Mlango mojawapo wa kuingia katika Ufalme wa Mungu ni kujiweka nafasi ya wengine. Licha ya mlango huu, mlango mwingine ni mlango wa shukrani. Kwa hiyo kuna milango miwili, shukrani na kujiweka nafasi ya wengine.
Wakati kuhani alipokuwa anafanya ibada ya upatanisho ili kuondoa dhambi za wana wa Israeli, ilimbidi kwanza ajitakase yeye mwenyewe kwanza pamoja na jamaa zake yaani familia harafu baada ya yeye kuwa safi atafanya ibada kwaajili ya jumuiya yote ya wana wa Israeli. Ikisha ataingia mahali watakatifu na makaa ya moto na ubani na kuvukizia moshi ilikufunika kifuniko cha Sanduku la Agano. Kumbuka, katika wiki ya shukrani tumejifunza kuwa, shukrani ni bayana ya mambo yasiyoonekana kwa macho, tukasema harufu. Lengo la kufunika kifuniko cha Sanduku la Agano, inamaanisha kutokujiangalia kimwili, yaani Sanduku ni miili yetu, sisi ni hekalu la Mungu.
Ndugu yangu, kujiweka nafasi ya wengine ndicho kitu ambacho kuhani alikuwa anafanya. Amri zetu kuu ni mbili tu, Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote na mpende jilani yako kama nafsi yako.
Nini kilichopo hapa, sisi sote tunamadhaifu, kuhani alikuwa anajitakasa yeye kwanza ikisha anawatakasa wengine. Je! wewe ukisamehewa huwezi kusamehe wengine? Ni rahisi kuwasamehe wengine kama hata wewe unajitambua na kujiona wewe ni mtu mwenye makosa, ulishakosa sana.
Ndugu yangu, watu hujiuliza ni kwa namna hani wanaweza kuachilia uchungu ambao unawaumiza, njia ni moja, ubongo wako unafanya kazi, je! wewe hujawahi kumuumiza mtu? Je! wewe hujawahi kumdanganya mtu? Usiseme huyu ameniumiza sana, Ndugu, chochote kile ambacho umemfanyia mtu mwingine kama hakifai huwezi kujua ni kwa kiasi gani kinaweza kuharibu maisha yake. Donge dogo la chachu huharibu chachu nzima.
Kama unaomizwa na uchungu ambao watu wamekufanyia, achilia kwa kukumbuka namna hata wewe ulivyowafanyia wengine, hii itakufanya ujione hata wewe hufai kitu na itakuwa rahisi kwako kusamehe. Kumbuka, ajikwezaye, hushushwa.
Kama mtu amefanya kosa usikimbilie kuhukumu bali angalia kwa jicho la upendo, hurumia, angalia mazingira ambayo yamesababisha kuwa katika hali hiyo. Hakuna jambo ambalo hutukia pasipokuwa na mbegu ya jambo hilo. Mara nyingi kila jambo ambalo kila jambo huwa linakuwa na nguvu hasi, nguvu hasi hii ndio husababisha ajali.
Kwa hiyo mpendwa, siku hii ya leo, jiweke katika nafasi ya wengine na kuwa na shukrani bayana na mambo ambayo huwezi kuona kwa macho yako. Siku zote huwa kunakuwaga na dalili na dalili ndiyo inakupa furaha. Shukrani huleta furaha na kujiweka nafasi kwa wengine huleta raha. Raha ya kuwa pamoja ambayo husabishwa na upendo. Upendo ni kuwa tayari kuchukua madhaifu ya wengine.
Katika maisha yako, vipe vipaumbele zaidi vitu hivi viwili. Kujiweka nafasi ya wengine na shukrani.
Kajifunze kutoka;
Walawi 16.
1Yohana 5.
Tunaendela na tabia ya zetu nne za kutoongoza kuishi maisha yenye maana. Ikiwa ni wiki ya Kutawala, leo tunaongozwa na kujiweka nafasi ya wengine. Jipe thamani, wape thamani wale ambao wamefanya makosa, warutubishe kwa sababu wewe umesharijua hili. Kuhani aliingia patakatifu wakati anajipatanisha mwenyewe akitoka anawapatanisha wenzake. Sisi sote ni kitu kimoja, haijarishi mtu amefanya kosa kubwa kiasi gani, kosa ni kosa yeye si kosa.
Kilicho ndani ya mwili huwa kinahitaji kutoka, kinatoka kwaajili ya wengine.
Kitu ambacho napenda katika maisha yangu, ni kuona wewe unatabasamu na tabasamu huja kwa kujitambua, madhaifu yako na maeneo ambayo upo bora. Na hapo marumaini ya kujiboresha huwa yanaanza ili kuhakikisha unafika katika viwango fulani baada ya kujiona. Wengi tunajitazama lakini hatujioni kwa sababu tupo bize kuwahukumu wengine, luwashabikia wengine na kujisahau kwa ajili yetu. Anza kujisoma.
Karibu kwa maswali juu ya hii program ya mwezi, nitumie ujumbe 0687000768. Tupo pamoja.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment