Ni wiki ya shukrani, ambayo imeanza leo. Binafsi ninafuraha kubwa sana ninapokuqndia makala haya, jambo ninaloweza kushukuru zaidi ni wewe kuendelea kuwa pamoja nasi.
Wiki ya shukrani katika program ya kuishi maisha ya maana kwa mwezi, binafsi ninafuraha sana na naendelea kufurahia maisha.
Katika wiki hii ya shukrani kuna mitazamo ambayo unapaswa kudumisha ili kuendelea kufurahia maisha. Mitazamo hiyo ni yale mafundisho ambayo yalifundishwa na Yesu maarufu kama mafundisho ya mlimani.
Mathayo 5:3-4, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
Mpendwa wangu ili kuendelea kudumisha furaha yako ni kwamba lazima uishi mtazamo chanya.
Usiangalie tatizo lako bali angalia ni kitu gani kitatokea baada ya kudumisha mtazamo wako chanya. Unajua mara nyingi sana watu tumekuwa tunafanya makosa, tunahuzunika tukitegemea kupata furaha, ni jambo ambalo haliwezekani kabisa.
Endelea kudumisha mtazamo wako chanya hata kwa wakati mgumu. Mambo mabaya hayana budi kuwepo lakini wewe kwa sababu ni mtu wa shukrani angalia tumaini lako la baadae. Haijarishi upo katika hali gani, zingatia kile kizuri wakati wote kwa sababu wakati unakuja utapokea tuzo lako. Ugumu unapita baada ya ugumu ulaini.
Usiangalie tatizo lako angalia tuzo lako. Endelea kufanya unachopaswa kufanya kwa sababu kila japo humtukia kwa wakati wake.
Una heri wewe ambaye ni maskini kwa sababu unaenda kuwa tajiri ukichukua hatua na kudumisha mtazamo wako chanya. Unaheri wewe ambaye unajisikia kuumwa kwa sababu kuumwa sio kifo bali ni mapito. Una heri wewe ambaye umeachwa kwa sababu huna lawama na mtu. Una heri wewe ambaye unasoma hapa na kufanya kazi lile ambalo unalisoma hapa kwa sababu harufu nzuri ya matumaini inanukia ya kuendelea kufurahia maisha.
Chochote kile ambacho ni kidogo, andelea kukipa thamani kitakupa majibu makubwa zaidi ya hayo.
Ishi kwa shukrani, usisahau ulikotoka ambako Mungu kakutoa, thamani kile ulichonacho sasa, furahia kile ambacho unatarajia kupokea.
Yape maisha yako thamani zaidi kwa shukrani, boresha zaidi maisha yako.
Sadick Kilasi wa
jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment