwaangalia watoto wadogo tunaona ni kama sisi hatuwezi kukua zaidi na tumefika mwisho na hata watoto wetu wanapaswa kufikia angalau viwango vyetu, wakue kama sisi. Tunatengeneza mipaka ambayo inawaandaa watoto kuwa kama sisi, tunataka waige vivuli vyetu vya mambo. Mwisho utakuta ukoo ama jamii fulani wanafanana kwenye kila kitu, kimafanikio na hata kifikra. Yote hii ni kwa sababu ya watu wanaojiona wakubwa, watu ambao kufanya kila kitu kwa mazoea na kuona kana kwamba haiwezekani kufanya zaidi ama kwa njia ya tofauti na jinsi ambavyo hufanya.
Tunaweza kuwaangali watoto wadogo wanapokuwa huwa wanakuwaje? Na hivi ndivyo inavyokuwa, inapaswa tuwe kama watoto wadogo, kuchukua hatari kama watoto wadogo, kupenda kujifunza kama watoto wadogo, kuwa watu wa haraka kuachilia msamaha kama watoto wadogo, ukishindwa kurudia kufanya kama watoto wadogo, unapaswa kukua kama watoto wadogo, kila kitu ambacho unakifanya fanya kama mtoto mdogo. Tunasafari ndefu sana, safari yetu ni kama kutoka chini ya ardhi kwenda mawinguni kwa miguu.
Usijione kama wewe ni mtu ambaye unaweza kila kitu, ujione kana kwamba unahitaji kufanya kitu bora. Usitundike kitu kwenye ubongo wako katika kufanya kitu. Kama nikikisea nikijua kwamba nimekosea na nikatubu basi ni bora kuliko kutokukosea harafu nikabaki katika hali ya kawaida na nisiadhiri chochote ama kuleta jambo jipya. Kufanya kawaida ni sawa na kubaki kawaida. Kawaida ni kitu ambacho tayari kimekufa.
Kama ni mtu mkubwa na unajiona kama ni mtu mkubwa acha kufikiri kimipaka. Anza kufikiri tofauti. Kile ambacho unapaswa kuishi tangu sasa ni kuipa thamani sasa kwa kufanya sasa kwa ubora wa hali ya juu.
Yesu Kristo alisema, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, hamwezi kuuuona ufalme wa Mungu.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment