Mungu ndiye Mfalme wa haki, mizani yake ni ya haki. Ni nani aliye kama Mungu?
Mwanadamu ipoumbwa mawazo yake yalikuwa ni kukusudia uovu tu ndani ya moyo wake Mungu akaleta gharika ya maji lakini baadae Mungu akasema, sitaiangamiza tena dunia kwa maji kwa sababu mwadamu tangu utoto wake hujiwazia uovu tu. Ndugu, tupo tayari kufanya maamuzi kama haya ili tuushinde uovu kwa wema? Tumwige Mungu japo sisi si wakamirifu, tujitahidi katika hili.
Wakati Esau alipokuwa anataka kuchukua mibaraka yote kwa baba yake Isaka dhidi ya ndugu yake Yakobo, Mungu alifanya kwa haki, akambariki Yakobo kupitia kwa baba yake Isaka kwa sababu Isaka alikuwa kipofu na baadae akambariki Esau wote wakawa watu wenye mali nyingi na matajiri. Tusifanye kwa upendeleo kwa sababu fulani bali tunapaswa kufanya kwa sababu tunapaswa kufanya. Tujitaidi katika hili.
Wakati Raheli alipokuwa mzuri machoni pa Yakobo na Lea alikuwa dhaifu, Mungu alimtia utasa kwa muda Raheli na kumjalia Lea watoto sita na mwisho akamjali Raheli watoto wawili. Mungu hufanya kwa haki, hakuna mwanadamu ambaye aweza kutambua mahesabu yake.
Ndugu yangu, inawezekana upo katika hali ambayo ipo nje ya uwezo wako, unapitia magumu kiasi ambacho kinakufanya ukate tamaa, usijiweke chini ya haki yako wewe mwenyewe binafsi bali jiweke chini ya haki ya Mungu. Mungu hufanya vitu vidhaifu kuwa vyenye nguvu. Mungu humjalia kila mtu ambaye yupo tayari kumtumania .
Machoni pa mwanadamu kila kitu kinaweza kuwa sawa lakini machoni pa Mungu mambo huwa tofauti.
Yusuph aliyezaliwa wakati wa uzee kwa Raheli akiwa mtoto ambaye alikuwa na ndugu mmoja kwa mama alipitia wakati mgumu lakini baadae alikuja kuwaokoa nduguze, huo nao ulikuwa mpango wa Mungu. Jina la Yusuph lilitukuka kwa sababu aliwaokoa ndugu zake, je! ni nani ni sawa mbele za Mungu? Ndugu zake pia wasingeokoka bila Yusuph.
Sisi wanadamu ni kitu kimoja, kila mmoja ni kwaajili ya mwingine na si kwaajili ya haki yake binafsi. Anayejua ni anajua kwa sababu ya yule asiyejua. Sisi sote kitu kimoja na tujiweke chini ya haki ya Mungu na tumwachie Mungu yeye pekee ahukumu kwa haki.
Asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment