Ili uwe na uwezo wa kutawala vingine ama wengine kwanza wewe mwenyewe lazima uwe na uwezo wa kujitawala kwanza.
Kujitambua, nguvu yako iko maeneo gani yaani kitu ambacho unaweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu, ama wakati mwingine inaweza ikawa kiafya, ni maeneo gani upo bora zaidi lakini pia kimadhaifu lazima utambue kwamba ni maeneo yapi wewe ni dhaifu, huwezi kufanya vizuri na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu kiafya.
Eneo la kutawala linahitaji utambuzi na uelewa mzuri. Hii inasaidia kujijua wewe ni nani na unahitaji kufanya nini na mipaka yako ni ipi. Lakini yote hii ni kuhakikisha kwamba tunaishi maisha yenye weledi, furaha na amani.
Unapokuwa na uwezo wa kujitambua mwenyewe unauwezo pia wa kuwatambua wengine pia. Lengo pia ni wewe uweze kujihimili ili uwahimili wengine pia. Kila mtu anaubora wake na udhaifu wake. Vyote hivi viwili kwa mtu mwenye uwezo wa kujihimili havimtii tatizo kwani hatari kubwa katika maisha kwenye udhaifu ni kutanguliza woga badala ya shukrani.
Paulo pamoja na kuwa alikuwa ni msomi mkubwa na Mungu alimmiminia hekima nyingi na kuhubiri injili kwa kiasi kikubwa, inasemekana alikuwa na madhaifu yake ndani ya mwili wake, alikuwa anatembea huku ameinama kidogo mgongo wake. Lakini Paulo hajawahi kulalamika, kuna mahala kwenye vitabu Paulo alikiri kuhusu hili lakini hakuchukulia kama tatizo. Ukweli ni kwamba, udhaifu wetu ukiunganisha na maeneo ambayo ni bora ndiyo nguvu yetu.
Kwahiyo jichunguze ni maeneo yapi upo bora ili uyabireshe zaidi na ni maeneo yapi wewe ni dhaifu ili ubadilishe kuwa nguvu yako. Pale ambapo huwa tunapatanisha sehemu dhaifu na zenye uimara na ndipo huwa tunapata nguvu na ndiomaana maneno matakatifu yatwambia, kaza viungo vyako usilegee.
Uwezo wa kutajitawala mwenyewe ni jambo la muhimu zaidi. Ukiweza kujihendo mwenyewe, unaweza kuwahendo wengine. Mungu hutaka nibadilike mimi kwanza ili niwabadilishe wengine lakini na wewe pia hilo linakuhusu. Badilika wewe ili uwabadilishe wengine pia. Kwa chochote kile unachofanya lazima iwe hivyo.
Nikukalibishe katika wiki hii ya kutawala, mwanzo wetu ndio huu na kitu cha kuangalia leo ni kuangalia wewe mwenyewe ni wapi upo bora na ni wapi dhaifu. Dunia ilianza katika hali hiyo, Mungu aliona ukiwa na utupu, giza likiwa juu ya vilindi vya maji lakini Roho alikuwa juu ya uso wa maji. Mungu akasema na iwe Nuru, ikawa nuru, uwepo wa Roho wake ndio ulisababisha Mungu atamke nuru ndani ya giza. Mungu akasema nuru ni njema kwenye giza. Kwahiyo wema wa nuru ni ulitokana na giza. Huku ndiko kutawala kutambua tofauti.
Karibu sana, yapo mengi ya kujifunza na kubadili mitazamo juu ya mambo mengi ambayo wewe huchukulia kama mzigo lakini kumbe kwa sababu ya mtazamo wako tu.
Asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment