Mwaka huu nilianza mwaka kwa kuishi falsafa ya mti, ninashukuru nilianza kwa kuelewa mambo mchache lakini mpaka sasa kuna sehemu kubwa ambayo nimejifunza kutoka kwenye mti.
Yapo mengi sana ambayo unaweza kujifunza kutoka kwenye mti. Binafsi mimi nimejifunza kwa kiasi changu namna ambavyo mti unaweza kunielewasha nini maana halisi ya maisha. Kabla ya mwaka huu kuisha nitakushirikisha mambo ambayo nimejifunza kutoka kwenye mti lakini pia kwenye kitabu cha Dunia Mama Haimtupi Mwanae, nimeeleza mengi juu ya mti.
Unajua tunapoishi hapa duniani ni kama tumetupwa kwenye sehemu ambayo hatuijui. Na hata wale ambao wametumika kutuleta duniani wameendelea kuishi bila kutafuta uhalisi kamili wa maisha. Japokuwa wapo wengi ambao wamefanya kwa kiasi kikubwa ila nasi hatuna budi kujua zaidi na kuendeleza pale ambapo wamefikia wenzetu. Vipo vitabu vitakatifu ambavyo ndiyo msingi wa haya yote. Lakini yote kwa yote kuweka mambo wazi wazi, sifa za Mungu ni kuficha hekima na mwanadamu kufichua hekima za Mungu.
Wapi Mwisho Wa Pumzi Yako?
Ushawahi kuiona miti, miti ambayo inakuwa chini ya miti mingine? Bila shaka ushawahi kuona.
Tunachoishi duniani ni kukua na kukua huwa kunategemea utupu yaani anga. Sasa anga lako likiwa jilani ni wazi kwamba hakuta kuwa na uwezekano wa kukua, kwa sababu utazuiwa kwa juu ili usiendelee mbele. Miti inafokasi kuelekea juu angani, inakuwa na pumzi kubwa kwa sababu ya utupu mkubwa.
Katika maisha ya kawaida kunauwezekano mkubwa sana wa kuzuia anga na kufanya pumzi yako isifanye kazi vizuri. Na hii hufanyika katika ubongo wako namna ambavyo unaendesha maisha. Tamaa ya mambo ya dunia fedha, wanawake inaweza kukuzuia usipumue vizuri katika maisha yako, watu wanaokuzunguka wanaweza kukuzuia usipumue vizuri. Jiulize namna ambavyo unaendesha maisha yako, je, wewe ni mti ambao upo chini ya mti mwingine? Unapaswa kuona anga likiwa wazi juu na sio kuwa chini ya kivuli kingine. Tunakuwa katika hali nne, ambazo tunapaswa kupata wakati wote, kwanza, Maji, pili udongo ama kitu, tatu mwanga na nne hewa. Sasa hapa leo tunazungumzia mwanga na hewa.
Ukiwa chini ya kivuli cha mti mwingine huwezi kupata mwanga vizuri. Ukiwa chini ya mti mwingine huwezi kupumua vizuri kwa sababu unazuiwa na aliyeko juu yako.
Kutawala sio kumiliki, kutawala ni utambuzi, kumiliki ni kujimilikisha na kuweka mipaka. Kumiliki huletaa tamaa, tamaa ambayo inasababisha kuwa mtumwa wa hicho ambacho unamiliki. Unachomiliki kinakuzuia usione mbele yako wewe kitu ambacho husababisha pumzi yako isiwe huru.
Ndugu, tumebarikiwa tuwe baraka. Vitu ambavyo ni vya dunia hii huzuia pumzi yetu isifanye kazi vizuri. Chunguza kile ambacho kinakunya kila siku uamke na kufanya kazi, je? kinakupa furaha ama kinazuia pumzi yako tu! pumzi inapotoka vizuri inakufanya ujiachilie vizuri.
Elewa maisha ili uishi maisha, ni kipindi cha hakati hiki, tunaweza kujikuta tunajiingiza katika mambo ambayo sio kisudi letu kuishi.
Elewa na uishi, ishi na uelewe.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment