Tumekuwa na wiki mbili, wiki moja ilikuwa ya shukrani na wiki ya pili ilikuwa wiki ya kutawala. Wiki hizi zote mbili zimekuwa wiki ambazi zimejenga misingi ya sisi kuendelea kuishi maisha yenye maana.
Kama umekuwa unachukua hatua kwa kile ambacho unajifunza, natumaini kwamba umeona mabadiliko kwa kiasi fulani katika maisha yako. Lengo letu kubaki na kuishi maisha ya kawaida, sisi kama washindi tulioushinda Ulimwengu tunaendeleza kile ambacho tumekianza na kuzidi kukua katika msingi huo.
Tumeingia katika wiki ya KUKUA, wiki ambayo inataka tuende hatua ya ziada kwenye vile ambavyo tunavifanya. Katika maisha kitu kizuri zaidi ni maamuzi bora ambayo yanaamuliwa kutoka katika msingi bora maana mbegu bora zimepandwa ndani mwetu zinahitaji kumwagiliwa ili kukua zaidi.
Unachiweza kufanya sasa ni kufikiri sahihi sasa na kufanya maamuzi ambayo yapo sahihi zaidi. Tunapaswa kukua kwenye kila kitu, tabia zetu binafsi, katika mahusiano, katika vile tunafanya na mengine zaidi.
Ninachoamini ni kwamba, si kile ambacho umekifanya katika ubora mkubwa ndicho kilicho bora zaidi na wala si kile ambacho hujakifanya na unategemea kufanya ndicho kitu bora zaidi bali kitu bora zaidi ambacho mimi naamini ni kile ambacho unakifanya kutokana na maamuzi yaliyo bora zaidi. Thamani ya maisha ni sasa, sasa inaweza kuharibu kabisa mambo yote mazuri uliyofanya nyuma na yale ambayo unatumai kufanya.
Biblia inatutaka wakati wote tuwashe taa, nuru iwe inang'aa.
Lengo letu si kuisha kawaida na kuishi kuwa wa kawaida bali kwa chochote kile ambacho kipo mbele yetu ama kinapita mbele yetu ama kufanywa nasi, kinatakiwa kipewe ubora wa kipekee ili kiwe bora zaidi. Boresha mahusiano yako, boresha shughuli zako, boresha ufikiri wako zaidi.
Kuwa zaidi, nenda viwango vya juu zaidi. Wiki ya kukua ndo imeanza leo, twende tukiwa tunataka kuwa na njizi kubwa zaidi. Natumai kwamba tayari una mbegu ya matumaini yako, mbegu ambayo inapaswa kuwa mti mkubwa.
Asante sana
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment