Mti hauwezi kulirudisha jani ambalo tayari limesha jiashilia na kudondoka kutoka kutika pale lilipokuwa.
Jani huusapoti mti kukua kwenda juu na kukua zaidi kwa kadili ambavyo lilikuwa tayari kuusapoti.
Ukweli ni kwamba, hatunauwezo wa kuwalipa watu ambao tayari wametufikisha hapa tulipofika. Hata tuwe na vipato gani hatuwezi kufanya chochote kwa wale ambao tayari wamefanya tufike hapa tulipofika.
Kila mtu kuna mtu amemsaidia kufikisha popote pale alipofika. Hatukufika tukiwa sisi wenyewe pekee yetu. Na kwa sababu walisha tutendea hatuwezi kilipa gharama ambayo tayari tumefanyiwa. Nimefika hapa nilipofika ni kwa sababu watu wengine walikuja kama majani na kunisapoti licha ya jani kuwa ni sehemu ndoto ya mti lakini hao ndio walionipa chakula. Sijajua kama wasingekuwa wao leo ningekuwa wapi?
Haijarishi walikuja kwa picha gani ya ubaya ama uzuri lakini walinichonga hivi leo ninafurahia maisha. Aliyekuja kwa ubaya ulibidi aje ili tuone na tuambatanishe na uzuri ili tupate nguvu. Aliyekuja kwa uzuri alikuja ili tuambatanishe na ubaya ili nguvu ipatikane. Basi, viungo haviwezi kufanya kazi bila joint ambayo sawa sawa na udhaifu.
Leo ninafurahia maisha kwa sababu walikuja kwangu kama zawadi yangu. Naam, nimejiona kupitia wao.
Ninawashukuru nyinyi nyote ambao mlikuja kwangu na sasa hampo, kutokuwepo kwenu bado kunaniruhusu mimi nijione. Mungu awabariki. Majani yaliyodondoka nyinyi.
Basi, Adamu akasema, wewe ni mfupa wangu.
Nyinyi nyote ni zawadi yangu.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment